Ni kusudi la Somo/Mada hii TUWE MATAJIRI WA MAANDIKO/MANENO YA MUNGU NA UFAHAMU SAHIHI WA KWELI ZA MUNGU ivyo tule Neno hadi tushibe tikitiki. Uwe huru kwa raha zako kuleta majibu ya jumla, Akili za kawaida, Ujuzi, Uzoefu, Ushuhuda, Ki-huduma na Karama ila ZAIDI SANA, leta NENO.
Tusome Maandiko kwanza!1 Samuel 13:13-14: 13 And Samuel said to Saul, You have done foolishly! You have not kept the commandment of the Lord your God which He commanded you; for the Lord would have established your kingdom over Israel forever;14 But now your kingdom shall not continue; the Lord has sought out [David] A MAN AFTER HIS OWN HEART and the Lord has commanded him to be prince and ruler over His people, because you have not kept what the Lord commanded you.NOTICE: ‘’A MAN AFTER HIS OWN HEART’’
Mdo. 13:22...Na alipokwisha kumwondoa huyo, akamwinua Daudi awe mfalme wao ambaye alimshuhudia, akisema, Nimemwona DAUDI, mwana wa Yese, mtu ANAYEUPENDEZA MOYO WANGU, atakayefanya mapenzi yangu yote. NOTICE: ‘’ANAYEUPENDEZA MOYO WANGU,’’
MASWALI YA MUONGOZO KTK KULA MKATE HUU:
Maelezo: Daudi aliua sana hata Mungu akamkatalia kumjengea Nyumba maana mikono yake imejaa damu-yaani una nia njema mno ya kufanya kitu cha Mungu lakini unakataliwa kwa sababu ume KILL mno/wengi- (1 Nyakati.22:8) na pia alichukua Mke wa Mtu kikatili sana kwa kumsakizia Mume-Uria Askari wake apangwe mstari wa mbele vitani ili auwawe na kisha Rais Daudi awe naye 24/7 Wife wa Mtu-Askari wake wa nguvu ila marehemu mtarajiwa/msakiziwa- 2 Samweli: 11 sura yote. Alisuka mpango huo wa kuua Askari wake baada Mfalme kufeli mara 2 kuficha mimba aliyompachika Mke wa Askari wake. Alimuondoa Askari huyo uwanja wa vita ili arudi nyumbani na akalale na Mkewe ili amsakizie ‘’bebi to be born’, lakini kajamaa-Kaaskari kalikua very committed na Kazi ya U-soja, akataa kwenda kwa starehe kwakua wenziwe wako vitani-ktk huduma VERY SERIOUS YA KULINDA/KUTUNZA USALAMA WA NCHI UHAI WA WATU WAKE
Rais hakuchoka, akaandaa bonge la menyu ili Uria anywe haswa na Biblia inasema kwa Kiingereza… ‘’HE MADE HIM TO DRINK-yaani akakusudia Askari wake huyo ‘agonge ‘Kilimanjaro Premier Lagaa’ za enzi zile nyingi ili imulaghai na akate net works kichwani, apoteze usmart wa kuwaza na kuamua vema kwa vipao mbele vipi vianze na vipi vingoje, iyo impelekee aende kulala na kufanya mapenzi na Mkwewe. Ingawa kweli inaonekana alizigonga chupa vema lakini, usoja- discipline na kutetea Nchi yake ilikua ni huduma ya moyo wake haswaaa na ivyo akakwepa kwenda nyumbani aliko Wife wake. Sasa Daudi kwa kupanic siri kumbuluka, kwa ukatili mwingine akaandika barua spesheli na kumpa Uriah-huyo huyo mume wa Mtu-Askari wake ili kuipeleka kwa Jemandari wa Vita uwanja wa mapambano-kumbe ndani ya hiyo barua ya Ikulu ndio kuna mpango mzima wa kumkata oxgen for real and forever.
Maswali:
MOJA: Upendezeshwaji wa Daudi kwa moyo wa Mungu, Je, ulikua wakati kako kadogo-kadogo kakijana mwororo kanachunga Kondoo za Baba yake na hakajajua hata ..‘I love u gal kwa maneno na kitandani’’ yaani wakati ule kanaua dubu na Goliati kwa Jina la Bwana au ni maisha yake yote hata wakati ameshakua Rais na kupiga faulu nyingi tu za kufa Mtu?
PILI: Mungu aliposema ‘Mtu aupendazaye Moyo wangu’ na kwa kua Mungu anaona na kuhitimisha mambo tokea Mwanzo kwa hivyo si kwamba anajua jambo wakati tukio limetokea, inakuaje au ni kwa nini amuite Mtu wa dizaini hii kua ni Wa Moyoni/anayependeza Moyo wake? Kuna siri gani? Nin spesheli yake huyu Rais?
TATU: Toa maandiko yanayoonyesha History njema-CV yake upande mzuri wa Daudi ili labda kwa hicho ndio tuone Mungu alimaanisha nini kusema huyu jamaa na mafualu yake ya hatari, imekuaje awe kipenzi ‘kyake kya moyo?’
NNE: Kuna Mtu yoyote ktk Biblia ambaye Mungu ameshawahi mtamkia kua ni ‘’Mpendwa/Mpenzi wa Moyo wake?’’ Au ‘’Anapendwaza naye?’’, Mtaje na tupia andiko ili tuwe matajiri wa kuyajua maandiko mengi kwa mambo mbalimbali
TANO: Unawalinganishaje( similarities and differences) hao Watu Wengine namba 4 na maisha ya Daudi upande wake mwema si ule wa mafaulu ya kutisha?
Press on eating and drinking the Bible, Amen.
Edwin Seleli
NNE: Kuna Watu/Mtu/ yoyote ktk Biblia ambaye Mungu ameshawahi mtamkia kua ni ‘’Mpendwa/Mpenzi wa Moyo wake?’’ Au ‘’Anapendwaza naye?’’, Mtaje na tupia andiko ili tuwe matajiri wa kuyajua maandiko mengi kwa mambo mbalimbali''. Sasa best embu gonga mzigo hapo kisha leta jibu, amen? good, nina/tunakungoja utulishe Mtumishi
Press on,
Seleli