Amani ya Bwana iwe pamoja nanyi enyi nyote,
Tunaposoma Neno, yako mambo/kweli/vitu unafanywa uyaone hadi unashangaa kua ivi hili na lile lilikuwepo hapo ktk sura/mstari siku zote nasoma kweli? halafu gafla hilo jambo linakua jipya kweli ktk moyo, akili na fahamu zako. Embu tusome haya maandiko 2 hapa.
LUKA: 4: 16-30….16 Basi, Yesu alikwenda Nazareti, mahali alipolelewa, na siku ya Sabato, aliingia katika sunagogi, kama ilivyokuwa desturi yake. Akasimama ili asome Maandiko Matakatifu kwa sauti. 17 Akapokea kitabu cha nabii Isaya, akakifungua na akakuta mahali palipoandikwa:18 Roho wa Bwana yu juu yangu, kwani amenipaka mafuta niwahubirie maskini Habari Njema. Amenituma niwatangazie mateka watapata uhuru, vipofu watapata kuona tena; amenituma niwakomboe wanaoonewa,19 na kutangaza mwaka wa neema ya Bwana." 20 Baada ya kusoma, akafunga kile kitabu, akampa mtumishi, kisha akaketi; watu wote wakamkodolea macho. 21 Naye akaanza kuwaambia, "Andiko hili mlilosikia likisomwa, limetimia leo." 22 Wote wakavutiwa sana naye, wakastaajabia maneno mazuri aliyosema. Wakanena, "Je, huyu si mwana wa Yosefu?"
23 Naye akawaambia, "Bila shaka mtaniambia msemo huu: Mganga jiponye mwenyewe, na pia mtasema: Yote tuliyosikia umeyafanya kule Kafarnaumu, yafanye hapa pia katika kijiji chako." 24 Akaendelea kusema, "Hakika nawaambieni, nabii hatambuliwi katika kijiji chake. 25 Lakini, sikilizeni! Kweli kulikuwa na wajane wengi katika nchi ya Israeli nyakati za Eliya. Wakati huo mvua iliacha kunyesha kwa muda wa miaka mitatu na nusu; kukawa na njaa kubwa katika nchi yote. 26 Hata hivyo, Eliya hakutumwa kwa mjane yeyote ila kwa mwanamke mjane wa Sarepta, Sidoni. 27 Tena, katika nchi ya Israeli nyakati za Elisha kulikuwa na wenye ukoma wengi. Hata hivyo, hakuna yeyote aliyetakaswa ila tu Naamani, mwenyeji wa Siria." 28 Wote waliokuwa katika lile sunagogi waliposikia hayo walikasirika sana. 29 Wakasimama, wakamtoa nje ya mji wao uliokuwa umejengwa juu ya kilima, wakampeleka mpaka kwenye ukingo wa kilima hicho ili wamtupe chini. 30 Lakini Yesu akapita katikati yao, akaenda zake.
ZINGATIA MSTARI WA 30…Lakini Yesu AKAPITA KATIKATI YAO, akaenda zake. Angalia pia andiko hili hili kutoka KJV-Bible Verse 30…’’ But He passing THROUGH THE MIDST OF THEM went his way,
Andiko Jingine……..
Yohana.8: 48-59….48 Wayahudi wakamwambia, "Je, hatukusema kweli kwamba wewe ni Msamaria, na tena una pepo?" 49 Yesu akajibu, "Mimi sina pepo; mimi namheshimu Baba yangu, lakini ninyi hamniheshimu. 50 Mimi sijitafutii utukufu wangu mwenyewe; yuko mmoja mwenye kuutafuta utukufu huo, naye ni hakimu. 51 Kweli nawaambieni, anayeuzingatia ujumbe wangu hatakufa milele." 52 Basi, Wayahudi wakasema, "Sasa tunajua kweli kwamba wewe ni mwendawazimu! Abrahamu alikufa, na manabii pia walikufa, nawe wasema ati, Anayeuzingatia ujumbe wangu hatakufa milele! 53 Je, unajifanya mkuu zaidi kuliko baba yetu Abrahamu ambaye alikufa? Hata na manabii walikufa. Wewe unajifanya kuwa nani?" 54 Yesu akawajibu, "Nikijitukuza mwenyewe, utukufu wangu si kitu. Baba yangu ambaye ninyi mwasema ni Baba yenu, ndiye anayenitukuza. 55 Ninyi hamjapata kumjua, lakini mimi namjua. Na, nikisema simjui, nitakuwa mwongo kama ninyi. Mimi namjua na ninashika neno lake. 56 Abrahamu, baba yenu, alishangilia aione siku yangu; naye aliiona, akafurahi." 57 Basi, Wayahudi wakamwambia, "Wewe hujatimiza miaka hamsini bado, nawe umemwona Abrahamu?" 58 Yesu akawaambia, "Kweli nawaambieni, kabla Abrahamu hajazaliwa, mimi niko." 59 Hapo wakaokota mawe ili wamtupie, lakini Yesu akajificha, akatoka Hekaluni.
ZINGATIA MSTARI WA 59: Hapo wakaokota mawe ili wamtupie, lakini Yesu akajificha, AKATOKA Hekaluni ILA alitokaje Hekaluni? Jibu ni Biblia ya KJV- Kiingereza inaweka vema hivi Verse 59…’’ Then took they up stones to cast at him: but Jesus hid himself, and WENT OUT OF THE TEMPLE, GOING THROUGH OF THE THEM, and so passed by....’’NOTICE: ‘’GOING THROUGH OF THE THEM’’
MASWALI:
MOJA: Aliwezaje kupita Katikati yao Watu wale waliokua wamejaa pumzi mbaya hata wamepania kumdhuru? Angalia walivyokua wamefyumu/jaa majazba ya kufa Mtu hapa…Luka. 4:28 Wote waliokuwa katika lile sunagogi waliposikia hayo walikasirika sana. 29 Wakasimama, wakamtoa nje ya mji wao uliokuwa umejengwa juu ya kilima, wakampeleka mpaka kwenye ukingo wa kilima hicho ili wamtupe chini’’’NA..Yohana. 8: 48 Wayahudi wakamwambia, "Je, hatukusema kweli kwamba wewe ni Msamaria, na tena una pepo?" 52 Basi, Wayahudi wakasema, "Sasa tunajua kweli kwamba wewe ni mwendawazimu! Abrahamu alikufa, na manabii pia walikufa, nawe wasema ati, Anayeuzingatia ujumbe wangu hatakufa milele! 53 Je, unajifanya mkuu zaidi kuliko baba yetu Abrahamu ambaye alikufa? Hata na manabii walikufa. Wewe unajifanya kuwa nani?" 58 Yesu akawaambia, "Kweli nawaambieni, kabla Abrahamu hajazaliwa, mimi niko." 59 Hapo wakaokota mawe ili wamtupie, lakini Yesu akajificha, akatoka Hekaluni
.
PILI:
Tukisema kilichotokea hapo ni sawa au kinafanana na hii nguvu hapa Yohana.18:4 Yesu,
hali akijua yote yatakayompata, akatokea, akawauliza, "Mnamtafuta
nani?" 5 Nao
wakamjibu, "Yesu wa Nazareti!" Yesu akawaambia, "Mimi
ndiye." Msaliti Yuda alikuwa amesimama hapo pamoja nao. 6 Basi,
Yesu alipowaambia: "Mimi ndiye", wakarudi nyuma, wakaanguka chini. 7 Yesu
akawauliza tena, "Mnamtafuta nani?" Wakamjibu, "Yesu wa
Nazareti!" 8 Yesu
akawaambia, "Nimekwisha waambieni kwamba mimi ndiye. Basi, kama
mnanitafuta mimi, waacheni hawa waende zao." 9 (Alisema hayo
ili yapate kutimia yale aliyosema: "Wale ulionipa sikumpoteza hata
mmoja.")
Angalia mstari wa 6… Basi, Yesu alipowaambia: "Mimi ndiye", WAKARUDI NYUMA WAKAANGUKA CHINI. Yaani kama alikua na uwezo huo wa kuwatandika askari wakakamavu ngwara ile isiyoonekana, kwa nini isiwe YESU KUPITA KATIKATI YAO wale Watu wameshamtait barabara kabisa kona zote, isiwe ilihusisha pia nguvu ya Uungu wake? Natafakari tu sina uhakika kwa kweli.
Press on.
Edwin Seleli