Watu wa Mungu;
Awalio ya yote nimshukuru sana Mungu kwa neema yake iliyo pamoja nasi katika kuishi kwetu kwa mambo ya rohoni na ya mwilini pia yaliyomilikiwa na nguvu ya Mungu!
Pili niwashukuru sana kiasi hapana maana niliona kusudi la Mungu duniani kupitia uwepo na harakati zenu kwa ajili ya maisha ya kila mmoja kiroho na kimwili pia maana ile karama ya Mungu kwa kila mmoja sawa sawa na alivyopatiwa hakika yaonekana kwa wema kabisa kabisa habari za Injili ya Kristo Yesu.
Naupenda udadavuaji wenu wa maswala mbali mbali napenda jinsi wengine wenu mlivyo wazamivu katika elimu hii ya Mungu napenda sana kwa jinsi muoneshavyo ya kuwa elimu hii ya Mungu imewakomboa katika mambo mengi.
Kwa hili sifa na Utukufu Jehova viwe vyake daima maana katika ninyi kwa namna mbali mbali kumeonekana ya kuwa ninyi kweli ni alama ya Kristo na Neno la Mungu.
Wapenzi; langu mimi kwenu na kwangu pia ni hili huu umahili wetu katika mambo yote yaletayo Uzima wa rohoni ili kuuhifadhi mwili na nafsi mbali na uangamivu usiishie katika namna ya kunena bali ikawe ni namna yetu dhahiri katika maisha yetu ya ndani na ya nje pia.
Maana kule kwetu kuwa alama ya Kristo hakutasomeka vyema mbele ya mataifa tusipoonesha ya kwamba sisi ni mbegu ileee ilivunwa katika mti ulee ulioota kutoka katika mbegu ilee iliyotoka mbinguni ili kuleta tofauti ya miche ya Mzabibu mwitu na Mzabibu mwema. Aaminaaa ???
Hapa ndani panaye thamani sana tena sana lakini ujifanyia uaminifu wewe toka ndani hata nje ili kile ukilacho na kujifunza mahali hapa kipate kuwa na nafasi ndani yako kuuteka ufalme wa uyapendayo mbali na elimu ya Mungu na kutawala ili kuyajenga yale yaliyo ya Mungu nawe ukapate kuishi ukiwa mwenye kheri duniani
Na watu wa mataifa wakaseme hakika huyu anamuishia Yesu Kristo.
Mbarikiwe sana!