Na kakirungu kangu

1 view
Skip to first unread message

Masoud Mahundi

unread,
Jun 17, 2011, 9:17:29 AM6/17/11
to Fundamental Group
Dada Zeyana karibu nyumbani. Nimeripoti kidogo kwako kuhusu nyumbani kuna hili niliona ni bora nikwambie kupitia hii fforum.
JAMBO JINGINE dada ni kupatwa kwa Mwezi, nadhani ulilishuhudia ukiwa Tanzania, au ulikuwa angani? Mwezi ukapatwa, alhamdulillah mtaani kwetu saa nne kasoro ile adhana zikarindima mtindo mmoja. Nami nikatoka na kakirungu kangu mkononi nikaelekea msikitini. Hata hivyo niliambiwa, baadae, kwamba wapo katika manasara waliodhani eti uislamu sio scientific kwa kuhangaika kuomba madua kwa tukio la kawaida kabisa kisayansi. Ila wapo pia waliosema 'duh hawajamaa kwa kila tukio wana ibada yake, wapo kamili sana'. Ingawa hao wa kwanza nao walishawishika kudhani hivyo kutokana na majibu ya baadhi ya waislamu 'tunauombea mwezi uachiwe na juwa', majibu ya mfano huu. Basin a kakirungu kwangu nikaenda Msikitini. Kufika pale nikashukuru kuona waislamu wapo kawaida tu, siyo hali ya woga, nikajuwa kumbe tunajuwa kwamba ni ibada tu.
Haya ikafika muda wa Swala, pakaqimiwa tukasimama. Sikutanii dada, kama dakika tatu tu baada ya kuanza sala tukasikia SubhanaLlah, kwamba imamu ameteleza kidogo. Akina siye roho nip ah.. pah …. Pah. Unajuwa tena ujinga una gharama kubwa sana. Huweza hata kugharimu thawabu zako. Tukachanganyikiwa zaidi tulipogunduwa kwamba imamu amesikia, anajuwa ameteleza, ila hajui usahihi ni upi. Akaenda rakaa mbili za kawaida tu kama Qabliya. Alipomaliza “kigogo” Mmoja akajitolea kutoa ufafanuzi. Ikaamuliwa ile sala irudiwe. Akina siye mumo humo tena. Niko safu ya mbele kabisa (labda sababu ya kanzu yangu kubwa?). Tukaisali ile sala dada kwa usahihi wake - lau kwa maneno ya kigogo yule. Nikasema nikipata nafasi ntamuomba shekhe Tawak-kal atudadavulie na hili, kama atakuwa na wasaa. Tujuwe asili, sababu na namna ya ibada hii. Haya tukamaliza pale, pakasomwa na khotuba then dua’h. Ghafla yakaanza kusemwa maneno hayo sintoyasema hapa. Kuhusu kupatwa ka mwezi. Nikashindwa kujizuwiya. Nikasema hata kama nilijifunza mwaka 1995-98, naamini bado nayakumbuka tu. Nikaomba kachaki na kale ka ubao ka wanachuo nikapewa. Nilitowa hadhari lakini kuwa nikikosea nisimamishwe nukta hiyo hiyo, si mpaka nimalize. Basi nikaanza kuto vimichoro pale na jinsi kupatwa kwa mwezi kunavyottokea, nikaongeza pia na kutokea kwa kupata kwa Jua, Alhamdulillah, nadhani kuna walionielewa.
Ni hayo tu dada. Karibu Tanzania
Wabillahi tAWFIQ
Zingatia: Funga na funguwa semi kwenye email hii hazimaanishi kunukuu
 
Without Wax

Masoud H. Mahundi
Department of Computer Science
University of Dar es Salaam
P.O Box 35062
Tel 255 22 410500 - 8 (or through ext 2466)
Mobile: +255 71 3832252
DUP Building - First Floor, Room No 206
Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages