Tambaza Hoi Matokeo ya Kidato cha Sita...

165 views
Skip to first unread message

William Kaijage

unread,
Jul 18, 2014, 5:33:07 AM7/18/14
to tamba...@googlegroups.com

Tambaza Hoi Matokeo ya Kidato cha Sita

 

*Shule za Kata zachomoza 10 bora

*RC Iringa atoboa siri ya ufaulu mzuri

 

DSC_4556.JPG

WAKATI shule zisizo na majina makubwa zikifanya vizuri katika mtihani wa taifa wa kidato cha sita, sekondari kongwe ya Tambaza, jijini Dar es Salaam, inashika mkia.

 

Matokeo ya mtihani huo uliofanyika Mei, mwaka huu, yalitangazwa jana na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dk. Charles Msonde.

 

Katika kundi la shule 10 za mwisho, Tambaza ni ya tatu, ikitanguliwa na Ben Bella ya Unguja na Fidel Castro (Pemba), ikifuatiwa na Muheza (Tanga), Mazizini (Unguja), Mtwara Technical (Mtwara), Iyunga Technical (Mbeya), Al-Falaah Muslim (Unguja), Kaliua (Tabora) na Osward Mang’ombe (Mara).

 

Tambaza ni miongoni mwa shule kongwe nchini zilizokuwa zikifanya vizuri katika mitihani, ambazo hivi sasa zinakabiliwa na changamoto kadhaa zikiwemo za uchakavu wa miundombinu, uhaba wa walimu na vifaa vya maabara.

 

Kundi la shule 10 bora linaongozwa na shule ya kata ya Igowole (Iringa), Feza Boy’s (Dar es Salaam), Kisimiri, ambayo ni ya kata (Arusha), Iwawa nayo ya kata (Njombe), Kibaha (Pwani), Marian Girls (Pwani), Nangwa (Manyara).

 

Zingine ni Uwata (Mbeya), inayomilikiwa na Katibu Mkuu Uamsho wa Wakristo Tanzania, Kibondo (Kigoma) nayo ya kata na Kawawa (Iringa), inayomilikiwa na Shirika la Uzalishaji Mali JKT (Suma-JKT).

 

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma, akizungumza kwa simu jana, alisema matokeo hayo yanatokana na ushirikiano mkubwa kati ya uongozi wa mkoa na wa shule hizo.

 

“Tunamshukuru Mungu kwa matokeo mazuri. Hata mwaka jana Igowole ilifanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne,” alisema.

 

Dk. Msonde akizungumzia ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule, watahiniwa 30,225 sawa na asilimia 85.73 wamefaulu kwa madaraja la kwanza hadi la tatu, kati yao wasichana ni 9,954 (asilimia 90.59) na wavulana ni 20, 271 (asilimia 83.53).

 

Kwa mujibu wa jedwali, wasichana wanaongoza katika daraja la kwanza na la pili, huku wavulana wakiongoza katika madaraja ya tatu, nne na sifuri (0).

 

Aliwataja watahiniwa 10 bora kwa masomo ya sayansi kitaifa kuwa, Isaack Shayo (St. Joseph Cathedral), Doris Noah (Marian Girls), Innocent Yusufu (Feza Boys), Placid Pius (Moshi), Benni Shayo (Ilboru), Abubakar Juma (Mzumbe), Mwaminimungu Christopher (Tabora Boys), Chigulu Japhaly (Mzumbe), Hussein Parpia (Al-Muntazir) na Ramadhani Msangi (Feza Boys).

 

Watahiniwa 10 bora kwa masomo ya Biashara kitaifa ni Jovina Leonidas (Ngaza), Nestory Makendi (Kibaha), Imma Anyandwile (Umbwe), Theresia Marwa (Loyola), Grace Chelele (Loyola), Betrida Rugila (Baobab), Jacqueline Kalinga (Weruweru), Tajiel Kitojo (Arusha), Shriya Ramaiya (Shaaban Robert) na Mwanaidi Mwanzema (Weruweru).

 

Kwa masomo ya Lugha na Sanaa kitaifa, watahiniwa 10 bora ni Lisa Mimbi (St. Mary Goreti), Rosalyn Tandau (Marian Girls), Joseph Ngobya (St. Joseph Cathedral), Aneth Mtenga (Marian Girls), Idda Lawenja (Marian Girls), Edna Mwankenja (Kisimiri), Catherine Kiiza (St. Mary’s Mazinde Juu), Nancy Swai (Mwika), Mohamed Salmin (Mwanza) na Idrisa Hamisi (Mwembetogwa).

 

Alisema NECTA imezuia kutoa matokeo ya watahiniwa 150 wa shule ambao hawajalipa ada ya mtihani hadi watakapolipa, pia watahiniwa tisa wa shule walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mtihani kwa baadhi ya masomo, ambao wamepewa fursa ya kuyafanya mwakani.

 

Dk. Msonde alisema watahiniwa 29 walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mtihani kwa masomo yote, ambao wamepewa fursa ya kufanya mitihani mwakani, huku wawili wamefutiwa matokeo baada ya kubainika kufanya udanganyifu.

 

Alisema watahimiwa 41,968 waliandikishwa kufanya mtihani, kati yao wasichana wakiwa 12, 674 (asilimia 30.20) na wavulana 29,294 (asilimia 69.80). Hata hivyo, waliofanya mtihani walikuwa 40,695 na waliofaulu ni 38,905.

 

Akizungumzia kuhusu matokeo ya ualimu, alisema watahiniwa waliojisajili kufanya mtihani wa daraja A walikuwa 10,827, kati yao wasichana ni 4,093 (asilimia 37.80) na wavulana 6,734 (asilimia 62.20).

 

Alisema asilimia 99.62 ya waliofanya mtihani huo wamefaulu, kati yao wasichana ni 4,049 (asilimia 99.66) na wavulana ni 6,646 (asilimia 99.60).

 

Kwa upande wa Stashahada ya Ualimu Sekondari, alisema waliofanya mtihani ni 4,931, kati yao wasichana ni 1,698 (asilimia 34.44) na wavulana 3,223 (asilimia (65.56).

 

Source: RAIA MWEMA http://raiatanzania.co.tz/index.php/habari/984-tambaza-hoi-kidato-cha-sita

Other  SOURCES
MAJIRA: http://www.majira.co.tz/index.php?page=read_more&name=news&id=2452
MWANANCHI: http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Matokeo-kidato-cha-sita-yatia-fora/-/1597296/2386998/-/11hwq0oz/-/index.html
BLOG: http://jumamtanda.blogspot.com/2014/07/matokeo-kidato-cha-sita-yatia-fora.html
HABARI LEO: http://habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/27318-ufaulu-kidato-6-juu
DAILY NEWS: http://www.dailynews.co.tz/index.php/local-news/33789-better-form-six-results-released


Mugisha Clement

unread,
Jul 18, 2014, 5:43:13 AM7/18/14
to tamba...@googlegroups.com

Kuna nini tambaza?

--
Tambaza1996 Facebook Group: http://www.facebook.com/groups/tambaza1996/
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Tambaza High School (1994 to 1996)" group.
To post to this group, send email to tamba...@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/tambaza1996.

Gesona Ngabo

unread,
Jul 18, 2014, 5:46:45 AM7/18/14
to tamba...@googlegroups.com
Hata wakati tunasoma kulikuwa na juhudi binafsi (Tuition kwa So Much) zaidi ya ufundishaji.

Apilike Gordon

unread,
Jul 18, 2014, 5:50:34 AM7/18/14
to tamba...@googlegroups.com
Nani mkuu wa shule pale sasa hivi? Kuna tatizo mahali....



Date: Fri, 18 Jul 2014 11:46:44 +0200
Subject: Re: [Tambaza1996] Tambaza Hoi Matokeo ya Kidato cha Sita...
From: ges...@gmail.com
To: tamba...@googlegroups.com

Gesona Ngabo

unread,
Jul 18, 2014, 5:52:12 AM7/18/14
to tamba...@googlegroups.com
Kama alumni tungekuwa tunajikusanya kusaidia vitu vidogo vidogo vitakavyoweza kusaidia watoto kufaulu au kujituma zaidi.

Apilike Gordon

unread,
Jul 18, 2014, 5:56:31 AM7/18/14
to tamba...@googlegroups.com

Tunahitaji kufahamu kwanza tatizo liko wapi 


Date: Fri, 18 Jul 2014 11:52:11 +0200

Shungu, Mahmoud

unread,
Jul 18, 2014, 5:57:54 AM7/18/14
to tamba...@googlegroups.com

Kama kuna kitu kimenikosesha raha baada ya kusikia matokeo ya shule niliyopitia, kati ya shule zilizo fanya vibaya kwenye mtihani wa kidato cha sita ni hili. Hii selection ipoje siku hizi, wanapeleka vilaza au uongozi? Tatizo nini jamani, hii sio ile Tambaza ya kutembea kifua mbele….

 

Mahmoud Shungu

Branch Supervisor

Tanga Branch

C&TM Operations

 

+255 (0) 27 2644638

+255 (0) 787 354448

mahmoud...@jti.com

                                                                                                                                                 

Tanzania Cigarette Company Ltd

A member of the JTI Group of Companies

J6 H349 Euckenford Street

P.O.Box 683, Tanga

 

jti.com

--

Ismael Kimirei

unread,
Jul 18, 2014, 6:15:16 AM7/18/14
to tamba...@googlegroups.com
Kweli imesikitisha. Nilisikia nikasema mzimu gani huu!
Anyways, yumkini kuna maelezo mujarab. Lakini pia ni kama nimesikia leo asubuhi waalimu walikuwa na kikao kutafakari kilichotokea. Na inasemekana kuna uchakachuaji umefanyika. Naamini hata wao hawaamini kuwa hayo haswa ndio matokeo ya the Mighty Tambaza! Tujipe muda. Tutasikia na kuona mengi. Ningekuona Oluochi ningemuuliza kama bado anafundisha Chemistry (physical) na kama kweli anapata muda kufundisha maana mishemishe zake balaa!
Kimirei
 
-------------------------------------
I.A. KIMIREI (PhD)
Centre Director
TAFIRI Kigoma
Box 90, KIGOMA
TANZANIA
Office:  +255 28 2802068
SkypeName: kimkiakim
ResearcherID:F-7385-2012
ORCID: http://orcid.org/0000-0002-1101-5262
-----------------------------------

Emmanuel Akili

unread,
Jul 18, 2014, 6:35:24 AM7/18/14
to tamba...@googlegroups.com
Very sad... Isije ikawa, Kuna shule mpya ya kata inaitwa Tambaza

Sent from my Windows Phone

Robert Kintu

unread,
Jul 18, 2014, 6:46:35 AM7/18/14
to tamba...@googlegroups.com

Yaani nimesikitika sana, inabidi tujue tatizo liko wapi ili at least we do something. Yaani shule yenye jina kubwa kama Tambaza inakuwa mkiani?

johnma...@yahoo.com

unread,
Jul 18, 2014, 7:33:42 AM7/18/14
to tamba...@googlegroups.com

Headmaster na walimu wrote watimuliwe! No alibi kama ya brazil kufungwa 7 !

Sent from Yahoo Mail on Android



From: Robert Kintu <robert.k...@gmail.com>;
To: <tamba...@googlegroups.com>;
Subject: RE: [Tambaza1996] Tambaza Hoi Matokeo ya Kidato cha Sita...
Sent: Fri, Jul 18, 2014 10:46:34 AM

Mugisha Clement

unread,
Jul 18, 2014, 7:38:02 AM7/18/14
to tamba...@googlegroups.com

Shida ni walimu au wanafunzi ? Au shida ipo kwa wote kunahaja kama kweli tumeguswa tuangalia kwa undani nini tatizo  na kama inawezekana kuwasaidia wasiidiwe angalau watoke  kwenye shule 10 mbovu

johnma...@yahoo.com

unread,
Jul 18, 2014, 10:04:50 AM7/18/14
to tamba...@googlegroups.com

Inabidi tupange twende pale shule ili kujua ukweli! Au mnaonaje? Hii ni fedhea kubwa, sasa hivi kusema umesoma tambaza ni aibu!bora kata!



From: Mugisha Clement <mcmu...@gmail.com>;
To: <tamba...@googlegroups.com>;
Subject: Re: RE: [Tambaza1996] Tambaza Hoi Matokeo ya Kidato cha Sita...
Sent: Fri, Jul 18, 2014 11:38:01 AM

joyce kavishe

unread,
Jul 18, 2014, 9:03:28 PM7/18/14
to tamba...@googlegroups.com
yaani ni balaa kubwa, inabidi watu CV kuondoa Tambaza maana wengine watagoogle nakuona hauko serious.

 But again mimi sishangai kabisa. Kupasi tambaza kwa muda mrefu sasa ilikuwa ni juhudi binafsi za wanafunzi, tuition etc na sio kwamba Tambaza ilikuwa shule nzuri. I hope haya majibu yatafungua watu macho.

gun...@yahoo.com

unread,
Jul 19, 2014, 4:51:33 AM7/19/14
to tamba...@googlegroups.com

Joyce ni kweli naunga mkono hoja. .. hivi kina Oluoch, Kitai wako wapi!? Namkumbuka Merchant alikuwa anajituma mwanzoni bdae naye akabwaga manyanga. .. akaita tambaza JABA



From: joyce kavishe <joyka...@gmail.com>;
To: <tamba...@googlegroups.com>;
Subject: Re: RE: [Tambaza1996] Tambaza Hoi Matokeo ya Kidato cha Sita...
Sent: Sat, Jul 19, 2014 1:03:27 AM

Apilike Gordon

unread,
Jul 19, 2014, 11:33:55 AM7/19/14
to tamba...@googlegroups.com
Ina maana siku hizi hizo tuition hamna au ni wanafunzi masharobaro hawasomi?

Something is seriously wrong somewhere….

Sent from Windows Mail

Bosco

unread,
Jul 19, 2014, 12:45:19 PM7/19/14
to tamba...@googlegroups.com
Inabidi ufanyike mpango wa kuinua elimu tambaza, tusitegemee siri kali... TAMBAZA ALUMNI MPOOOO... IANZISHWE ALUMNI ASSOCIATION itakayo jadili namna ya kuinua elimu bila kutegemea sirikali. 
 TOA MAONI TAFADHALI!!  


Pendo (Bosco) Urassa..


isackkwayu

unread,
Jul 19, 2014, 2:50:22 PM7/19/14
to Mugisha Clement, tamba...@googlegroups.com
Nafikiri kuna umuhimu wa sisi kuwatembelea hawa wadogo zetu kama sehemu ya kuwahamasisha.

what do you think about this idea?

I think we need to raise their confidence level.

Liyeko Makwinje

unread,
Jul 19, 2014, 3:07:27 PM7/19/14
to tamba...@googlegroups.com

Acheni wehu nyie mnaojadili matokeo ya Tambaza, vijijini kwenu hakuna shule ambazo matokeo ni mabaya? what have u done?? acheni kujifanya mnaumizwa fanyeni ktk familia zenu na extended family if u real want to help.

Gesona Ngabo

unread,
Jul 19, 2014, 3:59:29 PM7/19/14
to tamba...@googlegroups.com

Are you serious with your idiotic comment?
Kujadili Tambaza tumekuwa wehu?
Acha kuharibu hali ya hewa.

isackkwayu

unread,
Jul 19, 2014, 4:08:19 PM7/19/14
to Liyeko Makwinje, tamba...@googlegroups.com
Lyeko why don't start were you belong?

myself I Feel I Belong to Tambaza COMMUNITY

joyce kavishe

unread,
Jul 19, 2014, 8:55:27 PM7/19/14
to tamba...@googlegroups.com
Shule za vijijini kwetu haziko kwenye CV yangu, Tambaza ipo. It is in
my interest Tambaza kuwa na reputation nzuri. Unataka kusaidia kijiji
wakati wewe mwenyewe hujajisaidia????

Inabidi wanafunzi washauriwe kujitafutia elimu kwingineko kama shule
haina walimu/walimu hawataki kufundisha. Wakisubiri serikali ndio
matokeao kama haya yatazidi.

2014-07-20 6:08 GMT+10:00 'isackkwayu' via Tambaza High School (1994
to 1996) <tamba...@googlegroups.com>:

Moses Nkundwe Mwasaga

unread,
Jul 20, 2014, 8:19:29 AM7/20/14
to tamba...@googlegroups.com
Dear friends

These results are really shocking!! And i am as concerned as you all are. I agree with all of you that there is a smoking gun somewhere!!
But my initial analysis of the results http://www.necta.go.tz/matokeo2014/ACSEE2014/s0347.htm have deduced that this year calculation of divisions includes General Studies in the formula. As we can all remember it has been habit of many students,but not all students, to neglect this subject and maybe it is the cause of this fiasco.

No offence but during our time,this student (S0347/0503) ,with the results below, studying PCM with B of Physics, C of Chemistry and B of Advanced Math would comfortably  
 have been scored division one point 7. Please correct me if i am wrong!!! But the student has scored division three. Shocking!!!

S0347/0503

F

10

III

G/STUDIES - 'D' PHYSICS - 'B' CHEMISTRY - 'C' ADV/MATHS - 'B'


I am truly convinced that there is a smoking gun!!!


For your information,during our time,had the inclusion of General Studies occurred in the calculation of division,our results would have been interesting to put it mildly.

Once again we should be concerned with our Tambaza.

Kindest regards

Nkundwe Moses Mwasaga


modigwa mohamed

unread,
Jul 22, 2014, 5:23:02 PM7/22/14
to tamba...@googlegroups.com

It's a systematic problem.  Kuan zia wizarani kuja chini, no one cares abt hizi public schools, and wadogo zetu are quite different na sie as well. They need help, support and motivation , kutegemea govt ambayo watoto wakifeli solution ni kuongeza grading scales is a joke. So,if we really care, we should start to think abt these results, seriously.  Otherwise itafika wakati we wouldn't want to mention tumesoma Tambaza. I 2nd Gesona, personal effort I think haipo kabisa. What should we do?

Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages