KUKUTANA NA RAIS, WAZIRI, KATIBU,MFALME, RC, DC, MKURUGENZI MKUU

6 views
Skip to first unread message

Seleli Edwin

unread,
Jun 3, 2014, 9:27:01 PM6/3/14
to strictlygospel

Amani ya Bwana iwe nanyi enyi nyote,


KUKUTANA NA RAIS, MFALME, RC,DC,MKURUGENZI MKUU NA KUPIGA NAYE PICHA NI MUUJIZA NA BONGE LA UINGILIAJI KATI WA MBINGU KUKUZA NA KUKUINUA WEWE MTUMISHI AU KUKAZANA HADI UKUTANE NAO HAO WENYE MAMLAKA ni ulimbukeni fulani na kwa ukweli ni utoto au ujana ktk huduma unasumbua tu Mtu akikua ataacha hayo mambo?

Sijui why mimi waga havinigusagi kiviiile but unakuta mpendwa au mtumishi hata anafunga na kuomba, akutane na Presidaaa kisha hatafanya kosa, lazima atatwanga picha ili iwe ushahidi kua aliwahi kukutana na Rais.

Ingawa kukutana na wenye mamlaka inahesabiwa kua ni baraka na kibali na kuna raha yake hata kupata michongo na channel but kwanini iwe ni main burning desire hadi inatawala prayer items zako hata kukupepelekesha ktk maombi makali na kuteseka? why? nauliza ivi why?

Kwani ngoja kwanza, Usimuona uta dead kwani? au usipomuona na ukafaga bila- bila ndio umepungukiwa na nini VERY SERIOUS ktk Utumishi wako, u-binadamu wako na upendwa wako?

Nadhani Wandugu, tunahitaji kujichungulia ndani kulee kubalancee-balance masoftware yetu yawe na nidhamu na kujiamini, vitu vingine bwanaa tutakuta tunaabudu Wanadamu au kuwapapatikia saaaana hadi tuna-cross boda.

Na ajabu yake unaweza kuta wao kama Wanadamu tu, wana mambo moyoni mazito mno, wanatutamani ile mpaka basi sema hawasemi tu, wanakufa kibingwa, lakini bila kujua thamani yetu ya kutisha sana hapa hadi JUU, tunaenda sasa kujigonga-gonga na kujibamizwa kwa hao hao wanaotutamani tuwasaidie toka ndani ya vilindi vya mioyo yako!

JIAMINI, JITAMBUE NA KOMAA WAKATI MWINGINE KIVYAKO-VYAKO NA MUNGU MZIMA NA MKUU UNAYEMJUA SANA NA ANAKUJUA PIA.

Press on,

Edwin Seleli

Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages