Fw: nasiha

8 views
Skip to first unread message

ZEYANA HAMID

unread,
Oct 5, 2011, 12:43:46 AM10/5/11
to selwa hamid, maryam juma, fattma ali, Mimi, layla hafidh, biubwa ali, the-fund...@googlegroups.com
 

Nasiha hii ni ngumu lakini vizuri kujitahidi.

ASSALAM ALAIKUM WARAHMATULLAHI TAALAH WABARAKATUH

Ni wajibu kwa kila mmoja kumpa mwenzake nasaha njema.Na apewae nasaha ni wajibu wake kukubali bila ya kupinga, kwani kuzifuata ndio muongozo wa maisha yetu.

·        Tuhifadhi ndimi zetu na maneno machafu.

·        Kama hatuna la kusema basi tunyamaze kimya.

·        Neno tulifikirie kabla hatujalitamka mbele za watu.

·        Tujiepushe sana na kusema uwongo.

·        Sema ukweli katika kila jambo lako.

·        Usiseme uwongo hata katika maskhara.

·        Jiepushe sana na vikao vya wasemaji uwongo.

·        Kumbuka kwamba kusema kweli ni kinga hata mbele ya adui  yako.

·        Ikumbukeni adhabu kali ya wasemaji uwongo.

·        Epukana sana na maneno yatakayo kukaribishia na kitendo cha zinaa.

·        Mtaje Mwenyezi Mungu unapohisi fitina itakuzonga.

·        Tumia ulimi wako sana katika kumuomba Mwenyezi Mungu kwa  dua za kila aina.

·        Wacha kuwasema watu kwa ubaya.

·        Epukana na vikao vinavyowasema watu na vichekesho visivyo na maana.

·        Epukana sana kuyachukuwa maneno ya huyu kuyapeleka kwa yule kwa kusudi ya
         kuwagombanisha na wala usifuate siri za watu zisizokuhusu.
 
·        Wacha kuuliza sana mambo yasiyokuhusu.

·        Usijibu suala kama hulijui jawabu.

·        Usibahatishe kujibu katika sheria za ALLAH kama hujuwi hukumu yake.

·        Usione aibu kusema hujuwi utakapoulizwa.

·        Epukana sana na kuwafanyia watu maskhara.

·        Wacha kuwacheka watu waliokuwa vilema.

·        Usiwafanyie mzaha waumini.

·        Waheshimu Mashekhe na watu wote kwa jumla.

·        Jiheshimu utahishimiwa.

·        Kuwa na subira utakapochekwa na wengine.

·        Usichoke kutowa nasaha njema kwa kila aliyepotea katika njia iliyo sahihi.

·        Utumie ulimi wako kwa njia yenye kheri ili kupata malipo mema Duniani na Akhera.

·        Kila muislamu amuombee  muislamu mwenzanke dua nzuri ili tuoneshe mapenzi baina yetu.

Hizi ni nasaha ambazo Muislamu huweza kumpa ndugu yake.Ndugu zangu waislamu musichoke kutowa nasaha njema, kwani huwenda neno moja likaleta athari na faida kubwa katika sikio la msikilizaji na akanufaika na nasaha hiyo. Kila mmoja wetu awe ni mfano mzuri kwa ndugu yake, tuwache maradhi mabaya ya kuchukiana na kusemana na kuoneana choyo.

TAFADHALI MPELEKEE MUISLAMU MWENZIO


_______________________________________________
Zanzinet mailing list
Zanz...@zanzinet.net
http://zanzinet.net/mailman/listinfo/zanzinet_zanzinet.net



Get easy photo sharing with Windows Live™ Photos. Drag n’ drop

Win John Lewis vouchers with BigSnapSearch.com Search now
_______________________________________________ Zanzinet mailing list Zanz...@zanzinet.net http://zanzinet.net/mailman/listinfo/zanzinet_zanzinet.net

_______________________________________________ Zanzinet mailing list Zanz...@zanzinet.net http://zanzinet.net/mailman/listinfo/zanzinet_zanzinet.net

_______________________________________________ Zanzinet mailing list Zanz...@zanzinet.net http://zanzinet.net/mailman/listinfo/zanzinet_zanzinet.net


ATT00000

Mohammed

unread,
Oct 9, 2011, 12:16:48 AM10/9/11
to the-fund...@googlegroups.com
Ahsante Mamkwe.

Nimechelewa lkn nimeupatia "utulivu mzuri" wa kusoma hizi nasaha.

Allah Akubarik.

Sent from my BlackBerry® wireless device


From: ZEYANA HAMID <zeya...@yahoo.com>
Date: Tue, 4 Oct 2011 21:43:46 -0700 (PDT)
Subject: [The Fundametals:561] Fw: nasiha

--
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "the fundamentals" group.
To post to this group, send email to the-fund...@googlegroups.com.
To unsubscribe from this group, send email to the-fundamenta...@googlegroups.com.
For more options, visit this group at http://groups.google.com/group/the-fundamentals?hl=en.
Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages