Re: KUMFUATA KRISTO BILA KUJIKANA HAIWEZEKANI

806 views
Skip to first unread message

hopeminis...@gmail.com

unread,
Jun 17, 2013, 3:33:37 AM6/17/13
to strictl...@googlegroups.com
Ameen,barikiwa mtumishi

----------
Sent from my Nokia phone

------Original message------
From: Patrick Kamera <pka...@gmail.com>
To: <strictl...@googlegroups.com>
Date: Friday, June 14, 2013 4:19:56 AM GMT-0400
Subject: KUMFUATA KRISTO BILA KUJIKANA HAIWEZEKANI

34 Akawaita mkutano pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, Mtu ye yote
akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe, ajitwike na msalaba wake, anifuate.
35 Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza, na mtu
atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili, huyu
ataisalimisha.
36 Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya
nafsi yake?
37 Ama mtu atoe nini badala ya nafsi yake?
38 Maana kila mtu atakayenionea haya mimi, na maneno yangu, katika kizazi
hiki cha uzinzi na dhambi, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo,
atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu. – *Marko
8:34 -38 SUV*

Mara zote tunaona mkutano mkuu au umati ndio unamfuata Bwana Yesu, lakini
hapa mambo yalikuwa tofauti, Bwana Yesu mwenyewe aliwaita mkutano ambao
bila shaka ulikuwa ni watu wengi tu, pamoja na wanafunzi wake kwani alikuwa
na jambo la muhimu sana, jambo la msingi kabisa la kuwaambia. Tukumbuke pia
hapo nyuma kidogo walitaka kumfanya mfalme baada ya muujiza alioufuanya wa
kulisha wale wanaume 5000 bila kuhesabu wanawake na watoto, naye alifahamu
hilo akawakwepa. (*Yohana 6:15*)

Hakutaka waendelee kumfuata huku wakiwa na agenda zao wenyewe au mategemeo
yao wenyewe ya kubweteka na kula mikate na samaki bure tu na kupokea
miujiza ya uponyaji na mahitaji yao wao tu. Hapana., alitaka kuweka wazi
lengo la kuja kwake na ya kuwa kumfuata yeye kutawagharimu vyote iwe ni
umaarufu, heshima au hadhi zao katika jamii, kupendwa na watu n.k. Mahali
pengine alisema “mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya jina langu…”

Ni vizuri tukumbushane kuwa kumfuata Bwana Yesu ni kutangaza vita na
shetani, atafanya kila awezalo kujaribu kutukatisha tamaa lakini kama Neno
lisemavyo tunamshinda kwa Damu ya Mwana Kondoo na kwa Neno la ushuhuda
wetu, isitoshe tumepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge na nguvu zote za
yule adui na wala hakuna kitakachotudhuru. (*Luka 10:19*)

Hivyo basi kama mtu umeamua kumkiri Bwana Yesu kama Bwana na Mwokozi wako,
basi mfuate kwa moyo wako wote ukitambua ukweli huo, muda wa kujibaraguza
na kuchezacheza na dhambi haupo, usiku umeenda sana alfajiri ndio hiyo
inawadia, Bwana Yesu yuko mlangoni, amka wewe usinziaye....

Tukifanya uamuzi wa dhati kabisa wa kumwishia yeye, Mungu ni mwingi wa
neema na rehema naye ni mwaminifu, atatuwezesha na kutufanikisha kusimama
katika Kristo ila hatatulazimisha hata siku moja.

Maneno ya Bwana Yesu ni Roho tena ni Uzima, kutokuyazingatia ni
kutokujitakia mema…asomaye na afahamu!

Mbarikiwe na Bwana Yesu,

Patrick

--
Tafadhali zingatia msingi wetu ni Neno la Mungu, Lengo letu Kuujenga mwili wa Kristo, kushirikiana, amani na upendo. Yeyote yuko huru kuchangia, kufundisha, kukubali kufundishwa sawasawa na Msingi wetu Mkuu Neno la Mungu. Kujiunga na Team ya Injili au Maombi wasiliana nasi kwa simu 0714 915 424. Tuma Email. strictl...@yahoo.co.uk Facebook:https://www.facebook.com/pages/Strictly-Gospel/363180289370

Blog: www.strictlygospel.wordpress.com

Kujiondoa Kwenye Kundi Hili Tuma Email:
strictlygospe...@googlegroups.com



bupe berrums

unread,
Jun 18, 2013, 5:23:45 AM6/18/13
to strictl...@googlegroups.com
Amen kaka Patrick


Patrick Kamera

unread,
Jun 18, 2013, 8:29:49 AM6/18/13
to strictl...@googlegroups.com
Amen! Mbarikiwe watumishi wa Mungu Hopeministriestz na Bupe kwa maneno yenye kutia moyo. Tuendelee kujifunza Neno pamoja na kumtukuza Mungu.

Patrick


2013/6/18 bupe berrums <bber...@gmail.com>

Gladys JB

unread,
Jun 20, 2013, 6:03:21 AM6/20/13
to strictl...@googlegroups.com
Mpendwa Patrick,

Mungu wa mbinguni azidi kukutia nguvu na kukutumia apendavyo for His Glory.

Huku KUJIKANA leo ni neno adimu makanisani mwetu sasa huko kwenye ministries ndio hulikuti
kabisa.(simaanishi ministry zote) ILA ZILIZO NYINGI ZINAHUBIRI MAFANIKIO YA MWILI, YA ROHO JE?
Aaa mpendwa shtuka, tambua kuwa uendako siko BWANA wako alikokukusudia.
Kwako mpendwa uliyeipata neema hii ya kuweza kujikana wasaidie wengine kwa kuwafunza neno la kweli
ili waokolewe na ghadhabu ya Mungu iliyo karibu.

Tunaenenda sana ktk mwili leo, na kwa sehemu kubwa ndiyo mafundisho tunayoyapata.
Ni nadra sana kuwakuta wachungaji(sio wote) wanahimiza watu wao kutumika shambani mwa BWANA Yesu. kumbe kule kutumika kutamfanya mtu apende asipende ajikane ili huduma yake izae matunda yanayodumu, ili akwepe mishale ya adui ya kila mara ni sharti kujikana ktk mambo mengi ikiwemo mwenendo na kuuishi utakatifu ambao sio tu utamsaidia mtu husika kuwaleta watu wengi kwa Yesu bali pia ni DIRECT GATE PASS TO HEAVEN, Si imeandikwa .....na huo UTAKATIFIU ambao pasipo huo hakuna mtu atakayemwona Mungu. (Ebrania 12:14b)

Sasa jiulize bila kujikana utaupataje utakatifu? maana unatafutwa kwa bidii. Huna... ama huwezi.... si kwa sababu Mungu amekunyima, la hasha, huna na/ama huwezi;
 a)KUSAMEHE,
 b)KUTOA SADAKA, ZAKA NA DHABIHU KWA UAMINIFU,
 c)UAMINIFU KTK NDOA, HUDUMA YAKO, KAZINI NA HATA KTK MAHUSIANO MENGINE,
 d)UPENDO WA KWELI, N.K. kwa sababu hujaomba.
Mungu anatupa kwa kadri tumwombavyo, ng'ang'ana mpk akupe uwezo wa kujikana  nafsi yako ili uweze;
 i)kusamehe na kauachilia,
 ii)kuwa mwaminifu ktk mambo yote being it sadaka, zaka, dhabihu, biashara, ndoa, muda etc
 iii)Kuwapenda watu kama Yeye anavyowapenda etc etc.

Yesu anatwambia "Hata sasa hamjaomba neno lolote...Ombeni lolote kwa jina langu......" Yawezekana umeomba ila si ktk kile kiwango Mungu anakitarajia. Na bila neema ya kujikana nafsi huwezi kuomba. Lakini nasema Omba, omba , omba...wala usikate tamaa!

Watumishi na waumini wengi wanaonenda ki-mwilini sana leo si kwamba hawajaokoka, aa!  wamekosa tu kitu hiki KUJIKANA. kujikana inawezekana kama utaamua KUOMBA, KUTAFUTA NA KUBISHA. Yote yawezekana kwake aaminiye. (Marko 9:27)

Mungu atusaidie sote kadri tunavyozidi kujifunza.

Si kwamba mm nimekwisha kushika..... nazidi kuchuchumilia yaliyo mbele......

NAKUPENDA MAANA KRISTO ALITANGULIA KUKUPENDA.

Barikiweni nyote.

Gladys



From: Patrick Kamera <pka...@gmail.com>
To: strictl...@googlegroups.com
Sent: Tuesday, June 18, 2013 3:29 PM
Subject: Re: KUMFUATA KRISTO BILA KUJIKANA HAIWEZEKANI
Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages