Patrick my brother,
Ubarikiwe sana kwa majibu yako, nashawishika si mimi tu bali ni wengi
tunafaidika na kujengwa sana-sema tunatofautiana ktk moyo wa
appreciation lively, kwa jinsi Mungu anavyokutumia kwa mengi hapa SG
mara uchukuapo hatua na muda na kuukubalia moyo wako kushiriki
kanisani hapa live.Umebarikiwa sana wewe Mtu na nampa Mungu Utukufu
kwa ajili yako aliyekujaza hayo kwa kweli. Nilisoma mara tu ilipoigia
msg yako, nimekawia kujibu si kwa kua sikujali muda na kazi yako
uliyotenda but believe me, some stuff as too sweet and new life’s
pages openers hence staying with them for some time becomes the best
solution to at least chew all their lovable juicy muscles.
Kuna mambo napenda kuendelea kupata na kwa humble signature yako kila
mara unayomalizaga nayo ktk posts/inputs zako ya ..’’Tuendelee
Kujifunza’’ hence yafuatayo tuendelee kuyaangalia kidogo.
JIBU LAKO: Ukiwa umeitwa kufanya huduma fulani utajihisi
unavutwa/Msukumo upande huo wa huduma hiyo na Wapendwa watathibitisha
kwa kukuambia
MASWALI NYONGEZA:
(a) Huko kuvutwa, unasikia nini hasa?
(b) Kuvutwa uko kunatofautianaje na ile hamu tu ya kawaida ya kupenda
kufanya jambo/huduma ya kiroho labda kwa sababu ni kati ya vitu
unapenda-spiritual hobbies if you know me?
(c) Tunatofautishaje kuvutwa na huduma ambako kumetokana na kupangiwa
ufanye huduma/shughuli fulani kanisani na nje na kwa kua umeifanya
sana, say kuimbisha pambio or P& W au kufundisha kwa kua hakuna
wakujitolea, na wewe kwa kujisukuma na kujitia moyo na hata kwa
kuandaliwa notes then ukawa unafundisha /imba kila mara kwa muda mpaka
sasa ukaanza kuvutiwa/ikawa kama sehemu ya zamu/maisha yako?
JIBU LAKO: Utakuwa na upako wa kuifanya huduma hiyo
SWALI LA NYONGEZA: Kwa upako, u mean uthihirisho wa nguvu za Mungu
mara usimamapo kuifanya iyo huduma au uwezeshwaji wa ajabu unakupa
umaridadi/u-smart/ubora na uzuri sana unapofanya icho kitu?
JIBU LAKO: Wengine wataiona neema iliyoko juu yako kwa ajili ya huduma hiyo
SWALI LA NYONGEZA: Kwa kuona neema juu yangu, Wataona nini hasa hicho
mpaka wajue/wasema huyu Mtu ana hiki kwa kweli?
JIBU LAKO: Kama Mungu amekuagiza uache kazi yako basi ni heri kumtii
Yeye kwani anajua atakutunzaje.
MASWALI LA NYONGEZA:
(a) Kwa kua hili limeleta shida kubwa na kusababisha Watumishi kadhaa
kujiudhuru Utumishi, wengine wake zao kughairi kuendeea kuwa-join
Waume zao maana maisha magumu mno, hakuna pesa za kumtunza na familia,
MTU ANAONGOZWAJE KUACHA KABISA KAZI YAKE…hata kwa msukumo tu au in
this critical issue, bora strictly asiache mpaka asikie Sauti kabisa
ya RM ndani au ya nje?
(b) Vipi akiacha tu BILA uongozi huo normal-Msukumo au
extra-ordinary-Sauti ndani/nje kwa sababu ya nia njema tu ya kuwa na
muda wote kwa Bwana na altar maana si rahisi kuwatumikia ma Bwana 2
fully and efficiently, kuna soo?
(c) Ukishakua na kanisa kubwa/huduma kubwa inayoweza kukutunza kwa
kila kitu, kuna haja ya kutafuta uongozi wa Mungu kuacha kazi au ni
mara moja wewe kama Mtu kabisa kuamua tu simple namna iyo kuacha?
JIBU LAKO: Mungu anaweza kuwatumia wengine kukuthibitishia mwito wako
lakini LAZIMA yale kutoka kwa Watu yawe yanathibitisha
ulichonacho/unachojua
MASWALI LA NYONGEZA
(a) Ivi Ni lazima sana kua Watu watakuambia kile UNACHOJUA unacho
ukilinganisha na fact hii kua Wafalme/Manabii/Waamuzi walingizwa
hudumani, baadhi yao wakiwa hawana hata habari, wakichunga tu
kondoo-Daudi, wengine Kiurithi-Selemani toka kwa Daudi, Wengine
wakiwa wamejaa hasira wakipura nafaka hata na kuongea
mbovu-Malalamiko/Manung’uniko wakati Mungu(Malaika) anataka kuwaingiza
kwa huduma -Gideon?
(b) Vipi ukiingizwa huduma kwa Mchungaji wako kwa kukupaka Mafuta kwa
ajili ya huduma na kukuambia kuanzia leo, Utafanya hiki na kile na
wewe ukatii na kuchukua hatua ya kwenda porini uko au kuanza huduma
iyo kanisani au pembeni ya Jiji kama tawi la kanisa lake/lenu/la Yesu,
kuna tatizo mbele uko au peace tu na ni tuendelee kuchapa kazi?
(c) Na je ukiingizwa hudumani kwa maamuzi/maono/anavyokufahamu
Mchungaji wako, itahesabika kwa Mungu ni sawa, na Ni Mungu amekuingiza
na una haki/full confidence ya kujiita mimi ni Mtumishi wa Mungu au
kuna hatari wa kuchapa mzigo kwa miaka 20 only later to realize
uliingizwa na Pastor wako si Mungu?
JIBU LAKO: Wapendwa waliokuzunguka wanakupa shuhuda za jinsi
wanavyobarikiwa kila unapohudumu ukawa bado
ujiamini/haukubali/unasita, baadaye ukakutana na watu wa Mungu ambao
wala hamfahamiani na kila mmoja wao akakuambia maneno ya kukuambia
icho ulichonacho/walichosema wanaokufahamu
SWALI LA NYONGEZA:
(a) Hakuna uwezekano Wapendwa wanaokufahamu kusema maneno hayo mema
kwa kua tu basi wanabarikiwa na si kwamba Wanatumiwa na Bwana
kukuambia mwito/huduma yaani Mpendwa amefurahia tu kile unachotoa
kitamu na cha ukweli?
(b) Au kuondoa risk iyo ni bora kama ulivyosema, ithibitike na wengine
hata wasiokufahamu, wakafunuliwa pia?
(c) Na hii ya Wapendwa wanaokujua na wasiokujua kusema icho icho,
inaweza tosha Mhusika kufanya maamuzi na kuanza/kuingia hudumani bila
sauti specific ya RM?
Press on Tuendelee Kujifunza,
Edwin Seleli