Amani ya Bwana iwe pamoja nanyi enyi nyote.
Hili ni somo siyo mada na nimekusudia kupitia ninyi wote Watu wa Mungu wa Kanisa letu jema sana lililotupa faida kubwa na ambalo wa kwanza wao kusaidiwa na kupewa faida na ufahamu wa ajabu na mtamu mno wa mambo ktk NENO LA MUNGU, ni mimi. Yako mambo nilikua sijui kabisa yaani completely zero na pia mengine nilikua najua vibaya na mengine nilijua kwa ufahamu mdogo sana, na mengine nilijua vema sana ila nikaongezewa kitu kingine bora zaidi hivyo hakika Kanisa letu ni baraka na ninyi ndio wenye kubeba baraka izo mnaposaidia Watu kujua mambo ya Mungu zaidi na ziadi, I BLESS U ALL.
Sasa turudia kazini/hudumani….. HILI NI SOMO MUHIMU SANA, SANA KABISA KWA MTU WA MUNGU ILI TUWEZE KUA SALAMA, TUFANYE MAAMUZI SAHIHI, TUFANYE HUDUMA BORA SANA, TUENENDA KTK RAMANI YA MUNGU NA HATA KUJUA MAPENZI YA MUNGU KWA HAKIKA KWA YALE AMBAYO HAYAJAANDIKWA WAZI WAZI KTK NENO
Sitafundisha hili somo lote A-Z ila nitachokoza kwa kuweka skeleton, ninyi nyote jazeni nyama. Kwa kusoma Maandiko, vitabu kadhaa na uzoefu kiasi tu wa misha yangu mwenyewe na wa kihuduma na ibada, nimefahamu kua Mungu huzungumza/ongea/wasiliana na Watu tena pia hufanya ivyo kwa wote wawe wameokoka-wamejaa Roho Mtakatifu au la, wanaomjua au la na njia anazotumia ni kama izi(waweza ongezea nyingine…)
MOJA:
Neno-Matendo na Maneno ya Mungu yaliyoandikwa ktk Bible, usomapo, unasoma
taarifa/maneno yake hivyo ndivyo anawasiliana nawe
PILI:Sauti ya Wazi-masikio ya kibidamu yanasikia kabisaaa au Sauti ya Ndani-masikio ya kiroho ndio yanasikia, Roho Mtakatifu ananema ndani yako
TATU: Kukiwapo Amani,ushwari na utulivu ndani ya Moyo-kwamba ukihisi iyo hali basi unachowaza/panga Mungu amekitiki, endelea nacho
NNE: Kutokuwepo kwa Amani, Ushwari na Utulivu ndani ya Moyo- kwamba ukihisi iyo hali basi unachowaza/panga Mungu hajakitiki, usiendelea nacho, acha mara moja
TANO: Msukumo, msisitizo, muhamasisho au mzigo wa moyoni- unapata kitu moyo halisi kweli juu ya jambo fulani na hakikuachi hadi unajua kabisa kua una jambo moyoni si la kawaida
SITA:
Ndoto- ukiwa umelala-unaona vitu/picha/sikia sauti
SABA: Maono ya wazi-kuona kama TV both ukiwa umelala au hujalala au ya ndani-rohoni/moyoni kitu/jambo linakua la uhakika sana
NANE: Kwa ishara ktk mazingira ya Nje-Mungu anafanya jambo ktk mazingira yako
TISA: Watu- Wanaongea mazungumzo ya kawaida tu au Mtu ana hubiri/fundisha Neno, kupitia hayo, mambo fulani yananatishwa/kua na nguvu na maalumu sana na binafsi kweli kwako
KUMI:
Wanyama-Mungu kutumia Mnyama mfano Punda kusema na Mwanadamu
KUMI NA MOJA: Wazo-Mungu kukuingizia/angushia Wazo ndani yako au hata ktk akili/ufahamu wako
Karibu
ulete Ushuhuda, Maandiko au ufafanuzi kwa njia izo juu pia uzoefu wako wa
kutembea na Mungu na uliyosikia kwa wengine, lini na namna gani Bwana
alisemaga/anaongeaga nawe/nao?
Press on,
Edwin Seleli
--