Re: Réf. : Re: KUPANDIKIZWA MBEGU ZA KIUME ILI WAPATE WATOTO KWA MABINTI WALIOOKOKA NA KUJITUNZA ILA UMRI MKUBWA NA HAWAPATI WACHUMBA/WAUME

10 views
Skip to first unread message

stephenmabinza

unread,
Jun 27, 2014, 9:55:27 AM6/27/14
to Seleli Edwin, strictlygospel
Mpendwa Seleli na Wengine,

Ni Kweli napatikana KWA kustukiza sana hapa SG, ninapingamizi kidogo. Likojambo ambalo Bwana ameruhusu lisimame hapo kati, nimekuwa na mgonjwa kwa takribani miaka 6 sasa, lakini KWA kipindi cha miaka 2 hii, anekuwa hawezi zaidi na hiyo yupo kitandani! Hata hivyo, naamini Bwana Yesu kristo atanipa nafasi ili nijibu japo kwa uchache hoja za Mzee Seleli. Naomba mnitazanie hivi karibuni,hata leo, nani aijuaye huruma ya Bwana kwa uhakika? Naam, ni Watoto WA BWANA!

"Ufahamu ni chembe ya uhai!"


Seleli Edwin <selel...@gmail.com> wrote:

Stephen Mabinza,

Yaani na wewe nimekosa sana-mmh! bora nimekumiss sana Kaka hapa SG live, good to see u meeen.

Sasa kuna vitu umeshusha hapa, ni mawe ya thamani mnoooo aisee, glory to God, see below.....

''''Umhimu wa Mtu kuwa na Watoto ama kutokuwa nao,anapaswa awe nao Mungu, na kujua wakati gani utapata mtoto nikujisumbua!''''......EXCELLENT POINT indeed brother.

'''Ibrahim alipomsikiliza mkewe na kujipatia Mtoto kwa akili ya mkewe, alipomtaka Mungu ampe Solution juu ya kumfukuza mkewe mdogo na mwanaye Ishmael watoke nyumbani kwa Sara kama alivyotaka Sara, Mungu alimjibu Ibrahim kwamba, MSIKILIZE MKEO SARA!'''.....wow! very very excellent observation/Ufunuo indeed man, dah!

''''Eva alipomsikiliza shetani, tunaona aina ya mtoto aliyempata! ...dah! a big question my friend aiseeee!

Ila kali mwenzangu, fafanua  '''''Mpango wa kukusanya mbegu ili "KUZIZINISHA" ni mpango wa kimapepo'''.....Nini maana ya kuzini? huwezi zini na vyombo vya hospitali bwanaaa au? tehe tehe apo Kaka lete nondo za uhakika, sijakupata kabisa.

''''Ukipandikizwa mbegu, kisha mimba ile ikaharibika, na ukarudi tena kupandikizwa, pale Benki watakuwa bado wana mbegu zilezile?''........kwani issue nini hapo? unapopandikizwa-ongezewa damu zikaisha, si unarudi tu bank ya damu, shida nini kurudi bank ya mbegu za kiume? kwani lazima ukute damu ile ile? aaaa bwanaaaa, hapo leta kitu cha uhakika Man.

''''''utakuwa umezinishiwa wanaume wangapi? Mapepo bwana, kazi ipo!''... Tena sema maana ya kuzini na mapepo hapo yako wapi wakati hii ni fani Watu wanasomea darasani vema tu kama vile kusomea kutibu pua, macho, moyo, magonjwa ya Wanawake nk?

Hakika tu-press on tukijua...''"Ufahamu ni chembe ya Uhai!" tehe tehe Mabinza bwanaa ako kakibwagizo kako ako sijui ulikatoa wapi? ka aina yakeee eeee? tehe, safiiiiii

Edwin Seleli


2014-06-19 4:42 GMT+03:00 Seleli Edwin <selel...@gmail.com>:
Gladys,

Wow! siku nyingi rafiki yangu, '''nimekukosa''....( mmmh! hata hainogi iyo nadhani hii ndio yenyewe..''Nimeku-miss'' sana hapa Kanisani aisee, ulitwaliwa kwa muda kwenda JUU ili urudipo uje kutujuza mambo mazito?  ha ha ha ha ha Gladys, bless u)

Back to business now... yaani I am telling you, hizi parts zako zifuatazo, zina nguvu mmmmmnooooo

''''kuwa kutokuamini ni dhambi sawa na uchawi ama uongo na uzinzi'''.... yaani UMEONYESHA KUMBE HASWAAAA TATIZO NI KUTOAMINI siyo? great Ufunuo/reasoning indeed hadi nimekumbuka Somo moja niliwahi rusha hapa...''KUTOMWAMINI MUNGU NI DHAMBI MOJA MBAYA SANA KULIKO TUNAVYOWEZA FIKIRIA,yup? unakumbuka? safi sana Gladys.

''''We ukisema 35yrs umezeeka je umri huo ni sawa na dk ngapi ktk kanuni ya Mungu ya miaka 1000=1day?, Wenzako tuna miaka ZAIDI ya hiyo yako lakini tumaini la ndoa liko palepale.'''....dah! we mdada mwebrania kiboko, yaani unakuaga muwazi kweli, maana mabinti sayuni wengi marafiki zangu Makanisani uko, kutaja au hata kuashilia ana miaka mingapi, weeeee ni hatari sana, NEVER WILL THEY DO THAT-tehe and ofcoz it is understandable u know, sasa wewe ni namba nyingine kabisa ya Bwana, umetandika tu haraka, una ujasiri na imani kuu sana, ubarikiwe mnoooo kwa kujitumia wewe kama teaching aid ku-cement hoja yako, hapo nimekukubali Mwalimu na Mwinjilist fire-fire wewe, Amen

Press on coming live hapa SG,

Stephen Mabinza

unread,
Jun 30, 2014, 4:33:41 PM6/30/14
to strictl...@googlegroups.com, Seleli Edwin

Pendwa Seleli na wote wengine,
Naona nisipoteze muda nianzie hapa, ili kujibu kama alivyonitaka Seleli aliposema,
“Eva alipomsikiliza shetani, tunaona aina ya mtoto aliyempata! ...dah! a big question my friend aiseeee!”
Kwa upande wangu sioni kama kuna swali kuu hapa, sote tunajua kuwa Shetani ni Muuaji, na Biblia inasema hivyo, lakini pia Biblia inasema katika Yohana kuwa, “Mwana hufanya ambayo alimuona Baba yake akifanya” Sasa kama Tunaliamini Neno la Mungu, basi tunakubali kuwa anayeua ni mwana wa shetani, kwakuwa inasemwa kuwa shetani alikuwa ni muuaji tangu mwanzo, kwa maana hiyo, hiyo ndiyo iliyokuwa kazi yake na anaendelea nayo hadi leo, kwa hiyo nategemea pia na watoto wake wafanye uuaji kama kzi ya nyumbani mwao, kazi ya Baba yao;  Kwa hiyo,  na Kaini mtoto wa kwanza wa Eva ni mtoto wa shetani, muuaji, maana alimuua nduguye!
Zaidi sana, hata katika wana wa Adamu, ukoo ule, Kaini hayumo! Basi, kwakuwa kila mwanamme hapa Duniani alizaliwa na Mwanamke, labda kama hatuliamini Neno, tumuulize Eva, alimpata wapi Kaini, mbona hafanani na Adamu ambaye hata Bwana Yesu aliona ni sifa njema kujiita “Mwana wa Adamu!”? (Lakini, Bwana Seleli, hivi hakuna sehemu katika SG blog tulipata kulisemea jambo hili la uzao wa nyoka, au linalofanana na hilo?! – hebu tukumbushe mkubwa, ili tupate kupaangalia tena.)
 
Jambo jingine  ‘jirani yangu’ mwema Seleli alisema,
 
“Ila kali mwenzangu, fafanua  '''''Mpango wa kukusanya mbegu ili "KUZIZINISHA" ni mpango wa kimapepo'''.....Nini maana ya kuzini? huwezi zini na vyombo vya hospitali bwanaaa au? tehe tehe apo Kaka lete nondo za uhakika, sijakupata kabisa.”
 
Iko siku, Yesu ali fanya Kikoto cha kamba na kuwatimua mbio watu waliojaribu kubadirisha matumizi ya Hekaru, liwe Soko huru! Tunajifunza nini tunapotaka kubadili matumizi ya hekaru ambalo ni Bibi Harusi wa Kristo kwa kupandikiza mbegu za uzazi ambazo hazitokani na Mme halali wa mhusika? Je, hujapata kusoma pale ambapo Mwanamme mmoja alipotakiwa kumuinulia uzao nduguye, ambaye alifariki bila kuwa na uzao, yeye alipofanya tendo la ndoa akazimwaga chini zile mbegu badala ya kuziacha zipenye ndani ya lile tumbo la Yule mama,  kilichompata ulikiona? Alikufa palepale! Sasa huoni pia waliotoa mbegu zao na kuziweka Benki badala ya kuzipenyeza katika matumbo ya wake zao, isiwe nao tayari walisha kufa?!
 
 Mwili wa mtoto wa Mungu ni Hekalu takatifu,  na hekalu hilo ni Bibi harusi wa Kristo, sasa unaonaje, ikiwa Bibi harusi hafanyi ambavyo Bwana harusi atakavyo, je, Bibi harusi huyo anafaa kuwa mke wa Bwana harusi mtarajiwa? Bibi harusi akiingiza mbegu zisizotokana na huyo Bwana harusi, na Bwana Harusi akamuona Yule Bibi harusi wake ni mjamzito, huku Bwana harusi Yule anayo hakika kabisa kuwa hajawahi kumuingilia mkewe mtalajiwa huyo, Bwana harusi Yule hatomwacha? Hebu isome ile habari ya Yusufu na Mariamu kwanza; inatufundisha nini, kuhusiana na Kristo na Kanisa?
 
Mwisho , Seleli kasema huku akichekacheka kuwa,

“Ufahamu ni chembe ya Uhai!" tehe tehe Mabinza bwanaa ako kakibwagizo kako ako sijui ulikatoa wapi? ka aina yakeee eeee? tehe, safiiiiii”
Nikwamba kibwagizo kile ni Neno la Mungu, kinatoka na  Zab. 119:104, ukiuchukia uongo, utaupenda ukweli na ukiupata ukweli unakuwa huru kweli kweli, na aliye huru ni mtu hai! upo seleli?
 
“Ufahamu ni chembe ya uhai!”
MABINZA  LS.


Press on coming live hapa SG, --
Tafadhali zingatia msingi wetu ni Neno la Mungu, Lengo letu Kuujenga mwili wa Kristo, kushirikiana, amani na upendo. Yeyote yuko huru kuchangia, kufundisha, kukubali kufundishwa sawasawa na Msingi wetu Mkuu Neno la Mungu. Kujiunga na Team ya Injili au Maombi wasiliana nasi kwa simu 0714 915 424. Tuma Email. strictl...@yahoo.co.uk Facebook:https://www.facebook.com/pages/Strictly-Gospel/363180289370
 
Blog: www.strictlygospel.wordpress.com
 
Kujiondoa Kwenye Kundi Hili Tuma Email:
strictlygospe...@googlegroups.com


Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages