Tafadhali kuweni makini watu wote mnaotumia NBC internet banking, kuna wahuni wamecreate internet banking ya kwao na kuita NBC internet banking, wamenitumia ila nikaishutukia ukizingatia sina A/C NBC.
Walichofanya ni kudisplay page sawa na ya NBC kwenye login page ya Retail User and Corporate User.
Ukiclick link yao hapo chini inakupelekea kwenye web hii http://www.sicornot.com/retail.htm badala ya link halisi ya NBC hii hapa https://direct.nbctz.com/netbanking/RetailLogin.html , sasa kama wewe ni Mzee wa mikurupuko utaingiza detailed zako faster bila kuangalia web address kwenye web bar na ukidhani ni NBC kumbe unawapa hawa jamaa details zako zote na wakufanyie kitu mbaya
Ndugu watanzania wezangu forward hii email kwa watu wote unanao wajua wasije wakaliwa na hawa jamaa.