UKIPENDA KUA MTOAJI KUNA MAJARIBU YAKE SOMETIMES

41 views
Skip to first unread message

SELELI EDWIN

unread,
May 6, 2013, 3:20:07 PM5/6/13
to strictlygospel

Hellow SG,


Kidogo inauma lakini inabidi iwe ivyo, interesting indeed, kindly read to the end .Nawaza kua ingawa generally speaking as rule of the Bible, twapaswa kutoa,  lakini  ni hekima ku-apply  ukweli mwingine wa kuongozwa na Roho Mt SPECIFICALLY  ktk occasions fulani kabla hujatoa hasa utoaji kama changizo, au wa kuwapa watu vitu, msaada, ku-sponsor mambo ya Mungu, watu/watumishi wake, kutenda wema au kusaidia jambo. Kuongozwa specifically kutamuacha mtoaji salama kiroho(moyo wako wa ukarimu na kujali watu husigeuke kua mtego au wengine wenye nia zao kukuingiza matatizoni na pia kimwili kubaki salama( watu wakijua unazo- ziwe nyingi au ndogo ili mradi unaweza ukafanya jambo, wanaweza kula njama kukufanyizia au hawataisha kukufuata-fuata kila mara kwa mahitaji yao ya kweli na  wa uwongo mpaka  inakua kero/karaha na makwazo.


Kuna Mkaka mmoja, anapenda sana kujali, hurumia ivyo, akutanapo na mhitaji au akifuatwa na mhitaji, hata kama hana jinsi wakati huo kusaidia, huweza hata kuji-sacrifice kukopa mahala kutatua tatizo la mpendwa au ndugu tu wa damu, jirani, kisha kulipa baadae, raha yake yeye ni kuona  ishu iliyokua ina mbana mpendwa, jamaa imekwisha na yeye kafanyika kua sehemu ya suluhisho. Mkaka huyo anajijua ivyo kwa hakika ndani yake jinsi Mungu alivyomuwekea software iyo ya kutoa iwe mali, pesa, muda,moyo, vitu, ushauri yaani utoaji wa aina yoyote ili mradi mhitaji apate ahueni. Siku moja, aka-spot watoto wawili wa mpendwa ambao kila mara akiwaona ibadani, mikeshani, mifungo, seminar, wana nguo zile zile, watu wakikaa kunywa chai, soda baada ya ibada ya kwanza, wao wako pembeni tu, wanatamani kunywa chai,soda kama watoto wa wengine but no money na mama yao,  hubaki kanisani tu maana aende nje kufanya nini ilihali hana ela ya kuwanunulia watoto wake na yeye mwenyewe.Mkaka  yule akawaita siku moja na kuwapa ofa.Namna mtoto mdogo kati ya hao wawili alivyokamata chupa ya soda ya fanta baridi na kuipeleka mdomoni na kuanza kuimimina kwa throat, huhitaji ufunuo KUONA kua something has been terribly wrong or missing maskini. Wakanywa, kula na kufurahi kweli. Siku nyingine Mkaka huyo akawapa tena ofa na sasa  kila j2 almost huwapa ofa ya chai  na soda au juice, simple breakfast tu (chai ya strungi na maandazi au sconzi au chapati na wanashushia na soda u juice. Siku nyingine Mkaka akawachukua kwa mitumba market kule Karume na akawaambia wachangue kila wanachopenda kuanzia viatu,mashati, bukta, flana, jeans,makoti, kofia nk, walijimwaga kweli kuchagua, hawakuamini hayo yalikua yanatokea kweli. Siku izi wana-shine, wanabadilisha nguo na viatu, wana raha na furaha kweli na wamuonapo Mkaka uyo, wanasikia kupendwa kweli na wamependa sana mambo ya kanisa, huduma na bila shaka love yao kwa Bwana wao/wetu imeongezeka kama siyo kua revived greatly.


Siku moja Mkaka akapata sms toka kwa Mama yao ambaye ni single mother, aliyewahi kuolewa mara mbili, kua anataka kumuona, wakakutana na baada ya kushukuru na kubariki yote Mkaka aliyofanya, akasema jambo ambalo ilimchukua dk kadhaa kulitamka uku akitoa machozi, ‘TOKA NIZALIWE NA BAADA YA KUOKOKA, SIJAWAHI KUKUTANA NA MWANAUME ALIYENIONYESHA UPENDO KWA KINA HIKI, SIKUWAHI KUWAZA KATIKA KANISA KUBWA KAMA HILI NA LENYE WAHITAJI WENGI PAMOJA NA YATIMA,ANGETOKEA, MTU WA KUFANYA ALICHOWANYIA WANANGU, NIMEKUA NAKUOMBE SANA KWA MUNGU KWA UTOAJI WAKO NA UPENDO NA AMBAO WANANGU WAMENIAMBIA KWA MACHOZI, NA KILA MARA LAZIMA WANIPE HABARI ZAKO. HATIMAYE MOYONI NIMESIKIA KUKUPENDA NA KWA KWELI NASHUHUDIWA WEWE SASA UTAKUA BABA WA WATOTO WANGU. MIMI NIMEKUPENDA SANA NA NIMESHINDWA KUJIZUIA, IMEBIDI NIMUOMBE MUNGU KISHA NIKUAMBIE KUA NATAMANI TUISHI PAMOJA KAMA MUME NA MKE’’, alimaliza kusema uku akitetemeka na kuangalia chini. Mkaka alimshukuru kwa kumpeda na kumwambia anaheshimu sana upendo wake ila apewe nafasi kuuuliza Mungu. Wakaomba na kuachana.


Mkaka alifika home, akawa anawaza mengi mfano, mdada yule ni single mother, umri wake mkubwa kumzidi, pia alishawahi kua ktk ndoa ingawa waume walishakufa, ana wana wawili. Yote hayo yakamfanya hata hasiingie  maombini kwa kua aliona ni maombi yasiyo na tija na hata akawa anapotezea kumjibu Singe Mother baada ya ‘maombi’ yake. Single mother akakumbushia kwa sms, call kila mara hata kuwatumia wanae, Mkaka akaendelea kupotezea mwishowe sms mpaka saa 7usiku kila leo, zikazidi, akaamua kumpa audience kwa nia moja tu..kumwambia ukweli!. Siku ikafika na baada ya maombi ya kufungua ibada ya wawili, Mkaka ‘expected Baba watoto wa Single mother akafungua kinywa, NINAONA KWA VIGEZO VYOTE, SI MPANGO WA MUNGU MIMI NA WEWE TUWE MWILI MMOJA NA NILIFANYA WEMA KWA WANAO KAMA MKAKA WA VIJANA WENGI KANISANI NA KAMA NAVYOFANYA KWA WENGINE WENGI’’ alisema. Single Mother alitetemeka, kisha machozi.


Mkaka alikaa kimya akimwangalia analia mpaka huruma kweli zikamwingia then alipomaliza kulia, akamwambia, ‘Mungu wa mbinguni anajua haja yako, husipozimia moyo, atakudhibitishia kua anakupenda, tusonge mbele na mambo haya ya mimi na wewe kua mwili mmoja, yasiwepo tena baada ya leo maana kwa hakika hakutakuwepo ndoa iyo ila itakuwepo nyingine ambayo BWANA atakupa wewe mume bora na mimi, mke mwema’, kisha akaomba na wakaachana. Kuanzia hapo, Mkaka akapunguza utoaji wake kwa watoto na mwisho akaacha kabisa kwa miezi na mambo yakawa yamekwisha. Ghafla mwezi uliopita, Single mother akamtumia sms Mkaka kua anahitaji msaada kwa watoto wake wapate tuition na pia mtoto wa dada yake anahitaji shule ivyo anaomba aunganishwe na yeyote kanisani atakayeweza saidia ilo.Mkaka akikumbuka yaliyo tokea meizi kadhaa kwa yeye kujali maisha ya wanae, hakujibu sms na akachuna kabisa hata kuhakikisha hakuna kukutana kamwe iwe kanisani au hudumani. Mwishowe single mother akatuma sms ya kua amefanya uamuzi wa kutafuta appointment na Mke wa Mchungaji Kiongozi ili akaeleze yote yanayomsibu moyoni kuhusu yeye Mkaka na kwamba haoni kabisa kua kuna mume mwingine zaidi ya Mkaka uyo. Sasa Mkaka anawaza ivi, single mother ataongea nini kule, je ya ukweli au ulongo?  Na itakuaje shock ya kwanza atakayopata Mama Mchungaji maana anamfahamu sana Mkaka uyo na huduma na moyo wake? Yote haya yalimpata na yako njiani kumpata Mkaka, kisa wema/utoaji, out of his loving heart ya kusaidia/kuwapa watu vitu. Kweli utoajji mwingine, unamajaribu yake sometimes.


Pia Mkaka alishapata fedha nzuri miaka ya nyuma akiwa Wilayani. Kukatokea michango mingi kanisani kwa ajili ya maendeleo ya kanisa ilo mfano kununua vyombo vya kusifu na kuabudu na kuhubiria mikutano ya nje, watu wakawa wanaitwa na BWANA ivyo wakahitaji kuchangiwa karo kwenda vyuo vya Biblia, ujenzi wa kanisa na mikutano ya injili. Mkaka alikua anachukua nusu ya gharama ya mkutano, aliamua kuwasomesha wachungaji wanne na kuchangia gharama za vyombo robo ya thamani yote. Ikatokea hata baada ya kuhama uko, wapendwa wale wanakua wanataka sana kuja kwakwe Dar, kila wachungaji wajapo Dar, wanataka kufikia kwake, kila anayetaka kusoma Bible college, anamtumia Mkaka ombi, kanisa la kule kila likifanya shughuli, Mkaka anahusihushwa, vijana wakitaka kuoa na kuolewa, lazima wamfafute Mkaka wa Dar sasa aliyekua kwao uko Wilayani na inafika mahali Mkaka huyu amelemewa kwa kua kanisani kwakwe pia  kwa Dar sasa, ana husika na mambo mengi, yakiwemo pia ya kutoa


Maswali ya kutafakari


Unamshauri nini Mkaka ktk kikao kijacho ambacho kwa kweli hakipendi kwa heshima aliyo nayo kanisani, anajisikia kama atashusha P?

 

Au unadhani pengine Mkaka anakosea sana mpango/target kamili ya Mungu kwa kumkatalia singe mother pengine angeomba seriously, kweli single mother angethibitishwa kua ndiye wife?

Mkaka afanye nini/ali-relate vipi na watoto waliokwisha kua na raha sana, kupenda sana kanisa, kua na uhakika kila jumapili baada ya ibada wana breakfast na bila shaka wakampenda sana Yesu kwa jinsi Mkaka alivyowa-care lakini ameacha kwa kua Mama yao ameingiza agenda nyingine na anawatumia kama chambo au  point of contactig Mkaka?


Akikataa kutohusika kwa lolote kihuduma za kutoa/ku-care for uko Wilayani, akiwapangua  wapendwa wote wa uko na kubaki na wa Dar including kuwakwepa vibaya sana kwa kutojibu sms, call zao wanapokuja Dar ili wasifikie kwakwe la sivyo watapafanya a permanent centre kila wajapo jijini tena na ndugu na jamaa zao au hata Kwaya nzima inapokuja kurekodi, je amepungukiwa upendo?


Kwakua ktk changizo, ni mazoea siyo Bible, watu hutaja hadharani viwango(si kama sadaka), wale wapendwa wenye nazo, wanapotaja halafu kila likitokea jambo la idara za kanisa, binafsi, wapendwa huenda kuomba msaada kwao, mpaka wanalemewa na wengine walishafanyiziwa kwa kukabwa baada ya kutoka ibadani, je watoeje changizo? Kimya kimya kwa kuogopa kuombwa na wapendwa mikopo, kupigwa mizinga/kubom-iwa na kwa usalama wao pia?


Press on,


Edwin Seleli

Magreth Mkiwa

unread,
May 8, 2013, 9:02:41 PM5/8/13
to strictl...@googlegroups.com
kuna watu wenye kilema cha kutosema no? kila kitu kwao ni yes?.


From: SELELI EDWIN <selel...@gmail.com>
To: strictlygospel <strictl...@googlegroups.com>
Sent: Tuesday, 7 May 2013, 7:20
Subject: UKIPENDA KUA MTOAJI KUNA MAJARIBU YAKE SOMETIMES

--
Tafadhali zingatia msingi wetu ni Neno la Mungu, Lengo letu Kuujenga mwili wa Kristo, kushirikiana, amani na upendo. Yeyote yuko huru kuchangia, kufundisha, kukubali kufundishwa sawasawa na Msingi wetu Mkuu Neno la Mungu. Kujiunga na Team ya Injili au Maombi wasiliana nasi kwa simu 0714 915 424. Tuma Email. strictl...@yahoo.co.uk Facebook:https://www.facebook.com/pages/Strictly-Gospel/363180289370
 
Blog: www.strictlygospel.wordpress.com
 
Kujiondoa Kwenye Kundi Hili Tuma Email:
strictlygospe...@googlegroups.com
 
 


edmund oguda

unread,
May 9, 2013, 4:19:08 PM5/9/13
to strictl...@googlegroups.com
Dada Mkiwa,  ubarikiwee sana.nadhani, nako, huko kusema, YES, nayo nii Neema sana, especially zikiwapo ama zikikutembeleaga, na hata ikiwa hazipo, lkn, ktk ulimwengu w roho unaziona ziipo, na kuwa tayari ku sacrifice namna hiyo km hyo Mkaka. Mungu ambariki sana kwa kuendelea kusema YES, na aendelee mbele, kwani, ni uwezo w ule moyo ulioko ndani y hyo Mkaka, na huo moyo,., haujalishi km zipo, ama, hazipo, ni neema. Na mwengine, anazo kibao, na ht km hana zinamtembeleaga, lkn, ht ungaliihubiri juu ya kuwajali walio duni ama chini kimaisha, km Neema hyo hamna, itakuwa ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa, acheze, waaapi !!!                                                                                  Naam, kwa hbr za hyo kaka afanyeje  juu y huyo mama anayetaka kwenda kumwona Mch, yeye, ATULIE tu asikurupuke, ASUBIRI, km ATAITWA, AKAJITETEE mbele ya Kuhani, lkn, na AMUULIZE MUNGU, HEKMA juu y kumaliza hilo saga, sikiliza, RM aingilie kati maishani mwake.         Mubarikiwe.                    Oguda J.E.        


Date: Thu, 9 May 2013 02:02:41 +0100
From: mkiwam...@yahoo.co.uk
Subject: Re: UKIPENDA KUA MTOAJI KUNA MAJARIBU YAKE SOMETIMES
To: strictl...@googlegroups.com

elia kisigila

unread,
May 13, 2013, 6:38:29 AM5/13/13
to strictl...@googlegroups.com
Shalom wana SG wote! Napenda kutoa mchango wangu na angalizo juu ya mambo mengine tunayoyaandika humu... Awali ya yote huyo kijana hana haja ya kuogopa hapo, kama ni la Bwana litasimama tu ila kama ni la mwanadamu litaondoshwa... Wakati mwingine inaweza kuwa ni jaribu la huyo ndugu na pia inawezekana ni "DIVINE CONNECTION...." Tunatakiwa kuwa makini sana na kila kinachofanyika, wakati mwingine inawezekana Mungu ameyaweka mazingira hayo ili aupate ubavu wake. TUSIWAVUNJE MOYO watu kwa ajili ya utoaji, kwa maana kwa ujumbe huu inaanza kuonyesha kama watu waogope kutoa vile! Kitu ambacho sio sahihi hata kidogo. Mmebarikiwa



From: edmund oguda <oguda...@hotmail.com>
To: strictl...@googlegroups.com
Sent: Thursday, May 9, 2013 11:19 PM
Subject: RE: UKIPENDA KUA MTOAJI KUNA MAJARIBU YAKE SOMETIMES

Mathew Maduhu

unread,
May 14, 2013, 5:59:38 AM5/14/13
to strictl...@googlegroups.com

Shalom SG,

Kabla ya kushauri ni nini Mkaka huyo afanye, naomba nitoe maelezo yafuatayo. Kila kupenda kuna maudhi yake na  maudhi mengine ni endelevu. Biblia inatoa angalizo kuwa “Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa. – 2TIMOTHEO 3:12 (SUV msistizo added).  Na kama kusingekuwa na taabu katika kutenda mema Bwana asingetoa angalizo hili “Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho.” – GALATIA 6:9. (SUV msisitizo) Kuna kuchoka, kuna kuzimia roho. Ndiyo kusema kuna tatizo, ndiyo maana watu wanachoka na kuna ugumu ndiyo maana watu wanazimia njiani? Na haya yote yana chanzo chake – WAPENDWA (hapa nina maanisha Watumishi na Washirika kwa ujumla), hili ni TATIZO KUU.

 

Nina ujasiri katika hili, ninaandika haya kutokana na yale niliyoyaona katika muda wangu mfupi ktk wokovu. Hayo ambayo ‘mkaka’ huyu anayapitia, yapo katika makanisa mengi. Wapendwa wengine wamewafanya wenzao kuwa ng’ombe wa maziwa. Tumekosa kiasi na busara, tunaonyeshwa onyeshwa tu, lakini ukiangalia kunatokana na mtu kutaka sana msaada wa mhusika. Tuwaache watu watoe kwa moyo wa kupenda (KUTOKA 35:29) na kama alivyokusudia moyoni mwao (2KOR 9:7). Tusiwatolee nabii nyingi za kuwafanya watoe au kuwaona wao ndiyo mahala pa sisi kuponeapo, maana kwa kufanya hivyo tunawatwika mizigo ambayo mwisho itawalemea. Tabia kama hizi zinapaswa zikemewe kwa nguvu zote katika makanisa yetu. TATIZO jingine ni uchache wa wapendwa design ya ‘Mkaka’ huyu. Hivyo anapotokea mtu kama huyo, kila mpendwa hujikuta ‘anafukuzia’ hapo hapo na kumfanya mtoaji kukosa nafasi ya kupumua.

 

Sasa nitoe ushauri na kujibu maswali yaliyoulizwa kwa ujumla. Kwanza mkaka yule amshukuru Mungu kwamba kaguswa na kuwasaidia watoto wa mmama. Tatizo lingekuwa kubwa zaidi kama yule mmama angekuwa binti (anayempenda Mungu na mwenye uhitaji wa mme) na watoto wale ni wadogo zake wanaomtegemea mdada huyo, issue yake ingekuwa TOUGH kweli kweli. Kwa maana hilo lililomtokea mama wa wototo wale ni jambo la kawaida kabisa katika maisha haya, ni swala la kuchukuliwa kikawaida tu. Hisia zake zimeguswa mpaka akafikia kumdodokea kijna wa watu, huo ndiyo muono wangu. Kuna matukio mengi sana ya namna hii yamatokea, na hata watu wengine wameitumia hii kama njia ya kupata wanachokita – kugusa hisia za mtu. Kuna wadada wengi tu wamekubali kuolewa kwa kulipa fadhila walizofanyiwa!!! Hivyo tendo la mama huyo kutaka kumwona Mama Mchungaji lisimhuzunishe Mkaka yule. Hizo ni reaction baada ya mama yule kuguswa hisia zake. Ni vema likifika haraka kwa Mama Mchungaji, ili Mkaka awe huru kuwasaidia watoto wale wanaokosa msaada kwa sababu ya hisia za mama yao. Pia mama yule aelezwe ukweli huu kwamba, hisia zake azizuie kwa maana zinafanya watoto wake wakose msaada, asiwe mbinafsi kiasi hicho.

 

Kuhusu wingi wa wapendwa kutaka msaada kwa Mkaka huyu, Biblia inasema “Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.” – GALATIA 6:10 (SUV msisitizo added). Haijalishi ni wangapi na mara ngapi (frequency), Mkaka wewe angalia ni kwa kadiri utakavyopata nafasi. Usifanye kwa kulazimika au huzuni bali kwa moyo mkunjufu. Wakati nafasi hairuhusu waambie wapendwa ukweli huo na simamia usimamo huo. Nionavyo mimi sio vizuri kutojibu sms zao, badala yake ajivike ujasiri na kuwajibu sasa hivi sina nafasi ya kuwasaidia. Anapotaka kutoa, afanye kana kwamba yeye ndiye aliyeona mtu fulani ana tatizo hilo na ndipo achukue hatua ya kutoa.

 

Na hili la kuchangia kwa kutaja kiwango kwenye Public ya wapendwa, linaweza kutatuliwa na yule anayehamasisha michango kwa kuwaeleza KUSANYIKO mapema, atoe angalizo la maneno kama watakao ahadi hapo hamaanishi kuwa wao ndiyo wenye kipato kikubwa, au ahadi hizi zisichukuliwe na wapendwa kuwa watakaoahidi hapa ndiyo tiketi ya watu kwenda kuwaomba misaada mbali mbali kwao.

Naona nimeandika sana, niishie hapa.

 

Keep on watching,

Mathew.



This email and any attachments may contain confidential information for intended recipient only. If you have received this email in error please notify the sender. Note that any copying, disclosure or distribution of the message is strictly prohibited. Email recipient(s) should check this email and any attachments for viruses. Tanesco will not be liable for any damage caused by virus.

Daniel Nzali

unread,
Jun 27, 2013, 7:41:28 AM6/27/13
to strictl...@googlegroups.com
Brother SELELI,

  Nimejifunza mambo mengi kupitia habari hii.Na mengine yananigusa direct.. Mwisho wa habari hiyo umeuliza swali kuwa ni ushauri wa namna gani utolewe kumsaidia huyokaka..

Labda tu niseme kitu hiki, Wakristo wengi tunaomjua Mungu tunafanya mambo bila kumuhusisha na kufuata uongozi wa Roho Mtakatifu. Iwe ni katika kuombea mahitaji,au kuchagua kazi ya kufanya na hata katika Utoaji pia nk. Maana kama ni suala la utoaji tu, watu wenye uhitaji ni wengi kuliko unavyoweza kuwasaidia.Kwa hiyo mtu ukiamua kutoa tu bila kibali cha Mungu ndio unaweza kujikuta umejiingiza katika matatizo fulani ambayo kuchomoka kwake itakuwia vigumu kwa kuwa hukumshirikisha Roho Mtakatifu.

Kwa habari ya huyu kaka,kama kweli utoaji wake ulikuwa instructed na RM,katika jaribu alilonalo haitamuwia vigumu kwa yeye kuweza kulivuka salama tena bila hofu yoyote.

Uongozi wa Roho Mtakatifu ni kila kitu Brother SELELI. Mara nyingi huwa napata shida hata pale unakuta mtumishi fulani anatangaza kwa mfano '' KUTAKUWA NA MKUTANO WA INJILI,WALETE VILEMA,WENYE MAGONJWA, VIPOFU NAO WATAPONYWA'' Sasa  unajiuliza huyu Mtumishi yeye ndio Roho Mtakatifu ? au anampangia Roho Mtakatifu kazi ya kufanya.. Maana matendo Makuu ya Mungu yanafanyika ili kulithibitisha Neno lake.Na anafanya apendavyo yeye.. Sasa Mtumishi huyo akitangaza kwa style hiyo ndio mara nyingi unakuta Watu wanafika kwenye Mkutano wakitegemea Miujiza.Na hapo ndio utakuta Mtumishi anafanya Maombi kwa nguvu zake mpaka unakuta sauti imekauka,then anaishia kusema muhusika hana Imani pale na matokeo yake watu wanatoka Mkutanoni badala ya Kumtukuza Mungu inakuwa kinyume.

The same story hata katika utoaji, nafikiri si vyema sana kutoa bila kupata Maelekezo kutoka kwa Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu ndiye anayeweza kukuongoza nani Umsaidie na nani umwache. Ki ukweli mimi kama mimi kuna baadhi hata ya Michango ya Kanisa sometimes kuchangia huwa naona Roho yangu haijaguswa kabisa. Na hali kama hiyo ikinitokea huwa sitoi kabisa.
 
Ubarikiwe!


From: SELELI EDWIN <selel...@gmail.com>
To: strictlygospel <strictl...@googlegroups.com>
Sent: Monday, 6 May 2013, 22:20

Subject: UKIPENDA KUA MTOAJI KUNA MAJARIBU YAKE SOMETIMES

Mary Smith

unread,
Jun 27, 2013, 11:39:08 AM6/27/13
to strictl...@googlegroups.com
Imeandikwa wanaoongozwa na Roho wa Mungu ao ndiyo wana wa Mungu , huyo kaka kweli ana moyo wa kusaidia lakini ninamuombea ajifunze kutoa pale anapoongozwa na Roh mtakatifu kutoa, maana shetani anaweza kumpiga chenga  pesa yake ikaenda hata sehemu ambazo azipaswi kwenda.
 Pia asiwe na hofu kwa habari ya yule mama single, maana  wanadamu wanatazama sura za nje lakini Mungu uangalia mioyo 1 Samwli 16:6-7.
Ikitokea yule mama single akamsingizia yule kaka kwa lolote baya ambayo yule kaka hakutenda kaka asiwe na hofu maana Mungu ndiye mwamuzi wetu, ndiye mtoa sheria .Isaya 33:22. Ipo siku Mungu atafichua ukweli .
 Pili ajitahidi sana asiwe anatoa pesa na kusaidia hovyohovyo  pasipo uongozi wa Roh mtakatifu, na hasa kwa watu wanaokuja kumuomba pesa huwezi kujua ile pesa wanakwenda kufanyia kitu gani, cha kumletea Mungu utukufu au cha kufanya jina la Mungu litukanwe mitaani?
 Hii ninasema kwa kuwa na mimi yaliwahi kunikuta , nilikuwa nikimsaidia bibi fulani natuma pesa kwake imsaidie kununua sukari , chumvi, mafuta ya taa ngou n.k.
 nikaja kuambiwa na mtu wa karibu sana na yule bibi mjukuu wake  kuwa kila ninapotuma pesa kwa yule bibi anazitumia kwenda kwa waganga wa kienyeji AUCH!!!!!. it was a big pain in my heart. Nilijisikia kama huyu bibi alitaka nijiudhuru ktk wokovu, kwa kuwa niliona anafanya mambo ya kulifanya jina la Mungu wangu litukanwe , na kibaya zaidi alikuwa akienda kwa waganga wampe dawa yenye nguvu zaidi amfanyie mama yangu mimi hili mama  awe kichaa maisha yake yote . Lakini Mungu hakuacha anionee wala amtese mama yangu , ameshindwa ktk jina la Yesu . mimi ni nuru na kamwe giza haliwezi kuishinda nuru , nimeshinda na mama yangu ameshinda , na shimo alilokuwa akichimba kwa ajiri yetu yule bibi  amedumbukia yeye mwenyewe.
Zaidi ya yote yule kaka asije akajisikia vibaya mara atakapopangua  kuacha kusaidia watu wa style aliyokuwa anatumia kusaidia , nasema asiumie asipoona hajamsaidia mtu fulani akija kumuomba, hapa swala si kusaidia watu wote wanaokuja mbele yako , swala ni kuongozwa na Roh mtakatifu akuonyeshe na athibitishe  kwake ni  nani amusaidie na ni nani asimusaidie . Roh mtakatifu ndiye amusaidie yule kaka kufanya maamuzi ya Mwisho ktk kutoa. na hii itamsaidia kuwa na amani. Mbarikiwe sana wateule wa Bwana. ninawapenda . Mama K.

From: Daniel Nzali <nza...@yahoo.com>
To: "strictl...@googlegroups.com" <strictl...@googlegroups.com>
Sent: Thursday, June 27, 2013 7:41 AM
Subject: Re: UKIPENDA KUA MTOAJI KUNA MAJARIBU YAKE SOMETIMES
Brother SELELI,

  Nimejifunza mambo mengi kupitia habari hii.Na mengine yananigusa direct.. Mwisho wa habari hiyo umeuliza swali kuwa ni ushauri wa namna gani utolewe kumsaidia huyokaka..

Labda tu niseme kitu hiki, Wakristo wengi tunaomjua Mungu tunafanya mambo bila kumuhusisha na kufuata uongozi wa Roho Mtakatifu. Iwe ni katika kuombea mahitaji,au kuchagua kazi ya kufanya na hata katika Utoaji pia nk. Maana kama ni suala la utoaji tu, watu wenye uhitaji ni wengi kuliko unavyoweza kuwasaidia.Kwa hiyo mtu ukiamua kutoa tu bila kibali cha Mungu ndio unaweza kujikuta umejiingiza katika matatizo fulani ambayo kuchomoka kwake itakuwia vigumu kwa kuwa hukumshirikisha Roho Mtakatifu.

Kwa habari ya huyu kaka,kama kweli utoaji wake ulikuwa instructed na RM,katika jaribu alilonalo haitamuwia vigumu kwa yeye kuweza kulivuka salama tena bila hofu yoyote.

Uongozi wa Roho Mtakatifu ni kila kitu Brother SELELI. Mara nyingi huwa napata shida hata pale unakuta mtumishi fulani anatangaza kwa mfano '' KUTAKUWA NA MKUTANO WA INJILI,WALETE VILEMA,WENYE MAGONJWA, VIPOFU NAO WATAPONYWA'' Sasa  unajiuliza huyu Mtumishi yeye ndio Roho Mtakatifu ? au anampangia Roho Mtakatifu kazi ya kufanya.. Maana matendo Makuu ya Mungu yanafanyika ili kulithibitisha Neno lake.Na anafanya apendavyo yeye.. Sasa Mtumishi huyo akitangaza kwa style hiyo ndio mara nyingi unakuta Watu wanafika kwenye Mkutano wakitegemea Miujiza.Na hapo ndio utakuta Mtumishi anafanya Maombi kwa nguvu zake mpaka unakuta sauti imekauka,then anaishia kusema muhusika hana Imani pale na matokeo yake watu wanatoka Mkutanoni badala ya Kumtukuza Mungu inakuwa kinyume.

The same story hata katika utoaji, nafikiri si vyema sana kutoa bila kupata Maelekezo kutoka kwa Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu ndiye anayeweza kukuongoza nani Umsaidie na nani umwache. Ki ukweli mimi kama mimi kuna baadhi hata ya Michango ya Kanisa sometimes kuchangia huwa naona Roho yangu haijaguswa kabisa. Na hali kama hiyo ikinitokea huwa sitoi kabisa.
 
Ubarikiwe!

Jacob Issack

unread,
Jun 28, 2013, 11:47:42 PM6/28/13
to strictl...@googlegroups.com
Duh, hii kali ila zimekuwa ni tabia za baadhi ya wapendwa wanapomwona
mtu km huyo ktmfanyia vitendo km hivyo,kiukweli ni kero na vinavunja
moyo wa kuendelea kumtolea Bwana.ushauri wangu..akaze ktk maombi na
asiache kutoa hata kwa wale watoto.mbarikiwe.

On 5/6/13, SELELI EDWIN <selel...@gmail.com> wrote:
> Hellow SG,
> **
>
> **
> alipomaliza kulia, akamwambia, ‘*Mungu wa mbinguni anajua haja yako,
> husipozimia moyo, atakudhibitishia kua anakupenda, tusonge mbele na mambo
> haya ya mimi na wewe kua mwili mmoja, yasiwepo tena baada ya leo maana kwa
> hakika hakutakuwepo ndoa iyo ila itakuwepo nyingine ambayo BWANA atakupa
> wewe mume bora na mimi, mke mwema’,* kisha akaomba na wakaachana. Kuanzia
> *Maswali ya kutafakari*
>
> *
> *
>
> Unamshauri nini Mkaka ktk kikao kijacho ambacho kwa kweli hakipendi kwa
> heshima aliyo nayo kanisani, anajisikia kama atashusha P?
>
>
>
> Au unadhani pengine Mkaka anakosea sana mpango/target kamili ya Mungu kwa
> kumkatalia singe mother pengine angeomba seriously, kweli single mother
> angethibitishwa kua ndiye wife?
>
> Mkaka afanye nini/ali-relate vipi na watoto waliokwisha kua na raha sana,
> kupenda sana kanisa, kua na uhakika kila jumapili baada ya ibada wana
> breakfast na bila shaka wakampenda sana Yesu kwa jinsi Mkaka alivyowa-care
> lakini ameacha kwa kua Mama yao ameingiza agenda nyingine na anawatumia
> kama chambo au point of contactig Mkaka?
>
>
> Akikataa kutohusika kwa lolote kihuduma za kutoa/ku-care for uko Wilayani,
> akiwapangua wapendwa wote wa uko na kubaki na wa Dar including kuwakwepa
> vibaya sana kwa kutojibu sms, call zao wanapokuja Dar ili wasifikie kwakwe
> la sivyo watapafanya a permanent centre kila wajapo jijini tena na ndugu na
> jamaa zao au hata Kwaya nzima inapokuja kurekodi, je amepungukiwa upendo?
>
>
> Kwakua ktk changizo, ni mazoea siyo Bible, watu hutaja hadharani viwango(si
> kama sadaka), wale wapendwa wenye nazo, wanapotaja halafu kila likitokea
> jambo la idara za kanisa, binafsi, wapendwa huenda kuomba msaada kwao,
> mpaka wanalemewa na wengine walishafanyiziwa kwa kukabwa baada ya kutoka
> ibadani, je watoeje changizo? Kimya kimya kwa kuogopa kuombwa na wapendwa
> mikopo, kupigwa mizinga/kubom-iwa na kwa usalama wao pia?
>
>
> Press on,
>
>
> Edwin Seleli
>

SELELI EDWIN

unread,
Jun 28, 2013, 8:26:48 PM6/28/13
to strictl...@googlegroups.com
Nzali Daniel and dada Mary Smith,

Wonderful inputs and great ufafanuzi, shuhuda, angalizo and Word sharing, nime note pia vya kuviingiza ktk matendo. Much blessings  as you come here  more and more vivid.

Press on,

Edwin Seleli

2013/6/27 Daniel Nzali <nza...@yahoo.com>
Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages