JE TUNAOA/OLEWA
ILI KUTULIZA/KUSHINDA KABISA TAMAA YA MWILI AU KWA KUA kiakili,
kiumri, kijamii, kifamilia, kimpango wa maisha binafsi, ni wakati
umefika kufanya ivyo?
Imeandikwa...1Wakorinto. 7:1-9.... Lakini
kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila
mwanamke na awe na mume wake mwenyewe.Mume na ampe mkewe haki yake, na
vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake. Mke hana
amri juu ya mwili wake, bali mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya
mwili wake, bali mkewe.Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili
mpate faragha kwa kusali; mkajiane tena, Shetani asije akawajaribu kwa
kutokuwa na kiasi kwenu.Lakini nasema hayo, kwa kutoa idhini yangu, si
kwa amri.Ila nipendalo ni kwamba watu wote wawe kama mimi nilivyo;
walakini kila mtu ana karama yake mwenyewe itokayo kwa Mungu, huyu hivi,
na huyu hivi. Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni heri
wakae kama mimi nilivyo. 9 Lakini ikiwa HAWAWEZI KUJIZUIA, na
waoe; maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa
NOTICE pia
mstari wa 9-ktk Kiingereza..NIV...''But if they CANNOT CONTROL
themselves, they should marry, for it is better to marry than to burn
with passion.
Si ni kweli hapo Paul anashauri, kama mambo
yanakushinda, muda mwingi ni kuwaka-waka tu fire, full dreams, hamu,
hisia ziko sharp hazilalagi,temperature UP non stop, basi maliza kazi tu sasa yaani
oa/olewa?
Si ni ukweli pia indirectly/logically amesema pia kua kama unaweza kuji control, basi dunda tu na kazi ya Bwana na maisha?
Ni wakati gani kuwaka tamaa kutahusianishwa na swala la kuoa ili usiwake
na kupi ni kuwaka tamaa kwa kua tu ni mwili unakutumikisha au pepo basi kabisa
wala si maisha mapya ya rohoni?
Au ni ilimradi tu ukiwaka waka ma fire basi ndio malizia tu bora ujitwalie binti sayuni officially na kuoa?
Halafu inaonekana Wanaume sisi ndio nambari one kuwakawaka nini maana
Paul anasema na sisi kwakua amesema heri KUOA si kuolewa? so men wanawakawaka sana/haraka than women siyo?
Je ni kweli kua Waliooa/olewa waga hawawakagi katu kamwe tamaa maana kua ktk ndoa imemaliza kila ghasia?
Press on,
Edwin Seleli