Assalaam alykum
bila shaka hizi ni habari njema. Allah mjaalie upole na utii kama Nabii Ismail, Ushujaa kama Sayyidna Omar... awe mja wa kheri wa kuwafaa wazazi wake na jamii ya kiislam kwa ujumla.
|
From: ZEYANA HAMID <zeya...@yahoo.com> |
Assalaam Alaykum
Jamani hii group mail ilipoanzishwa mi sikuwa na habari. Naona wachache tu wanaoandika au ndio washiriki wote hawa: Sheikh Mahuni, Dada Zeyana na Sheik Tawakal.
Nipeni chimbuko la group hii nami niipe kipaumbele
Ali Jabir Mwadini
Addis
|
From: Masoud Mahundi <mmahu...@yahoo.com> |
Waaleykumus-salaam brother Ali Jabir
Swali lako nimelipenda sana kwani limeonesha umakini ulionao kwenye kufuatilia mambo
Kuliwahi kuwa na mijadala tu ya mambo mbali mbali ulioshirikisha baadhi ya member wa group hili ambayo kwa kiasi fulani iliwakutanisha watu tena lau ki-fikra.
Haya mambo yalipoanza kuwavuta watu kiufahamu na kihisia, pakaonekana ni vema kuanzisha discussion group, ambayo itahusisha na wengine pia, ili kupata kusikika kile ambacho muislamu angependa wenzake wakisikie. Ni kama kusema muislamu anapata e-audience.
Ingawa hii inakwenda zaidi pale ambapo kunakuwa na maswali na wengine kuchangia. Si lazima msemaji ndio ajibu ila yeyote mwenye uelewa anaweza kujibu
Kundi hili likaitwa “The Fundamentals”
Mpaka sasa mada zilizowahi kujadiliwa ni pamoja na;
Umuhimu wa isti'adha
Ni nani Ahmadiya, na wapi wanapotoa watu
Qul-latayn ni nini
Uhalali wa kuoa watu wa kitabu (ni sahihi kwa sasa, ni akina nani hao ahlulkitaab kwa mazingira yetu, nchi zetu je)
Majukumu ya vijana wa kiislamu (hata pakataka kutolewa azimio la mwaka huu)
Na mengine wenzangu wanaweza kukumbushia
Memba wa kundi hili ni wengi kiasi fulani, na kila mmoja kati yao ana nafasi sawa, na hadhi sawa mbele ya memba wengine. Kuchangia, kuuliza, na kusema mtu aonacho ni vizuri wenzake waislamu wakijue.
Ni kweli kwamba Sheykh Tawak-kal, Bi Zeyana, DOC Mohammed, Sheykh Kisilwa, Maalim Mdoe, Sheykh Ijumaa na mimi ndio inaonekana tumeshiriki sana, lakini nafasi ziko wazi kwa yeyote kushiriki.
Mpaka sasa kundi hili lina memba 46 ambao wote ni watumiaji wazuri wa kiswahili na kiingereza kwenye kuwasiliana (Nadhani kifaransa ni wachache kidogo)
Baada ya kusema hayo naomba nikukaribishe kwenye 'jukwaa'
Karibu sana
MM
CONGRATULATIONS SISTER. MAY ALLAH RAISE HIM TO BE THE MOST RESPONSIBLE PERSON IN HIS RELIGIOUS LIFE.
From: the-fund...@googlegroups.com [mailto:the-fund...@googlegroups.com] On Behalf Of ZEYANA HAMID
Sent: Monday, March 23, 2009 4:34
PM
To: the-fund...@googlegroups.com
Subject: [The Fundametals:104] New
Arrival
I am writing to announce the birth of my second born Abdallah R.M Ramia he is one week old now and is doing quite fine Alhamdulillah.
| ZEYABA, Allah Akukuzikie mwanao, awe msikivu na mtiifu kwa Mola wake na dini yake bila kusahau wazazi wake. |
|
| Nashukuru sana Sheikh Mahundi kwa maelezo yako mwanana. Bila shaka umetumia muda kuandika yote na hiyo ni ishara ya kujali kwako. Nakuhakikishia na kuwahakikishia wengine kwamba nani nimejali. Wengi uliowataja sina hakika kwamba nawajua kwa sura. Ingefaa siku moja karibuni tukakutana mahali fulani kama watu hawa wapo Dar tukabadilishana mawazo. Jambo hilo huenda litaongeza ari ya watu kuchangia katika hili Jukwaa. Kwa sasa nipo Addis hadi tarehe 27 inshaallah. Mambo mengine nitasema katika mail zijazo. Kifaransa kinyamazie tu. Vyema tutumie kiswahili. Asante Ali Jabir ADDIS |
ULIYOKUWA HUYAFAHAMU KATIKA GHAQIQAH AFANYIWAYO MTOTO MCHANGA
Ghaqiqah ni mnyama ambaye huchinjwa kwa ajili ya mtoto mdogo kama tulivyotangulia kusema. Jambo hili ni katika mlango wa kumshukuru Allah. Kuna pia vyakula vingine ambavyo ni katika mlango huu wa kumshukuru Allah na vinafaa kuliwa kisheria navyo ni;
1. Walima chakula au karamu ya harusi
2. Qiraa chakula cha mgeni, kile cha mgeni njoo wenyeji tupone!
3. Maadaba ambacho ni chakula cha mwaliko
4. Tuhfa ambacho ni chakula cha mwenye kutembelea pahala
5. Khiraasu ambacho ni chakula cha kujifungua
6. Ghadiira ambacho ni chakula cha wakati wa khitaani au kutahiri wanawake au wanaume
7. Naqiigha ambacho ni chakula cha anayekuja kutoka safari
8. Wakiira ambacho ni chakula baada ya kumaliza kujenga
Isipokuwa chakula cha msibani au cha siku ya tatu au cha khitima au arobaini vyakula nilivyotaja hapo juu vinafaa kuliwa Kisheria. Jariri Ibn Abdillah anasema kuwa kukusanyika kwa wafiwa na kupikiwa chakula ni miongoni mwa mambo aliyokataza Mtume wetu Mtukufu.
Wabillah Tawfiiq
Imeandikwa na ndugu yako katika uislamu;
Tawaqal Juma Hussein
Chuo Kikuu cha Waislamu
P.O Box 1031
Morogoro
Tanzania
A'ALAYKUM WARAHMATULLAH WABARAKAATUH
Nashkuru sana, asante tutakaribia ktk uwanja |
Asante sana Sheikh wangu
Inshallah tutaonana |
|
Assalaam Alaykum
Jamani kijana wetu amepotea tangu Ijumaa tarehe 27 Machi 2009.
Jina lake Khamis Haji Khamis,
Alitoweka Ijumaa saa nne na nusu eneo la Maji Matitu, Mbagala.
Alionekana Ijumaa hiyo maeneo ya Nzasa, Charambe. Alikuwa anaongea maneno yasiyoeleweka hivyo hakujieleza. Anaonekana kurukwa na akili. Katika hali ya kawaida anaweza kujieleza.
Alivaa t-shirt ya light blue, bila shaka kama bado anayo imechafuka sana. Suruali ya kijivu, ameikaba sana tumboni, anasumbuliwa na vidonda vya tumbo. Mara nyingi anatapika na kujisongasonga. Mwembamba sana, rangi yake maji ya kunde, nywele nyeusi, umri miaka 13 hivi.
Tunaomba msaada katika kufikisha taarifa hizi kwa watu wengine. Yeyote atakaepata taarifa zake tunaomba awasiliane nasi kwa simu zifuatazo:
1. 0773 308863
2. 0777 874484
3. 0732 992616
4. 0777 996929
5. 0773 500238
6. 0784 874485
7. 0773 848014
Tunatanguliza shukurani
|
‘Aqiyqah Afanyiwayo Mtoto Mchanga
Tawakkal Juma Husayn
1. ‘Aqiyqah ni jina lililopewa kichinjwa (mnyama) achinjiwacho mtoto mchanga aliyezaliwa ni mamoja awe ni wa kike au wakiume.
2. Ni Sunnah si waajibu. Ushahidi wa hili ni uko katika maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliposema: "Atakayepata mtoto na akapenda amchinjie basi na afanye hivyo; kwa mwanamume mbuzi wawili na kwa mwanamke mbuzi mmoja". Hadiyth hii imepokewa na Maimaam Abuu Daawuud na An-Nasaaiy kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu). Kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “na akapenda amchinjie” ni dalili kuwa ‘Aqiyqah si lazima bali ni jambo linalopendeza Muislamu kulifanya. Lakini kwa mwenye uwezo wa kufanya hivyo basi iliyo bora zaidi kwake ni kufanya ama yule asiye na uwezo wa kufanya hivyo, basi si lazima kwake maana Mwenyeezi Mungu Haikalifishi nafsi yoyote ila yale yaliyo sawa na uwezo wake na pia Hakufanya uzito katika dini.
3. Imethibiti kutoka kwa Mtume wa Allah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa yeye kasema: “Kila mtoto azaliwaye anafungamana na ‘Aqiyqah yake, anachinjiwa siku ya saba, ananyolewa kichwa chake na anapewa jina.” Wanachuoni wamelizungumzia neno ‘kufungamana’ hapa kuwa linaweza kuwa linamaanisha mambo mengi, miongoni mwa mambo hayo ni:
4. Iliyo bora zaidi na timilifu ni kuwa wale mbuzi wawili au kondoo wawili ambao anatakiwa mtoto wa kiume achinjiwe wanatakiwa wawe ni wenye kufanana au kukaribiana kufanana kimaumbile na kiumri. Lakini kama itashindikana kuwapata mbuzi wawili wenye sifa kama hizo itafaa hata kama watatofautiana kiumbile na kiumri maadamu tu wana sifa zinazofaa kisheria kwa ajili ya ibada hii. Sifa hizo tutazitaja baadaye.
5. Iliyo bora zaidi na timilifu ni kumchinjia mtoto wa kiume mbuzi wawili lakini ikiwa mtu atashindwa kabisa kuchinja mbuzi kama kutokana na yeye kupata mbuzi mmoja tu au kumiliki kiwango cha mbuzi mmoja tu basi huyo huyo mbuzi mmoja atatosha.
6. Sunnah ni kumchinjia mtoto atakapofikisha siku ya saba kama ilivyokuja katika Hadiyth ya Samrah, lakini ikiwa mtu hakuweza kuchinja siku ya saba basi na afanye hivyo siku yoyote atakayojaaliwa.
7. Ibada hii ya kuchinja hufanyika hata kama mtoto kafariki maadamu tu alizaliwa hai au hata kama mimba ilitoka lakini mtoto tayari alikuwa ameviviwa roho, yaani alikuwa amefikisha miezi minne au siku mia na ishirini na kuendelea lakini kama alikuwa hajafikisha miezi minne au siku mia na ishirini hapo hatofanyiwa ‘Aqiyqah.
8. Kuna imani imeenea kwa watu wengi kuwa kichinjwa cha ‘Aqiyqah hakivunjwi mifupa hii ikiwa kama ishara ya kumtakia mtoto salama na asivunjike maishani mwake. Hili si sahihi wala halina mashiko katika Qur-aan wala Sunnah. Kwa hiyo ieleweke wazi kuwa mifupa ya ‘Aqiyqah inafaa kuvunjwa wala hii haitokuwa sababu ya kuvunjika kwa mtoto hata kama itatokea kama watu wanavyoamini. Vile vile kuna jambo jingine nalo ni kuwa nyama ya ‘Aqiyqah huchanganywa au hupikwa kwa maji yaliyotiwa vitu vitamu vitamu kama sukari au huchanganywa na asali wakati wa kuliwa, hii ikiwa ni kama ishara ya kumtakia mtoto tabia njema; hili nalo pia halina mashiko. Hivyo iwekwe chumvi na kupikwa kama nyama ya kawaida
9. Kinachotakiwa kuchinjwa katika ‘Aqiyqah katika wanyama ambao kishari’ah wanaitwa Bahiymatul An’aam ambao ni; mbuzi, kondoo, ng’ombe na ngamia. Kwa mantiki hii haifai kumchinja farasi kwa ajili hii, wala swala hata kama anafugwa na amekuwa kama mbuzi kitabia na pia haifai kuchinja kuku wala bata kwa ajili ya ibada hii
10. Ama kuhusiana na umri unaofaa wa kichinjwa ni miaka mitano kwa ngamia na miaka miwili kwa ng’ombe, dume la mbuzi na dume la kondoo ni mwaka mmoja na mbuzi jike na kondoo jike ni miezi sita
11. Ni sharti katika kichinjwa cha ‘Aqiyqah kiwe kimesalimika na aibu mbalimbali kwa kifupi kabisa kichinjwa hichi kinafanana na kichinjwa cha ‘Iydul Adhwhaa au Idi kubwa yaani kisiwe na chongo cha wazi, kiguru cha wazi, kilichokonda sana, wala kisiwe ambacho kimetobolewa masikio yake wala kisiwe kilichokatwa mkia au kukatika pembe.
12. Ikiwa mtu anamiliki takribani wanyama wote wanaofaa kuchinja kwa ajili ya ‘Aqiyqah kiasi kuwa anaweza akitaka akachinja ng’ombe au ngamia au kondoo au mbuzi, iliyo bora zaidi ni kuchinja mbuzi maana ndiye aliyetajwa katika Hadiyth.
13. Inafaa mtu kuipika nyama ya ‘Aqiyqah au kuigawa pasina kuipika lakini iliyo bora zaidi ni kuipika nyama ya ‘Aqiyqah kuliko kuigawa kwa kuwa kwa kufanya hivyo utawarahisishia masikini na majirani gharama za kupika.
14. Hakuna ubaya wowote katika kula nyama ya ‘Aqiyqah kwa aliyechinja, kwani kwa hakika hii ni nyama kwa ajili ya kumshukuru Allaah na kile ambacho ni kwa ajili ya kumshukuru Allaah kinafaa kuliwa kishari’ah wala hapana ubaya bali hii ni kama nyama ya ‘Iydul Adhwhaa.
15. Pia inafaa kuiweka nyama ya ‘Aqiyqah katika jokofu pasina kuigawa lakini iliyo bora zaidi na timilifu katika ibada hii ni kuigawa kwa mafaqiri na marafiki hata kama ni kidogo.
16. Haifai kununua mbuzi aliyechinjwa na kumfanya kuwa ni ‘Aqiyqah bali ni lazima kumununua mbuzi mzima na kisha kumchinja kwa nia ya ‘Aqiyqah
17. Ikiwa baba hayuko, kama kwa mfano kafariki, mama atasimamia jukumu la kufanya ‘Aqiyqah.
18. ‘Aqiyqah ni Sunnah kwa baba kumfanyia mtoto wake lakini mtoto hakufanyiwa ‘Aqiyqah na akapenda ajifanyie mwenyewe inafaa hata kama ni ni kitambo kirefu kimepita na umri ukawa mkubwa.
19. Inafaa kumchinjia mtoto wa kiume mbuzi hao wawili kwa utaratibu wa kugawa kwa maana ya kuwa anamchinja mbuzi mmoja mwezi huu na mwengine akamchinja mwezi mwingine wala haishurutishwi wachinjwe mara moja, bali inafaa kwa mtoto akajichinjia mbuzi mwingine ikiwa baba alimchinjia mbuzi mmoja kwa sababu ya hali yake kifedha. Bali inafaa kumchinjia mbuzi mmoja sehemu moja na mwengine sehemu nyingine wala si sharti wachinjwe wote sehemu moja wala si sharti wachinjwe sehemu alipo mtoto anayefanyiwa.
20. Haifai kisheria kupigia thamani ya mbuzi wa ‘Aqiyqah na kuwapa kiwango hicho masikini bali ni lazima achinjwe mbuzi
21. Haifai kushirikiana watoto katika ‘Aqiyqah kwa mantiki ya kuwa wachangie kwa mfano mbuzi wawili watoto wawili wa kiume. Watoto wawili wa kiume wanapaswa wachinjiwe mbuzi wanne hata kama ni mapacha. Kama ni mapacha wawili wa kike watachinjiwa mbuzi wawili, kama mmoja ni wa kike na mwengine ni wa kiume watachinjiwa mbuzi watatu. Bali ngamia na ukubwa wake hafai kuwachinjia watoto wawili na ikifanyika hivyo inazingatiwa ni kwa ajili ya mtoto mmoja. Bali haitofaa kwa watoto wawili ambao hawakufanyiwa ‘Aqiyqah kwa wao kujiamulia kuchinja ngamia mmoja ili awe ni ‘Aqiyqah kwa wote wawili. Bali ngamia huyo atazingatiwa kuwa ni kwa ajili ya mtoto mmoja tu.
22. Si lazima wakati wa kumchinja mnyama wa ‘Aqiyqah kusema kuwa hii ni ‘Aqiyqah bali inatosha mtu kunuia moyoni mwake na kilicho lazima kutamka ni BismiLlaahir Rahmaanir Rahiym.
23. Si lazima kuwaambia waliohudhuria kuwa watakula nyama ya ‘Aqiyqah, lakini ni vizuri kuwaambia ili wamuombee mtoto du’aa njema, uongofu, uchaji, kutengenekewa na kheri za dunia na Akhera.
‘Aqiyqah ni mnyama ambaye huchinjwa kwa ajili ya mtoto mdogo kama tulivyotangulia kusema. Jambo hili ni katika mlango wa kumshukuru Allaah. Kuna pia vyakula vingine ambavyo ni katika mlango huu wa kumshukuru Allaah na vinafaa kuliwa kishari’ah navyo ni:
a. Waliymah: chakula au karamu ya harusi.
b. Qiraa: chakula cha mgeni, kile cha mgeni njoo wenyeji tupone!
c. Ma-adabah: ambacho ni chakula cha mwaliko.
d. Tuhfah: ambacho ni chakula cha mwenye kutembelea pahala.
e. Khiraasu: ambacho ni chakula cha kujifungua.
f. Ghadiyrah: ambacho ni chakula cha wakati wa khitaani au kutahiri wanawake au wanaume
g. Naqiy’ah: ambacho ni chakula cha anayekuja kutoka safari.
h. Wakiyrah: ambacho ni chakula baada ya kumaliza kujenga.
Isipokuwa chakula cha msibani au cha siku ya tatu au cha Khitmah au arobaini. Vyakula nilivyotaja hapo juu vinafaa kuliwa Kishari’ah. Jariyr bin ‘Abdillaah anasema kuwa kukusanyika kwa wafiwa na kupikiwa chakula ni miongoni mwa mambo aliyokataza Mtume wetu Mtukufu.
WabiLlaahit Tawfiyq
ASSALAAM ALAYKUM.
Kaka Tawakkal, naomba nianze kwa kukushukuru kwa kuutumia muda wako mwingi kutufahamisha mambo mbalimbali katika dini yetu tukufu. nakiri wazi kwa wana undamentali wote ya kwamba pamoja na kwamba sula hili lizungumziwalo hapa linaonekana la kawaida masikioni mwangu na mwa wengi, sikuwa nalifahamu kiundani hivi kabla ya kunijuza haya. waalimu wangu masheikh doctor ijumaa na mahundi hawakunifunza haya kabla, ikiwa kama adhabu kwa kuwa sikutokea darasani siku hiyo ya somo hili. hivyo hapa nafaidika sana.
Baada ya utangulizi huu naomba unisaidie kidogo juu ya kifungu namba saba cha somo lako kama kinavyoonekana na kusomeka hapa chini katika maandishi ya rangi nyekundu
“7. Ibadan hii ya kuchinja hufanyika hata kama mtoto kafariki maadamu tu alizaliwa hai au hata kama mimba ilitoka lakini mtoto tayari alikuwa ameviviwa roho, yaani alikuwa amefikisha miezi minne au siku mia na ishirini na kuendelea lakini kama alikuwa hajafikisha miezi minne au siku mia na ishirini hapo hatofanyiwa ‘Aqiyqah’”
SEHEMU NIIITAKIAYO MAELEZO NI JUU YA KUTAMBUA NI MBUZI WANGAPI WA KUCHINJIWA MTOTO AMBAYE BADO NI MIMBA MAANA UTAMBUZI WA PENGINE NI WA JINSIA YA KIKE AU YA KIUME UNAKUWA MGUMU. AU KUNA IDADI MAALUMU YA VIUMBE MIMBA HIVI AMBAVYO NI TOFAUTI NA IDADI INAYOTAMBULIKA KWA WATOTO WALIOZALIWA HAI?
TAFADHALI NISAIDIE JUU YA HILI ILI KIU YANGU YA KUKAMILISHA UELEWA SAHIHI USO SHAKA JUU YA SOMO HILI UKAMILIKE UKINIACHA NIKIWA NA FURAHA JUU YA NILICHOJIFUNZA. NATANGULIZA SHUKRANI ZANGU KWA MARA NYINGINE.
KISILWA, ZAHARANI
INSTITUTE OF ACCOUNTANCY ARUSHA
NJIRO HILL, ARUSHA
MOBILE: +255 715 000 635