Amani ya Bwana iwe nanyi enyi nyote,
Katika Biblia, tunaona maeneo kadhaa NENO/HABARI NJEMA inafikishwa kwa njia ya mazungumzo au maongezi ya Mtu na Mtu au Mtu na kikundi mfano Yesu na Nikodemusu, Zakayo, Farisayo Tajiri, Msamalia Kisimani, Kijana Tajiri, Wanafunzi wake, Wote aliowaponya, pia Filipo na Tohashi wa Kushi, Paul na Agripa na Festos, Mlinzi wa gereza nk, Petro na Wanadamu siku ya pentekoste, Wakuu na Watu, kwa Kornelio, Hekaluni Nje baada ya kuponya kiwete nk
Hii leo Wengine hadi
Mtu anapaliwa na kukohoa….’’okohooo kohooooo’’.., anapiga chafya, ana hema
mithili ya mbio za Marathoni, mic anayotumia inajaa ‘’natural mvua’’ kiasi
kwamba mwingine kuitumia baada yake ni kinyaa na perfume ya kutisha sana yatoka
pale. Mtu toka dk moja anashika Biblia
hata salamu tu yaani ni kuwaka tu kwa sauti kubwa, mfurulizo bila pozi. Yawezekana
tuko sahihi au la, kama tuendelea au tuwe tuna adjust wakati mwingine. Kupata
ufahamu wa hili ili kila mmoja aamue kibyake-vyake ama kuendelea kufyatuka nonstop
au ku-adjust, Embu tule Neno hapa kwa kuchunguza Maandiko haya yanayoonyesha
Watumishi wakihubiri na kufundisha Neno
Mathayo: Sura zote za 5, 6, 7...YESU anafungua kinywa na kuanza kuwafundisha AKISEMA hapo sura zote na aliyosema yanafahamika kama HOTUBA/UJUMBE WA/YA MLIMANI…Alihutubu/hubiri/fundisha.
Luka.3:2-19… Hapa Yohana Mbatizaji anaanza kuwahubiri Watu AKAWAAMBIA ”7 Yohana AKAWAAMBIA wale waliokuja ili awabatize, “Enyi watoto wa nyoka! Ni nani aliyewaonya muepuke hukumu ya Mungu ita kayokuja? Yuko tayari na pepeto lake mkononi, tayari kusafisha mahali pake pa kukusanyia mazao. Nafaka safi ataiweka ghalani lakini makapi atayachoma kwa moto usiozimika.”18 Yohana alitumia mifano mingine mingi KUWAONYA watu na KUWATANGAZIA Habari Njema.
Matendo. 2:14-47.. Petro anaongea na Watu baada ya ujazo wa RM na Wananchi kushangaa kusikia kila Mtu na lugha yake toka unenaji lugha mpya waliokua wanasema Wanafunzi, Watu wengine kuwadhihaki Wanafunzi kua walikua wamelewa, ndipo Kamanda Patro ANAPAAZA/INUA SAUTI YAKE kisha kusema Neno la Mungu hadi mstari wa 37, imeandikwa kua ‘’ Basi, watu waliposikia hayo, walichomwa moyo, wakawauliza Petro na wale mitume wenzake: "Ndugu zetu, tufanye nini?"
Matendo. 6:8-16 na 7:1-60.. Stephano anafanya miujiza na ishara nyingi kisha analetwa ktkt ya Baraza la Wakuu wa Watu na Dini naulizwa na akawambia Ndugu na Baba, SIKILIZENI.. kisha akaendelea hadi sura ya 7:51-54 … “Ninyi watu wenye shingo ngumu! Wenye mioyo ya kipagani! Mmekuwa viziwi kwa neno la Mungu wala hamchoki kumpinga Roho Mtakatifu! Kama walivyofanya baba zetu nanyi leo mnafanya vivyo hivyo. 52 Je, kuna nabii hata mmoja ambaye baba zetu hawa kumtesa? Waliwaua hata wale waliotabiri habari za kuja kwake yule Mwenye Haki, ambaye ninyi mmemsaliti kisha mkamwua. 53 Ninyi mlizipokea sheria za Mungu zilizoletwa kwenu na malaika lakini hamkuzitii.”54 Basi wale viongozi waliposikia maneno haya walijawa na hasira, wakasaga meno yao kwa ghadhabu.
Mdo. 3:1-26. Baada ya kumponya kiwetu wa Mlango Hekaluni,2 Petro alipoona watu wamekusanyika ALIWAAMBIA, “Watu wa Israeli, kwa nini mnastaajabu kuhusu jambo hili? Mbona mnatukazia macho kwa mshangao? Mnadhani ni kwa uwezo wetu au utakatifu wetu tumemwezesha mtu huyu kutembea? 13 Sivyo! Mungu wa Ibrahimu na Isaka na Yakobo na wa baba zetu amemtukuza mtumishi wake Yesu kwa muujiza huu. Ninyi mlimtoa ahukumiwe kifo na mkamkana mbele ya Pilato ijapokuwa Pilato alitaka kufuta mashtaka na kumwachilia. 14 Ninyi mlimkataa aliyekuwa Mtakatifu na Mwenye Haki mkaomba mpewe yule muuaji. 17 “Na sasa ndugu zangu, najua ya kuwa mambo mliyomtendea Yesu, ninyi na viongozi wenu, mliyafanya kwa kutokujua
Mdo.4:1-22.. 8 Petro, akiwa amejawa na Roho Mtakatifu AKAJIBU, “Waheshimiwa viongozi na wazee wa watu, 9 kama mnatuhoji kuhusu mambo mema aliyotendewa kilema, na jinsi alivyoponywa, tungependa ninyi na watu wote wa 10 Israeli mfahamu kwamba, ni kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye ninyi mlimsulubisha lakini Mungu akam fufua kutoka kwa wafu, kwa uwezo wa Yesu, huyu mtu anasimama mbele yenu akiwa mzima kabisa. 11 Huyu Yesu ndiye ‘lile jiwe ambalo ninyi wajenzi mlilikataa, ambalo limekuwa jiwe kuu la pembeni.’ 12 Wokovu unapatikana kwake tu; kwa maana hakuna jina jingine duniani ambalo wamepewa wanadamu kuwaokoa ila jina la Yesu, na ni kwa jina hilo peke yake tunaweza kuokolewa!”
Mdo. 17:22-24… 22 Kwa hiyo Paulo alisimama kati kati ya Areopago akasema, “Ndugu wa Athene! Nimeona katika kila jambo kuwa ninyi ni watu wa dini hasa. 23 Kwa kuwa nilipokuwa nikitembea mjini niliona sehemu nyingi za kuabudia. Niliona pia madhabahu moja iliyoan dikwa, ‘Kwa Mungu asiyejulikana.’ Huyo Mungu mnayemwabudu bila kumfahamu, ndiye ninayemtangaza kwenu. 24 Mungu aliyeumba dunia na vitu vyote vilivyomo, ambaye pia ni Bwana wa mbingu na nchi, haishi katika mahekalu yaliyojengwa na wanadamu.
Mdo.18:24-28….26 Apolo ALIHUBIRI/ONGEA kwa ujasiri mkubwa katika sinagogi. Lakini Prisila na Akila walipomsikiliza walimchukua nyumbani kwao wakamfundisha njia ya Mungu kwa ukamilifu zaidi. 27 Na alipoamua kwenda Akaya, ndugu wa Efeso walimtia moyo wakampa na barua ya kumtambulisha kwa ndugu wa huko. Alipofika aliwasaidia sana watu wengi ambao kwa neema ya Mungu walikuwa wameamini; 28 maana kwa uwezo mkubwa aliwakanusha hadharani Wayahudi waliokuwa wakipinga Habari Njema kwa kuwaonyesha kutoka katika Maandiko kuwa Yesu ndiye Kristo.
MASWALI:
Kutoka ktk maandiko hayo, how do u feel/see the Preachers-JESUS, PETRO, PAUL, STEPHANO, APPOLO, FILLIPO? Walikua wanafyatuka na kupasuka mwanzo mwisho kwa sauti kubwa, kelele na vurugu nyingi?
Kama kuna Wakati Mungu aliwaambia baadhi ya Watumishi-Manabii na Mitume kupiga kelele/kupaaza sauti-kusema Neno lake/kuonya Wanadamu, Je haikua so SPECIFIC kwao tu? kwa nini sisi inakua kama ndio staili ya kiiiila tusimamapo kusema Neno ni kuwaka tu, kuupaaza sauti, kupiga kelele na kuunguruma?
Je Tunaweza kukubaliana
kua jinsi tuhubirivyo leo, ni mambo ya kibinadamu zaidi na si fasheni ya
kuhubiri iliyomo ktk Biblia?
Na kama tuhubirivyo leo ni ya kibinadamu tu labda kwa sababu ya utamu wa kuhubiri na kufundisha kitu kitamu na unachokipenda ktk Neno au kile ulicho na ‘maconfo’ nacho kwa sababu umekisomea Chuoni au kukisoma na kujiandaa vema kabisa au kwa kua unafahamu kwa moyo na mzigo umuhimu wa ujumbe wako kwa wanadamu ili wapone ndio maana tunakua na munkari, makeke, vurugu, kufoka, kuwaka, kupiga kelele, basi kumbe tunaweza ku-adjust wakati mwingine, tukawa na staili nyingine na si kila siku kukoroma/unguruma kama Simba dume au kufyatuka kama tuna hasira kila mara ya BWANA kumbe na ya kwetu humo humo, imo imo tunaikatia ka-kiu kidogo kwa kwa Wanadamu hawatusikii na wanatubeza wakati tunawapenda ili waokoe maisha yao kwa Neno la Upatanisho tulilopewa?
SIJASEMA KUA NI DHAMBI KUKOROMA/UNGURUMA/FYATUKA KAMA FATAKI ZA MWAKA MPYA ILA FIKIRI TU KWAMBA, JE KUNA ULAZIMA WA KUHENYESHA NA KUUMIZA KOO, KOROMEO, PUA, ULIMI, MBAVU, MGONGO, KIFUA NA HASA HASA ‘’VOCAL CORDS’’? = olds of membranous tissue that project inward from the sides of the larynx to form a slit across the glottis in the throat, and whose edges vibrate in the airstream to produce the voice.
Press on.
Edwin Seleli
![]() |
|
Salamu kwako Edwin!
Dan!!! utafiti nzuri kabisa!!!! Umegundua neno zuri linalo jibu fupi kabisa.
Niwatangazie wanaofundisha wote hivi: "Acheni RM ndiye awape style ya kutumia, wala msijiandae kufoka, nk... bila RM kuwaagiza"
Anyway, ikiwa RM ndiye anaingilia kati vyote ni vizuri. Si wakati wa makesha, watu huimba mpaka vacal cords zinapata shida? Ikiwa ni RM anaeagiza, hizo vacal cords zitalindwa tu. Na kama zikiharibika kwa utukufu wa Mungu, haya....
Mara na mara tunaona walimu tuliozoea wakiwa "wataratibu" kama ndugu yangu Seleli anavyosema, siku nyingine, tunawaona wakifoka!!!!! Heeeeee, kumbe anaehubiri si mtu, bali RM. Na hilo shule la RM halikwepeki.
Aibu ni kwamba kuna wengine wanaoiga. Tuwaache wafikie kiwango cha kuiga kukemea pepo wachafu..... heee.... watawachanachanaaaaaaaa,. watawaambia: "Yesu, tunamjua lakini ninyi hamjulikane".
Yesu Kristo akubariki kaka yangu.
Alphonse Ziragora ![]() ----Message original-------
De : Seleli Edwin
Date : 04/06/2014 03:27:32
A : strictlygospel
Sujet : TUFOKE-FOKE, KUUNGURUMA, KUFYTUKA SAUTI KUBWA AU YA TARATIBU NA KAWAIDA WAKATI WA KUFUNDISHA AU KUHUBIRI NENO? |
-- Tafadhali zingatia msingi wetu ni Neno la Mungu, Lengo letu Kuujenga mwili wa Kristo, kushirikiana, amani na upendo. Yeyote yuko huru kuchangia, kufundisha, kukubali kufundishwa sawasawa na Msingi wetu Mkuu Neno la Mungu. Kujiunga na Team ya Injili au Maombi wasiliana nasi kwa simu 0714 915 424. Tuma Email. strictl...@yahoo.co.uk Facebook:https://www.facebook.com/pages/Strictly-Gospel/363180289370 Blog: www.strictlygospel.wordpress.com Kujiondoa Kwenye Kundi Hili Tuma Email: strictlygospe...@googlegroups.com |
Key words: Kufundisha na Kuhubiri Neno na hata maandiko ya Watu waliohubiri nimetoa, swala la kufyatuka wakati wa kukemea, ni issue nyingine kwa mada hii.
Press on,
Edwin Seleli
Hizo ni mbembwe zinazotumika ili kuonyesha kuwa "uwepo" umeshuka! Wengine wanazutumia hata kwenye maombi.
--