Usingizi wa Kiroho

1,574 views
Skip to first unread message

Strictly Gospel

unread,
Aug 6, 2013, 10:15:59 PM8/6/13
to Strictly Gospel Group

Bwana Yesu asifiwe…

Kuna mambo mengi sana yanatokea tunapokuwa tumelala kiroho.Adui huamka tunapokuwa tumelala. Dhumuni la adui ni kuharibu, kwa kuiba kile tulichopewa na Bwana Mungu,maana kile tulichopewa na Mungu ni kitu chema sana

*Hivyo kunam-badilishano usio wa halali tunapokuwa tumelala kiroho.Ubadilishano huu ni wa kutumia nguvu za giza/nguvu za kimapepo(A demonic change)

*Wakristo wengi leo wamebadilishiwa vitu au mambo yao ya thamani walipokuwa wamelala pasipo kujijua.Siku ya leo nataka uyajue haya,na tunaanzia kwa andiko hili;

Tunasoma 1 Wafalme 3:19-20;
“ Na mtoto wa mwanamke huyu akafa usiku, maana alimlalia.  Akaondoka kati ya usiku, akamwondoa mtoto wangu ubavuni pangu, mimi mjakazi wako nilipokuwa usingizini, akamweka kifuani pake, na mtoto wake mwenyewe, aliyekuwa amekufa, akamweka kifuani pangu.”

*Katika andiko hilo, tunaona habari za wanawake wawili makahaba. Ambao walikuwa wakiishi nyumba moja.Wote wawili wakafanikiwa kuzaa watoto,baada ya kuzaa,mmoja wapo alimlalia mtoto hata kufa nyakati za USIKU.

Biblia inatuambia wakati wa usiku ndipo pakatokea UBADILISHANO/EXCHANGE baina ya mtoto aliyekufa kwa mtoto asiyekufa(1 Wafalme 3:20)

• Mbadilishano/exchange huo ulitokea nyakati za usiku wakati mama wa mtoto asiyekufa alipobadishiwa mtoto wake na kupewa mtoto aliyekufa.

Hivi ndivyo adui afanyavyo wakati tunapokuwa tumelala,
-anajaribu kukuchukulia mtoto wako aliye hai na kukupa aliyekufa,
-anajaribu kukubadilishia Ndoa yako aliyo hai,na kukupa iliyokufa,
-anajaribu kukubadilishia kazi yako nzuri na kukupa mbaya,
-anajaribu kuondoa kizazi kilichowekwa na Mungu ndani yako,na kukupa UTASA.N.K

• Adui ni muongo siku zote,akitaka ukubaliane naye kirahisi kwa kukubadilishia kitu kizuri kwa kitu kibaya.

*Mungu hajakupatia kitu kinyonge,
*Mungu hajakupatia Ndoa yenye matatizo,
*Mungu hajakupatia kazi yenye misukosuko,
*Mungu hajakupatia afya ya magonjwa,
*Mungu hajakupatia kuishi katika umasikini,BALI ADUI NDIYE ALIKUBADILISHIA NYAKATI ZA USIKU ULIPOKUWA UMELALA USINGIZI WA KIROHO.

Haleluya…
Jina la Bwana lisifiwe…

Tazama andiko hilo vizuri (1 Wafalme 3:16-20),  utagundua kwamba haikuwa rahisi kwa mama yule aliyebadilishiwa mtoto wake,maana watoto wote walikuwa ni wachanga mno.

Hivyo adui akapata mwanya wa kutaka kumlazimisha yule mama akubali kumchukua mtoto ambaye si wake,ambaye ni maiti.

Na ndivyo Adui afanyavyo kwetu sisi tunapokuwa tumelala katika usingizi wa kiroho,yeye adui hutulazimisha kukubaliana naye kwa mazingira aliyoyaandaa yeye,akijua kwamba itakuwa si rahisi sisi kugundua.

Sasa angalia;
1 Wafalme 3 :21
“ Nilipoondoka asubuhi nimnyonyeshe mtoto wangu, kumbe? Amekufa. Hata asubuhi nilipomtazama sana, kumbe! Siye mtoto wangu niliyemzaa.” Neno linaposema, “Nilipoondoka asubuhi…” Hapa maana yake ni kwamba ASUBUHI ni mahali ambapo pana MWANGA wa kutosha,ambao ulimfanya yule mama aliyebadilishiwa mtoto wake kumtambua kwa haraka alipomtizama sana.

Sasa Bwana Yesu Kristo ndiye asubuhi yetu,Yeye Yesu Kristo ndiye MWANGA wetu unaotupa kutambua UBADILISHAONO HUO ULIOFANYIKA USIKU.

Kwa maana nyingine ni kwamba yule mama aliyebadilishiwa mtoto wake,hasingeweza kumtambua mtoto wake nyakati za USIKU, Hivyo alihitaji mwanga ili aweze kumtizama vizuri mtoto wake,kisha amtambue.
Vivyo hivyo sisi wenyewe hatuna UWEZO wa kutambua mambo yetu yaliyobadilishwa katika ulimwengu wa roho pasipo kuwepo NURU,ambayo hiyo NURU ndiye Yesu Kristo.

--Gasper Madumla

festus chongoma

unread,
Aug 7, 2013, 1:12:23 AM8/7/13
to strictl...@googlegroups.com
MUNGU AKUBARIKI SAAANA MTUMISHI A MUNGU,NIMEJIFUNZA MAMBO MENGI MNO
PIA NIMEGUNDUA MBINU ZA SIHETANI
> --
> Tafadhali zingatia msingi wetu ni Neno la Mungu, Lengo letu Kuujenga mwili
> wa Kristo, kushirikiana, amani na upendo. Yeyote yuko huru kuchangia,
> kufundisha, kukubali kufundishwa sawasawa na Msingi wetu Mkuu Neno la Mungu.
> Kujiunga na Team ya Injili au Maombi wasiliana nasi kwa simu 0714 915 424.
> Tuma Email. strictl...@yahoo.co.uk
> Facebook:https://www.facebook.com/pages/Strictly-Gospel/363180289370
>
> Blog: www.strictlygospel.wordpress.com
>
> Kujiondoa Kwenye Kundi Hili Tuma Email:
> strictlygospe...@googlegroups.com
>
>
>

Siaka Nyanchiwa

unread,
Aug 7, 2013, 12:56:16 AM8/7/13
to strictl...@googlegroups.com
Shaloom mbarikiwe kwa neno hili nzuri. haipaswi kulala usingizi wa kiroho. maana ndiko utokeeapo uharibifu wote ktk ulimwengu wa kiroho na baadaye kimwili. Tusilale usingizi wa kiroho kabisa sisi wacha Mungu.
        Siaka Nyanchiwa
  


From: Strictly Gospel <strictl...@yahoo.co.uk>
To: Strictly Gospel Group <strictl...@googlegroups.com>
Sent: Tuesday, August 6, 2013 7:15 PM
Subject: Usingizi wa Kiroho

florence majani

unread,
Aug 7, 2013, 3:27:20 AM8/7/13
to strictl...@googlegroups.com
Bwana Yesu asifiwe. Ahsante kwa neno hili. Wiki iliyopita nikiwa usingizini lakini katika ulimwengu wa roho walikuja watu watatu, wanawake wawili na mwanaume mmoja. Walikuja katika sura za kutisha na nilianza kuwakemea katika ulimwengu wa roho. Ilikuwa ni vita na hatimaye walikimbia. Naamini kuwa mambo mengi yanatokea ktk ulimwengu wa roho tukiwa usingizini ndiyo maana tunashauriwa kufanya MAOMBI YA USIKU WA MANANE. Mbarikiwe.


From: Strictly Gospel <strictl...@yahoo.co.uk>
To: Strictly Gospel Group <strictl...@googlegroups.com>
Sent: Wednesday, 7 August 2013, 5:15
Subject: Usingizi wa Kiroho

edmund oguda

unread,
Aug 10, 2013, 12:26:35 AM8/10/13
to strictl...@googlegroups.com
Amen, ndg yangu Gasper. Mungu akubariki sana kwa kutukumbusha mambo hy ya kizani. Ni mengi mno tunayoporwa au kuibiwa na mwovu hyo usiku w kiza. Pia, niongezee hili, wajua hata kuna kanisa moja kule Singida, robo tatu ya watoto w Sunday school ktk kanisa walikuwa 'initiated' na wachawi usiku w kiza na kujifunza uchawi, huku mzee mmoja w kanisa hilohilo akirahisha jambo hilo km agent wa kishetani. Watoto hao walikuwa na uwezo w kushuka ht kuzimu na kurudi,na kufanya chochote kile  kanisani na mitaani pia ktk jamii. Mpaka Mungu alipomleta Nabii toka mbali ndddo akaliona hilo na kulifumua, ndipo, uponyaji ulipojiri ktk hilo kanisa.                                                   Mungu awabariki.                                                               Oguda J.E.  

> Date: Wed, 7 Aug 2013 13:12:23 +0800
> Subject: Re: Usingizi wa Kiroho
> From: festusc...@gmail.com
> To: strictl...@googlegroups.com
Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages