Amani ya Bwana iwe pamoja nanyi enyi nyote.
Napoendelea kukuzana kujifunza NENO na kufurahia kula gombo, NAONA KTK HALI YA UPEKEE mambo matamu sana kila siku nishikapo Biblia na kuila. Kuhusu Ndoa au mambo ya Mke na Mume katika Neno, yametajwa kwingi kama vile, Yesu kuwajibu Mafarisayo kisha Wanafunzi kuhusu taraka-Marko.10:1-11, Yesu kuwajibu Wanafunzi waliposhituka na kusema kama mambo ya Me/Ke ndio ivyo basi kasheshe, Petro na Paul kutoa mafundisho namna ya Me/Ke wanavyotakiwa kuishi-1Peter.3:1-7, Waefeso. 5:22-23, 1Wakorinto.7:1-40 nk. Lakini kwa kusoma kwangu Neno, nashawishika kusema kua HAKUNA SEHEMU YOYOTE KTK BIBLIA ILIYOELEZEA VEMA KULIKO KAWADA HATUA A-Z YA NAMNA MKE ALIVYOPATIKANA ZAIDI YA MWANZO.24:1-67 kuhusu Isaka kupata Mke-Rebeka
Ni sehemu pekee ktk Bible kuelezea WAZI-WAZI toka hatua ya
kwanza hadi mwisho ya kupatikana kwa Mke kulikuaje kwa wenzetu enzi izo na niliposoma
hapo, nikatambua kwa namna ya kipekee
tena vitu vingi vya kujifunza/note ambavyo nitavitengenezea posts navyo ili
tuweze kubarikiana kwavyo ambavyo ni
……..Send off party (kumbe zilianza zamani),
…….Mungu kuongoza kupata Mke kwa ishara madhubuti( kumbe
Bwana anaweza husika kabisa waziwazi ukimshirikisha kukuthibitishia Mke wako ni
yupi)
……Msichana kuulizwa kama ana ridhia( kumbe hata kama Mungu amehusika 100% bado hakuna kulazimishana au kutishana bali ni hekima kutoa nafasi kwa Binadamu-Binti kutumia Utashi wake kukubali ama la)
….Baba Mzazi ndio wa Kwanza kuona na kuamua Kijana aoe/apewe Mke( Kumbe zamani ni tofauti na sasa ambapo Vijana wanaamua wenyewe, ni maeneo machache sana ktk dunia hii ya leo, Wazazi kumuamulia Mtoto kuoa/olewa, utapelekwa mahakama na Mtoto wako mwenyeewe au vikundi vya Watetezi wa Haki za Binadamu au Wanaharakati wa kutetea jinsi za Kike
….Utunzaji wa maagano ktk kupata Mke-kuoa wa kutoka Ukoo wao( kumbe si kuoa-olewa tu mradi umeshafikisha Umri au unawakawaka kibailojia bali ni kuzingatia pia kuoa/olewa kimaagano)
…..Isack kumkubali/penda Msichana alipomuoa( kumbe kuna kuridhia pia kwa Mkaka lakini ni ajabu tu unampenda Mdada ghafla sana wakati ulikua hujamuona au kuzoeana au kusoma pamoja au kusali wote-hii tutajadili sana ktk post mpya ilikuaje ilo likawezekana?)
…. Nafasi kubwa ya Mke kwa Mume-Rebeka alifanyika faraja kwa Isack kufiwa na Mama yake.( ni ajabu kabisa Mke anaondosha huzuni nzito ya Mume kuondokewa na Mama yake Mzazi)
Ni kutokana na mambo hayo niliyoyaona ktk andiko hilo, napenda leo tutafakari/tuelimishane hilo la mwisho mstari wa mwisho kabisa wa Mwanzo.24:67 unasema..’’ Isaka akamwingiza Rebeka katika hema ya mama yake, Sara, akamtwaa Rebeka, akawa mkewe, akampenda; Isaka akafarijika kwa ajili ya kufa kwa mamake.
Angalia tena kipande hiki…..’’ Isaka akafarijika kwa ajili ya kufa kwa mamake’’
Poleni sana wa wenzetu wenye uzoefu mbaya sana na uchungu kwa yale Mama zao Wazazi waliowatendea, lakini WENGI wetu, Wote tunajua utamu, thamani, raha, faraja ya kua na Mama Mzazi, mapenzi hujisikiayo na kutaka kuyaonyesha kwa Mama Mzazi Mpenzi, uponyaji ktk moyo na nafsi uupatao kwa kua na Mwanamke pekee ambaye Mungu alimteua wewe kuwasili uku Duniani. Wote tunajua nini maana ya Mama Mzazi Mpenzi wa moyo na nafsi zetu, LAKINI BIBLIA INASEMA HAPA KUA MKE ALIFANYIKA FARAJA KWA ISAKA BAADA YA MAMA MZAZI KUFA.
Kama Mke anawezakua/fanyika baraka kiasi icho cha kuponya donda lililosababishwa na kifo cha MAMA MZAZI MWENYE UZITO HUO WA AJABU MMNOOO KWA KILA ALIYEZALIWA NA MWANAMKE,hakika NIMEONA KITU LEO KTK MAANDIKO na kila mwenye Mwili uliokua siku moja miaka kadhaa tumboni kwa Mama yake kisha akakua na kupata Mke na hata yule anayekwenda kupata Mke na aseme aaaamen kubwa kama radi, Aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaamen.
Enyi Wake ndani ya Ndoa na Watarajiwa, leo nimegundua mko Tanzanite Stones za kutisha kwa thamani ktk Maisha yetu
Press on.
Edwin Seleli