YAH: KENYA: JAJI MKUU NA MAHAKAMA ZA KADHI

3 views
Skip to first unread message

adam philip

unread,
Oct 9, 2011, 12:51:11 AM10/9/11
to muslims friends
Assalaam aleykum Watukufu Waislamu,
 
Jaji Mkuu wa Kenya, Willy Mutunga, amesema hivi karibuni kuwa ataanza kuteua wanawake kuwa Makadhi katika Mahakama za Kadhi, pamoja na mambo mengine, kwa sababu zifuatazo;-
 
1. Kwamba ni kuleta usawa wa kijinsia katika vyombo vya maamuzi Nchini Kenya
2. Kwamba ni kutekeleza matakwa ya Katiba Mpya ya Kenya inayohimiza usawa wa kijinsia
3. Kwamba hawezi kuacha "mfumo, mazoea na/au utaratibu" fulani unaokandamiza "kundi" fulani katika jamii uendelee kinyume na Katiba 
4. Kwamba Qur'an iko "kimya" katika suala hilo na hivyo haliiathiri imani husika
5. Kwamba ana mamlaka hayo Kikatiba kumteua Mkenya ye yote "mwenye sifa" kushika nafasi yo yote katika vyombo na mfumo wa Makahama kadri anavyoona inafaa
 
Hoja yangu:-
 
1. Je, ni nini msimamo wa Uislamu katika hilo? (Wanawake kuwa Makadhi?)
2. Je, Jaji Mkuu wa Kenya akitekeleza anachosema, tunawashauri nini wenzetu wa Kenya? Au, tunawashauri nini kwa sasa?
2. Je, tunajifunza nini katika harakati zetu (Waislamu) katika kuliendea suala la Mahakama ya Kadhi hapa kwetu?  
 
Tanbihi: Suala husika nililiona likiripotiwa kwenye TV ya Citizen, hivyo basi hicho ndicho chanzo cha habari hii.
 
Wajuzi watujuze, InshaAllah.
 
Allah aalam.
 
Adam Philip
 
Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages