Tangazo la nafasi ya Udereva

126 views
Skip to first unread message

Tanzania Mailing

unread,
Apr 15, 2026, 7:17:48 AM (8 days ago) Apr 15
to arusha...@googlegroups.com, tanzania...@googlegroups.com

 

Planet Lodges & Lairs

 

TANGAZO LA NAFASI YA KAZI – UDEREVA

Kampuni: Planet Lodges & Lairs
Mahali: Arusha,Serengeti na Tarangire
Mwisho wa Maombi: Jumamosi, tarehe 18 Aprili 2026

Planet Lodges & Lairs inatangaza nafasi ya kazi ya dereva mwenye uzoefu, mwaminifu na uwezo wa kufanya kazi katika mazingira mbalimbali,mjini na porini.

MAJUKUMU YA KAZI:

  • Kuendesha magari ya kampuni kwa usalama na ufanisi kulingana na sheria za barabarani
  • Kuhakikisha usalama wa abiria na mali wakati wote wa safari
  • Kutunza na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa gari
  • Kutoa huduma bora na yenye heshima
  • Kutekeleza majukumu mengine atakayopangiwa na uongozi

SIFA ZA MWOMBAJI:

  • Awe na umri kati ya miaka 25 hadi 45
  • Awe na uzoefu wa kutosha katika kuendesha magari makubwa, yakiwemo:
    • Kenta
    • Fuso
    • Magari ya abiria
    • Aina nyingine za magari makubwa
  • Awe na leseni halali ya udereva ya Class C na kuendelea
  • Awe tayari kufanya kazi katika mazingira yote (mjini na porini)
  • Awe na nidhamu ya hali ya juu, mwaminifu na anayejituma
  • Awe na afya njema na uwezo wa kufanya kazi kwa bidii

JINSI YA KUTUMA MAOMBI:

Maombi yote yawasilishwe getini kwa mlinzi, ofisi za Planet Lodge,Moshono kona – Arusha.

Mwisho wa Kupokea Maombi:
Jumamosi, tarehe 18 Aprili 2026

ZINGATIA: Planet Lodges & Lairs haitozi malipo yoyote katika mchakato wa ajira. Ni waombaji watakaochaguliwa tu ndio watakaowasiliana nao kwa ajili ya usaili.

Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages