DHAMBI INAYOZINGA/NG’ANG’ANIA KWA UPESI!!!!!!

71 views
Skip to first unread message

Seleli Edwin

unread,
Apr 27, 2014, 2:32:01 PM4/27/14
to strictlygospel

Amani ya Bwana iwe nanyi enyi nyote,


Mambo mengine ukisoma ktk Neno ni kama ya kawaida  na unapita kwa haraka shwaap!  lakini siku nyingine ukisoma hapo hapo, ghafla unasimamishwa taap! Halafu unaangalia/tafakari kisehemu cha Neno/sentensi au sentence nzima kama si nusu au sura nzima then ghafla inakua kama inafunuka kwa upya au inakusitua/kubip upaangalie kwa upya na kisha ukitekeleza, unashangaa sana kua ivi icho kisehemu kilikuwepo hapo kila siku unasoma au kimewekwa jana!


Imeandikwa:


Waebrabia: 12:1- Sisi tunalo kundi hili kubwa la mashahidi mbele yetu. Kwa hiyo tuondoe kila kizuizi kinachotuzuia, NA DHAMBI ILE INAYOTUNG’ANG’ANIA. Tupige mbio kwa uvumilivu katika mashindano yaliyowekwa mbele yetu


Hebrews: 12:1..Therefore then, since we are surrounded by so great a cloud of witnesses [who have borne testimony to the Truth], let us strip off and throw aside every encumbrance (unnecessary weight) and that SIN WHICH SO READILY (deftly and cleverly) CLINGS TO AND ENTANGLES, and let us run with patient endurance and steady and active persistence the appointed course of the race that is set before us, …AMP-Bible


Hebrews: 12:1: Therefore, since we are surrounded by such a great cloud of witnesses, let us throw off everything that hinders and the SIN THAT SO EASILY ENTANGLES US. And let us run with perseverance the race marked out for us-NIV-Bible


MASWALI: ( Yako A hadi F, mengine yanajitegemea na mengine yanajirudia ili kufafanua mengine au angaliza issue zingine/interested)


A: Ni ipi iyo dhambi inayotu au taka kututait/kamata/suffocate so easily/sharply/faster?


B: Kila mmoja anayo yake spesheli inayomuwinda/nyemelea nini au zipo na tuna-share kwa kua wote tu Wanadamu?


C: Kwani iyo dhambi inatoka wapi jamani wakati tulisha takaswa na kusamehewa? Kwa devo, dunia hii au tunazalishaga wenyewe?


D: Kama inayotokana na sisi Wanadamu, source yake ni yale ma-file na ma-folder ya Misri nini? Kwani  Misri softwares si zilishagavunjiliwa mbali siku ile tulipoamua kutwaa softwares za Canaan au?


E: Kwanini ni kweli kabisa kama Mtu akitaka kua mkweli wa nafsi yake kwamba, zile dhambi za zamani kabla ya kuja nuruni, ndizo izo izo waga sometimes zinakuja kusabahi na ku-cross-cross by your side? Why? Kwani utakaso haukufuta hata iyo memory card/experience ya kidevo na kimwili cha kale?

 

Zingatia  maandiko haya pia

Mwanzo: 4: 1-7:1  Adamu akamjua Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema, Nimepata mtoto mwanamume kwa Bwana. 2  Akaongeza akamzaa ndugu yake, Habili. Habili alikuwa mchunga kondoo, na Kaini alikuwa mkulima ardhi. 3  Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana. 4  Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake; 5  bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana. 6  Bwana akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana? 7  Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.

Notice: Mungu anamwambia Kaini kua kuna dhambi inamuotea!(sin is crouching at your door; it desires to have you)

Warumi: 7:13-23: 13Kwa maana twajua ya kuwa torati asili yake ni ya rohoni; bali mimi ni mtu wa mwilini, nimeuzwa chini ya dhambi. 14  Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda. 15  Lakini kama nikilitenda lile nisilolipenda, naikiri ile sheria ya kuwa ni njema. 16  Basi sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu 17  Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati. 18  Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo. 19  Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu. 20  Basi nimeona sheria hii, ya kuwa kwangu mimi nitakaye kutenda lililo jema, lipo lililo baya. 21  Kwa maana naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani, 22  lakini katika viungo vyangu naona sheria iliyo mbali, inapiga vita na ile sheria ya akili zangu, na kunifanya mateka ya ile sheria ya dhambi iliyo katika viungo vyangu. 23 Ole wangu, maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?

Notice: Paul analalamika/analia kua anatumikia dhambi na mwili wa mauti, kizuri anachotaka kufanya chema, hakifanyi na kibaya ambacho hataki kufanya, anakifanya!

F: Dah! Tunabalance vipi KWELI moja kua sisi ni VIUMBE VIPYA NA TUMESHATAKASWA na equally KWELI nyingine kua KUNA DHAMBI au UMAUTI ndani ya MWILI huu ambao pia ni Hekalu la Roho Mtakatifu, unatamaniwa na DHAMBI inayokua beneti-beneti na sisi? Aisee! dah!


Press on,


Edwin Seleli

Imani Kapinga

unread,
Apr 29, 2014, 10:54:54 AM4/29/14
to strictl...@googlegroups.com
Kaka Seleli

Mwili mwili, hauna jema, mwili haupendi kutenda yampendeayo Mungu.

Mwili unatiishwa na kiwango cha investment yako kiroho. Kila mtu kuna dhambi flan zilikuwa ni burudani zakeau utumwa kwake  back then so ni silaha ya kwanza shetani ataitumia kumshawishi nayo. Mfano mie hata kabla sijaokoka sikuwahi kuipenda pombe so anajua hata nikikaa mahali watu wanatwanga mipombe walasishtuki lkn kuna mwingine (esp ukiwa bado mchanga) inakudondosha easily. 

Kuna dhambi  zinahitaji mikakati madhubuti si kiroho tu bali kimazingira, kijamii(marafiki au ndugu) kuishinda. Hata ufunge vipi huwezi kudhani utaushinda uzinzi wakati kila siku unatoka, kuwasiliana na kuvinjari na kimada wako.........hapo i hekima ya kujidiscipline na kujitenga na watu ama mazingira.

Kuna dhambi nyingine sijui ndo miiba yenyewe, zipo around sana zinahitaji neema kila kukicha coz kila kukicha zina-kuwait....Unaweza kushinda ulevi/uchawi once and for all LKN imagine umbeya, chuki, visasi, wakwazaji wamejaa kila kona, home, ofsn, kanisani kila mahali

Tunahitaji neema na jitihada binafsi kila siku kuchukia dhambi za aina zote km ngozi ya mwili inavyohakikisha haichoki kuulinda mwili kwa kutoruhusu au kupambana na aina zote za wageni wanaotaka kuingia ndani na kuharibu systems. Tusichoke kuubu na kumlilia Mungu, as long as tunaishi hatujawa wakamilifu BUT 'WE PRESS ON TOWARDS PERFECTION'

Tujitie nguvu kwa haya
2 Wakorintho 12
7 Na makusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa mafunuo hayo nalipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani ili anipige, nisije nikajivuna kupita kiasi. 8 Kwa ajili ya kitu hicho nalimsihi Bwana mara tatu kwamba kinitoke.9 Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.10 Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu.

Galatia 5;
6 Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.17 Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.18 Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria.19 Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, 21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu. 22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, 23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. 24 Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.25 Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.
 


--
Tafadhali zingatia msingi wetu ni Neno la Mungu, Lengo letu Kuujenga mwili wa Kristo, kushirikiana, amani na upendo. Yeyote yuko huru kuchangia, kufundisha, kukubali kufundishwa sawasawa na Msingi wetu Mkuu Neno la Mungu. Kujiunga na Team ya Injili au Maombi wasiliana nasi kwa simu 0714 915 424. Tuma Email. strictl...@yahoo.co.uk Facebook:https://www.facebook.com/pages/Strictly-Gospel/363180289370
 
Blog: www.strictlygospel.wordpress.com
 
Kujiondoa Kwenye Kundi Hili Tuma Email:
strictlygospe...@googlegroups.com



--
Imani Kapinga

Titus 2;10-14; 
For the grace of God has appeared, bringing salvation for all people, training us to renounce ungodliness and worldly passions, and to live self-controlled, upright, and godly lives in the present age,waiting for our blessed hope, the appearing of the glory of our great God and Savior Jesus Christ.

Seleli Edwin

unread,
May 1, 2014, 1:08:17 AM5/1/14
to strictlygospel
Imani Kapinga,

U made it! look at this.......'''Kuna dhambi nyingine sijui ndo miiba yenyewe, zipo around sana zinahitaji neema kila kukicha coz kila kukicha zina-kuwait....Unaweza kushinda ulevi/uchawi once and for all LKN imagine umbeya, chuki, visasi, wakwazaji wamejaa kila kona, home, ofsn, kanisani kila mahali'''....... thas good point of understanding pia hiki kipande nimecheka kweli hiki...''' dhambi nyingine zipo around sana ..... coz kila kukicha zina-kuwait''''..... tehe tehe...kweli aisee, dah!

Asante kwa maandiko pia, great and meaning is your  LIVELY fellowship  in here, aiiiiimen

Press on,

Edwin Seleli

Alphonse Ziragora

unread,
May 2, 2014, 3:25:34 AM5/2/14
to strictl...@googlegroups.com
Mpendwa Seleli,
 
Topic yako ni ya maana sana ndugu yangu kwani ni wengi wanaojiswali , pengine hawapati jibu.
 
Nalipoitafakari, niliona mambo yote yamefungwa katika kifungo kile ulichotutolea cha Warumi: 7:13-23.
 
Pia Paulo akasema: "2Timotheo 4: 6-7: Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika.
 Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda;"
 
Hivi Paulo, pamoja na imani aliyokuwa nayo na upako mwingi kutoka RM, ilihitajika apige vita.  Hiyo vita ni ya kulinda imani ya roho wakati mwili inampeleka dhambini. Alipiga vita yake kwani ana mwili wake, nasi imetupasa kuipiga yetu kwani tunayo miili. Hence, kila mtu ana vita yake; inayo maana hiyo dhambi inayozinga iko mlangoni mwa kila nafsi kwa namna ya kipekee, kwani Paulo anasema yeye amepiga vita wala hasemi tumepiga vita. Roho itakayopiga vita vizuri ndiyo itapata ushindi.
 
Mbarikiwe.
 
 
-------Message original-------
 
Date : 05/01/14 04:24:26
Sujet : Re: DHAMBI INAYOZINGA/NG’ANG’ANIA KWA UPESI!!!!!!
tulip2.jpg
IMSTP12.gif

prayer Request

unread,
Jun 3, 2014, 9:27:22 PM6/3/14
to strictl...@googlegroups.com
Kujua tabia tabia ya dhambi;

dhambi ina tabia zake ni hiyo ni moja wapo!
> Tusichoke kuubu na kumlilia Mungu, as long as tunaishi hatujawa wakamilifu
> BUT 'WE PRESS ON TOWARDS PERFECTION'
>
>
>
>
>
> Tujitie nguvu kwa haya
>
>
>
> 2 Wakorintho 12
>
> 7 Na makusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa mafunuo hayo
> nalipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani ili anipige, nisije
> nikajivuna kupita kiasi. 8 Kwa ajili ya kitu hicho nalimsihi Bwana mara
> tatu
> kwamba kinitoke.9 Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu
> hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha
> nyingi,
> ili uweza wa Kristo ukae juu yangu.10 Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na
> ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo
> dhaifu ndipo nilipo na nguvu.
>
>
>
>
>
> Galatia 5;
>
> 6 Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za
> mwili.17
> Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili;
> kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka.18 Lakini
> mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria.19 Basi matendo ya mwili ni
> dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,20 ibada ya sanamu, uchawi,
> uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, 21 husuda, ulevi,
> ulafi
> com/pages/Strictly-Gospel/363180289370
>
>
>
> Blog: www.strictlygospel.wordpress.com
>
>
>
> Kujiondoa Kwenye Kundi Hili Tuma Email:
>
> strictlygospe...@googlegroups.com
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
>
> --
>
>
>
> Imani Kapinga
>
>
>
>
>
> Titus 2;10-14;
>
> For the grace of God has appeared, bringing salvation for all people,
> training us to renounce ungodliness and worldly passions, and to live
> self-controlled, upright, and godly lives in the present age,waiting for
> our
> blessed hope, the appearing of the glory of our great God and Savior Jesus
> Christ.
>
> --
>
> Tafadhali zingatia msingi wetu ni Neno la Mungu, Lengo letu Kuujenga mwili
> wa Kristo, kushirikiana, amani na upendo. Yeyote yuko huru kuchangia,
> kufundisha, kukubali kufundishwa sawasawa na Msingi wetu Mkuu Neno la
> Mungu.
> Kujiunga na Team ya Injili au Maombi wasiliana nasi kwa simu 0714 915 424.
> Tuma Email. strictl...@yahoo.co.uk Facebook:https://www.facebook
> com/pages/Strictly-Gospel/363180289370
Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages