TUSIIPUNGUKIE NEEMA YA MUNGU

914 views
Skip to first unread message

Patrick Kamera

unread,
May 2, 2013, 1:01:46 AM5/2/13
to strictl...@googlegroups.com
14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao; 
15 mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo. – Waebrania 12:14-15 SUV

Neno la Mungu linatuhimiza kutafuta kuwa na amani na watu wote kwa bidii tena bila kubagua, maana tukiishi kwa amani na wote wanaotuzunguka tutaweza kuwavuta kwa ushuhuda wa maisha yetu kwani sisi ni barua ya wazi inayosomwa na wote. Lengo kuu mojawapo la kuishi kwa amani na wote ni ili nao wapate fursa ya kuisikia Injili na kuokolewa, kwa maana tukiishi na majirani zetu kiugomvi ugomvi, kiukorofi ukorofi tutakosa ujasiri wa kuwashuhudia, licha ya kwamba tutawafanya waifunge mioyo yao washindwe kuipokea Injili toka kwetu. 

Yatupasa kuishi maisha ya utakatifu. Utakatifu wa Mungu hatuupati kwa kujitahidi kwa juhudi zetu kuzishika zile amri kumi, la hasha. Katika zama hizi za Agano Jipya, baada ya Bwana Yesu kukamilisha kazi ya kutukomboa na kutupatanisha na Mungu, tunavikwa utakatifu na Mungu mwenyewe kwa Neema yake tunapomwamini Bwana Yesu kama Bwana na mwokozi wetu. Roho wa Mungu ndani yetu anatuongoza katika njia za Haki kwa ajili ya jina lake, anaiandika sheria yake mpya ndani yetu, sheria ya Roho wa Uzima (Romans 8:2) na amri mpya ya Upendo (Yohana 13:34, 1 Yohana 4:19 -21). Utakatifu tunaupata toka kwa Kristo mwenyewe, kwani yeye alifanyika kuwa dhambi ili sisi tuweze kufanyika kuwa Haki ya Mungu (2 Wakorintho 5:21). Ndani yake sisi tunafanyika kuwa wana wa Mungu, watakatifu, watu waliotengwa mahususi kwa ajili yake ili tupate kuzitangaza sifa zake. Utakatifu ulioko ndani yetu utadhihirika katika mienendo yetu iliyojaa upendo, furaha na amani katika Roho Mtakatifu, na wale wasiomjua Mungu wataweza kumwona na kumfahamu kupitia sisi. 

Kuishi kwa amani na wote na kuwa na utakatifu vinawezekana pale tu tutakapohakikisha kuwa hatuipungukii Neema ya Mungu. Neema ya Mungu ni fadhila zake na wema wake ambao hatuustahili ila anatukirimia bila kikomo kwa sababu ya kazi kamilifu ya ukombozi aliyoifanya Bwana Yesu kwa kufa na kufufuka kwake. Katika Kristo tuna haki zote mbele za Mungu kama watoto wake wapendwa, tunao ujasiri wa kwenda mbele zake bila hofu, kwani dhambi zetu zilizotutenganisha naye Bwana Yesu alishazichukua zote katika mwili wake juu ya msalaba. Kwa hiyo leo hii vyote tunavyopokea maishani mwetu tukiwa ndani ya Kristo ni kwa Neema yake, siyo kwa jitihada zetu. 

Tunapojaribu kupokea chochote toka kwa Baba kwa jitihada zetu wenyewe tukidhani zitatustahilisha mbele zake tunaipungukia Neema ya Mungu na matokeo yake shina la uchungu linaanza kuchipuka ndani yetu, hasa pale tuwaonapo wengine wakibarikiwa na kufanikiwa “kirahisi tu” bila kufunga sana na kukesha sana wakiomba sana kama sisi. Tafadhali nielewe, kufunga, kukesha na kuomba kuna nafasi yake, lakini kamwe siyo vigezo vya kutustahilisha kupokea chochote toka kwa Mungu leo hii. Vyote tunavyovihitaji kwa ajili ya maisha haya na utauwa leo hii viko ndani ya Kristo na tunavipata kwa kuzidi kumjua sana yeye aliyetuita kwa utukufu na wema wake (2 Petro 1:3). Ahadi zote za Mungu kwetu sisi tulio katika Kristo ni ndio nasi tunasema amina na kuzipokea! 

Wapendwa tusiipungukie Neema ya Mungu na kuruhusu shina la uchungu lichipuke na kututia unajisi sisi wenyewe na wale wanaotuzunguka, na kama tunajikuta na hatia katika eneo hilo tusikubali adui atutese kwa kutujazia shutuma na hukumu tujione hatufai. Neno linasema ikiwa mioyo yetu inatuhukumu yeye ni mkuu kuliko mioyo yetu naye anajua yote kwa hiyo basi tusiendelee kulea shina la uchungu mioyoni mwetu tutubu kwa kukiendea Kiti cha Rehema ili tupate Neema na Rehema ya kutusaidia wakati wa mahitaji. Mbarikiwe! 

Kumbuka ya kuwa Baba yako wa mbinguni anakupenda sana na hataki ukose kupokea,kushiriki na kufurahia vyote alivyo navyo kwa ajili yako. Anayo makusudi mema na maisha yako. Mpendwa, Mungu yuko upande wako, hayuko kinyume nawe ndio maana anakuasa na kukutia moyo usiipungukie Neema yake. Kwa imani pokea wingi wa Neema na kipawa cha Haki upate kutawala pamoja Kristo (Warumi 5:17)

   Mungu na azidi kuwabariki, 

    Patrick

SELELI EDWIN

unread,
May 2, 2013, 9:09:30 AM5/2/13
to strictl...@googlegroups.com
Patrick,

This is straight forward brother,  in JESUS NAME,amen and amen, alleluya to God.

Blessings,

Edwin Seleli

2013/5/2 Patrick Kamera <pka...@gmail.com>

--
Tafadhali zingatia msingi wetu ni Neno la Mungu, Lengo letu Kuujenga mwili wa Kristo, kushirikiana, amani na upendo. Yeyote yuko huru kuchangia, kufundisha, kukubali kufundishwa sawasawa na Msingi wetu Mkuu Neno la Mungu. Kujiunga na Team ya Injili au Maombi wasiliana nasi kwa simu 0714 915 424. Tuma Email. strictl...@yahoo.co.uk Facebook:https://www.facebook.com/pages/Strictly-Gospel/363180289370
 
Blog: www.strictlygospel.wordpress.com
 
Kujiondoa Kwenye Kundi Hili Tuma Email:
strictlygospe...@googlegroups.com
 
 

Mathew Maduhu

unread,
May 3, 2013, 10:38:43 AM5/3/13
to strictl...@googlegroups.com

Patrick, Mtumishi wa Mungu,

Mungu akubariki kwa msg hii, inatupa angalizo na kujichunguza katika maisha yetu ya kila siku. Hata hivyo ili tupate full msosi, ninaomba uya-expand zaidi mambo haya matatu;

·        Moja ni Mambo gani yanayoweza kutufanya wapendwa tukajikuta tumeipungukia Neema ya Mungu,

·        Mbili ni nini  dalili zinazoonyesha kuwa mpendwa kaipungukia Neema ya Mungu, ili nizionapo niweze (kwa haraka) kumsaidia mpendwa mwenzangu,

·        Tatu ni kwa jinsi ipi mtu aliyeipungukia Neema ya Mungu anaweza kurejeshwa katika Neema hiyo.

Sitajali sana hata uwe ni mkeka kiasi gani!!! Naamini na wapendwa wana SG pia hawatajali. Natamani sana na ninausubiri mkeka huo kwa hamu.

 

Keep on digging

Mathew.

--

Tafadhali zingatia msingi wetu ni Neno la Mungu, Lengo letu Kuujenga mwili wa Kristo, kushirikiana, amani na upendo. Yeyote yuko huru kuchangia, kufundisha, kukubali kufundishwa sawasawa na Msingi wetu Mkuu Neno la Mungu. Kujiunga na Team ya Injili au Maombi wasiliana nasi kwa simu 0714 915 424. Tuma Email. strictl...@yahoo.co.uk Facebook:https://www.facebook.com/pages/Strictly-Gospel/363180289370
 
Blog: www.strictlygospel.wordpress.com
 
Kujiondoa Kwenye Kundi Hili Tuma Email:
strictlygospe...@googlegroups.com
 
 



This email and any attachments may contain confidential information for intended recipient only. If you have received this email in error please notify the sender. Note that any copying, disclosure or distribution of the message is strictly prohibited. Email recipient(s) should check this email and any attachments for viruses. Tanesco will not be liable for any damage caused by virus.

Patrick Kamera

unread,
May 4, 2013, 3:41:33 AM5/4/13
to strictl...@googlegroups.com
Amen! Mtakatifu Matthew ubarikiwe kwa hii changamoto uliyonipa, labda nianze kwa kuielezea kidogo Neema ya Mungu. Neema ya Mungu ni fadhila zake ambazo hatuzistahili ila Yeye Mwenyewe anatukirimia bure, hatuwezi kufanya chochote kitakachoweza kutustahilisha Neema ya Mungu. Neema ni tofauti kabisa na Torati au Sheria ya Musa.


Kaitka Sheria ya Musa, ukitii unabarikwa ukiasi unalaaniwa, katika Neema unabarikiwa kwa sababu ya kazi kamilifu ya ukombozi aliyoifanya Bwana Yesu peke yake na siyo kwa sababu ya jitihada zetu binafsi. 
Katika Sheria ya Musa, unahesabiwa haki ukiweza kuishika na kuifuata Torati vilivyo lakini ukija kwenye Neema unahesabiwa haki pale unapomwamini Mungu. Vilevile Neno la Mungu linasema tumeokolewa kwa neema:


Basi baada ya kuokolewa siyo kwamba neema ya Mungu imemaliza kazi yake, la hasha. Tunapaswa kuendelea kukua katika Neema hiyo maana ni Neema ya Mungu ambayo inatuwezesha kuishi maisha ya kumpendeza Mungu. 


Sasa ni jinsi gani tunavyoweza kuipungukia neema ya Mungu:

Neno la Mungu linasema:


Neema ya Mungu inafundisha namna ya kuenenda, tusipoitii au tukiitii nusu nusu tunaanza kuipungukia neema hiyo.

Tunapojaribu kuhesabiwa haki kwa juhudi zetu kwa kujaribu kuishika Torati ya Musa,  tunakuwa kumeipungukia neema yake, actually tunakuwa tumeanguka toka kwenye neema. To fall from grace is not to fall into sin as many think, no it is to fall back into trying to be justified by keeping the Law of Moses, something a Christian should never do.
 

Dalili za kuipungukia Neema ya Mungu:

Ukiona mtu aliyeokoka lakini kila kukicha anaangushwa na dhambi moja baada ya nyingine, hiyo ni dalili tosha ya kuwa neema ya Mungu haiko effective katika maisha yake, yaani ameipungukia yeye mwenyewe,notice, Neno linasema tusiipungukie neema siyo neema itupungukie, maana Mungu anatukirimia neema kwa wingi, nasi tunatakiwa kwa imani tuipokee kwa wingi itufanikishe katika kile ambacho Mungu amekusudia maishani mwetu.



Vilevile Mpendwa daima kujiona ana hatia mbele za Mungu, daima kujiona hakubaliki mbele za Mungu kwa sababu ya dhambi zake ambazo alishazitubu, Ile hali ya kujiona daima you do not measure up, you are not holy enough, you are not righteous enough, you are not good enough zote hizo ni dalili za kuwa mpendwa hajaielewa neema ya Mungu na jinsi inavyotenda kazi. 

Kaitka Agano Jipya Miungu ameshaahidi kuwa dhambi zetu hatazikumbuka tena kabisa, sasa wewe kwanini unaendelea kuzikumbuka? Katika Kristo Mungu anakuita wewe kuwa ni mtoto wake, mwenye haki zote za mwana wa Mungu, tena ametuketisha (past tense) pamoja na Kristo katika ulimwengu wa Roho juu ya falme zote na mamlaka (Waefeso 2:6), na tena umeunganishwa kuwa roho moja na Mungu (1Wakorintho 6:17). Sasa wewe leo kwanini ujione uko mbali na Mungu? Mara nyingi tunajiangalia sisi kama binadamu na mapungufu yetu halafu ibilisi anatunong'oneza tujisikie kuwa inabidi tujitahidi kwa nguvu zetu ili tukubalike mbele za Mungu wakati Mungu katika Kristo alishatukubali na alishatusamehe dhambi zetu. 

Kwa yule aliyeipungukia Neema ya Mungu: 

Ikiwa umeipungukia neema ya Mungu, hakuna formula ya kufuata, cha kufanya ni kwenda mbele za Baba yako akupandaye upeo. Amini ya kuwa Bwana Yesu alishazichukua dhambi zako zote katika mwili wake pale msalabani maana alifanyika kuwa dhambi ili sisi tuweze kufanyika kuwa Haki ya Mungu mbele zake pale tunapomwamini kama Bwana na Mwokozi. 


Baada ya kutambua ya kuwa umefanyika kuwa mweny Haki mbele za Mungu utakuwa na ujasiri wa kukikaribia Kiti cha Neema  na kupokea wingi wa neema, rehema na kipawa cha haki ili upate kuishi kwa ushindi


Kama kuna mtu ambaye angekuwa na sababu nzito ya kuipungukia neema ya Mungu basi ni Mtume Paulo, maana alilitesa Kanisa la Kristo, aliwaua na kuwatupa gerezani watu wa Njia Ile wengi tu. Sasa inagine kama angeruhusu majuto na hatia guilty feelings, shame and condemnation over his past sins, asingeweza kutumiwa na Mungu kwa jinsi alivyotumiwa. Aliliamini Neno la Mungu na akasonga mbele maana mwenyewe anasema hivi kwa habari za neema ya Mungu maishani mwake:


Naona niishie hapa, natumaini nimeweza kufafanua kidogo vipengele alivyovianisha ndugu Matthew. 

Tufuate mfano wa Mtume Paulo, neema ya Mungu na isiwe bure maishani mwetu, ituwezeshe kuyatimiza mapenzi ya Mungu.

Mbarikiwe watakatifu, 

Patrick.


2013/5/3 Mathew Maduhu <Mathew...@tanesco.co.tz>

SELELI EDWIN

unread,
May 4, 2013, 4:13:02 PM5/4/13
to strictl...@googlegroups.com
Patrick,

Amazing  and blessing Ufafanuizi indeed,....well, siku izi tunatumia phrase yako njema sana hii kua, bila kuharibu yale ya msingi na mazuri mno kuhusu Kutoipungukia Neema ya Mungu uliyofundisha  in details safi kabisa, najua ni Mathew Maduhu alikuuliza ufafanuzi na umemwa-address yeye, nonetheless ni  kwa SG wote na nimebarikiwa sana tu yet jinsi ulivyo eelezea Neema ya Mungu isivyo tupungukia na yale Bwana aliyotutundea sisi,  mtu anaweza dhani/chukulia kua/kuelewa kua umetufundisha  sisi hatuna part ya ku-play kua watakatifu, kukazana sisi kama sisi kupata ya rohoni/mwilini! is this all balanced? WHY asking this, see below:

''Kaitka Sheria ya Musa, ukitii unabarikwa ukiasi unalaaniwa, katika Neema unabarikiwa kwa sababu ya kazi kamilifu ya ukombozi aliyoifanya Bwana Yesu peke yake na siyo kwa sababu ya jitihada zetu binafsi. Katika Sheria ya Musa, unahesabiwa haki ukiweza kuishika na kuifuata Torati vilivyo lakini ukija kwenye Neema unahesabiwa haki pale unapomwamini Mungu. Vilevile Neno la Mungu linasema tumeokolewa kwa neema'', kwa kua tukishamwamini tunahesabiwa haki-kitu ambacho ni core ingredients ktk true faith yetu, why tena matendo yote haya tunayafanya eg kutoa, kufunga, kuomba, kujikana nafsi, kubebe cross, kujiepusha na ili na lie, kukataaa, kupinga, kuweka bidii ktk maswala kadhaa nk? where/how do we balance ukweli wa kwanza juu pale na huu wa pili, wapi yana-connect ili yasionekane ni vitu viwili tofauti au havihusiani kabisaaa ili hisije kueleweka visivyo tukabaki wazembe makanisani  kwetu uko na maisha yetu personal ya kumtafuta BWANA na nguvu zake tukapose tuuuu u know!


Pia ''Ukiona mtu aliyeokoka lakini kila kukicha anaangushwa na dhambi moja baada ya nyingine, hiyo ni dalili tosha ya kuwa neema ya Mungu haiko effective katika maisha yake, yaani ameipungukia yeye mwenyewe,notice, Neno linasema tusiipungukie neema siyo neema itupungukie, maana Mungu anatukirimia neema kwa wingi, nasi tunatakiwa kwa imani tuipokee kwa wingi itufanikishe katika kile ambacho Mungu amekusudia maishani mwetu''
.. who is responsible neema kutokua effective? who activates His/his neema ili mpendwa hasianguke anguke?


What about this one..''Tunapojaribu kuhesabiwa haki kwa juhudi zetu kwa kujaribu kuishika Torati ya Musa,  tunakuwa kumeipungukia neema yake, actually tunakuwa tumeanguka toka kwenye neema. To fall from grace is not to fall into sin as many think, no it is to fall back into trying to be justified by keeping the Law of Moses, something a Christian should never do'' While  i agree kwamba we are no more  keeping  m23  thing lakini si tuna sheria mpya? je izo hatupwashwi kukazani kuzishika ili kuhesabiwa haki? si unajua Yesu alisema haki yetu isipozidi ya jamaa wale wa m23, never will we enter up there?!


Press on,

Edwin Seleli



2013/5/4 Patrick Kamera <pka...@gmail.com>

Mathew Maduhu

unread,
May 6, 2013, 2:11:44 AM5/6/13
to strictl...@googlegroups.com

Kamera ya Bwana Yesu,

Asante kwa Fundisho la Mitume. Nimeelewa, nimepata kitu kamili na kubarikiwa kiukweli. Nime-copy na ku-paste. Barikiwa Mtumishi.

Keep on digging,

Mathew.

jwmsella .

unread,
May 6, 2013, 9:05:38 AM5/6/13
to strictl...@googlegroups.com
Kaka Patrick,

Mungu akubariki sana, tena sana, kwa kutushirikisha neno hilo. Ni mafundisho ya msingi ya Ukristo, lakini naweza kusema kuwa si wengi wetu tunaoelewa mambo hayo. Jambo hilo linadhihirika ukiangalia ni Wakristo wengi kiasi gani wanaosema wameokolewa lakini wanajaribu kutafuta kuhesabiwa / kujihesabia haki kwa kutii sheria fulani fulani - ama za enzi za Musa au mapokeo ya dini/madhehebu yao. Siyo siri, kwa kiwango kikubwa tunalikosa (we are missing) fundisho la mitume - ila tunakutana kila kona na mapokeo ya wanadamu ambayo yana sura na mfano wa nguvu za Mungu.

Sasa naomba nije kwenye swali la Seleli, naomba nitoe mchango wangu kama mwana SG na anayetafuta kulielewa "kusudi lote la Mungu" (Matendo ya Mitume 20:27). Ijapokuwa ni kama Seleli alilielekeza swali hili kwa kaka yangu Kamera, natumaini hatajali nikitoa my two cents hapa! Nitaenda taratibu na hatua kwa hatua.

Nianze kwa kunukuu aliyoandika Seleli:

"What about this one..''Tunapojaribu kuhesabiwa haki kwa juhudi zetu kwa kujaribu kuishika Torati ya Musa,  tunakuwa kumeipungukia neema yake, actually tunakuwa tumeanguka toka kwenye neema. To fall from grace is not to fall into sin as many think, no it is to fall back into trying to be justified by keeping the Law of Moses, something a Christian should never do'' While  i agree kwamba we are no more  keeping  m23  thing lakini si tuna sheria mpya? je izo hatupwashwi kukazani kuzishika ili kuhesabiwa haki? si unajua Yesu alisema haki yetu isipozidi ya jamaa wale wa m23, never will we enter up there?!" (msisitizo (bold) upo katika maandishi ya Seleli)

Tuanze kwa kuangalia maneno ya Bwana wetu Yesu Kristo ambayo wengi wetu tumekuwa tukiyaelewa tofauti na kusudi lake kwa ufahamu wangu mdogo.

Baada ya kufundisha kuhusu zile heri saba pale mlimani, Bwana wetu Yesu Kristo aliendelea na hotuba yake, akasema,

Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.  Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie.  Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.  Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.  Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu.  Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto.  Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako,  iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako. (Mathayo 5:17-24 SUV, msisitizo wa kwangu)

Neno la Kigiriki lililotafsiriwa "kutimiliza", kwa mujibu wa kamusi ya Strong (Strong's Hebrew and Greek Dictionary) maana yake mojawapo ni "to fill (up), (be, make) full, complete"; yaani, kufanya kitu fulani ambacho kilikuwa na upungufu fulani kuwa kamili. Ukiangalia maneno ya Yesu katika kifungu hicho hicho cha Maandiko utaona jinsi alivyoielezea hoja yake kwa kutumia mfano wa ile amri ya "usiue" (mfano soma Kutoka 20:13).

Waandishi na Mafarisayo waliielewa amri hiyo kwamba ilikataza kuua kwa jinsi ya mwili, kwa mfano mtu X anavyoweza kumchoma kisu mtu Y, na kusababisha roho ya Y iachane na mwili. Ni kweli amri hiyo ya torati ilimaanisha hivyo. Lakini Bwana Yesu alikwenda mbali zaidi na kuongezea kitu ambacho kilipungua katika amri hiyo (ili kuitimiliza - so as to make it full/complete) kwa kusema kuwa hata X akimkasirikia na kumtolea Y maneno makali bila sababu itampasa adhabu (Mathayo 5:22). Hapo X hata hajainua upanga au kumwonyesha kisu au bastola lakini tayari ana hatia sawa na yule ambaye amemchoma kisu au kumtwanga risasi mwenzake! Tuangalie Biblia ya Kiingereza inavyosema katika mstari huo:

But I say unto you, That whosoever is angry [become exasperated] with his brother without a cause shall be in danger of the judgment: and whosoever shall say to his brother, Raca [thou worthless as a term of utter vilification], shall be in danger of the council: but whosoever shall say, Thou fool [dull or stupid], shall be in danger of hell fire. (Mathew 5:22, emphasis and underlined translation from original Greek, according to Strong's dictionary, mine)

Kwa kuwa si nia yangu kutumia muda mwingi kuzungumzia kwa undani maana ya andiko hili na kuchambua maneno yaliyotajwa, nisema tu kwamba, mtu akimghadhibikia mwenzake na kumtolea maneno makali ya kumdhalilisha atakuwa na hatia sawa na yule aliyeua. Hicho ndicho kiwango ambacho hakikuwepo katika torati ya Musa ambayo ilikuwa inaangalia kuua kwa kutenganisha roho na mwili tu. Hiyo ndiyo tofauti ambayo Bwana Yesu alikuja kuikamilisha, maana katika torati ya Musa ilipungua. Na ndiyo maana tunasoma, "Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji: nanyi mnajua ya kuwa kila mwuaji hana uzima wa milele ukikaa ndani yake." (1 Yohana 3:15)

Waandishi na Mafarisayo walijihesabia haki kwa kuangalia ni kwa jinsi gani waliitii torati ya Musa (na walikuwa na mapokeo yao pia, lakini sitaki kwenda huko), lakini Bwana Yesu akawaambia wanafunzi wake - na ujumbe wake huo unatuhusu sote hivi leo ambao ni wanafunzi wake - kuwa haki yao haina budi kuzidi ile ya waandishi na mafarisayo.

Inaizidi kwa vipi sasa?

Haki yetu haiizidi haki ya waandishi na mafarisayo kwa kushindana nao katika kutii torati, la hasha, bali kwa kuhesabiwa haki na Mungu kupitia imani yetu katika Kristo Yesu (soma taratibu Warumi 3:10-30). Tunapohesabiwa haki, tunapata neema ya kuweza kufuata amri ya Mungu iliyo kuu, ambayo iko juu sana kuliko torati ya Musa. Amri hiyo ndiyo iliyoikamilisha torati, yaani, imejaziliza pale ambapo torati imeshindwa.

Bwana Yesu alisema:

Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo. (Yohana 13:34)

Tukirejea kwenye huo mfano wa amri ya kutokuua, ukitii amri ya upendo huwezi kumwua au hata kumghadhibikia mwenzako kiasi cha kumtolea maneno makali na ya kudhalilisha. Na ukiangalia kwa makini, ukimpenda mwenzako automatically hutafanya yale yanayopelekea kukiuka zile amri nyingine kama vile kumshuhudia jirani yako uongo, kutamani mke au mali ya jirani yako, nk.

Haki tunayohesabiwa kupitia Kristo Yesu ndiyo ya kiwango cha juu sana kupita ile ya waandishi na mafarisayo ambao walikuwa wakijihesabia haki kwa kupima ni kwa jinsi gani walikuwa wanatoa zaka, wanafunga, nk. Sisi tunapomtolea Mungu, kuomba, kufunga, nk kamwe matendo hayo hayatufanyi tuwe na haki zaidi bali yanatufanya tuweze kuwa kumtumikia Mungu kwa mali zetu na kuwa karibu naye katika ibada na maombi. Ni makosa makubwa kufikiri kuwa tunaweza kufanya matendo ya sheria ili Mungu atuhesabi kuwa ni wenye haki. Ndio maana mtume Paulo aliwaandikia Wakristo waliokuwa kule Galatia:

Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa?
Nataka kujifunza neno hili moja kwenu. Je! Mlipokea Roho kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imaniJe! Mmekuwa wajinga namna hii? Baada ya kuanza katika Roho, mnataka kukamilishwa sasa katika mwili?  Mmepatikana na mateso makubwa namna hii bure? Ikiwa ni bure kweli.  Basi, yeye awapaye Roho na kufanya miujiza kati yenu, je! Afanya hayo kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani?  Kama vile Ibrahimu alivyomwamini Mungu akahesabiwa haki.  Fahamuni basi, ya kuwa wale walio wa imani, hao ndio wana wa Ibrahimu.  Na andiko, kwa vile lilivyoona tangu zamani kwamba Mungu atawahesabia haki Mataifa kwa imani, lilimhubiri Ibrahimu habari njema zamani, kusema, Katika wewe Mataifa yote watabarikiwa.  Basi hao walio wa imani hubarikiwa pamoja na Ibrahimu aliyekuwa mwenye imani.
(Wagalatia 3:1-9, msisitizo wangu)

Mungu awabariki.

Joel


2013/5/6 Mathew Maduhu <Mathew...@tanesco.co.tz>



--
Love, the sum of whole law.

Patrick Kamera

unread,
May 7, 2013, 1:04:28 AM5/7/13
to strictl...@googlegroups.com
Edwin na wana SG wote,

Fundisho alilotoa Joel limetosheleza kabisa.

Labda niseme haya yafuatayo kwa kifupi tu: 

Kuokolewa kwetu kwa neema na kuhesabiwa kwetu haki kwa njia ya imani hakumaanishi ya kuwa sasa tubweteke tuu tusubiri kwenda mbinguni. Hapana kwani neema hiyohiyo iliyotuokoa inatufundisha kuikataa dhambi na pia inatuwezesha kutembea katika mapenzi ya Mungu (Tito 2:11-12). Kama watoto wa Mungu, tumeokolewa kwa neema, tunaishi kwa neema, tunakua katika neema, yaani maisha yetu ni Neema ya Mungu tokea mwanzo hadi mwisho. 

John Newton yule mtunzi wa wimbo ule maarufu wa Amazing Grace alipata ufunuo wa neema ya Mungu (baada ya kuokolewa na kukombolewa toka kwenye biashara haramu ya utumwa aliyokuwa akiifanya) alipoutunga wimbo ule, kwenye ubeti mmoja anasema: 

Tis grace hath brought me safe' thus far,
And grace will lead me home.

Mtume Paulo alimwomba Mungu ili amwondolee mwiba ule, Mungu alimwambia "Neema yangu yakutosha" na kweli Neema ya Mungu ilimwezesha kuishi kwa ujasiri na ushindi dhidi ya mwiba ule, ukuu wa Mungu uliendelea kudhihirika maishani mwake, hata leo hii tumepata sehemu kubwa ya Agano Jipya kupitia kwake. 

Katika zama hizi za Agano Jipya, hatuko tena chini ya Torati, hivyo basi wala hatutakiwi kuishika, tunayo sheria mpya ambayo Roho wa Mungu anaiandika katika mioyo yetu ili tuenende sawasawa nayo. Hatuishiki ili tuhesabiwe haki bali tunaitimiza kwa sababu tumeshahesabiwa haki. Mungu alipotangaza nia ya kuleta Agano Jipya kupitia kwa nabii Yeremia alisema hivi:


Na pia ni vizuri tukumbushane ya kuwa Mungu ametuokoa ili tuenende katika matendo mema ambayo tayari alishatuandalia na hata nia ya kutenda mema tayari ameshatupa Yeye Mwenyewe.Ni muhimu tuelewe kuwa hatutendi mema ili tuhesabiwe haki bali tunatenda mema kwa sababu katika Kristo tayari tumeshahesabiwa haki. Mti hauzai matunda mema ili uwe mwema, hapana bali mti ukiwa mwema basi utazaa matunda mema. 



Neema ya Mungu imetufanya tukubalike mbele zake Mungu na kuhesabiwa haki kwa imani bila ya jitihada zetu binafsi, Yaani kwa kuwa tumemwamini Kristo na kazi ya kamilifu ya kutukomboa basi hilo peke yake limepelekea sisi kupatanishwa kabisa na Mungu without any reservations. Sasa tukielewa ya kuwa tumeshapatanishwa na Baba yetu wa Mbinguni na wala hana nia ya kutudhuru tutakuwa na shauku ya kweli ya kumpendeza yeye katika maisha yetu, hatutakuwa na nidhamu ya woga.  

Sasa tunao wajibu wa ku-respond to God's grace maishani mwetu, kumbuka Mungu hata siku moja hatatulazimisha kufanya chochote, wala hatugeuzi kuwa maroboti. Sisi tuliookolewa tunao uwezo wa kuikataa dhambi na kuchagua kutenda mema tofauti na ambao hawajaokolewa ambao wanaburuzwa na dhambi.Ndio maana mtume Paulo alisema hiyo neema ya Mungu kwake haikuwa bure, bila shaka utakubaliana nami kuwa neema ya Mungu kwa baadhi ya wapendwa kwa jinsi wanavyoishi ni kama imekuwa bure (in vain) ndo wanaoishia kubweteka tu:
Kwa kuhitimisha niseme kuwa personal responsibility haiwi voided na neema ya Mungu, ndio maana Neno linatuambia kuwa kila mmoja wetu, sisi tuliookolewa, tutasimama mbele za Kristo kutoa hesabu ya yale tuliyofanya, na kazi zetu zitapimwa kama ni za nyasi, miti au mawe au mawe ya thamani kazi zetu zote zitapimwa kwa moto na na thawabu zitatolewa accordingly, ila hakuna atakayetupwa motoni hata kama kazi yake itateketea siku hiyo.

11 Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu Kristo. 
12 Lakini kama mtu akijenga juu ya msingi huo, dhahabu au fedha au mawe ya thamani, au miti au majani au manyasi, kazi ya kila mtu itakuwa dhahiri. 
13 Maana siku ile itaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto wenyewe utaijaribu kazi ya kila mtu, ni ya namna gani. 
14 Kazi ya mtu aliyoijenga juu yake ikikaa, atapata thawabu. 

Mbarikiwe sana watu wa Mungu,

Patrick

2013/5/4 SELELI EDWIN <selel...@gmail.com>

Patrick Kamera

unread,
May 6, 2013, 11:55:26 PM5/6/13
to strictl...@googlegroups.com
Joel,

Ubarikiwe sana...excellent points my brother, I'm loving this! 

Patrick


2013/5/6 jwmsella . <joel....@gmail.com>

Mathew Maduhu

unread,
May 7, 2013, 9:51:53 AM5/7/13
to strictl...@googlegroups.com

Patrick,

Barikiwa sana Mtumishi, specifically nimeipenda sana hii Mti hauzai matunda mema ili uwe mwema, hapana bali mti ukiwa mwema basi utazaa matunda mema” To me thing is a wonderful quote.  JW Msella, Jei Wi wa Bwana Yesu asante kwa additional inputs. Umeniongezea ufahamu kwenye uelewa wangu. Hebu ona hii Neno la Kigiriki lililotafsiriwa "kutimiliza", kwa mujibu wa kamusi ya Strong (Strong's Hebrew and Greek Dictionary) maana yake mojawapo ni "to fill (up), (be, make) full, complete"; yaani, kufanya kitu fulani ambacho kilikuwa na upungufu fulani kuwa kamili.” Edwin na SG wote hii church taaamu sana wapendwa. Maria (mama wa ma-link) atukuzwe Mungu aliyekupa ufunuo huu.

 

Mathew.

 

From: strictl...@googlegroups.com [mailto:strictl...@googlegroups.com] On Behalf Of Patrick Kamera
Sent: Jumanne, Mei 07, 2013 8:04 AM
To: strictl...@googlegroups.com
Subject: Re: TUSIIPUNGUKIE NEEMA YA MUNGU

 

Edwin na wana SG wote,

SELELI EDWIN

unread,
May 7, 2013, 6:18:41 AM5/7/13
to strictl...@googlegroups.com
Patrick Kamera,

Oooh Yes, now landed fully...this one...Na pia ni vizuri tukumbushane ya kuwa Mungu ametuokoa ili tuenende katika matendo mema ambayo tayari alishatuandalia na hata nia ya kutenda mema tayari ameshatupa Yeye Mwenyewe.Ni muhimu tuelewe kuwa hatutendi mema ili tuhesabiwe haki bali tunatenda mema kwa sababu katika Kristo tayari tumeshahesabiwa haki. Mti hauzai matunda mema ili uwe mwema, hapana bali mti ukiwa mwema basi utazaa matunda mema. 

Sasa bwanaa....kama kuna maswali mengine hujajibu, i promise nitayajibu mimi mwenyewe tukifia mbinguni tutakapo kua tunasalimiana, tehe tehee...

Nimebarikiwa sana, sana and i hope/know any body who followed up this somo and questions raised by Maduhu and Me, GREAT WORK Patrick in Jesus name,amen.

Press on,

Edwin Seleli

2013/5/7 SELELI EDWIN <selel...@gmail.com>
Joel Msella,

I ririzi Mwaaaa to this...Sisi tunapomtolea Mungu, kuomba, kufunga, nk kamwe matendo hayo hayatufanyi tuwe na haki zaidi bali yanatufanya tuweze kuwa kumtumikia Mungu kwa mali zetu na kuwa karibu naye katika ibada na maombi. Ni makosa makubwa kufikiri kuwa tunaweza kufanya matendo ya sheria ili Mungu atuhesabi kuwa ni wenye haki.

Ndio maana mtume Paulo aliwaandikia Wakristo waliokuwa kule Galatia:

Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa?Nataka kujifunza neno hili moja kwenu. Je! Mlipokea Roho kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imaniJe! Mmekuwa wajinga namna hii? Baada ya kuanza katika Roho, mnataka kukamilishwa sasa katika mwili?  Mmepatikana na mateso makubwa namna hii bure? Ikiwa ni bure kweli.  Basi, yeye awapaye Roho na kufanya miujiza kati yenu, je! Afanya hayo kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani?  Kama vile Ibrahimu alivyomwamini Mungu akahesabiwa haki.  Fahamuni basi, ya kuwa wale walio wa imani, hao ndio wana wa Ibrahimu.  Na andiko, kwa vile lilivyoona tangu zamani kwamba Mungu atawahesabia haki Mataifa kwa imani, lilimhubiri Ibrahimu habari njema zamani, kusema, Katika wewe Mataifa yote watabarikiwa.  Basi hao walio wa imani hubarikiwa pamoja na Ibrahimu aliyekuwa mwenye imani. (Wagalatia 3:1-9, msisitizo wangu)

Kwa iyo mie mjinga siyo? umenitukana Joel..aaah? hahahah...come on...cheers

ooh meen..i love your inputs, great job Jo, the above para in yellow and red,  is a huge thing, indeed foundational faith ingredient

NB: Maswali mengine, yasipojibiwa na wewe au Patrick then, malaika Gabriel, will do..tehe!
Pia NEVER FORGET KILE KIPANDE/SOMO LA MOTIVE BEHIND UTOAJI, AS LONG AS JESUS WILL DELAY, WILL SUFFOCATE YOU BADLY KUKUkUMBUSHA AND i think you know my ''anointing'' ya kukomaa...hahahahaha...Natamani bro wangu ulete ilo somo coz God has blessed you with oil from above not vaseline from Tandale.

Press on,

Edwin Seleli



2013/5/6 jwmsella . <joel....@gmail.com>

SELELI EDWIN

unread,
May 7, 2013, 6:04:44 AM5/7/13
to strictl...@googlegroups.com
Joel Msella,

I ririzi Mwaaaa to this...Sisi tunapomtolea Mungu, kuomba, kufunga, nk kamwe matendo hayo hayatufanyi tuwe na haki zaidi bali yanatufanya tuweze kuwa kumtumikia Mungu kwa mali zetu na kuwa karibu naye katika ibada na maombi. Ni makosa makubwa kufikiri kuwa tunaweza kufanya matendo ya sheria ili Mungu atuhesabi kuwa ni wenye haki.

Ndio maana mtume Paulo aliwaandikia Wakristo waliokuwa kule Galatia:

Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa?Nataka kujifunza neno hili moja kwenu. Je! Mlipokea Roho kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imaniJe! Mmekuwa wajinga namna hii? Baada ya kuanza katika Roho, mnataka kukamilishwa sasa katika mwili?  Mmepatikana na mateso makubwa namna hii bure? Ikiwa ni bure kweli.  Basi, yeye awapaye Roho na kufanya miujiza kati yenu, je! Afanya hayo kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani?  Kama vile Ibrahimu alivyomwamini Mungu akahesabiwa haki.  Fahamuni basi, ya kuwa wale walio wa imani, hao ndio wana wa Ibrahimu.  Na andiko, kwa vile lilivyoona tangu zamani kwamba Mungu atawahesabia haki Mataifa kwa imani, lilimhubiri Ibrahimu habari njema zamani, kusema, Katika wewe Mataifa yote watabarikiwa.  Basi hao walio wa imani hubarikiwa pamoja na Ibrahimu aliyekuwa mwenye imani. (Wagalatia 3:1-9, msisitizo wangu)

Kwa iyo mie mjinga siyo? umenitukana Joel..aaah? hahahah...come on...cheers

ooh meen..i love your inputs, great job Jo, the above para in yellow and red,  is a huge thing, indeed foundational faith ingredient

NB: Maswali mengine, yasipojibiwa na wewe au Patrick then, malaika Gabriel, will do..tehe!
Pia NEVER FORGET KILE KIPANDE/SOMO LA MOTIVE BEHIND UTOAJI, AS LONG AS JESUS WILL DELAY, WILL SUFFOCATE YOU BADLY KUKUkUMBUSHA AND i think you know my ''anointing'' ya kukomaa...hahahahaha...Natamani bro wangu ulete ilo somo coz God has blessed you with oil from above not vaseline from Tandale.

Press on,

Edwin Seleli



2013/5/6 jwmsella . <joel....@gmail.com>
Kaka Patrick,

jwmsella .

unread,
May 7, 2013, 12:05:59 PM5/7/13
to strictl...@googlegroups.com
Umenichekeshaje Edwin!

Lile somo la motive ya utoaji ninalikumbuka sana....linakuja punde.

Mungu awabariki wana SG wote; amina.

JWM


2013/5/7 SELELI EDWIN <selel...@gmail.com>

--Maria

unread,
May 8, 2013, 9:40:44 AM5/8/13
to strictl...@googlegroups.com
Ameen pastor Utukufu kwa Mungu wetu. Mungu awabariki woote wasomaji, waleta mada,mafundisho,mitazamo yao nk..

--Mary
Sent from my BlackBerry® smartphone, powered by Cricket.

From: Mathew Maduhu <Mathew...@tanesco.co.tz>
Date: Tue, 7 May 2013 16:51:53 +0300
Subject: RE: TUSIIPUNGUKIE NEEMA YA MUNGU
Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages