SWALI:
Assalam allaykum warahmatullahi
Kwanza napenda kuwapongeza wote wanaoshiriki katika kazi hii ya kuelimisha umma wa kiislam hasa kwa sisi ambao tuko kwenye nchi hizi za kimagharibi . Ahsanteni sana na allah atawajaza majazo mema leo duniani na kesho akhera. Suali langu ni hili tokea kukaribia kumi la mwisho la mwezi huu mtukufu wa ramadhan nimekuwa napokea email kutoka watu mbali mbali zinazoelezea kuhusu sala ya laylatul Qadri ambayo husaliwa kwa rakaa zaidi ya kumi na moja pamoja sura zake maalum kwa kila siku (yaani kila siku na sura zake maalum) kwa mfano kuna siku usome sura zinazoanza na haa mim na nyenginezo pia ikiwemo salatul tasbihi. hivyo naomba nasaha zenu watu wa alhidaaya kwani tumo ndani utata mkubwa waislam. Assalam alaykum warahmatullhi
Barua yenyewe ni hii:
ASSALAM ALAYKUM,
NDUGU ZANGU WAISLAM NAWAOMBA TUFANYE BIDII NA JITIHADA NA KUHAKIKISHA
KILA MMOJA WETU ANATEKELEZA SALA HII PINDI HALI IKIMRUHUSU, INSHAALLAH.
JIBU:
Sifa zote njema anastahiki Allah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Hakika ndugu Waislamu, kutokana na utamaduni wa mawasiliano siku hizi kwa kupatikana njia nyingi za kutuma ujumbe kupitia barua pepe (e-mail) au katika simu za mkono (text messages) n.k, uzushi mwingi umekuwa unarushwa na kuwafikia Waislamu wengi ambao nao bila ya kujua wanapata mafunzo yasiyo sahihi, nao wanawatumia wenzao, hivyo hivyo inaendelea hadi kuwafikia maelfu wa Waislamu.
Yafutayo ni maelezo tunayowatahadhirsha ndugu zetu wote kuhusu ujumbe huu:
Tunatoa nasaha kwa ndugu zetu katika Iymaan musiwe na haraka ya kueneza mambo ambayo yanadhaniwa ni Hadiyth au mafunzo ya Dini na hali ni utungo tu kutoka kwa wasio na kazi ila kuwashughulisha watu na kuwapotezea muda wao kwa mambo ambayo hayawezi kuwapatia ujira bali watarudishiwa wao na kutopata kitu zaidi ya kupoteza muda. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kapinga hilo sana na kalikemea vikali pale aliposema:
(Mwenye Kuzusha jambo katika DINI yetu hii, basi litarejeshwa kwake) [Al-Bukhaariy na Muslim]. Yaani hatopata kitu zaidi ya kuua muda wake na kujichosha bure!
Tujihadhari na barua nyingi tuzipatazo kwenye internet kwani nyingi huwa ni mambo ya uongo na kutungwa na pia kusingiziwa nayo Dini na Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye ametuonya kwa maonyo makali kama haya:
((ï؟½ï؟½ ï؟½ï؟½ï؟½ ï؟½ï؟½ï؟½ ï؟½ï؟½ï؟½ï؟½ï؟½ï؟½ ï؟½ï؟½ï؟½ï؟½ï؟½ï؟½ï؟½ ï؟½ï؟½ï؟½ï؟½ï؟½ ï؟½ï؟½ ï؟½ï؟½ï؟½ï؟½ï؟½)) ï؟½ï؟½ï؟½ï؟½ ï؟½ï؟½ï؟½ï؟½
((Atakayeniongopea makusudi basi ajitayarishie makazi yake motoni)) [Al-Bukhaariy Na Muslim]
Tunawaomba ndugu zetu msome makala MUHIMU zifuatazo ambazo zina maelezo mengi kuhusu hatari ya kusambaza uzushi, ili kila mmoja wetu ajiepushe na uovu huo:
Bonyeza hapa:
Waislam Tuache Kumzulia Mtume (Swalla Allaahu ï؟½Alayhi Wa ï؟½Aalihi Wa Sallam) Uongo
Hatari Ya Kueneza Hadiyth Dhaifu Na Visa Vya Uongo
Mwenye Kufanya Na Kuelimisha Sunnah Nzuri Katika Uislam Na Mwenye Kuelimisha Uzushi
Tambueni kuwa ujumbe wowote unaoonekana wa kidini lakini usio na DALILI ndani yake, kama huu ulivyo, hauna DALILI, USHAHIDI kuliposemwa maneno hayo, nani kasema? Wapi kasema? Nani kapokea, Vitabu gani n.k.!!
Ukitaka kujua ujumbe kama huu una madhara, tujiangalie katika sisi, wangapi washaanza kuuhifadhi kati yetu, au wangapi washaanza kuusoma na kuufanyia kazi, na bila shaka wengi leo hii na kuendelea washaanza kuziswali Swalah hizo na kuacha kuswali Swalah za Qiyaamul-Layl kama zilivyofundishwa, au kusoma Qur-aan na mengine mengi YENYE USHAHIDI kama tunavyoona kwenye MAKALA hizi ninazowawekea hapa chini kuhusu LAYLATUL-QADR na QIYAAMUL-LAYL na mambo ya kufanywa katika masiku kumi haya mwisho.
Bonyeza hapa:
LAYLATUL-QADR - VIPI TUNAWEZA KUUPATA USIKU HUU MTUKUFU
SIKU KUMI ZA MWISHO ZA RAMADHAAN
FADHILA ZA QIYAAMUL-LAYL- 1
Tunawaombea sana Allaah Awataqabalie Swawm zenu na matendo yenu, na Awaongoze katika yale ya kheri na yaliyo SAHIHI na Awaruzuku elimu yenye manufaa na iliyo ya sawa inshaAllah. Na sisi tunaomba sana Du'aa kutoka kwenu.
Na Allaah Anajua zaidi