TANGAZO LA NAFASI YA KAZI – ULINZI
Kampuni: Planet Lodges & Lairs
Mahali: Arusha,Serengeti na Tarangire
Mwisho wa Maombi: Jumatano, tarehe 03 Juni 2026
Planet Lodges & Lairs inatangaza nafasi ya kazi ya mlinzi mwenye uzoefu, mwaminifu na uwezo wa kufanya kazi katika mazingira mbalimbali,mjini na porini.
MAJUKUMU YA KAZI:
- Kudhibiti na kufuatilia watu, wageni, wafanyakazi, na magari yanayoingia au kutoka katika eneo la kampuni.
- Kufanya doria mara kwa mara ndani na nje ya eneo la kazi ili kubaini na kuzuia hatari za kiusalama au matukio yasiyo ya kawaida.
- Kulinda mali za kampuni, wageni, wafanyakazi, na vifaa dhidi ya uharibifu au wizi.
- Kuchukua hatua za haraka pale panapotokea dharura, vurugu, au matukio ya kiusalama na kutoa taarifa kwa viongozi husika.
- Kuweka kumbukumbu sahihi za wageni, matukio ya kiusalama, na shughuli za kila siku za ulinzi.
- Kuhakikisha sheria, taratibu, na kanuni za usalama za kampuni zinafuatwa.
- Kukagua milango, kufuli, mageti, na mifumo mingine ya usalama ili kuhakikisha ipo katika hali nzuri.
- Kusaidia kudhibiti utulivu na usalama wakati wa shughuli maalum au matukio yenye mkusanyiko mkubwa wa watu.
- Kuripoti mara moja uharibifu, wizi, au mazingira hatarishi yanayoweza kuhatarisha usalama.
- Kushirikiana na idara nyingine kuhakikisha mazingira ya kazi yanakuwa salama muda wote.
SIFA ZA MWOMBAJI:
- Uzoefu wa kazi ya ulinzi au kazi zinazofanana.
- Uelewa wa msingi kuhusu shughuli za ulinzi na taratibu za usalama.
- Uwezo wa kutambua na kushughulikia changamoto za kiusalama kwa ufanisi.
- Afya njema na uwezo wa kufanya doria au kusimama kwa muda mrefu.
- Uwezo wa kufanya kazi chini ya shinikizo na kubaki mtulivu wakati wa dharura.
- Uwezo mzuri wa mawasiliano na uandishi wa taarifa za msingi.
- Cheti au mafunzo ya masuala ya ulinzi ni faida ya ziada.
UJUZI NA UMAHILI:
- Umakini mkubwa na uwezo wa kuchunguza kwa makini
- Uwezo mzuri wa mawasiliano na mahusiano kazini
- Uwezo wa kufanya kazi chini ya shinikizo
- Uadilifu, uaminifu, na weledi wa kazi
- Nidhamu na uwajibikaji
- Uwezo wa kutatua changamoto na kufanya maamuzi
- Uwezo wa kufanya kazi kwa ushirikiano na timu
- Uwezo mzuri wa kimwili na kuwa makini muda wote
- Usimamizi mzuri wa muda na majukumu
- Uelewa wa taratibu za usalama na ulinzi
JINSI YA KUTUMA MAOMBI:
Maombi yote yawasilishwe getini kwa mlinzi, ofisi za Planet Lodge,Moshono kona – Arusha.
Mwisho wa Kupokea Maombi:
Jumatano, tarehe 03 Juni 2026
ZINGATIA: Planet Lodges & Lairs haitozi malipo yoyote katika mchakato wa ajira. Ni waombaji watakaochaguliwa tu ndio watakaowasiliana nao kwa ajili ya usaili.