Bwana Yesu asifiwe!

10 views
Skip to first unread message

fbensony

unread,
Aug 6, 2014, 12:17:00 AM8/6/14
to strictl...@googlegroups.com
Elimu ya Mungu ni NURU isiyokaa ndani yao watu wabaya; Nao waijuao ndiyo waliofungwa pamoja na Mungu ili utukufu wake ukae kwao na katika hayo basi;

Tunayo thamani kubwa sana sisi tulioipata NEEMA ya kuwa hifadhi ya NURU ya MUNGU tujapo kuwa katika miili hii korofi, miili hii tata, miili hii dhalimu, miili hii yenye tamaa, miili hii yenye kila aina ya adha yenye kuona kiu, njaa na kuumwa, 

Lakini je sie yaani sisi;

La kutufaa ni lipi? Hakika wema wa Mungu uliojificha machoni pa wapumbavu ulio wazi kwao wenye uhitaji ndilo jambo lililo bora saana katika sisi. 

Ama ninyi mwaona ni?
Maana kama si katika hilo sisi tungejivuna katika lipi? Ama umahili wetu wa kulitaja jina la BWANA pasi na kuyaishi mapenzi yake?

Ni jambo la kumshukuru Mungu wetu ambaye kwa yeye tumekuwa hivi tulivyo; yaani wenye kunena mema ambayo twayaishi, wenye kumulika gizani ili kuleta mwanga!

Basi tujitunze mioyo na nafsi zetu ili tusije tekwa akili na fahamu zetu na ile kawaida ya dunia ikapelekea sisi kuwa waasi wa ile haki ya Mungu iletayo amani na kujenga furaha maishani mwetu!

Mbarikiwe.


Only God for Me

James Otieno

unread,
Aug 6, 2014, 8:39:12 AM8/6/14
to strictl...@googlegroups.com
Amina maneno ya kujenga Roho zetu kweli Bwana Yesu atukuzwe na Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo ainuliwe kwa Neno lake.


--
Tafadhali zingatia msingi wetu ni Neno la Mungu, Lengo letu Kuujenga mwili wa Kristo, kushirikiana, amani na upendo. Yeyote yuko huru kuchangia, kufundisha, kukubali kufundishwa sawasawa na Msingi wetu Mkuu Neno la Mungu. Kujiunga na Team ya Injili au Maombi wasiliana nasi kwa simu 0714 915 424. Tuma Email. strictl...@yahoo.co.uk Facebook:https://www.facebook.com/pages/Strictly-Gospel/363180289370
 
Blog: www.strictlygospel.wordpress.com
 
Kujiondoa Kwenye Kundi Hili Tuma Email:
strictlygospe...@googlegroups.com



--
Evangelist James Joel Otieno
Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages