Amani ya Bwana iwe pamoja nanyi nyote,
Mathayo 11:1-15.. Ikawa Yesu alipokwisha kuwaagiza wanafunzi wake kumi na wawili, alitoka huko kwenda kufundisha na kuhubiri katika miji yao. 2 Naye Yohana aliposikia huko gerezani matendo yake Kristo, alituma wanafunzi wake, kumwuliza, 3 Wewe ndiwe yule ajaye, au tumtazamie mwingine? 4 Yesu akajibu akawaambia, Nendeni mkamweleze Yohana mnayoyasikia na kuyaona; 5 vipofu wanapata kuona, viwete wanakwenda, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa habari njema. 6 Naye heri awaye yote asiyechukizwa nami. 7 Na hao walipokwenda zao, Yesu alianza kuwaambia makutano habari za Yohana, Mlitoka kwenda nyikani kutazama nini? Unyasi ukitikiswa na upepo?
8 Lakini mlitoka kwenda kuona nini? Mtu aliyevikwa mavazi mororo? Tazama, watu wavaao mavazi mororo wamo katika nyumba za wafalme. 9 Lakini kwa nini mlitoka? Ni kuona nabii? Naam, nawaambia, na aliye mkuu zaidi ya nabii. 10 Huyo ndiye aliyeandikiwa haya, Tazama, mimi namtuma mjumbe wangu Mbele ya uso wako, Atakayeitengeneza njia yako mbele yako. 11 Amin, nawaambieni, Hajaondokea mtu katika wazao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji; walakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkuu kuliko yeye. 12 Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka. 13 Kwa maana manabii wote na torati walitabiri mpaka wakati wa Yohana. 14 Na ikiwa mnataka kukubali, yeye ndiye Eliya atakayekuja. 15 Mwenye masikio, na asikie.
ZINGATIA MSTARI HUU…12 Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni HUPATIKANA KWA NGUVU NAO WENYE NGUVU WAUTEKA
Angalia mstari huu ktk Kiingereza:
International Standard Version-"From the days of John the Baptist until the present, the kingdom from heaven has been forcefully advancing, and violent people have been attacking it
King James Bible-And from the days of John the Baptist until now the kingdom of heaven suffers violence, and the violent take it by force
Amplified Bible-(AMP)And from the days of John the Baptist until the present time, the kingdom of heaven has endured violent assault, and violent men seize it by force as a precious prize share in the heavenly kingdom is sought with most ardent zeal and intense exertion.
ZINGATIA MANENO HAYA YANAYOONYESHA HIKI KISWAHILI… ‘’’HUPATIKANA KWA NGUVU NAO WENYE NGUVU WAUTEKA’’’ nayo ni
…….. has been forcefully advancing, and violent people have been attacking it….
….. suffers violence, and the violent take it by force…..
…… has endured violent assault, and violent men seize it by force as a precious prize share in the heavenly kingdom is sought with most ardent zeal and intense exertion…..
Angalia tena haya…..….. ‘’suffers violence, and the violent take it by force’’….
Tafsiri ya moja kwa moja isiyo rasmi ya kipande cha juu hapo ni .....''Ufalme unaugua/pata fujo-fujo na vurugu na wenye fujo-fujo/vurugu wanauteka kwa nguvu'''
MASWALI YA KUJADILI:
MOJA: Je ni nguvu/force za Kiroho au Kimwili ambayo kwayo twateka Ufalme wa Mungu?
PILI: Violence-fujo-fujo/vurugu-vurugu gani izo Ufalme ume-suffer toka Yohana Mbatizaji hadi sasa? gani
TATU: Kwa nini Ufalme wa Mungu unahusishwa na Nguvu na kua na Mafujo-fujo ili kuutwaa?
NNE: Mtu afanye nini ili aonekane/awe wa aina ya ‘’the violent one’’ ili kuweza teka kwa force Ufalme?
Press on,
Edwin Seleli
![]() |
|
Seleli,
Biblia ina lugha yake. Najua unafahamu hilo jambo.
Mtu huokolewa kwa kuamini na kuendelea chunga imani yake. Hapa ndipo kuko changamoto. Twajuwa sote kama wakati wa agano, siyo imani iliokoa mtu. Wengi waliokoka kwani babu aliokoka, nk. Ina maana katika agano la kale si wote walijitaabisha ili waokoke. Lakini kwa kipindi hiki cha neema, kinachosemwa ni kuamini Yesu. Tusiwaze kama ni rahisi kuwa na hiyo imani na kuizingatia wakati Ibilisi naye anafanya kampeni yake. Ndio maana hiyo imani hupatikana kwa nguvu. Tukishika kama ni fujo nayo ni kweli kwani tanafanya fujo na Ibilisi, kumchapa mateke ili imani yetu ikamilike.
Otherwise, tukiwaza kama kuwa na imani ni jambo rahisi, ndipo tutajiswali kwa nini kutumia nguvu.
Ubarikiwe.
-------Message original-------
De : Seleli Edwin
Date : 06/26/14 02:30:20
A : strictlygospel
Sujet : HUPATIKANA KWA NGUVU NAO WENYE NGUVU WAUTEKA UFALME WA MUNGU TOKA ENZI ZA YOHANA MBATIZAJI HADI SASA! |
-- Tafadhali zingatia msingi wetu ni Neno la Mungu, Lengo letu Kuujenga mwili wa Kristo, kushirikiana, amani na upendo. Yeyote yuko huru kuchangia, kufundisha, kukubali kufundishwa sawasawa na Msingi wetu Mkuu Neno la Mungu. Kujiunga na Team ya Injili au Maombi wasiliana nasi kwa simu 0714 915 424. Tuma Email. strictl...@yahoo.co.uk Facebook:https://www.facebook.com/pages/Strictly-Gospel/363180289370 Blog: www.strictlygospel.wordpress.com Kujiondoa Kwenye Kundi Hili Tuma Email: strictlygospe...@googlegroups.com |
![]() |
--