TATIZO SI TATIZO KUWEPO BALI IMANI KUTOKUWEPO

464 views
Skip to first unread message

SELELI EDWIN

unread,
Oct 21, 2013, 9:15:30 AM10/21/13
to strictlygospel
Greetings in Jesus name,

Wakati mwingine kuwepo kwa matatizo, vikwazo, madhila ya maisha,
maudhi, mambo mabaya, magumu yanayotukwamisha kukua na kumfanania
Kristo zaidi, yanayoharibu maisha au huduma hata kupelekea kukosesha
raha, vuruga amani, nyima furaha, katiza tusisonge mbele, ni
udhihirisho wa KUTOKUWEPO KWA IMANI KABISA AU IPO LAKINI IMEPUNGUA!!
Kwa mantiki iyo, si Mungu, wala Wanadamu wenzetu na hata Shetani wa
kulaumu!


Imeandikwa:

Luka.17:5-6…’’Mitume wakamwambia, Bwana, TUONGEZEE imani. Bwana
akasema, KAMA mgekua na imani kiasi cha chembe ya haradali,mgeuambia
Mkuyu huu, Ng’oka ukapandwe baharini, nao ungewatii’’( unaweza soma
maneno yote ya Bwana na Wanafuzi ktk mistari 1-10)
Mathayo.17:20… ‘’Yesu akawaambia, Kwa sababu ya UPUNGUFU WA IMANI
YENU. Kwa maana, amin, nawaambia, MKIWA NA IMANI kiasi cha punje ya
haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka;
wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu’( unaweza soma maneno yote
ya Bwana na Wanafuzi ktk mistari 14-21)


Marco.9:24…. Mzazi wa mtoto akalia na kusema, Bwana Ninaamini,
NISAIDIE KUTOKUAMINI KWANGU( unaweza soma maneno yote ya Bwana na
Mzazi na Wanafuzi ktk mistari 14-29)

Ufafanuzi Kwa baadhi ya Maneno ya Maandiko muhimu kwa somo hili:

Chembe ya haradali ni sawa na kusema mbegu ya haradali, inaweza
fafanishwa na chembe ndogo kama ya mbegu ya mchicha au chini ya iyo
kwa ukubwa)

Mkuyu/Mlima- lugha- picha kumaanisha ugumu wa jambo/
tatizo/kikwazo/jambo la kuondolewa nk

KWA NINI OMBI LA TUONGEZEE IMANI? Wanafunzi walisema, Bwana TUONGEZEE.
Bila shaka waliona alilofundisha Yesu kuhusu Kusamehe ndugu
aliyekukosa mara 7 kwa siku moja ni ngumu mno kulitekeleza,
wakajiona/pima kisha kujua/jisikia kwamba hawana imani ya kutosha
kutembea ktk viwango ivyo vya kimo na kina alichoeleza Kristo
kuhusu kusameheana ndugu kwa ndugu.


KWA NINI KILIO CHA MZAZI KUA NINAAMINI, NISAIDIE KUTOKUAMINI KWANGU?
Ni kwa sababu kama mzazi alikua na uchungu sana/upendo wa dhati kwa
mwanae( Mwandishi Marko anasema, Mzazi alipiga kelele kwa sauti
AKILIA(fikiri mwanaume mtu mzima tena mzazi kulia hadharani kwa sauti
ya uchungu ya juu!!!!), kwaiyo ilikua ni msiba mkuu kama Yesu
angezingatia kasoro ya kiwango cha imani na kuacha kumsaidiia
mwanae, ukizingatia pia tayari alishaona dalili za kurudi nyumbani
kwa huzuni kubwa kwa kuendelea kuyashuhudia mateso ya mwanae kwakua
Wanafunzi nao hawakua na imani ya kutosha ivyo walishafeli mara ya
kwanza kumtoa pepo. Kilio cha ‘Ninaamini, nisaidie kutokuamini kwanga’
ni sawa na kusema, ‘’Bwana kwa kweli nisaidie tu hata kama imani yangu
haitoshi, nakusihi, nihurumie na ufanye Wewe kama Wewe,
usiiangalie/zingatie imani yangu maana haina viwango/haitoshi/ina
kasoro na kuna hatari TATIZO LIKABAKI KWA MWANANGU!


KWA NINI WALIULIZA KUSHINDWA KWAO KUTOA PEPO na Bwana kutofurahia
kushindwa kwao na hata kuwaambia kwa ukali/masikitiko kua
achukuliane/kukaa nao hata lini? Bila shaka walijisikia aibu/vibaya,
kwanza walishitakiwa(shushwa hadhi/chongewa/aibishwa fulani ivi) na
Mzazi kua walishindwa kumponya mwanae na kibinadamu hakuna anayependa
kushindwa-shindwa mambo, pili, karipio/lalamiko la Yesu kwa wao
kutokua ktk kiwango maridadi kuweza fanya ya Mungu, liliwachoma
ndani(pata picha hii- kulalamikiwa/shangawa na Bosi/Mkuu wako
unayempenda sana na kumuheshimu kiasi kwamba uko tayari kuishi maisha
ya kukekesha ili uwe makini kuhakikisha haumuudhi au kumkoroga Mkuu
wako huyo akachukia na kukuona bure kabisa, pia kibinafsi kama Watu
wapendao kuukulia wokovu na huduma, walitamani waweze mambo/kazi za
Mungu(ni raha kuweza jambo) na mwisho, walishangaa vipi kwa Yesu
imekua rahisi kiasi kile kutimua pepo yule na ivyo wakataka kujua
siri ni nini hasa!


Bwana Yesu anaonyesha wazi kua kama imani ingekuwepo ngaa kwa kiasi
kidogo sana sana, Mlima/Mkuyu- ungeng’oka/ungetii, yaani ugumu wa
jambo/tatizo/kizingiti/kushindwa jambo kungefutika kama imani ipo tena
ya kiasi kidogo kwelikweli, wala si kubwa sana kama mlima!


Biblia inasisitiza kua kua pasipo imani HAIWEZEKANI kumpendeza Mungu
–Waebrania.11:6a, ukiondoa Imani kwa Mungu basi mahusiano yetu na Yeye
yatakua magumu mno na yasiyo na udhihirisho wa ukuu wake kwetu. Mungu
MKUU SANA na MWENYE UWEZO WOTE na ANAYEWEZA KUFANYA CHOCHOTE-
Ayubu.42:2a maana kwakwe hakuna lililogumu la kumshinda na hakuna
litakalokua haliwezekani-Luka.1:37, bila kua na imani, atabaki Mungu
mwenye sifa za kutisha kama izo lakini hazina tija ktk maisha yetu ya
Kimwili na kiroho. Bado Milima na Mikuyu itasimama/ zingira/
vuruga/tesa/ kaba/rarua /haribu/funga/zuia mambo yetu na kumbe tatizo
si Mungu wala shetani bali SISI. Katika changamoto/misiba mingi
tuliyonayo/ tunayokutana nayo(Mikuyu na Milima), Hakuna JINSI TUNAWEZA
MLAUMU/SUKUMIA MZIGO MUNGU BABA-discredit God -kwakua kashafanya na
kutupa mengi tunayohitaji ili kuishi juu ya matatizo na si ndani au
pamoja nayo yakitukaba kila leo kama si kila mara. Ifike wakati
Tumwamini Mungu na kua na imani naye kisha kusambaratisha kila
kinachotunyima raha ktk maisha haya haya aliotupa Bwana kabla ya
kuondoka. Tunapaswa na ni haki kufurahia pia hapa hapa chini kabla ya
kula furaha kuu JUU.


Kama Hatuna Imani kwa Mungu au iko pungufu na hatufanyi lolote
iongezeke, au pengine tunamwamini kwa baadhi ya mambo na mengine
tunasitasita na kutia shaka au tunamwamini kwa muda kisha kuzimia
moyo/roho, hakika tatizo kweli litakua tatizo na litabaki kua tatizo
haswa.

Mungu anisaidie/atusaidie sana, Amen.

Press on,

Edwin Seleli

Daniel Nzali

unread,
Oct 23, 2013, 4:15:21 AM10/23/13
to strictl...@googlegroups.com
 Ni Kweli Mtumishi, Ubarikiwe kwa somo zuri.

Imekuwa ni kawaida ya Kibinadamu, inapotokea ukiwa unapitia katika hali ngumu sana, akili inafikia sehemu inaanza kukuondoa katika kuamini kuwa Mungu anaweza kufanya na unajikuta taratiiiibu unaanza kutafuta ufumbuzi kwa njia za kibinadamu ambazo  mara nyingine zinakuwa hata za kumkosea Mungu.

Suala la kutokuwa na Imani ni changamoto kwa tulio wengi, Tumekuwa tukikiri tu kwa kinywa kuwa Mungu anaweza, lakini Imani hiyo haina mizizi katika Mioyo yetu.Pasipo Imani kumpendeza Mungu ni ''0''.  Tumekuwa tukiangalia ukubwa wa Matatizo yetu badala ya kuwa na Imani kuwa Mungu anaweza yote. Yeye anasema Hutengeneza njia pasipo na njia. ''Kwa Imani'', pale inapofikia sehemu Maji yako shingoni ndipo ambapo Mungu anahitaji kupewa nafasi ili aweze kujitwalia utukufu. 

''1 Wakorintho 10:13''

Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili. 

Tukiwa tumeokoka kweli kweli, Jaribu /Tatizo lolote tunalokutana nalo linatakiwa lisitutoe katika uwepo wa Mungu, maana lazima limekuja kwa sababu maalumu na ni njia mojawapo ya kutuimarisha Kiroho na pia kutuinua Imani hata Imani.

Ubarikiwe SELELI.






--
Tafadhali zingatia msingi wetu ni Neno la Mungu, Lengo letu Kuujenga mwili wa Kristo, kushirikiana, amani na upendo. Yeyote yuko huru kuchangia, kufundisha, kukubali kufundishwa sawasawa na Msingi wetu Mkuu Neno la Mungu. Kujiunga na Team ya Injili au Maombi wasiliana nasi kwa simu 0714 915 424. Tuma Email. strictl...@yahoo.co.uk Facebook:https://www.facebook.com/pages/Strictly-Gospel/363180289370

Blog: www.strictlygospel.wordpress.com

Kujiondoa Kwenye Kundi Hili Tuma Email:
strictlygospel+unsub...@googlegroups.com

SELELI EDWIN

unread,
Oct 28, 2013, 4:01:03 PM10/28/13
to strictl...@googlegroups.com
Daniel Nzali,

Brother, you inputs are valuable man of God, I am double blessed

Keep the fire coming bro


Press on
> strictlygospe...@googlegroups.com
>
> --
> Tafadhali zingatia msingi wetu ni Neno la Mungu, Lengo letu Kuujenga mwili
> wa Kristo, kushirikiana, amani na upendo. Yeyote yuko huru kuchangia,
> kufundisha, kukubali kufundishwa sawasawa na Msingi wetu Mkuu Neno la Mungu.
> Kujiunga na Team ya Injili au Maombi wasiliana nasi kwa simu 0714 915 424.
> Tuma Email. strictl...@yahoo.co.uk
> Facebook:https://www.facebook.com/pages/Strictly-Gospel/363180289370
>
> Blog: www.strictlygospel.wordpress.com
>
> Kujiondoa Kwenye Kundi Hili Tuma Email:
> strictlygospe...@googlegroups.com
>

Stephen Mabinza

unread,
Nov 3, 2013, 7:35:31 AM11/3/13
to strictl...@googlegroups.com

Mpendwa wangu Seleli,
 
Uendelee sana kubarikiwa na Bwana wetu Yesu Kristo. Mimi hupenda sana kukufuatilia kila unapoonekana katika site hii huru ya SG. Ki ukweli fundisho ulilolileta hapa ni la pili kwa ukubwa likiongozwa na fundisho juu ya kanuni za wokovu!
 
Matatizo ni kinyume cha Amani, na matatizo ni moja ya kitu mhimu sana kinachoitofautisha hali ya Duniani na Mbinguni, aitha matatizo ndiyo hasa siraha ambayo shetani huitumia kutuangaminza, maana kwa matatizo wengi huliacha Neno; Mungu alivyo mtakatifu hafanyi wala hajichanganyi na kuwa sehemu ya matatizo ya aina yeyote!
 
Matatizo ya aina yoyote ile hutupata wakati Mungu akiwa na taarifa zote za kuanza na kumalizika kwa tatizo pamoja na matokeo ya tatizo husika. Lakini matatizo yoyote hutupata tokana na hila za shetani, katika namna mbili kuu, kwanza tatizo hufanikiwa kutukamata, kwa sababu ni ADHABU kutokana na kutotii Neno la Mungu, mfano huu utauona ukisoma, kitabu cha Mwanzo, kutoka, waamzi, hesabu, Joshua, wafalme nk. pili hutupata kwa lengo la Mungu kama MTIHANI ili Mungu atukuzike na mshindi apate kupanda  daraja, mfano wa hilo tunaliona kwa Ayubu; Ndiyo maana maandiko utayakuta yakisema “yeye ashindaye nitampa taji, au nitafanya kuwa nguzo ama nitampa jina…nk”!

Ieleweke wazi kuwa, matazizo ndiyo ndunia na kwamba huja si kwa zaidi ya tulivyo. Mfano matatizo hayawezi yakaja na nguvu za kishetani na kuzizidi nguvu za Mungu kiasi kwamba yakaweza kutushinda na hata kuhama katika IMANI ya Kristo mwenyewe (NENO)! Ikitokea hivyo, ndiyo ile unayoisema wewe Seleli kuwa ni Upungufu wa Imani, maana imani huja kwa kusikia, na kusikia huko ni kwa Neno la Kristo!.
 
Lakini hapa niweke sawa kwamba, uwe na Imani kubwa kiasi gani ama ndogo kiasi gani MATATIZO LAZIMA YAKUPATE, kama si kwa shetani kutumwa na Mungu akuletee basi ni kwa KIBURI na mamlaka yake shetani, kama mfalme wa ulimwengu! Wapendwa wengi, wapatwapo na matatizo hujikwamisha wenyewe na kuingia katika shida na kuishi kwa mashaka makubwa sana kwa sababu tu ya kutokuwa na ufahamu wa kutosha juu ya tatizo lililopo.
 
Ili kulimudu tatizo lazima uwepo ufahamu na maarifa ya kutosha juu ya Neno la Mungu, tatizo linapokupata ni lazima kwanza ujue aina ya tatizo pia umuulize Mungu ili ujue kama, linatokana na Mungu au ni la hira za kishetani, hiyo itakupa uhakika kujua kwanini lipo, ndipo utapata njia rahisi ya kushughulika na tatizo lako!
 
Wapendwa wengi, hukemea tu kila waonapo wenzi wao wana shida fulani au wao wenyewe wanapokuwa katika tatizo fulani.  tabia kama hiyo, huwatoa wengi katika kweli ya Mungu na kujikuta wakitangatanga kwenda kuombewa kila kanisa, wakidhani kuwa huyu wa kwanza hana upako ama hana karama vya kutosha kuing’oa shida ile! Wanasahau kuwa, Neno linasema “KILA MWENYE KUAMINI NA KUBATIZWA ATAMBATANA NA VIPAWA” Kuliacha Neno, ndiko hasa kutokuwa na Imani, na jambo lolote lisilo la imani Biblia inasema ni dhambi, na kama ni dhambi basi ni dhahili pia kuwa, Mungu hamsikilizi mwenye dhambi!
 
Lakini kabla mtu hajaanza kushughurika na shida ama tatizo linalomwandama ni lazima kwanza AMUULIZE MUNGU ili amfahamishe maana ya shida hiyo. Kutojua hivyo, kutamfanya mwenyeshida akazane kuomba na kuomba ili shida imuache bila mafanikio, kumbe shida ile imeruhusiwa na Mungu ili ikuweke vizuri maan yeye huwarudi awapendao. Ukisha jua maana ya shida ile kama ipo kama “mtihani” basi muombaji, hujua namna ya kusema na baba yake juu ya shida ile. La kama ipo tu kwa hira za shetani, basi, ni rahisi kama kumsukuma bata kwenye mto, ni kusema tu, tena mara moja pasipo kurudiarudia na bila hata mishipa ya shingo kukutoka “TOKA SHETANI KWA JINA LA YESU!”
 
Kukemea ama kuombea jambo ambalo tayari unalijua kunakuweka katika MAPENZI ya Mungu na hivyo kufanikiwa kwa urahisi na kwa mara ileile maombi hujibiwa. Tatizo linguine ilnalokuwa ni dhahili ni la kutokuwa na imani ni Kuombea ama kukemea jambo moja kwa kurudia rudia,utasikia, “kwa jina la Yesu pepo toka, nakwamru toka katika jina la Yesu, toka sasa hivi katika jina la Yesu, toka nenda kuzimu katika jina la Yesu nk” Kwanza uelewe kuwa shetani haishi kuzimu kumrudisha huko na tayari kulishafungwa ni kujidanganya, pili kukemea jambo ambalo Mungu ameruhusu liwepo kama mtihani ni kupoteza muda, kwani jambo kama hilo lipo na litaondoka kwa wakati unaokubaliwa. Ni vema kufahamu kuwa, usipokuwa sawa sawa na Neno, Mungu hatendi, ndipo shetani hufurahi, maana analijua Neno!
 
Sababu nyingine inayodhibitisha kukosekana kwa Imani ni kule kutazamia matokeo ya kuomba ama kukemea kuonekane mara ile, papo kwa papo, Neno linasema, “mkiomba aminini kuwa mmekwishapata na tayari yamekuwa yenu” Tunapoomba ama kukemea si juu yetu jibu litokee pale pale ama baadaye,swala la lini itimie ama ni kwa namna gani itakuwa si letu, Biblia inasema “si kazi yenu kuujua wakati wa Mungu”
Kwa hiyo Tatizo haliji wala halitegemei muda wa kudumu kwake eti kwakuwa huna Imani ama una Imani haba, lipo, litakuwepo na litatoka kwa wakati wa Mungu na kwa sababu zake maalumu. Biblia inasema, “Majaribu hayanabudi kuwako, lakini si kwa kumzidi mwamini”
 
“Ufahamu ni chembe ya uhai!”
 
Mabinza LS.
 




> strictlygospel+unsub...@googlegroups.com

>
> --
> Tafadhali zingatia msingi wetu ni Neno la Mungu, Lengo letu Kuujenga mwili
> wa Kristo, kushirikiana, amani na upendo. Yeyote yuko huru kuchangia,
> kufundisha, kukubali kufundishwa sawasawa na Msingi wetu Mkuu Neno la Mungu.
> Kujiunga na Team ya Injili au Maombi wasiliana nasi kwa simu 0714 915 424.
> Tuma Email. strictl...@yahoo.co.uk
> Facebook:https://www.facebook.com/pages/Strictly-Gospel/363180289370
>
> Blog: www.strictlygospel.wordpress.com
>
> Kujiondoa Kwenye Kundi Hili Tuma Email:
> strictlygospel+unsub...@googlegroups.com

>

--
Tafadhali zingatia msingi wetu ni Neno la Mungu, Lengo letu Kuujenga mwili wa Kristo, kushirikiana, amani na upendo. Yeyote yuko huru kuchangia, kufundisha, kukubali kufundishwa sawasawa na Msingi wetu Mkuu Neno la Mungu. Kujiunga na Team ya Injili au Maombi wasiliana nasi kwa simu 0714 915 424. Tuma Email. strictl...@yahoo.co.uk Facebook:https://www.facebook.com/pages/Strictly-Gospel/363180289370

Blog: www.strictlygospel.wordpress.com

Kujiondoa Kwenye Kundi Hili Tuma Email:

SELELI EDWIN

unread,
Nov 4, 2013, 5:28:59 AM11/4/13
to strictl...@googlegroups.com
Brother Mabinza,

Kwa kweli Sifa na Utukufu toka moyoni anakoniona Bwana hata sasa,
namrudishia kwa yote mema uliyosema, appreciation yako ina nguvu sana
na inatia moyo….kusema unapenda kunifuatilia kila nitokeapo humu SG,
imeniingizia moyo kufanya zaidi nikijua kumbe, sipotezi muda, bali
nahudumu kweli na wako mnaopenda na kusoma. Muulize Mwandishi au
anayeshea mambo yoyote kwa halaiki, anapopata feed- back, kama yuko
free and open guy kama mie, atakuambia bila kupoteza muda kua ina raha
sana na inatia moyo mno, so excellent bro kwa roho yako njema ya
appreciation na congratulation kwa participation yako ktk kuumega mana
hii.

Umetamka statements kadhaa, zina mafuta mazito, ni furaha
kuzirudia/kuzi-summary hapa kama msisitizo mzuri.

• Matatizo ya aina yoyote ile hutupata wakati Mungu akiwa na taarifa
zote za kuanza na kumalizika kwa tatizo pamoja na matokeo ya tatizo
husika

• Matatizo hayawezi yakaja na nguvu za kishetani na kuzizidi nguvu za
Mungu kiasi kwamba yakaweza kutushinda na hata kuhama katika IMANI ya
Kristo mwenyewe (NENO)!
• Ili kulimudu tatizo lazima uwepo ufahamu na maarifa ya kutosha juu
ya Neno la Mungu

• Lakini kabla mtu hajaanza kushughurika na shida ama tatizo
linalomwandama ni lazima kwanza AMUULIZE MUNGU ili amfahamishe maana
ya shida hiyo. Kutojua hivyo, kutamfanya mwenyeshida akazane kuomba na
kuomba ili shida imuache bila mafanikio, kumbe shida ile imeruhusiwa
na Mungu ili ikuweke vizuri maan yeye huwarudi awapendao..


• Ni vema kufahamu kuwa, usipokuwa sawa sawa na Neno, Mungu hatendi,
ndipo shetani hufurahi, maana analijua Neno!

Such above are great understandings Mabinza, bless u and glory to God,
keep flowing Man.


Pia Ubarikiwe kwa kwa kunivunja/unganisha mbavu zangu kwa hii…..
‘’Kama Tatizo lipo tu kwa hira za shetani, basi, ni rahisi kama
kumsukuma bata kwenye mto, ni kusema tu, tena mara moja pasipo
kurudiarudia na bila hata mishipa ya shingo kukutoka’’’…. Ha ha ha ha
ha, sometimes to be sincere with you Mabinza, kwa kweli mishipa
unitoka mie nikichachama! Lo! kumbe hamna haja! Ingawa sioni jinsi ya
kuing’oa pepo diplomatically/smartly nikishafyumu inavyometsa mtu hapo
chini jamani, da! Anyway, ndio tunafundishana ivyo new fashions


Labda kidogo tu Mtumishi Mabinza, unifafanulie hili…. ‘’Tatizo haliji
wala halitegemei muda wa kudumu kwake eti kwakuwa huna Imani ama una
Imani haba, lipo, litakuwepo na litatoka kwa wakati wa Mungu na kwa
sababu zake maalumu’’’

MASWALI:

(a)Mbona Neno linasema, Mkiwa na Imani kama chembe ya haradali,
mtauambia mlima(tatizo) ng’oka na utatii Au Mbona imeandikwa, Mkiwa na
Imani…HAKUTAKUWEPO LA KUSHINDIKANA kwenu/kwake aaminiye?


(b) Kama KUA NA IMANI haitatusaidia kitu bali mpaka Mungu mwenyewe
sababu zake maalumu ziishe/zikamilike kwa ilo lililotupata, kuna haja
gani ya kua na imani/kukazana kumwamini wakati kumbe Yeye
ana-timetable yake na mambo zake anti-clockwise na imani zetu hata
kama tunazo safi kabisa za kufyatua kila Mkuyu na Mlima mbele zetu?


Press on
>> strictlygospe...@googlegroups.com
>>
>> --
>> Tafadhali zingatia msingi wetu ni Neno la Mungu, Lengo letu Kuujenga
>> mwili
>> wa Kristo, kushirikiana, amani na upendo. Yeyote yuko huru kuchangia,
>> kufundisha, kukubali kufundishwa sawasawa na Msingi wetu Mkuu Neno la
>> Mungu.
>> Kujiunga na Team ya Injili au Maombi wasiliana nasi kwa simu 0714 915
>> 424.
>> Tuma Email. strictl...@yahoo.co.uk
>> Facebook:https://www.facebook.com/pages/Strictly-Gospel/363180289370
>>
>> Blog: www.strictlygospel.wordpress.com
>>
>> Kujiondoa Kwenye Kundi Hili Tuma Email:
>> strictlygospe...@googlegroups.com
>>
>
> --
> Tafadhali zingatia msingi wetu ni Neno la Mungu, Lengo letu Kuujenga mwili
> wa Kristo, kushirikiana, amani na upendo. Yeyote yuko huru kuchangia,
> kufundisha, kukubali kufundishwa sawasawa na Msingi wetu Mkuu Neno la Mungu.
> Kujiunga na Team ya Injili au Maombi wasiliana nasi kwa simu 0714 915 424.
> Tuma Email. strictl...@yahoo.co.uk
> Facebook:https://www.facebook.com/pages/Strictly-Gospel/363180289370
>
> Blog: www.strictlygospel.wordpress.com
>
> Kujiondoa Kwenye Kundi Hili Tuma Email:
> strictlygospe...@googlegroups.com
>
> --
> Tafadhali zingatia msingi wetu ni Neno la Mungu, Lengo letu Kuujenga mwili
> wa Kristo, kushirikiana, amani na upendo. Yeyote yuko huru kuchangia,
> kufundisha, kukubali kufundishwa sawasawa na Msingi wetu Mkuu Neno la Mungu.
> Kujiunga na Team ya Injili au Maombi wasiliana nasi kwa simu 0714 915 424.
> Tuma Email. strictl...@yahoo.co.uk
> Facebook:https://www.facebook.com/pages/Strictly-Gospel/363180289370
>
> Blog: www.strictlygospel.wordpress.com
>
> Kujiondoa Kwenye Kundi Hili Tuma Email:
> strictlygospe...@googlegroups.com
>

kadinari king

unread,
Nov 4, 2013, 10:51:27 AM11/4/13
to selel...@gmail.com, strictl...@googlegroups.com
Ubarikiwe kwa messeji yanye ujumbe mzuri

----------
Sent via Nokia Email
Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages