KUSHIRIKI SIKUKUU ZA SERIKALI/NCHI/JAMII/KOO KWA MTU WA MUNGU

4 views
Skip to first unread message

Seleli Edwin

unread,
Jun 11, 2014, 7:17:29 PM6/11/14
to strictlygospel
Amani ya Bwana iwe pamoja nanyi enyi nyote,

Tunafanyaje kuhusu yafautayo…

MOJA: Ukoo/Jamii/Familia yako inafanya harusi au sherehe za Ukoo kuhusu aliyekufa, Dada yako anaolewa na wote hawajaokoka ila wanataka mchango wako na unajua kabisa mchango wako utahusika sana kununua vileo, mbuzi ya kuchinja ktk vichaka vya maBabu na Ma-Bibi walikolala huku maneno-maneno yakisemwa ya ibada fulani, Je uchangia harusi izo za ndugu zako na sherehe za Ukoo na family au kamwe usichangie hata kama ni Ndugu wa kuzaliwa tumbo mmoja?

PILI: Umejaa Roho lakini wewe ni Rais, Waziri, Mbunge, Speaker, Jaji, RC, DC, WEO, VEO na kuna shughuli za Mwenge-‘ibada ya Kisasa’ ya Miaka Nchi TZ au siku ya kuwakumbuka Mashujaa waliokufa kwa kusimama na kutoa heshima kwa Wafu waliolifia Taifa ktk Mapigano ya Uhuru au Kiongozi Mkuu alikufa juzi, week ijayo tunaanza kikao lakini kabla wote kusimama kwanza kwa dk chache kumkumbuka/ombea nk? Kwa nafasi/cheo chako, ufanyeje? Usishiriki/ususie/uombe udhuru? na ni mpaka lini utaomba excuse ukiwa ni Kiongozi Msimamizi au mhusika sana wa jambo hilo mfano liko Chini ya Wizara au eneo lako la Utawala?

Tafakari yangu Kibinadamu: Isije ikawa Mungu haturuhusu wengi wetu kupanda juu na kua ktk mamlaka za maamuzi au uwajibikaji Mkubwa maana anajua itakua ngumu sana kuwa wasafi 24/7 na siku ile ikatukuta kama mwivi ajapo bila taarifa ivyo kwa kua anatupenda na hataki kutupoteza Jehanum basi atahakikisha hata kama utaomba na kutaka sana, itabaunsi tu,mmh! Ila sijui ni kweli? Maana mbona tumehaidiwa kua vichwa and mbona tuna akina Yusufu, Daudi, Daniel na wenzake? ILA, twende mbele turudi nyuma tena, kua mbona pia ni kweli uko juu kuna unajisi Nje nje?-Daniel aligomea hata aina ya vyakula sembuse kusaini mikataba, kuachia pesa kwa shughuli tokana na shinikizo la Wakubwa kwa haya ma-sherehe na sikukuuu ukiwa kama Wewe Waziri wa Fedha, Gavana wa BOT aliyejaa Roho?

Tutafakari na kuelimishana kwa Neno pia Akili/Ufahamu Bwana amekupa na hata Uzoefu nao, sawa kabisa.

Press on.

Edwin Seleli
Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages