
Kama ungeliijua karama ya Mungu naye ni nani akuambiaye, ‘Nipe maji ninywe’, ungalimwomba yeye naye angelikupa maji yaliyo hai. … Kila anywaye maji haya [kutoka kisimani] ataona kiu tena; walakini yeyote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele (Yohana 4:10, 13-14).
Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama na kupaza sauti yake, akasema hivi: ‘Mtu akiona kiu na aje kwangu anywe. Aniaminiye mimi kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake.’ Na neno hilo alilisema kwa habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye; kwa maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa (Yohana 7:37-39, TLR. Maneno mepesi kukazia).
Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu, lakini kaeni humu mjini hata mvikwe uwezo utokao juu (Luka 24:49 – Maneno mepesi kutilia mkazo).
Si kazi yenu kujua nyakati wala majira, Baba aliyoyaweka katika mamlaka yake mwenyewe. Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi (Matendo 1:7-8. Maneno mepesi kutilia mkazo).
Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka, asiyeamini atahukumiwa. Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio: kwa jina langu watatoa pepo, watasema kwa lugha mpya (Marko 16:15-17. Maneno mepesi kutilia mkazo).
Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja. Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka (Matendo 2:1-4. Maneno mepesi kutilia mkazo).
Lakini [WaSamaria] walipomwamini Filipo, akizihubiri habari njema za ufalme wa Mungu na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake. … Na mitume waliokuwako Yerusalemu waliposikia ya kwamba Samaria imelikubali neno la Mungu, wakawapelekea Petro na Yohana, ambao waliposhuka, wakawaombea wampokee Roho Mtakatifu, kwa maana bado hajawashukia hata mmoja wao, ila wamebatizwa tu kwa jina lake Bwana Yesu (Matendo 8:12-16).
Ndipo wakaweka mikono yao juu yao, nao wakampokea Roho Mtakatifu. Hata Simoni alipoona ya kuwa watu wanapewa Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono ya mitume, akataka kuwapa fedha akisema, ‘Nipeni na mimi uwezo huu, ili kila mtu nitakayemweka mikono yangu apokee Roho Mtakatifu’ (Matendo 8:17-19).
Anania akaenda zake, akaingia mle nyumbani, akamwekea mikono akisema, ‘Ndugu Sauli! Bwana amenituma, Yesu, yeye aliyekutokea katika njia uliyoijia, upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu.’ Mara vikaanguka machoni pake vitu kama magamba, akapata kuona, akasimama, akabatizwa (Matendo 9:17, 18).
Petro alipokuwa akisema maneno hayo Roho Mtakatifu akawashukia wote waliolisikia lile neno. Na wale waliotahiriwa, walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu Mataifa nao wamemwagiwa kipawa cha Roho Mtakatifu. Kwa maana waliwasikia wakisema kwa lugha na kumwadhimisha Mungu. Ndipo Petro akajibu, ‘Ni nani awezaye kuzuia maji, hawa wasibatizwe, watu waliopokea Roho Mtakatifu vile vile kama sisi?’ Akaamuru wabatizwe kwa Jina lake Yesu Kristo (Matendo 10:44-48a).
Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu. Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao, wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri. Na jumla yao walipata wanaume kumi na wawili (Matendo 19:5-7).
Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao? (Luka 11:13).
Maana ni yupi kwenu aliye baba, ambaye mwanamwe akimwomba mkate atampa jiwe, au samaki, badala ya samaki atampa nyoka? Au akiomba yai, atampa nge? Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba yenu wa mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao? (Luka 11:11-13).
Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka (Matendo 2:4 – Maneno mepesi kutilia mkazo).
Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanzakunena kwa lugha (Matendo 19:6 – Maneno mepesi kutilia mkazo).
Maana nikiomba kwa lugha,roho yangu huomba, lakini akili zangu hazina matunda. Imekuwaje, basi? Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia, nitaimba kwa roho, tena nitaimba kwa akili pia (1Wakor. 14:14-15).