Tena kwa kuongezea da Asina hata ile mihadhara ya mpe huyo (biblia) imejikita manzese kwa bakhressa wakichoka magomeni kagera,(siwapondi na criticize) hilo la magerezani nilishawahi kuwafikishia watu (si humu ukumbini) we acha tu hakuna hata mmoja aliyenisapoti. any way nami nisiseme naanza kurukia ya magerezani wakti ya mradi wa twisheni temeke na warsha vimenishinda na kunidodea ila niseme tu kwa mujibu wa wafungwa wawil na askari magereza mmoja niliowahi kuzungumza nao HALI MAGEREZANI NI MBAYA MAPAMBIO, INJILI NA KURITADI KUMEPAMBA MOTO Wagala hawakosi kwenda kuhubiri sisi.....oh no si tunajenga mashule ya kiislam misikitini, ok si tunaendesha camp za vijana kujisomea, hayatoshi kwani??? TAFAKARINI HILO LA MAGEREZA. Kazi nyingi hufanywa na wachache Ushahidi wa hili si mnamwona yule mtuhumiwa mtoto wa mauaji al maarufu Ramadhan mla watu
anavyotinga Kisutu na zinga la msalaba shingoni kila siku ukicheki majina Ramadhani bin Mussa, dini Islam. Kazi ipo........ Da Asina nimeongeza wadau wengine hapa katika email yako kwa kuwa ni watu ninaowa feel sana katika mambo yetu haya Asante
--- On Wed, 2/17/10, asina omari <asina...@googlemail.com> wrote:
Abeid na wengine,
hapo ndipo tulipo fikia na ninadiriki kusema na bado tuendeleako ni kubaya zaidi,
saa nyingine mie huwa najiuliza kosa ni la nani? kule kwingine hivyo hivyo ...
nawaambia tampro angalu organize misaada hata kama hamna uwezo wa kwenda wapeni hao walioko huko ... kimyaaaaa
kila siku watu wana waona akina sister jane na brother michael wa all saints n.k
ni the same thing na ukienda katika magereza ...
jamani daawah sio kuwalingania watu misikitini peke yake ... after all msikitini you are preaching to the converted ....
hivi khadija wa pale kilosa akiokoka kwa vile walokole ndio waliowengi kule wanaomba na kutoa misaada tuta mlaumu? sie athari yake katika jamii ni nini? jamani nina miaka mingi sana sia sikia mtu amesilimu kwa vile amevutiwa na tabia za waislamu au maisha ya waislamu .... well ukiacha wale wa peace tv au noor tv n.k
eeh ngoja nisiseme sana ila kazi kweli kweli mungu atunusuru
A.
2010/2/10 abeid othman <aaoy...@yahoo.com>
AAWW Nafurahi kuwa mjadala umeshtadi, mengi yanasemwa na hakika wapo wanaojifunza na kutenda kwa yale yanayojadiliwa humu. Ila naomba niwajulishe kile alichokisema Da Fatma kuwa tatizo linaweza lisiwe huo mtihani bali system nzima na namna shule zetu na umma kwa ujumla zilivyojipanga kuendesha mambo. Naomba niwape kisa nilichokutana nacho jana usiku maeneo ya Ubungo Kibangu hapa Dar es Salaam
Nikiwa narudi nyumbani kutoka ofisini wanawake wawili walikuwa wakizungumza kuhusu maombi kanisani, masikio hayana simile hasa yakiwa ya mtu wa aina yangu, hivyo nikawasikia wakizungumza kama ifuatavyo (sehemu ya mazungumzo)
mwanamke wa kwanza: Mimi nimeokoka mwanmke wa pili: Heh umeokoka we si Muislam? mwanamke wa kwanza: bwana we Mungu si yule yule Niliumia kwa majibu haya na walipoachana ikanibidi nimfuate yule mwanmke wa kwanza, kujua kwa nini amemua kufanya hivyo huku akiwa Muislam ilibidi nimpe shule na kumwambia atafakari maneno yangu
Kimsingi alionekana kunielewa japo alikuwa akisisitiza kuwa yeye Quran kaisoma na wala haoni tatizo kuokoka kwani Mungu ni yule yule mmoja Waheshimiwa hapa ndipo tulipofikia, huyu anadai amesoma madrasa hali ndiyo hiyo vipi wale ambao hata alifu imewapitia kushoto?
Fatma amesema tatizo ni zaidi ya hili lililopo sasa wakt tunajadili haya tujue vile vile kuwa tuna akina Alicia Rashid Kawawa, na Magdalena Khamis Al sheikh kibao mitaani Asanteni
--- On Tue, 2/9/10, Haji Rubibi <hru...@gmail.com> wrote:
From: Haji Rubibi <hru...@gmail.com> Subject: Re: MATOKEO KIDATO CHA NNE - SHULE ZETU
To:
Date: Tuesday, February 9, 2010, 10:51 PM
AAWW!
Kwangu Sotele ni miongoni mwa shule bora za waislam:
--> Ndio shule pekee ninayoifahamu ambayo haifukuzi (haichuji) wanafunzi eti kwasababu wamekosa credit saba, tano, nk.katika mtihani wa kidato cha tatu (au vidato vingine) na still hutoa matokeo yenye kuridhisha-kuna division zero moja tu mwaka huu.
--> Kuna wanafunzi kadhaa ninaowafahamu walioondolewa baadhi ya shule za Kiislam na kupokelewa Sotele na Alhamdulillah leo tuongeapo wanafanya mtihani wa kidato cha sita. Na wengine walijiunga na vyuo vya Ualimu baada ya kumaliza na sasa wapo makazini.
Hata hivyo, hii haimaanishi kwamba haihitaji kuboreshwa zaidi katika maeneo mbalimbali.
Haji.
2010/2/9 Fatmah Khamis <fatmah...@yahoo.com>
Aaww.
Tuna hali mbaya sana jamani hivi tutaponea wapi dunia hii? Inapofikia shuke inapata ZERO 117 ni hali ya hatari. Nimejaribu kutathmini matatizo ni nini sijapata jibu. Niliuliza swli pia hivi ni kwa nini tunapata matokeo ya aina hii katika shule zetu za kiislamu? Zaidi ya kubahatisha matatizo na sababu kwa njia ya "kupiga ramli" je tumewahi kufanya tathmini ya kitaalamu kuhusu hali hii kama wasomi wa jamii yetu na kushauri hatua za vitendo?
Njia sahihi kutatua hali hii ni kupitia mifumo na taratibu (systems). Je, kuna chombo cha kupanga, kusimamia na kutoa ushauri wa kitaalamu wa elimu cha kiislamu? Nani mhusika wa elimu kwa waislamu tumbane?
Anachofanya dda Riziki ni a good step, na wengine wanaofuatilia michakato iliyoshauriwa na Mbeyu na Abou Hajira. Lakini nachotahadharisha, inawezekana kabisa kilichosababisha hiyo misaada isifuatiliwe huko alikosema Mbeyu ni huku kukosekana mfumo. Dada Riziki atakwenda kuonana na Dr. Mcharazo, kama nani? Mwalimu wa Diplomasia? Ex-MSAUD? TAMPRO? a friend of "South Alliance"? au mama mwenye uchungu na elimu ya watoto. Mungu si Athumani, akihama nchi kesho au akafariki dunia na maktaba Mafia kwa heri!
Mie naomba tuliangalie hili swala kwa mapana na tusipapase. Kama tunaweza kushauri na ku-plan kwa ajili ya mashirika, maSerikali nk, vitu vya kiduni kwa nini hatupangi vya kwetu?
Sotele shule yetu chini ya Wataalamu TAMPRO, kwa nini hatuanzi na hapo kwanza? Wasomi walio Wizara ya Elimu na Taasisi za Elimu za ndani na za kimataifa tunawatumiaje kiushauri?
Mtu mmoja aliwahi kuniambia tatizo shule za BAKWATA ndio zinatia aibu zinafelisha sana hazina utawala mzuri wa elimu, nguvu kazi sahihi nk. Lakini zipo shule za mashirika yenye fedha na wataalamu kama Al-Farouq, Ununio, Kunduchi, nk hali ni ile ile.
Leo tunahaha na matokeo ya Form Four, sasa hivi kuna decline hadi kwenye matokeo ya darasa la saba na huko atasaidia nani? Tunahaha ha Form Four, wale wa Form six yakitoka hovyo pia tutafanyaje. Higher education ukiuliza wanafunzi wangapi wa PhD Tanzania waislamu hawafiki 10.
Mimi naaomba pamoja na hatua hizi ndogo ndogo za kufuatlia hiki na kile kwa kujitolea mmoja mmoja, but pia tuchimbe zaidi kuweka mkakati mkubwa wa elimu na mipango ya utekelezaji wake kwa miaka 100 ijayo na sio siku 80.
Ni mtazamo wangu.
“OUR EFFORTS TOGETHER, OUR DEVELOPMENT FOREVER”
Fatmah M. Khamis
(Ummu Rahmah)
BCOM (DAR), MBA ( SSE,Stockholm ), MSc - Economics ( SDU, Odense ), EMBA (CEU/UMEA), PhD (CEU, Budapest )
--- On Tue, 2/9/10, Haji Rubibi <hru...@gmail.com> wrote:
From: Haji Rubibi <hru...@gmail.com>
Subject: MATOKEO KIDATO CHA NNE - SHULE ZETU
AAWW!
Tumejaribu kujibu swali la dada Asina katika kiambatanisho.
NB:
- Tumechagua shule (66) zenye kujinasibisha na Uislam/Waislam kwa namna moja au nyingine.
- Kama kuna shule tumiacha, tukumbushane tuiongeze kwani hatuzijui zote.
- Kuna shule kadhaa zenye wanafunzi wengi wasio waislam kuliko hata waislam mfano ISLAMIYA na TAQWA
- Interesting, katika usajili mivumoni ni ya pili toka mwisho kwenye orodha ya shule hizo lakini imefanya vema.
Maoni yangu:
- Kwa ujumla ufaulu si mzuri sana. Vijana wenye sifa za kuendelea ni wachache kuliko waliokosa.
- Shule iliyofanya vema zaidi (overall) ni Nyasaka.
- Shule za Bakwata ndio huchukuwa wanafunzi wengi na ndio zenye idadi kubwa ya waliofeli.
- Seminary nyingi zaonyesha kufanya juhudi za kuondoa division zero kuliko kupata division one.
Kumradhi kwa ku-edit subject, lengo ni kutaka tusichanganye mada. Hii inaweza kuwa ya kujifanyia tathmini na ile ya kujikwamua jamii kielimu.
Haji
2010/2/7 asina omari <asina...@googlemail.com>
Aaww,
unfortunately nimekuja katika mjadala late kidogo but that means alot has already been said,
hongera zangu kwa wahitimu na walimu wao pamoja na wengineo wote
Kaka Haruna, analysis yako ni nzuri sana but i must say its overily generalized and stereo typed, am glad Aunt yangu Riziki has given a live example ya kwa nini nasema hivo!
shule zetu nyingine vipi?
enhe sie wakusini tunajiandikisha wapi maana kwa kweli tumechelewa
A.
2010/2/7 abeid othman <aaoy...@yahoo.com>
aaww Naafiki mawazo yako Bi Riziki --- On Sun, 2/7/10, Riziki Shahari <riziki...@yahoo.com> wrote:
From: Riiki Shahari <riziki...@yahoo.com>
Subject: Re: MATOKEO KIDATO CHA NNE
|
AAWW.
Alhamdulillah, hakika Mwenyezi Mungu ni muweza wa kila jambo!
Nawashukuru Haruna, Abeid na AbouHajirah kwa michango yenu - changamoto na mapendekezo mliyotoa. Shime Wanakusini na Wanapwani Februari inayoyoma hiyo, tumesikia huyo Dr huko Kilwa, hatuna cha kusubiri. Mimi ni mmoja wa makundi yote hayo mawili kwa mujibu wa Uislamu lakini pia kwa asili za wazazi wangu wawili.
Namba ya ofisi ya Katibu pale Msikiti wa Mtambani ni 022 2666744 lakini kwa wiki kadhaa ilikuwa ikiita bila kupokelewa, ambayo si hali ya kawaida, nahisi ina matatizo.
Jingine ni tahadhari tu. Ni kuhusu kutoa tuzo kwa vijana wetu walotufuta mchanga wa macho. Hapa namaanisha vigezo (criteria) zitakozotumika. Tahadhari ninayopenda kutoa inahusiana na mawazo ya Kaka Haruna kuhusu wanafunzi wa shule kama za Feza na nyingine kama hizo. Sikumbuki ni mwaka gani hasa lakini ni hivi karibuni ambapo Feza ilitoa THE BEST PERFORMER, yaani namba moja nchi nzima kwa Form VI. Alikuwa kijana wa Kiislamu, mtoto wa MJASIRIAMALI MLALAHOI wa Tandika, na nadhani alikuwa na mama tu wakati huo! Ilikuwaje? Feza waliamua kumsomesha bure baada ya kuona KICHWA cha kijana huyo katika matokeo ya Form IV. Jamani kuna vijana wa Kiislamu wanapata Div 0 wakiwa Feza, Al-Muntazir na Ilboru / Kibaha / Mzumbe!!! Nadhani Kaka Haruna na wengine mmenielewa.
Hivyo pendekezo langu ni kuwa wote wanastahili kupongezwa isipokuwa Aboubakar anaweza kupewa na nyongeza maalum kama tuzo ya "OVERCOMING ALL ODDS" kutokana na mazingira ya alipopatia matokeo yake. Walimu na Shule yake nao inshaAllah tutawatuza.
NAOMBA WANA MAKUNDI MAALUM (PWANI NA KUSINI) MJITAJE HUMU KWENYE MTANDAO TUANZE KAZI MAPEMA INSHAALLAH, HATA KAMA NI KUWAHI BAADA YA KUCHELEWA!
|
WWWW
Ushauri wangu kwa watu wa Kilwa na hata mikoa ya kusini kwa ujumla ukiwemo mkoa wa Pwani wafanye yale yanayofanywa na wenzao wa maeneo mengine
Kivipi? wasomi wa maeneo haya ndiyo wanaopaswa kuwa vinara wa kuchochea maendeleo Wajitafute walipo wasomi ndani na nje ya nchi waji organise wanaweza kuanzisha hata mifuko ya elimu kama walivyo wenzao wa mikoa mingine
Huku sioni haja ya kuwa na skuli maalum za kiislam kwani zilizopo tayari asilimia kubwa ni Waislam cha muhimu ni plan za maendeleo ili skuli zipatiwe vifaa husika
Nakumbuka kun Dr mhitimu wa Muhimbili amepangiwa Lindi anasema mahala alipo kuna shule zaidi ya 20 hazina mwalimu wa sayansi zote watoto ni wa Kiislam hata yeye amechoka kwani hawezi kujigawa
So natoa changamoto kwa wasomi wa pande hizi kutaneni/tukutane si lazima iwe kwa sura ya dini japo kwa sura ya kitaifa mtaweza kusaidiwa mnakumbuka Lowassa enzi zile alitoa kiasi gami katika mfuko wa elimu wa Bukoba? yeye na Bukoba wapi na wapi?
--- On Sun, 2/7/10, AbouHajirah Abdallah <binabda...@yahoo.com> wrote:
From: AbouHajirah Abdallah <binabda...@yahoo.com>
|
Asalaam aleikum warahmatullah wa barakatuh,
Matokeo yamefika, je ni msimu wetu wa kuanza kulalamika , kulumbana, kutukanana?
Bro Haruna ameongea mengi tunashukuru kwa kutuamsha tulolala.
Hali ni ngumu ila vijana wetu waliofanya vyema inastahiki wapewe pongezi na kuenziwa ili wawe mfano bora kwa wengine, Vijana wetu waliofanya vyema tuwakurubishe kwetu ,
tuwape zawadi kwa juhudi zao walizofanya, ni kazi ngumu wamefanya Mabrouk kwa juhudi za skuli hizi zenye maono ya mbali na maendeleo ya waisilamu, Shime wana ukumbi tuwasaidie hawa vijana wetu angalau tuanzishe mfuko maalum(Award za waliofanya vyema) na kuwapa support ili kuendeleza libeneke Inshallah.
Wadau naanza kwa kutoa shilingi alfu Ishirini ya mwanafunzi na alfu ishirini kuchangia maktaba ya skuli Inshallah.Napendekeza kaka Abeid , Dada Asinah na dada Fatmah wawe wapokeaji wa hizi amana.Pia namba za simu za skuli zingewekwa hapa ukumbini ili tuwpe hongerza zao waalimu na kuwaandaa wanafunzi wengine.
Pia nachokoza kuhusu watu wa kusini(Kilwa) kama alivyogusia al-Akhi Haruna hali zao mbaya, je hatuwezi kufanya harambee ya kujenga angalau skuli moja?Pia suala la wanawake/wasichana inabidi tutafute mbinu mpya ya kuwainua katika jamii zetu na skuli zetu kama ilivyofanya Marian na seminary zingine!
|
www
Naafiki wazo la kaka Haruna la kupitisha bakuli kumpa motisha kijana huyo.Walio karibu wanaweza kuu contact uongozi wa shule pale msikiti wa Mtambani na walio mbali wanaweza kutafuta njia za kufikisha sadaqa zao.
Ni wazo zuri hili ama mwaonaje masheikh wa masheikhat?
Aaww. Napenda kuwapa pongezi vijana wetu haswa Abuubakari Ally kutoka shule ya Mivumoni Islamic School(shule iliyopo msikitini- Mtambani-Kinondoni) ambaye ni miongozi mwa wanafunzi bora kwa Wavulana, wapo na vijana wengine kama Hamidu Mbonde na Said Abdallah toka Feza Boys,nimeegemea zaidi kwa Abubakari kutokana na mazingira duni ya shule aliyosomea.
shule hii ya Mivumoni huu ndio mtihani wao wa kwanza kitaifa kushiriki, hivyo sina budi kuthamini mchango wa walimu wao chini ya Ustadh Nsumba kuweza kutoa mwanafunzi bora kitaifa hii ni faraja kwetu sote.
Aidha kwa vile hali ya shule ilikuwa ngumu basi naamini wanafunzi wengi wao wanatoka katika mazingira kama yangu ya Tandale kwa Mtogole ambao wanakuwa hawana hata mtu wa kumuomba kitabu au msaada wa kimasomo.
Inawezekana kabisa Abubakari akawa ndio mwanafunzi wa kwanza kwenye familia yake kwenda kidato cha tano, ndio maana mafanikio yake yamenigusa sana,wale waliosoma FEZA kama jina la shule linavyojieleza huenda wakawa wametoka kwenye familia bora kama jina la shule yao linavyojieleza(Familia zenye Fweza),Sababu nyingine wale waliomaliza Feza tayari wameona mifano ya wenzao wakifanya vizuri kwa miaka kadhaa.huyu wa Mivumoni yeye ndio darasa lao la kwanza kufanya mtihani wa kidato cha nne na hakuna A level shule kwake.
Mafanikio ya Mwannafunzi shuleni au chuoni yanachangiwa na mambo mengi watalaam wa SOCIOLOGY mnajua zaidi, kuwa mazingira na hali ya familia vina mchango mkubwa kwenye mafanikio ya mwanafunzi,Mimi wa Tandale kwa Mtogole ninayesoma Mivumoni rafiki zangu ni kutoka Vingunguti Kiembe
Mbuzi na Manzese Uwanja wa Fisi(Peer Group) yule wa Feza na Mzizima rafiki zake ni kutoka Masaki,Mbezi Beach na Oysterbay.
Mwalimu wa Mivumoni akisema anataka apewe kitabu cha Nelkon au Ramsden itabidi asubiri kofia ya siku ya Ijumaa na inawezekana asipate kitabu hicho,yule wa Mzizima anakutana na orodha ya vitabu na mazingira mazuri ya kazi,
Niliwahi kuwa mbishi wa juu ya standards za shule na vyuo mbali mbali duniani.jamaa akaniambia kuwa Chuo kikuu cha Harvard au Oxford hakiwezi kuwa sawa na Udsm au St.Augustine na hata uwezo wa kiakili wa wanafunzi utakuwa tofauti sana wale waliopo Oxford watakuwa ni cream toka shule mbali mbali bora duniani na wale wa Tumaini University watakuwa si wa calibre ya Harvard.
peer group ya Obama akiwa Harvard sio sawa na peer Group ya Mwanafunzi wa Tumaini iliyopo Iringa au Chuo kikuu cha Mwenge,bado hujataja tafiti mbalimbali na pesa zinazotengwa kwa ajili ya research,Kuna vitengo maalum kwenye vyuo vya kufanya tafiti,mfano kuna rafiki yangu alisema kuwa Research Methodology kwa ajili ya Dissertation yake alifundishwa na wahadhiri nane tofauti na chuo kwao kuna online Journal zaidi ya mia tano kwenye fani yake amabazo chuo kinanunua kwa gharama kubwa sana,
Nazungumza kwa ushahidi nimewahi kuitembelea shule yetu hiyo ya Mivumoni na kuona mazingira halisi ya shule, hawakuwa na vitabu vya shule vya kutosha sidhani hata 40 vilikuwa vinafika kwa idadi kiasi cha mwaka na ushee nilipokwenda shuleni hapo.lakini walimu na viongozi wa shule waliongozwa na Slogan ya Change we Need na kujiaminisha kuwa kweli tunaweza (YES WE CAN).
Mafanikio ya Mivumoni ni jibu sahihi kwa wale wanaoendelea kulia na Mfumo Kristu badala ya kujipanga na kuweka mikakati,kila tunaposhindwa kufikia malengo kisingizio kinaletwa kuwa kuna mfumo kristu na Bakwata inatumiwa na serikali kuharibu mipango yetu,lakini kwenye mambo yetu binafsi tunafanikisha bila kusema kuwa Mfumo Kristu umetubana, hivi leo hii OilCom au Manji akitaka kiwanja katikati ya jiji anaweza kukikosa kwa kisingizio cha kuwa kuna Mfumo kristu umemzuia?
Biashara ya madawa ya kulevya inapigwa vita sana Duniani lakini yule King hapa mjini ni Muislam anaishi Oysterbay na wanaohusika na kupambana na biashara hiyo wanakwenda kuchukua pesa na kumuacha akidunda, nazungumzia mtandao wa juu kabisa sio kete moja au mbili za hapa kwetu Tandale,
Kwa vile tumekuwa sio wakweli kwenye kuleta maendeleo kwa jamii yetu basi hatukosi visingizio kama Kocha wetu Maximo,tukishindwa mechi utasikia sababu Godfrey Bonny ana miaka 28 hivyo ni mzee ameshindwa kusema kuwa Giggs wa Manchester ana 37 au Van desar ana 40, au Ricaldo Fuller wa Stoke City ana 38 na mchango wake uwanjani unaonekana,
Mara Boban na Chuji hawana nidhamu ndio maana tumefungwa wakati Rio Ferdinand alikimbia kupimwa kwa vile alikuwa kavuta bangi akafungiwa mwaka mzima Kocha wake akamfanya captain wa timu na Capello kampa timu ya Taifa awe captain,George Best alikuwa mlevi wa kutupwa,Paul Gascoigne-Gaza,Tony Adams wote ni walevi na makocha wazuri walitafuta mbinu za kuwafanya waendelee kuchezea timu zao za taifa,
Boban na Maradona nani mtovu wa nidhamu?.leo hii Rooney kama angepewa Maximo basi asingekuwepo uwanjani kwa makuzi mabovu aliyokulia nayo lakini Meneja Fergusson anajua nini maana ya ualimu,
Mara Maximo atakuja na mpya kuwa sikuja kuleta kombe ila kujengwa misingi na mpira unaanzia chini kwa watoto, kama hivyo ndivyo anavyoamini kwanini asichukue timu ya watoto na wakubwa akawaacha watu wenye uwezo kama kocha wa Simba au huyu mzungu wa Yanga muda mfupi kabadilisha kiwango.
Msingi wa hoja yangu ni kuwa tutimize wajibu wetu kwanza halafu ndio tuanze kutafuta mchawi.Jamani tuwe wakweli wanafunzi wa Twayybat na Marian Girls wako sawa?Mazingira ya Marian Girls na Twayybat ni sawa? mfano huo huo uipe timu ya Manyema yenye makao yake dukani kwa Ali Mmanga mtaa wa Lindi na uifananishe na timu ya Yanga au Manchester United,
kwa mfano Marian Girls katika walimu wao walichukua walimu walioifanya Al-Haramain iwe juu ilikuwa ya tatu kitaifa, wenzetu wanafuatilia vipaji na kuvifanyia kazi hawabahatishi,
Ni kweli kuna hila za hapa na pale lakini kama kuna nia thabiti na dhamira za kweli hakuna wa kutuzuia kwani ahadi hiyo katupa Mwenyezi Mungu kuwa ushindi uko kwetu kama tutafanya kwa nia dhabiti na kwa ajili yake.
Hivi karibuni kuna mtu kanitafuta kuwa nitafute mtu anayeweza kusaidia Computer moja kwa ajili ya shule moja ya kiislam ili kuinua kiwango cha taaluma aliyenitumia ujumbe ni mkuu wa taaluma,nikamwambia siwezi kufanya hivyo hao wenye uwezo wa kuchangia hawatanielewa,sababu shule hiyo niliiombea Computer 50 kwa wasamalia wema, wakapewa tena mpya kabisa.mimi nikaenda kupiga picha na kuwatumia wale waliotoa,muda si mrefu wenye shule wakaamua kwenda kufungua Internet Cafe kwa kutumia zile Computer kama mradi wao binafsi,jee kwenye hilo Mfumo kristu umeingia vipi?
Nikirudi kwenye mada yetu ya kijana Abubakar wa Mivumoni naona kuna haja ya kumpongeza tuliopo hapa tunaweza kuamua nini tumfanyie ili ahisi kuwa mafanikio yake ni yetu sote,tutakuwa tume Mmotisha na kuwapa Motisha wale walio nyuma yake ili wafuate nyao zake, nadhani umefika wakati wa kuwa hamasisha vijana wetu,kuna watu niliona wana program inaitwa Elimu-ILMU AWARDS,tunaweza kukubaliana hapa kila mwenye mia tano au elfu tutachanga na tukawa na wajumbe kadhaa wakaenda kumkabidhi kijana wetu huko shuleni kwake,mfano ustadh Poyo,dada Asina na Fatma wakatuwakilisha kwenda kuongea nao na kumkabidhi zawadi,lakini pia kijana kama huyu anatakiwa apate watu wa kumtizama na kumpa ushauri kadri anavyokwenda na masomo yake,
Mfano John Mnyika wa Chadema alipata division one ya points saba akiwa O level huko A level akachemsha vibaya kiasi cha kukosa sifa za kusoma Chuo kikuu lakini lazima niseme kuwa Mnyima ana General knowledge kubwa sana kutokana na Exposure,
Kwenye mchango kama tutakubaliana na wajumbe basi tunaweza kumnunulia vitabu vya A level na mambo mengine ili muradi apate zawadi itakayoendana na mambo ya Elimu, isije akatokea Cousin wangu kwa vile siku hizi toka Drogba aje hapa nyumbani basi naye kajenga Interest ya Mpira akasema tumnunulie jezi ya Chelsea iliyoandikwa Drogba,
baadhi ya wajumbe niliwatumia email kuwa Cousin alikwenda kushuhudia mtanange wa Taifa Stars na Ivory Coast Live kwa mara ya kwanza ,yaani siku ile Cousin wangu alikuwa na furaha sana,
au Cosuin wangu akasema tumnunulie simu awe na line nne kama zake yeye,hapo tutakuwa tunamshughulisha mtoto wa watu,mnajua kuwa cousin ana line nne za Zain,Voda,Tigo na Zantel na ana zingine tatu za kutuma sms za matusi jumla saba, mie nina wasi wasi kama Cousin wangu ni mzima kichwani,
kiakili haiwezekani DR.Abeid Gasper akawa na line nne,kuna mtu kaniambia kuwa unajua kuwa cousin yako ana line nne, nikamjibu inawezekana alipokuwa mtoto hakuchezea vifuu na toys,wana saikolojia wanasema kuwa mtoto akikosa kufanya baadhi ya mambo udogoni basi atayafanya ukubwani,
jaribu kupata picha Cousin yuko na familia yake wanakula chakula cha jioni halafu simu ya kwanza inaita,mtoto anakuja baba Voda yako inaita, mara mie nami nampigia line ya wanyonge Tigo mtoto mwingine anamletea baba na hii inaita, mara Zain imeingia,hata watoto watafikiri kuwa baba anacheza na toys.
lakini msimlaumu sana Cousin wangu hata Mzee Mandela kwa vile alikaa sana jela kama miaka 27 fashion za nguo nyingi zilimpita akiwa jela, ndio maana mara alipoachiwa huru akawa havai suti sana ila anakula pamba za vijana,leo shati hii kesho lile alimuaradi afidie Fashion zote.
Cousin najua ukiona ujumbe huu si sms hizo za kuporomosha matusi,naomba nikufahamishe kuwa simu yangu nimeBlock sms zako kwa muda kuna kitu nafanya nikimaliza nitakushtua,kwani zinanipa afya na nina zipenda endelea tu Cousin,
tukirudi Mivumoni wametuonesha njia kuwa kwenye nia pana njia hivyo tuwe na mikakati nini tunataka sio kulia kila dakika,Mivumoni wametutumia ujumbe kuwa OUR FUTURE,IT'S IN OUR HANDS,lakini tuwe makini asije kutokea mtu akasema kijana huyo apelekwe shule ya Mivumoni hapo hapo kwa vile kuna kidato cha tano kinaanza,tumwache aende kama ni Kibaha, Mzumbe au Ilboru akakutane na wenye vipaji wenzake,kama ni Tuition atasoma hapo Mivumoni,lakini nafasi yake special school aende,
Ustadh Nsumba anaingia kwenye lile kundi la Fine Teacher amablo lina watu kama Issa Maige,Professor Njozi,Ustadh Tego,Dr,Abeid Gasper n.k,Mwanafalsa William A.Ward anasema "A mediocre Teacher tells,a better Teacher explains,a good Teacher demonstrates,but a FINE TEACHER INSPIRES" sijui Cousin wangu anaingia wapi kwenye hilo kundi kama akisema ni Mwalimu.
Kitu kingine tumuombe Mwenyezi Mungu awaongoze watu wa mivumoni isije kuwa kupata Division one Abubakar ndio ikawa licence ya kuifanya elimu biashara,hivi sasa jamii yetu imekumbwa na balaa hili la kuifanya elimu ni bidhaa na si huduma,
mtu hapati elimu kwa uwezo wake wa akili bali uwezo wa pesa ndio tiketi ya kupata elimu,hivi karibuni Kardinar Pengo alikuwa akihutubia sherehe ya kidato cha nne kwa shule ya wavulana Bagamoyo ikiwa ndio graduation yao ya kwanza, akawaambia kuwa anawaomba wakatoliki wote Tanzania wajitahidi wasiingie kwenye mtego wa kuifanya elimu Biashara,
iendeee kubaki kuwa huduma,leo hii kuna waislam wamesoma kwa taabu kwa bakuli za waislam hadi kwenye level za Masters wamesomeshwa kwa bakuli leo hii wanawasaliti waislam kwa kujiingiza kwenye biashara ya kuuza Elimu,
ukiwapigia simu mbona ada mamilioni utasikia kila kitu anapata shuleni huyo mwanafunzi yaani pen na madaftari, hivi karibuni waziri mkuu Mizengo Pinda alifanya ziara mkoani Lindi na akapita Kilwa kwenye hotuba yake alisema kuwa umasikini uliopo kilwa ni mkubwa sana kwani pato la mwaka la mtu wa Kilwa ni shilingi laki moja na nusu,
leo tunafungua miradi ya shule huyo mtoto wa Kilwa atasoma?mji wa Kilwa umekuwa nyuma kwa kukumbatia Uislam,watawala wa mwanzo walishindwa kuuendeleza wakijiua kuwa watakuwa wakiwaendeleza Waislam,sasa leo sisi tunapofanya Elimu Biashara tunawafikiria watu hawa wa Kilwa?
Mtu anaropoka kuwa Shule yetu tunataka watu wa upper class kwani wana uhakika wa kulipa ada,mara tunatengeza shule ambayo itawasaidia waislam wa Upper Class kupeleka watoto wao,
kwenye uislam hakuna aya wala hadithi inayosisitiza kuwa mtu awe concern na watu wa Upper class, tumesisitizwa tuwajali wanyonge,mafakiri,masikini, mayatima n.k huo ndio ubinafsi wenzetu wakiendelea tunatafuta visingizio,
Upper class watapeleka watoto wao Feza, Mzizima,Al Muntazir na hata nje ya nchi,wana njia nyingi za kusomesha watoto wao,Fikirieni wanyonge ndugu zanguni, hata kama biashara ziko za kufanya, sio kwenye Elimu na Matibabu,msi take advantage ya kiu ya elimu kwa jamii kujitajirisha,kwani wewe umepata elimu kwa vile familia yako ilikuwa kwenye upper class?
tukipata elimu basi maendeleo yatapatikana,leo hii daktari mkuu wa Malkia wa Uingereza ni DR.Mohammed ndio mwenye final say ni Elimu ndiyo imemfikisha hapo,wengi wamefanikiwa kupitia elimu huku familia zao zikiwa duni,lakini wakishapata elimu hiyo wanaziba mianya hiyo kwa kizazi kijacho.
AAWW Hatimaye Baraza la Mitihani Tanzania limetangaza matokeo yaliyokuwa yakisubiriwa kwa hamu ya kidato cha nne Nimejaribu kukusanya mawili matatu nikaona ni heri
kama nita share nami yafuatayo 1 KIWANGO CHA UFAULU kwa mwaka 2009 kiwango kimeshuka kwa asilimia 11 ukilinganisha na mwaka 2008 Kama kawaida somo la Hesabu limeendelea kuwa changamoto tete kwa wanafunzi wengi
Zanzibar kama kawa haina hata shule moja katika zile zinazosemwa kuwa shule bora kumi 2.SHULE 10 BORA (Watahiniwa 35 na Zaidi) Marian Girls,(Pwani)St.James Seminary(Kilimanjaro),Don Bosco Seminary(Iringa),St Francis
Girls,(Mbeya)St Mary Junior Seminary(Pwani) Uru Seminary(Kilimanjaro),Feza Boys(Dar es Salaam),Anwarite Girls(Kilimanjaro)Maua Seminary(Kilimanjaro) na St. Mary Goreti (Kilimanjaro).
3.SHULE 10 BORA WATAHINIWA CHINI YA 35 Feza Girls(Dar es Salaam), Mafinga Seminari (Iringa), St. Joseph-Kilocha Seminari(Kilimanjaro) na Queen of Apostles-Ushirombo (Shinyanga).
Seminari ya Dungunyi (Singida), Seminari Rubya(Kagera), Seminari ya Sengerema (Mwanza), Bethelsabs girl (Iringa),Thomas more Machrina (Dar es Salaam) na Hellen’s(Dar es Salaam).
4.MAJINA YA WANAFUNZI BORA WA MWANZO KITAIFA Immaculate Mosha Marian Girls(Pwani), Gwamaka Njobelo Mzumbe(Morogoro),Wolfgang Seiya Majengo (Kilimanjaro)Vanessa Chilunda Marian Girls(Pwani),Faith
Assenga Marian Girls(Pwani)Doreen Philbert Marian Girls(Pwani),Zahra Meghji Usagara(Tanga),John Kimbari St James Seminary(Kilimanjaro),Said Abdallah Feza Boys(Dar es Salaam) na Evans Lwanga Feza
Boys(Dar es Salaam). 5.WAVULANA BORA Gwamaka Njobelo Mzumbe (Morogoro)Wolfgang Seiya Majengo(Kilimanjaro) John Kimbari St James Seminary(Kilimanjaro) Said Abdallah Feza Boys(Dar es
Salaam),Evans Lwanga Feza Boys (Dar es Salaam),Abuubakari Ally Mivumoni Islamic Seminary (Dar es Salaam),Gabriel Aniseth Moshi Technical (Kilimanjaro), Hemed Koplo Feza Boys (Dar es Salaam) Hamidu Mbonde Feza Boys(Dar es Salaam) na
Innocent Nambuo Faraja Seminary(Kilimanjaro). 6.WASICHANA BORA Immaculate Mosha Maria Girls,(Pwani), Vanessa Chilunda Marian (Pwani)Faith Assenga Marian (Pwani), Doreen
Philbert Marian (Pwani), Zahra Meghji Usagara(Tanga), Inviolata Chami Mariani (Pwani) Catherine Ballali St Francis Girls(Mbeya) Patricia Mmbaga Anwarite girls (kilimanjaro), Jovita Byemerwa St Francis girls (Mbeya) na Flora Munuo
Anwarite Girls (Kilimanjaro) 7.KIOJA CHA KARNE Mtahiniwa mmoja kutoka shule ya Kadoto yeye aliamua kushusha matusi mazito katika makaratasi ya majibu 8. TUNAJIFUNZA NINI?
|
|
|
|
|
--
---------------------- “The heart of the matter lies in the sense of justice and fairness” - Liepollo Lebohang Pheko
------------------------------------------------ Asina A. Omari Assistant Lecturer, Faculty of Law,
University of Dar es Salaam. P.O.Box 35093 Dar es Salaam Tel: +255 713 453 639 +255 784 111 009
Help protect the environment, Please don't print this email unless you absolutely need to. Thank you.
|
|
-- ---------------------- “The heart of the matter lies in the sense of justice and fairness” - Liepollo Lebohang Pheko
------------------------------------------------ Asina A. Omari Assistant Lecturer, Faculty of Law, University of Dar es Salaam. P.O.Box 35093 Dar es Salaam Tel: +255 713 453 639 +255 784 111 009
Help protect the environment, Please don't print this email unless you absolutely need to. Thank you.
|