Salome,
Nimamalizia ushuuda wa kupata kazi..
kwa mpango na nyakati za Mungu hata kama tumeshafanya na kutaka kweli kazi kwa nyakati zetu na kwa namna yetu njema tu kama wanadamu wengine.
Hatimaye Mkaka alichoka kuaapply na akaamua kuacha kabisa, akamwambia Mungu ivi, ''sitaapply tena na kama jitihada za kibinadamu, nimefanya kwa uaminifu na nguvu zote ikifika wakati utaamuru mtu mmoja uko na uko maofisi mengi barua zangu zilipokwenda au utajua ufanyaje nini kama Mungu si tena jitihada zangu za kibinandamu mana nimefanya sana na nimefell''. Kweli akacha kuaaply, na akatoa muda mwingi ktk huduma kanisani na kusema kweli alishai maisha ya kubangaiza, mara wapendwa kuguswa, mara yeye kuwagusisha, mara dayworker, mara, siku nyingine anakula mlo mmoja na wakati mwingine analala ivyo mpaka kesho yake. Kukiwa na maombi ya mfungo ya siku 7 kufungua jion tu kwa uji, inakua kwakwe sherehe maana imeondoa officially bajeti rasmi ya kula na jioni ile wapendwa hawawezi kufungua kunywa uji bila kuguswa na kutoa ofa. Siku zikapita wa akiwa anaendelea na huduma ndani na nje ya kanisana. ikatokea mpendwa mmoja akamjia na kumwambia kua ''amesikia kuna NGO moja inatafuta vijana wadogo wa form 4,6 labda kidogo na Diploma kwenda kufanya survey ya mwezi Wilaya moja wapo magharibi mwa Tz, unaonaje ukajaribu tu ktk interview,hata wakikukataa, upoteze kitu''. Kwakua Mkaka alishazidiwa sana na hali ya maisha, akujali level yake ya shule/status wala umri wake kua mkubwa kwenda kujichanganya na watoto. Akaenda na cha kwanza akakutana nacho nje pale ni baadhi ya wanafunzi wake aliowafunisha wajati anajishikiza hapa na pale, wakashangaa kweli na hata kucheka kirafiki wakiuliza ...'''aah! teacher..na wewe umekuja huku kuvizia chance za madent wako, aaa teacher bwanaa'', ili kuondoa aibu, Mkaka Mwalimu akachekacheka tu na kuzugu ivi kisha kuwapigisha story ili waachane na ile topic na alifanikiwa.
Katika interview panel..umri wake, vyeti vyake ilikua kama kituko kidogo walimwona! ni kama waikua wanasema uyu naye vipi, amekwendaje mtu mzima ivyo kwa kikazi kilicholengwa kwa watoto-anasema aliona sura zao wazi kabisa zinamwambia ujumbe huo-lakini akajikaza tu. Ajabu, hawakumfanyia usaili bali wakamwandikisha moja kwa moja na kumfanya supervisor wa surveyors/watoto wote. Kabla ya kuondoka Dar, mkaka aliitwa na Mzee wake wa kinisa
anayemfahamu mkaka vema, akamwambia statement hii. Ninasikia moyoni
kukuambia kua ''si kila wakati utahitaji kusema sana kujitetea, wakati
mwingine kaa kimya, usiongee kitu hata kama unaonewa, mpe Roho wa Mungu nafasi akunong'oneze nini cha kusema na kisha angalia Bwana anavyokutetea'''..Mkaka alikodoa
macho na kujiuliza kwanini Mze amemwambia ivyo? akamuuliza Mzee,
''kwanini amemwambia ivyo, akajibu, ''mimi sijui lakini kwamba Roho
Mtakatifu amesema nikuambie ivyo, ilo nina uhakikia nalo kabisa', basi mkaka
akaomba maombi, akamukea mikono na Mze wa kanisa akaomba kisha waachana,
mkaka akisumbuka na mafikra yake, kwanini Mze/RM aseme vile, kuna
nini/maana yake nini? lakini hakuna jibu.Wakaenda Wilayani, NGO ilikua inapokea ela toka shirika kubwa la Umoja wa mataifa kufanya kazi zake( NGO iyo ilikuani implementing partner wa Shirika la umoja wa mataifa). Kabla ya kutoka Dar es Salaam, baadhi ya watoto wale, wanandugu kule shirika la UN na waliwaambia ela wanayotakiwa kupewa baada ya mwezi mmoja kwa kazi ile ni laki 9 kila mmoja ata wakawapenyezea contract paper copy ya shirika na NGO ile.Badala ya kufanya kazi mwezi, NGO ile ikawapigisha kazi haraka-haraka, over worked mpaka usiku na kwa week 2 tu kazi ya mwezi kwisha. vIjana wale na Mkaka mkubwa wakafurahi kweli kua wamepiga kazi kwa muda mfupi hata kama walikua wanachoka na kuchukia kumbe hatimaye imekua safi kwa kua wanawahi toka porini uko na kuja Dar-wengi walikua watoto wa jijni-maisha ya pori ilkua msalaba.
Kazi imekwisha, inabidi kurudi nyumbani. Siku ya kulipwa ujira na kuagwa ikafika, Wakaitwa wote kupewa pesa na kila mmoja anajua ni fungu tamu la laki 9, kumbe ile kufanyishwa kazi week 2 ilikua ila, wakasainishwa laki 6 na nusu! Kukazuka mtikisiko mkubwa, watoto wakatoa contract copy ya UN...ilikua kazi, Mkaka mkubwa akakumbuka matatizo yake ya ukoo, familia yao, miasha Dar, akakumbuka madeni na aibu zote, akaanza kuwasha moto mkali na alipotaka kuinua simu kupiga Shirina la UN, ghafla akakumbuka..''''si kila wakati utahitaji kusema sana kujitetea, wakati
mwingine kaa kimya, usiongee kitu hata kama unaonewa, mpe Roho wa Mungu
nafasi akunong'oneze nini cha kusema na kisha angalia Bwana
anavyokutetea''', mmh! akajizuia na kukaa kimya.Hata wale watoto wakawa wana shangaa Mkaka Mkubwa/supervisor vipi, kimya kabisa ghafla. Watoto wanitwa kusign wachukue ela ile isiyo kamilifu, wakagoma, baadaye Coordinator wa NGO akasema, anayetaka fedha akasain, asiyetaka, aache na asilaumu mtu! lo! nani aache! taratibu,mmoja bada ya mwingine kimya kimya akaenda kusign. Wakawa wamekata laki 3 nzima kila kichwa NGO ile na mashirika shirikishi mengine-NGO's i.e implementing partners wa UN, wakaamua kufanya sherehe kubwa ya kuwaaga surveyors..ilikua ni zoezi kubwa ivyo liihusisha NGO 4 na surveyors wakutosha.Surveyors wakashirikishwa katika kuandaa sherehe , kila mmoja akapewa jukumu lakini kaka mkubwa akaombwa awe MC msaidizi. Jioni ikafika, ukumbi ukawa umejaa wakuu wote wa NGO's and Shirika la UN kati ya wageni waliokuja, walikua hawajui Kiswahili-kutoka Kenya, Uganda, Ethiopia Kazakstan. Sherehe ikawa haianzi, wanamtafuta MC mkuu apatikani na amezima simu. Kumbe alikua hajui Kiingereza na ilhitajita MC anayeweza lugha zote ili na wakubwa wajue kinachoendelea. Mc Msaidizi muagwa( Mkaka surpervisor)naye alichelewa kufika ukumbini na hata ivyo hakua na haraka kwa kua MC mkuu yupo,yeye aliwekwa ili mradi tu.. Ghafla Mc msaidizi akasikia sauti ya gari imekuja kasi sana na kufunga break za fujo nje ya nyumba kisha makele....Mkaka anaitwa atoke nje haraka kwenda kuendesha sherehe, nusu saa imepita , wakubwa wameshaka, kila mtu yuko tayari, MC mkuu hapatikani. Alikwenda Mkaka na akafanya u-MC kwa lugha zote Kiswahili na Kiingereza na pia manjonjo yote( usheshi, kushawishi, changamsha, stories,kukaribisha speeches, summarization ya wanayosema wakubwa nk). Baadae wakati watu wanasherekea na ni wakati wa DJ sasa na mambo yake MC main task imekwisha, akatoka nje kupumzika kidogo kisha kwenda kupumzika. Akiwa nje, Wakuu wa Mashirka wakawa wana toka, wakimkuta MC msaidizi, wanampongeza kweli kwa furaha na kusema ana kipaji cha ajabu cha kuongea na ku-entertain, ajabu zaidi Mkuu wa Shirika la UN akaenda mbele zaidi na kuuliza Mc anafanya nini jijini Dar, ana mpango gani anapoondoka kwenda uko nk! boss yule Mkazakstan akamuomba Mc-kua kama anaweza kwenda ofisini kwake kesho yake kwa maongozi kidogo
Alipofika ofisni, Boss akamwambia wazi..'''Ofisi yetu imekua kwa mwaka sasa inaandaa post na ofisi itakayohusu ''Taarifa kwa Umma'' na nimevutiwa sana na kipaji chako cha kuongea na kuwasilina na watu ktk sherehe ya jana, nimekuambia tu mpango huu wa ofisi kama rafiki, siyo official, usimwabie mtu.Halafu akamuuliza Mkaka, ''unajua kutumia computer? da! wakati mkaka anataka kutoka jasho ajibuje-( maana hata kuaaply on line ilkua jaribu kule internet cafe), Boss akamuuliza ile pale ni program gani? (anamuonyeshea kwenye computer yake on the screen), bahati njema Mkaka alishajua/kariri kua kunapotokea viboma-viboma/mistari mingi inayotengeneza tuvyumba kwa monitor, hua ni excell, so akajibu ni excel, Mzungu akafurahi na kusema '''aaaaa safi kumbe unajua akasema basi sawa, itakapofika wakati, utahitajika.Mkaka aliona ivi anaota, anaona maono au ni kweli! hakuamini kwanza kuingia ofisi kubwa kama ile kisha kuambiwa yeye ni rafiki wa Mzungu wakati ndio kwanza walikutana usiku tu ktk sherehe na kisha kuaminiwa kwa kuambiwa tip/ plan ya ofisi na kana kwamba hiyo haitoshi, akachukuliwa kwenda lunch ktk mgahawa mmoja wa bei ya juu Wilayani pale. Mkaka anasema, alivyokua amechoka namely nguo, viatu, kuingia na kukaa ktk gari ile safi ya VX za UN yenye mkonga wa satellite na mitambo ya ajabu ya radio call ndani, aliona kama anachafua vile au wataghairi ghafla na kumshusha, watoe gari jingine kumbeba.
Baada ya mlo, wakaagana, usiku NGO ile iliyowapa kazi, ikawapigia simu surveyors wote ku-report ofisini kabla ya kuondoka kila mtu na kwao. Walipofika, wakaambiwa wamapata maagzio toka UN agency kua, wanahitaji baadhi ya surveyors wabaki kusaidia NGO ile kuingiza data na ivyo, wanataka kuwafanyia interviews ili kupata hao wachache.Kesho yake usaili ukafanyika na kwakua ela waliyolipwa ilkua inaendlea kuishia ktk guest hata kusafiri to Dar bado, ikabidi waombwe watoe matokea siku iyo iyo.Wakaitwa na yakatangwa matokeo kua ni surveyors 4 wakabakizwa kama staff wa NGO ile na Mkaka akaambiwa '''yeye amepangiwa kazi nyingie si ktk NGO ile''. Wote wakatawanyika kurudi jijini. Maisha yakaendelea, ela waliyolipwa kule ikaisha kulipia madeni, sadaka, fungu la kumi, na kutuma nyumbani kidogo. Kukapita miezi 2 na nusu, Mkaka hoi, akawaza Mzungu amedanganya au alisema tu vile kwa changamko lake la nafsi? akajiuliza pia baada ya interview ile mbona aliambiwa kua amepangiwa kazi nyingine? kuna nini sasa tena? akaendelea na kazi ya Bwana, kanisani sana na kufanya vikazi vya hapa na pale na hata kujaribiwa kuanza tena upya kutafuta kazi. Akarusha barua tena nyingi kama mwanzo na akaedelea ivyo mara kwa mara. Sku moja anatembea pale manyanya, ghafla simu ikaingia, kuangalia ivi, akaona namba ya simu land line, kupokea, akasikia ''habari? naongea na Kaka fulani? ndio. tafadhari kuna dharura, unaweza ukafika makao makuu hapa UN agency? kama huwezi, usijali hata kesho!'' aisee! Mkaka akasema kidogo adondoshe simu(kupokea ujumbe toka UN agency)! ''sasa ivi naja''- akajibu mkaka.Alikua ana akiba ya alfu 5 mfukoni, hakaamua kuchukua taxi mara moja alfu 5 mpaka makao makuu pale na hakujali kama atarudije.. Alipofika, ofisi ya HR ofisa akaanza kwa dhati na unyeyekevu kweli kumuomba msamaha kwa kua wali-misplace email na kwamba walitakiwa wamwambie miezi miwili iliyopita kua anatakiwa awe ameshafika Wilayani kule kama staff mpya wa UN agency. Mipango ikafanyika haraka. Mkaka akafika na kuanzi kazi. Toka NGO ya nchini na U-mc to UN agency. Hakuwahi kuwaza kazi njema aliyokua anataka iwe ya viwango ivyo, wala kufikiri hata siku moja kua nagekuja kua na CV yenye History ya kufanya kazi na UN agency. Kazi ilitakiwa ifanyike kwa mkupuo mmoja ivyo ivyo alipewa miezi mitatu contract lakini kwa neema aliyompa Bwana na kwa kua post ile ilkua ndio imeundwa/mpya, ktk utendaji kazi akawa na bidii na creativities hatimaye miezi mitatu ikazaa miaka 2 na miezi 2. Mshahara aliokua anapata na mafao yake baada ya miaka 2 na miezi 2, ilifanya baraka kubwa kwa maisha ya mkaka, familia na ukoo wao pia ktk nyumba ya Mungu na watu wake sana. Aliweza kusomesha/kuchangia gahrama za Wachungaji 6, yatima mmoja toka shule ya msingi mpaka sekondari mbali na michango mingine Sehemu kubwa ya baraka hii, aliingiza ktk kazi ya Bwana na watu wake na pia watu wa nyumbani kwake..Mbaii na mshahara, safari tu nje ya kituo cha kazi kama akija DAR, kila akilala na kuamka, laki 1,50,000, Kgm laki 1,43,000, wakati mwingine unakaa nje ya kituo mwezi mzima au 2! Mungu ana njia ya kulipa yote kwa muda mfupi si lazima kufanya kazi maika 30 ndio upate sana, Bwana anaweza fupisha
Press on,( CONTRACT NA UN AGENCY ILIPOKWISHA, kawaida watu hurudi nyumba mara moja kuanza biashara na mafao wanayopata makubwa na kutafuta kazi nyingine na hasa ukiwa na Cv yenye kuonyesha ulishafanya na UN inaku na upako wa aina yake kama ukipenda kazi za kuajiriwa. Wakati anajiandaa kurudi, UN agency hao hao, MbInguni wakawakamata, wakafanya kitu cha ajabu kabisa, hakijawahi tokea na ni kinyume na utaratibu wa kawaida kwa UN system kote duniani, ilikuaje? nikipata muda tena nitakushuhudia jinsi gani uyo Mkaka Mungu alivyoamua kushughulikia mambo yake hata kama alipitia njia ya kukatisha tamaaa sana toka primary to Chuo to kutafuta kazi)
Fuatilia conclusion yangu ya maneno ya Mungu-nina-share maandko machache kwa next email mpendwa, nakutia moyo sana, sana kabisa, one day, you will write a book dada Salome hata kama unaona mbinguni kuko kimya, you will be suprised, a day is on the way kama ukikomaa na Bwana mpaka mwisho.