Hope you are all good and continuing with everyday duties. today I am here asking on the legitimacy and if it right or wrong and perhaps kupata mafundisho ya mtume in times like this together with the recent happenings. hope to get different opinions and a good discussion
1. mbagala crisis that was caused by two kids and resulted in the riots and as they say kuchomwa na kuharibiwa makanisa,
katika hili, mimi sina hadithi kamili kwa sababu hamna hadithi mbili nilizosikia zinafanana. ila tunachojua ni kua kuna mtoto aliukosea heshima msahafu na kuukojolea. wote tunakubaliana hili ni kosa, ila kilichotokea baada ya hapo ni sahihi? katika pande zote, yaani polisi kwa hatua walizochukua, wandamanaji na wazazi, na nini ilikua ni mafundisho ya mtume (yaani ingekua enzi za Mtume S.A.W) ni nini angefanya. na je hii nikuonesha kua waislam tumeumizwa sana na kitendo hichi, au kuna other social/ economic problems ambazo sasa tunaziona zikitoka, na kama hii ndio sababu ni sahihi kutumia dini kwa mtu kuonyesha kama amechoka na hali ya maisha?
2. Kukamatwa kwa Sheikh Ponda na madai yote wanayomtuhumu.
hili kwa mimi linautata mkubwa kwa sababu sina ushahidi wowote, ila ninachojua in a fragile times kama hizi serikali/ vyombo vya usalama should now better how handle mambo kama haya. lakini pia kwa upande mwengine nimesikia kupangwa kwa maandamano, ambayo bila shaka yataelekea kuleta vurugu kati ya polisi na waandamanaji, na mwenyezi mungu apishe mbali watu kumizwa na hata kufa. lakini mpaka sasa sijasikia kama kuna any negotiations kati ya viongozi wa dini na vyombo vya usalama, wala sijasikia viongozi wa dini kutoa muongozo kwa waumini. je Kipindi cha Mtume nini kulifanyika, busara gani zilitumika, na je katika nyakati hizi, tunajitahidi kutumia hizi busara kusuluhisha mambo na kuupeleka mbele uislam? Je tumejaribu njia zote zimeshindikana tumeona hii ndio inafaa?
3. Zanzibar na Kundi la Uamsho.
knoledge yangu kuhusu Uamsho, ni kikundi ambacho kilikua kimejizatiti katika kutoa elimu ya dini, lakini kinavyokua pictured siku hizi ni kama kikundi cha kutafuta utengano wa znz na bara, kama focus ni kua bara inanyonya visiwa, which is political, je tumeangalia the part ya kua waislam pia tunakua tumetengwa? basi hata kama ni hivyo basi tujaribu kudai haki na kuvunja muungano bila kuharibu tasia za dini, kwa sababu tutakua tunapigana vita tusivyojua, na tunatakua tunatua sera ambazo tunazipinga kwa kusema yule alikutwa katikati ya mapigano anakua victim of the circumstances.
4. mimi nadhani kama Jamii ya Kiislam, tumefundishwa mengi sana na Mtume wetu S.A.W. kwa kuonyesha kama tunampenda ni vizuri tukamuenzi kwa kufuata mafundisho yake, kama tunavyosema ISLAM is a way of life, hamna kichosahaulika. tujaribu kutumia nguvu zetu vizuri,
5. bila kusahau, kuna kesi nyingi za bakwata kuuza viwanja, kuna uhalali kwenye hili? and kama upo kwenye katiba/ mwongozo wa bakwata wamefuata matakwa ya wanaowaongoza? and kama wa katiba why not ammending na iwe stated bakwata hawana haki ya kuuza mali? mimi nadhani hii ikitokea mali nyingi zitakua zimelindwa.
people, haya ni maoni yangu, nadhani sasa hivi tumekua tunawapa kipaumbele wengi walio kwenye siasa na mashekh wetu kuliko kutoa kipaumbele kwa mafundisho tuliorisishwa na Mtume S.A.W ili kuwemza kumcha Allah.
more comments and maelimisho tafadhali wadau ili tuweze kupeana mwanga.
wasalaam.
--
Yusuph Kassim Kulindwa,
University of Dar Es Salaam,
College of Information and Communication Technology (CoICT),