HITIMISHO LA MADA YA UNYWAJI WA POMBE

282 views
Skip to first unread message

strictly.gospel

unread,
Dec 20, 2013, 8:33:00 AM12/20/13
to Strictly Gospel Group

Halleluya wana wa Mungu,

Ashukuriwe Mungu, Yeye ambaye sikuzote hutufanya tuandamane kwa ushindi tukiwa ndani ya Kristo.

Basi haya ndiyo majivuno yetu na Dhamiri yetu inatushuhudia kwamba tumeenenda katika ulimwengu na hasa katika uhusiano wetu sisi kwa sisi, katika utakatifu na uaminifu utokao kwa Mungu. Hatufanyi hivyo kwa hekima ya kidunia bali kwa neema ya Mungu. Kwa maana kuyaelewa maandiko matakatifu ni kwa neema na uvuvio wa Roho Mtakatifu. Na kwa dhamana hii ambayo Mungu mwenye enzi katuvuvia kulinda kundi lake hili, tukiwa kama wadhamini wa kristo YESU. Tofauti na watu wengine wengi, sisi hatuchuuzi neno la Mungu kwa ajili ya kupata faida, sifa au Kinyume chake, bali katika Kristo tunalisema neno la Mungu kwa unyofu, kama watu tuliotumwa kutoka kwa Mungu ili tuishike dhamana hii ndani ya Kundi la SGM. Basi ‘’Kwa wale wanaopotea sisi ni harufu ya mauti, lakini kwa wale wanaookolewa sisi ni harufu nzuri iletayo uzima’’.

Katika mada hii iliyo endelea sana humu tumeona sisi hatuwezi kukaa kimya wakati watu wanaweza potezwa kuhusu kunywa POMBE au DIVAI. Sisi  ndio barua ya kristo na ya mababa zetu wa imani yetu iliyoandikwa katika mioyo yetu, inayojulikana na kusomwa na kila mtu hapa duniani. Ni barua itokayo kwa Kristo ambayo haikuandikwa kwa wino bali kwa Roho wa Mungu aliye hai, si katika vibao vya mawe, bali katika vibao ambavyo ni MIOYO ya wanadamu. Hili ndilo tumaini tulilo nalo mbele za Mungu kwa njia ya Kristo. Si kwamba sisi tunafikiri kuwa tunaweza kufanya jambo lo lote wenyewe,Hapana ni katika nguvu  inayotoka kwa Mungu. Yeye ndiye aliyetufanya sisi kuwa wahudumu wa Agano Jipya, si wa ANDIKO bali wa Roho, kwa kuwa ANDIKO HUUA bali ROHO HUTIA UZIMA.

Basi imekuwa faida gani katika kujengana imani hii juu ya je, tunywe DIVAI AU POMBE au tusinywe? Twatambua kuwa maandiko yanaposomwa yatupasa tutambue tamaduni za wakati ule maandiko yalipoandikwa na tamaduni za wakati huu tunaposoma neno katika eneo letu. KULE ISRAEL ukiweka juice ya zabibu, bia, redbull, malta, fanta, pepsi, ndovu, Kilimanjaro zooote hizi kule ISRAEL NI DIVAI(wine) maana wanapenda kutengeneza vitu vyao kwa mazao ya shamba zao ikiwemo zabibu. (Wines made from produce besides grapes are usually named after the product from which they are produced (for example, rice wine,pomegranate wine, apple wine and elderberry wine) and are generically called fruit wine. The term "wine" can also refer to starch-fermented or fortified beverages having higher alcohol content, such as barley winehuangjiu, or sake). 

Kama Bwana Yesu "aligeuza maji kuwa divai" na haikuwahi kutokea hapo kabla na haijatokea tena hadi leo; KINYWAJI HICHO NI DIVAI ITOKANAYO NA MAJI. Ambayo maandiko yanabainisha ilikuwa "mpya na njema" haina mwanzo kama divai nyinginezo zitokanazo na mazao.

Mfano; shampeni isiyo na kilevi na ile yenye kilevi zote ni SHAMPENI isipokuwa lebo ya NON---Alcoholic inayooeleza kilichomo, sasa tunaona matumizi ya neno divai ndiyo yanayoleta shida kwetu maana kwetu mtu akisema divai moja kwa moja inamaana ni pombe. Ila kwa uhalisi wa neno DIVAI(WINE)NI ILIYOCHACHUKA AU ISIYOCHACHUKA. Swali la kujiuliza ktk ROHO MTAKATIFU YESU ALITENGENEZA DIVAI (WINE) ILIYOCHACHUKA AU ISIYOCHACHUKA.???

Basi tukiwa wote ni mali ya Kristo, tukumbuke kuwa kama alivyo Kristo, vivyo hivyo na sisi ndivyo tulivyo. kujisifu kwetu zaidi kuwe ni kuhusu mamlaka tuliyo nayo kama wana (ambao majina yao yameandikwa mbinguni) ambayo Mungu alitupa katika Kristo si kuonekana katika kujiamini na kujisifu kwa akili zetu zenye nguvu na hekima ya dunia hii. tusithubutu kujiweka kwenye kundi moja au kujilinganisha na hao wanaojitukuza wenyewe kwa mashindano yasiyo na hekima ya KIUNGU wala ROHO MTAKATIFU. Kwa kujipima na kujilinganisha wenyewe kwa wenyewe kana kwamba , tunaonyeshana ya kuwa na busara zaidi au ufahamu zaidi wa mandiko YASIYOVUVIWA NA ROHO MTAKATIFU.

 Tusijivune kupita kiasi, lakini tujue tumaini letu ni imani yetu inayozidi kukua katika eneo letu la utendaji wetu miongoni mwetu wenyewe. Lakini , ‘‘Yeye ajisifuye ajisifu katika Bwana, kwa maana si yeye ajisifuye  bali ni Bwana humsifu na humvuvia NENO litokalo katika kina cha moyo sikivu uliyojaa uweza na nguvu na mamlaka ya ROHO MTAKATIFU. Maana uweza wa BWANA WETU YESU KRISTO NDANI YETU UMEJAA HEKIMA, NGUVU NA MAMLAKA ISIYO YA KAWAIDA. Kama tutashindana na kubishana basi kuwe katika JINA KUU LA YESU KRISTO. PIA IWEPO FAIDA KUBWA KWA KANISA. Lakini tukirudi kwenye ubishani wa divai au pombe kwa mkristo, naam, athari ni nyingi zaidi kuliko faida na wengi wetu tuna ushuhuda mkuu. Je ukisema pombe kikombe au glass moja una maana ya pombe ipi?? Angalia hizi zooote ni pombe tena zenye madhara makuu hata ukiangalia kibandiko chake tu kwa akili ya kawaida;

  • Kilimanjaro, Safari, Reds, Senator, Mzinga, Malta, Konyagi, Gongo, Ulanzi, Kangara, Chibuku, Kiroba, Mnazi, Ulanzi, Serengeti, Guiness, Mbege........-n.k.

 

Hivyo basi tukiukomboa wakati basi,  siyo yetu iwe SIYO, na ndiyo yetu iwe NDIYO si kwa kujitukuza utu wetu huu utakaoangamizwa siku moja, bali ROHO ZETU Zitainuliwa na kristo YESU katika utukufu wake. Naamini kabisa hakuna humu ndani ya SGM asiyeelewa kwamba kunywa pombe ni dhambi akiwa na ujasiri ktk ROHO MTAKATIFU ISIPOKUWA AMEKUFA ANGALI ANATEMBEA.

 

Kwa kuwa twabishana na kushindana ili tupate uthibitisho kwamba Kristo alikunywa divai(pombe) au si pombe(wine) kwa kutumia mabishano makali. Naam,yeye si dhaifu katika kushughulikia hili, na wala hajasafiri, wala hajalala, bali nguvu ni ileile tuliyoshuhudiwa UOMBE MUNGU. Kwa maana alisulibiwa katika udhaifu, lakini anaishi kwa nguvu za Mungu. Na sisi tukiwa dhaifu alitutoa katika udhaifu na unyonge na kuonewa kwa kuwashughulikia watesi wetu kwa nguvu za Mungu.

Hivyo tujichunguzeni wenyewe tuone kama twaishi katika imani ileile ya kweli?. Je tumesahau ya kuwa Yesu Kristo yeye yumo ndani yetu? Kama sivyo, basi, tumeshindwa kufikia kipimo hicho ambacho BWANA YESU alituachia. Kwa maana hatuwezi kufanya lo lote kinyume na kweli iliyomo ndani yetu, bali kuithibitisha kweli tu. 

Tuwatakie mafanikio ya rohoni na mwilini tukifarijiana, tukinia mamoja, tukiomba amani kwa Mungu wa upendo naye atakuwa pamoja nasi.

NOTE:

Tafadhali fungua kiambatanisho cha video ambayo inaonyesha mhubiri anayehimiza unywaji wa pombe kama baadhi ya walio humu wafanyavyo. Wengine walioko huko Dsm Tanzania wanaweza kuwa wamemuona pamoja na mambo mengine HUSISITIZA KUOA WAKE WENGI kama yeye alivyofanya.

Tazama kwa makini, jifunze halafu utafakari na uchukue hatua.

 

Neema ya Bwana Yesu Kristo na upendo wa Mungu na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote.

Amen!

VID-20131116-WA0000.mp4

Tusekelege Tuse

unread,
Dec 31, 2013, 2:12:16 AM12/31/13
to strictl...@googlegroups.com
 
ZAKARIA ALIPOTOKEWA NA MALAIKA KWAMBA MKE WAKE ELIZABETH ATAPATA MIMBA ALIPEWA MASHARTI ASIONJE MVINYO YEYE NA MKE WAKE KWANI ATACHOKIZAA NI KITAKATIFU.
 
THE SAME TO MARIAM  MALAIKA HUYOHUYO IKIWA TOFAUTI YA MIEZI SITA ALIMPA MASHARTI MARIAM HAYOHAYO.
 
NA KATIKA MAMBO YA WALAWI ILIKUWA MTU AKIWA KATIKA KUJITAKASA ALIPEW MASHARTI ASIONJE KITU CHOCHOTE CHA MZAO WA MZABIBU.
 
SASA BWANA YESU KATIKA HARUSI YA KANA ALIBADILISHA MAJI KUWA DIVAI ILIYOKUWA NZURI NA TAMU KULIKO YOTE.
 
WAKRISTO WALIAMUA KWA UWEZA WA MUNGU ONDOA RC BAANA YA MATUKIO YA BABA ZETU KINA NUHU,LUTTH,DAUID,
NK.UNAKUMBUMBA WATOTO WA LUTH WALICHOFANYA HATIMAYE WAKALALA NA BABA YAO.
 
KUTOKANA NA MATUKIO MENGI  YA MADHARA YA POMBE NDIPO WALIAMU HIVYO KWAMBA AS CHRISTIAN TUSINYWE POMBE KABISA.
 
WENGINE WAAKAAMUA KUENDELEA, NA KATIKA BIBLIA POMBE IMEHESABIWA KAMA MAVI,NA SEHEMU INGINE IMEANDIKWA MPE MASIKINI POMBE ANYWE ALEWE ASAHAU SHIDA ZAKE.
 
UKITAKA KUWA MTAKATIFU USINYWE KABISA.HATA KATIKA MAANDIKO HAYASEMA KAMA YESU ALIKUNYWA ILA ALITENGENEZA KWA UTUKUFU WAKE.
 
BE BLESSED.
NA MUNGU ANAPENDEZWA NA WATAKATIFU WALIOPO DUNIANI.
 
 

--
Tafadhali zingatia msingi wetu ni Neno la Mungu, Lengo letu Kuujenga mwili wa Kristo, kushirikiana, amani na upendo. Yeyote yuko huru kuchangia, kufundisha, kukubali kufundishwa sawasawa na Msingi wetu Mkuu Neno la Mungu. Kujiunga na Team ya Injili au Maombi wasiliana nasi kwa simu 0714 915 424. Tuma Email. strictl...@yahoo.co.uk Facebook:https://www.facebook.com/pages/Strictly-Gospel/363180289370
 
Blog: www.strictlygospel.wordpress.com
 
Kujiondoa Kwenye Kundi Hili Tuma Email:
strictlygospe...@googlegroups.com


Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages