Ndoa ni zaidi ya Sherehe ya Harusi!

10 views
Skip to first unread message

Strictly Gospel

unread,
Oct 7, 2013, 7:28:50 AM10/7/13
to Strictly Gospel Group

ukumbi

Ndoa hazidumu kwa sababu kabla ya kufunga ndoa watu wanakuwa Obssesed na Wedding Ceremony Imaginations, bila kujua Ndoa inaenda mbali zaidi! Kuna Ndoa na kuna Harusi...Wengi mnapenda zaidi harusi, na mnapowaza Ndoa picha inayowajia ni Suti kali, Boonge la Shela kutoka Uturuki, Make Up ya ukweli ya bibi harusi kutoka Maznat Mikocheni, Marafiki kuingia ukumbini na Wimbo nyimbo za vigeregere,Wanafiki kukomeshwa kwa jinsi pati yako itakavyokuwa kali pale Karimjee Hall..

Je, umewahi kuwaza Mmeo au mkeo akiumwa miaka 5 mfululizo utaweza kumvumilia?? Umewahi kuwaza Watoto watakapozaliwa na ulemavu utawa-care namna gani?? Mtakapokosa watoto miaka 6 ya ndoa utahimili maneno ya Mama Mkwe na Mawifi kwamba unawajazia Choo cha kaka yao na huna kizazi?? Ndoa ni zaidi ya Sherehe ya Harusi.

Baada ya yale Matarumbeta kuzimika usiku kifuatacho ni Majukumu mazito na Kiapo kisichovunjika. Achana na Fantasy za Kwaito,waza mbali kidoogo... Je, Uko tayari kuwa Mme au Mke wa mtu mmoja tu au Ma-Ex watarejea kidogo kidogo kama hupati Satisfaction ya kutosha kama ya Ex wako??? Huwa mnawaza hayo au mnawaza Zawadi ya Kamati itatoa Verossa ya kuanzia maisha?? Sidhani... Kabla ya kuoa na kuolewa jiulize,Unatamani Ndoa au ni tamaa ya Sherehe ya Harusi????

--Henry Mavulla

hope katemba

unread,
Oct 7, 2013, 8:52:12 AM10/7/13
to strictl...@googlegroups.com
mh i like your ideas,asante kwa kutukumbusha mpendwa



2013/10/7 Strictly Gospel <strictl...@yahoo.co.uk>

--
Tafadhali zingatia msingi wetu ni Neno la Mungu, Lengo letu Kuujenga mwili wa Kristo, kushirikiana, amani na upendo. Yeyote yuko huru kuchangia, kufundisha, kukubali kufundishwa sawasawa na Msingi wetu Mkuu Neno la Mungu. Kujiunga na Team ya Injili au Maombi wasiliana nasi kwa simu 0714 915 424. Tuma Email. strictl...@yahoo.co.uk Facebook:https://www.facebook.com/pages/Strictly-Gospel/363180289370
 
Blog: www.strictlygospel.wordpress.com
 
Kujiondoa Kwenye Kundi Hili Tuma Email:
strictlygospe...@googlegroups.com

fle...@yahoo.com

unread,
Oct 7, 2013, 9:02:20 AM10/7/13
to Strict Gosple
Umenena Mwana wa Mungu na umesomeka
Download the latest BlackBerry® applications from Zantel on www.zantel.com/zantelapps

From: hope katemba <hopek...@gmail.com>
Date: Mon, 7 Oct 2013 15:52:12 +0300
Subject: Re: Ndoa ni zaidi ya Sherehe ya Harusi!
Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages