KUNENA KWA LUGHA BAADA YA KUAMINI NA KUJAZWA ROHO MT, NI LAZIMA AU SIYO?

723 views
Skip to first unread message

Seleli Edwin

unread,
May 4, 2014, 6:17:34 PM5/4/14
to strictlygospel
Amani ya Bwana iwe nanyi enyi nyote,

Ni vema sana kama Waamini ktk Imani ya Kristo na maneno yake ktk Biblia kua na tabia njema ya Kiroho ya kupenda Neno hata kupata nafasi ya kuyachunguza maandiko kama hawa-Mdo.17:11 na kutafakari ili kupata KWELI na kukuza uwezo wetu wa  kulijua Neno na kuwahudumia wengine.

Tumefundishwa na kufundisha UKWELI tu kwamba ukisha amini na kujazwa Roho Mt ‘’lazima’’ uwe na ishara ya kunena kwa lugha, Ni sawa kabisa kulingana na yanayojili ktk maandiko kadhaa mfano- Mdo.10:45-47, Mdo.19:1-6 .Tusome Maandiko hayo-nimeongeza na fafanuzi kidogo:

Mdo.10: 44-47 Petro alipokuwa akisema maneno hayo Roho Mtakatifu akawashukia wote waliolisikia lile neno. 45 Na wale waliotahiriwa, walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu MATAIFA nao-waliokua si waamini- wakawa waamini- wamemwagiwa kipawa cha Roho Mtakatifu. 46  Kwa maana waliwasikia  WAKISEMA KWA LUGHA, na kumwadhimisha Mungu. Ndipo Petro akajibu, 47  Ni nani awezaye kuzuia maji, hawa wasibatizwe, watu waliopokea Roho Mtakatifu vile vile kama sisi?

Mdo.19:1-6: 2  akawauliza, Je! Mlipokea Roho Mtakatifu MLIPOAMINI? Wakamjibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia. 3  Akawauliza, Basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, Kwa ubatizo wa Yohana. 4  Paulo akasema, Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu. 5  Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu. 6  Na Paulo,  alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, ROHO MTAKATIFU AKAJA JUU YAO; wakaanza KUNENA KWA LUGHA na kutabiri.

LAKINI…..

Mdo.2:36-41…. 36  Basi nyumba yote ya Israeli na wajue yakini ya kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo mliyemsulibisha kuwa Bwana na Kristo. 37  Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu? 38  Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. 39  Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie. 40  Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi. 41  Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu.

Notice: Hapa Watu wanalipokea Neno-Wanakua Waamini halafu si tu hatuoni wanaombewa kujazwa bali pia hatuoni wakinena kwa lugha ingawa Petro anatamka swala na kupokea Roho Mtakatifu

Mdo.9:17-20 Kuhusu Saul (Paul)…imeandikwa.. 17  Anania akaenda zake, akaingia mle nyumbani; akamwekea mikono akisema, Ndugu Sauli, Bwana amenituma, Yesu, yeye aliyekutokea katika njia uliyoijia, upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu. 18  Mara vikaanguka machoni pake vitu kama magamba, akapata kuona, akasimama, akabatizwa;19  akala chakula, na kupata nguvu. Akawa huko siku kadha wa kadha pamoja na wanafunzi walioko Dameski. 20 Mara akamhubiri Yesu katika masinagogi, kwamba yeye ni Mwana wa Mungu.

Notice: Inaonyesha tu Anania anatamka kua Saul atapata kuona na kujazwa Roho Mt lakini haionyeshi kua alinena kwa lugha hapo baada ya kuamini

Sasa, tunafundishaje swala la Kunena kwa Lugha kama Ishara madhubuti ya Mtu akiamini na Kujazwa -Marko.16:17.. Na hizi ndizo ishara zitakazoandamana na wale wata kaoamini: Kwa kutumia jina langu watafukuza pepo; WATANENA/SEMA KWA LUGHA MPYA, ilihali kuna wenzetu Waliamini na kujazwa lakini kunena kwa Lugha haikusemwa kwa wao?

Ukipewa seminar kufundisha somo hili, utazichanga karata vipi ili ubaki salama mbele za Mungu wewe kama Mwl maana hukumu  ni kubwa na pia kundi lisichanganywe na jambo hili tukufu na nyeti sana kwa maisha ya Wana wa Mungu?

Press on,

Edwin Seleli

thobiasi mosha

unread,
May 7, 2014, 6:19:38 AM5/7/14
to strictl...@googlegroups.com
NI LAZIMA KAMA KWELI UNADHAMIRIA KWENDA MBINGUNI
--
Tafadhali zingatia msingi wetu ni Neno la Mungu, Lengo letu Kuujenga mwili wa Kristo, kushirikiana, amani na upendo. Yeyote yuko huru kuchangia, kufundisha, kukubali kufundishwa sawasawa na Msingi wetu Mkuu Neno la Mungu. Kujiunga na Team ya Injili au Maombi wasiliana nasi kwa simu 0714 915 424. Tuma Email. strictl...@yahoo.co.uk Facebook:https://www.facebook.com/pages/Strictly-Gospel/363180289370
 
Blog: www.strictlygospel.wordpress.com
 
Kujiondoa Kwenye Kundi Hili Tuma Email:
strictlygospe...@googlegroups.com


Emmanuel Nshimirimana

unread,
May 7, 2014, 7:19:32 AM5/7/14
to strictl...@googlegroups.com
Merci beaucoup!!

Wapendwa Bwana Yesu asifiwe!
Jambo hilii kunena kwa lugha ni karama iliyopatikana ktk agano jipya tu na ni Yesu aliyelitamka mala ya kwanza
 Mariko 16:17. Kama yesu aliliweka katika ishara juu ya wale wamuaminio si jambo la kupuuzia ni la kufatilia kwa makini na ni la maana katika maisha ya kiroho. Nafasi ikipatikana tutaongelea kuhusu umuhimu wa karama hii.

Sasa, kuna tafauti  kati ya KUPOKEYA ROHO MTAKATIFU na KUJAZWA ROHO MTAKATIFU.

1. Yohana 20:22 .... akawambiya (Yesu) pokeyeni Roho Mtakatifu.
2.Mtdo1:8  "Nanyi mutapokeya nguvu, Roho Mtakatifu atakapowajia JUU (Juu)..."
Japo wamepewa Roho Mtakatifu (Yoh.20:22) iliwalazimu tena kupokea nguvu ( Mtndo 2) siyo jamani? kwanini sasa?

Kupokea Roho (sawa na yah.20:22) inatupa uwezo wa kufanyika  mwana wa Mungu Yohana 1:12; Yohana3:5-6
Kujazwa Roho Mtakatifu ambako kunafuatana na kunena kwa lugha ni nguvu special.
Roho ni yule yule ila ni kiwango kingine.

Ndugu Paulo hatuone anaombewa kujazwa na kunena kwa lugha lakini mwenyene anashuhudia kwamba ananena tena sana kuliko wengine ( 1 wakorinto 14:18) tukumbuke ya kwamba Paulo anashuudia kwamba ameingia mpaka mbingu ya 3 na akaambiwa siri nyingi sana kwahiyo tuamini kuwa na siri ya lugha mpya aliambiwa hiyo ikampa imani na akanena zaidi ya watu wote. na alieleza wakorinto ubora wa unenaji wa lugha mpya: kama kuongea na Mungu, Kujijenga , kunena siri za za kiroho...(.1wakorinto 14)

 Kwa hiyo jambo hili ni razima sana tena sana lakini kama bado halijatimia kwa mtu huu ao mwengine, haijawa dhambi lakini ni hasara.

Ndugu Msomaji uwe radhi usipoelewa kiswahili cangu ni lugha ngeni kwangu. ninaco kiamini ni kwamba sote n watoto wa Baba Mmoja.




--

Seleli Edwin

unread,
May 11, 2014, 2:00:27 PM5/11/14
to strictlygospel
Nshimirimana

Nimependa salamu hii ya kifaransa ila mwenzangu nimetoka kapa ktk kujibu kidogo ninene ha ha ha ha...'''Merci beaucoup!!'' najibuje? au nayageuza tu fasta maneno hayo nyuma-mbele, right? simple like this... ''beaucoup'  Merci''..tehe tehe,

Anyway thank u for your mchango, good job na lile  SWALI kuhusu Kwanini hatuoni Paul ana nena kwa lugha baada ya kuombewa RM, umelijibu VEMA, SANA,SANA kabisa,excellent indeed my brother.

Nonetheless, nina maswali yafutayo rafiki yangu toka kwa yale umesema kama ifuatavyo, nia yangu ni njema tu-ili tujifunze zaidi na pia yanakupa nafasi wewe kufanya zaidi ili kukata kiu yangu/yetu ya kula Neno bila kuacha chenga wala mchanga, sawa? aya Karibu Kamanda wa Bwana chini  maelezo na maswali:

Umesema kua  '''Kama yesu aliliweka  Kunena kwa Lugha katika ishara juu ya wale wamuaminio si jambo la kupuuzia ni la kufatilia kwa makini na ni la maana katika maisha ya kiroho.

Embu tusome andiko hilo tena...:Marko.16:17-18..Na hizi ndizo ishara zitakazoandamana na wale wata kaoamini: Kwa kutumia jina langu watafukuza pepo; watasema kwa lugha mpya; wataweza hata kuwakamata nyoka na kunywa sumu lakini wasidhurike; watawawekea wagonjwa mikono, nao watapona.” 

MASWALI: 

MOJA:Kwa nini tunakazania na kusisitizia sana Ishara iyo moja ya kunena lakini mistari hiyo imetaja ishara nyingine kama..watafukuza pepo;  wataweza hata kuwakamata nyoka na kunywa sumu lakini wasidhurike; watawawekea wagonjwa mikono, nao watapona,

PILI: Huoni kwa miaka mingi wamefanya/tumefanya kosa la kifundi hapo ktk kuwafundisha Watu KWELI yote ya Neno?


Kwamba  '' kuna tafauti  kati ya KUPOKEA ROHO MTAKATIFU na KUJAZWA ROHO MTAKATIFU kwa maandiko haya  Yohana 20:22 .... .
2.Mtdo1:8  na kwamba iliwalazimu tena kupokea nguvu na kwamba kupokea inatupa UWEZO kua Wana na Kujazwa inatupa NGUVU special

MASWALI:

MOJA: Kuna tofauti yoyote ya msingi kati ya kupata UWEZA na NGUVU special?

PILI: Mtu akipewa UWEZA wa kua Mwana kwa kupokea RM, ina maana hana nguvu hadi apokee RM tena kwa ajili ya nguvu spesheli izo umesema?

TATU: Huyu Mwana wa Mungu aliyepokea UWEZA tu kua mwana na hajapokea NGUVU special, waga yukoje-koje ili kumjua yule ana UWEZA tu na huyu ana vyote yaana UWEZA na NGUVU?


Umesema kua... ''jambo hili- la KUNENA kwa Lugha ni razima sana tena sana lakini kama bado halijatimia kwa mtu huu ao mwengine, haijawa dhambi lakini ni hasara.

MASWALI: 

MOJA: NI hasara zipi anazipata yeye asiyenena kwa lugha bado?

PILI: Kwani kosa la nani ikiwa Mtu anataka na ameshaokoka na anampenda Mungu lakini hajazwi au akijazwa, haneni, wengine hata miaka? hujawahi waona?

Ubarikiwe unapojiandaa kujibu maswali hayo, yatakua yameweka sana hoja zako

Nakupenda my brother na haya majina yenu nafahamu waga mengi yao, yana ujumbe wa kimbinguni-mbinguni ivi ha ha ha-hili lako Nshimirimana bila shaka ni moja wapo na ni tamu hata kulitamka, nina rafiki yangu anaitwa Akizimana-ujumbe mzuri sana hapoo ha ha ha ha Aaaaaaiiiiiiiiiiiimen.

Press on,

Edwin Seleli


2014-05-10 19:04 GMT+03:00 Seleli Edwin <selel...@gmail.com>:
Thobias Mosha,

Umesema ni LAZIMA! Kivipi kwa kuzingatia hoja za Mistari hii, why hakuna kunena hapa:

Mdo.2:36-41…. Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. 39  Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.  41  Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu.

Mdo.9:17-20 Kuhusu Saul (Paul)…imeandikwa.. 17  Anania akaenda zake, akaingia mle nyumbani; akamwekea mikono akisema, Ndugu Sauli, Bwana amenituma, Yesu, yeye aliyekutokea katika njia uliyoijia, upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu. 18  Mara vikaanguka machoni pake vitu kama magamba, akapata kuona, akasimama, akabatizwa;19  akala chakula, na kupata nguvu. Akawa huko siku kadha wa kadha pamoja na wanafunzi walioko Dameski. 20 Mara akamhubiri Yesu katika masinagogi, kwamba yeye ni Mwana wa Mungu.

Unaweza jengea hoja yako msingi kwa kufafanua haya maandiko ili iyo ''ni Lazima'' uliyosema, iwe na mashiko? la sivyo itatupwa nje ikiwa utakutana na Watu wenye kuyachunguza maandiko kama Waberoya aliokutana nao Paul hadi akawakukubali kwa umakini wao

Bless u and welcome back to establish substance of your claim./mandatory statement my brother

Press on,

Edwin Seleli

Seleli Edwin

unread,
May 10, 2014, 12:04:54 PM5/10/14
to strictlygospel
Thobias Mosha,

Umesema ni LAZIMA! Kivipi kwa kuzingatia hoja za Mistari hii, why hakuna kunena hapa:

Mdo.2:36-41…. Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. 39  Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.  41  Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu.

Mdo.9:17-20 Kuhusu Saul (Paul)…imeandikwa.. 17  Anania akaenda zake, akaingia mle nyumbani; akamwekea mikono akisema, Ndugu Sauli, Bwana amenituma, Yesu, yeye aliyekutokea katika njia uliyoijia, upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu. 18  Mara vikaanguka machoni pake vitu kama magamba, akapata kuona, akasimama, akabatizwa;19  akala chakula, na kupata nguvu. Akawa huko siku kadha wa kadha pamoja na wanafunzi walioko Dameski. 20 Mara akamhubiri Yesu katika masinagogi, kwamba yeye ni Mwana wa Mungu.

Unaweza jengea hoja yako msingi kwa kufafanua haya maandiko ili iyo ''ni Lazima'' uliyosema, iwe na mashiko? la sivyo itatupwa nje ikiwa utakutana na Watu wenye kuyachunguza maandiko kama Waberoya aliokutana nao Paul hadi akawakukubali kwa umakini wao

Bless u and welcome back to establish substance of your claim./mandatory statement my brother

Press on,

Edwin Seleli

2014-05-07 13:19 GMT+03:00 'thobiasi mosha' via Strictly Gospel <strictl...@googlegroups.com>:

Alphonse Ziragora

unread,
May 15, 2014, 3:25:04 AM5/15/14
to strictl...@googlegroups.com

Hello Nshimirimana!

Salut Nshimirimana!

"Merci beaucoup!" to you too.

Waliyookoka wote hawana karama moja.

...........................................................................................................

"1 Wakorintho 12:

4.Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule.

5 Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule.

6 Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote.

7 Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana.

8 Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na MWINGINE neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule;

9 MWINGINE imani katika Roho yeye yule; na MWINGINE karama za kuponya katika Roho yule mmoja;

10 na MWINGINE matendo ya miujiza; na MWINGINE unabii; na MWINGINE kupambanua roho; MWINGINE aina za lugha; na MWINGINE tafsiri za lugha;

11 lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye.

12 Maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo.

13 Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.

14 Kwa maana mwili si kiungo kimoja, bali ni vingi.

15 Mguu ukisema, Kwa kuwa mimi si mkono, mimi si wa mwili; je! Si wa mwili kwa sababu hiyo?

16 Na sikio likisema, Kwa kuwa mimi si jicho, mimi si la mwili; je! Si la mwili kwa sababu hiyo?

17 Kama mwili wote ukiwa jicho, ku wapi kusikia? Kama wote ni sikio ku wapi kunusa?

18 Bali Mungu amevitia viungo kila kimoja katika mwili kama alivyotaka.

19 Lakini kama vyote vingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi?"

........................................................................................................
 
MWENGINE (l'autre), ina maana for "un" kuna karama fulani na (et) for an other(pour un autre) ingine karama.
 
Hebu kila anaedhani ameamini Yesu Kristo  atazame kama amekosa hata karama moja ndipo ajihukumu.
 
Dieu te bénisse(Mungu akubariki)...... AMEN.
 
 
 
-------Message original-------
 
Date : 14/05/2014 21:12:25
Sujet : Re: KUNENA KWA LUGHA BAADA YA KUAMINI NA KUJAZWA ROHO MT, NI LAZIMA AU SIYO?
tulip2.jpg
IMSTP12.gif

Emmanuel Nshimirimana

unread,
May 26, 2014, 10:33:17 PM5/26/14
to strictl...@googlegroups.com
Mpendwa, Bwana Yesu asifiwe sana!!!
Kwanza ninashukuru sana kwa ukarimu wako na ninaamini siku mmoja tutaonana ana kwa ana.
Sasa ninaona nifunguwe shule  la kufundisha french, lakini itakuwa kula kulipa!!!!!! ninamaanisha kwamba na wewe utanifunza kingreza ao vipi?
Neno hili "merci beaucoup" siyo salamu bali shukrani mana yake neno merci (mersi) ni Asante na beaucoup (boku) maanaake "SANA".Haya ubarikiwe sana kila lugha itamutukuza Bwana amen!!!!!!!

Asante sana kunitia moyo na ninasema kama mtume Paulo .... ninataka kumjuwa sana (Yesu).....
So  Biblia ni kama mti wenye matunda mbali mbali inatupasa kucuna kwa kila aina. Yesu alisema mtu hataishi kwa mkate ila kwa neno la Mungu. kwa hiyo tuelewe hivi: Mwili unaishi kwa cakula ca kawaida ca aina mbali mbali ili upate afya bora pia na roho inahitaji cakula ca roho ambaco ni neno ili afya ya kiroho iwe bora kabisa.
Sasa kama kuna kukazia sana kuhusu kunena kwa lugha, na kuacha kufundisha mengine, maisha ya kiroho yatakuwa na upungufu mkubwa. Hosea anatabiri akisema kwamba watu wa mungu wanaangamiya kwa kukosa maarifa (ufahamu)
Ktk neno hili la Mrk 16:17-18 yesu alisema ...na hizi ndizo ishara zitaambatana na wale watakaoniamini...cunguza vizuri hajazema moja katika ishara hizi itaambatana... hapana ,ukilinganisha na Waefeso 4:11" ....naye alittowa wengine kuwa MITUME, wengine kuwa NABII, na wengine kuwa WAINJILISTI, na wengine kuwa WACHUNGAJI  na WALIMU".Hakuna utafauti mtu alieokoka leo na wewe wa myaka 40 ukiokaka Mungu anawacukuwa sawasawa (wanae) ndiyo maana ishara hizi wote walioamini na kuzaliwa mala ya 2, ni haki yawo probleme ni kwamba ...watu hatujuwi. Luka 15 ni hadhisi ya mwana mpotevu ukishuka chini utaona huu mpotevu akifanyiwa sikuku , ila huu alie baki nyumbani anakasilika sana akidahi naye haki yake ya kufurahi katika mali ya baba yake, Ndugu yangu, baba yake alimujibu namna gani? Mwana ngu vyote nilivyo navyo ni vyako ( bahati yake mbaya hakujuwa) Hizi ishara zote ni haki ya walioamini,ni vizuri kufundisha sana na ni wajibu wa kila Mukristo kuyajuwa ili kufanikiwa 100%.

2. Ni lazima kanisa lifundishwe ukweli wote. Kwahiyo walimu wanahitajika sana kanisani. ninamaanisha waefeso 4:11 bila hivo kutakua ulemavu kiroho kanisani. Ndugu , Tuombe Baba ili Huduma ya uwalimu ionekane sana kanisani na ifanye kazi hapo watu wataimarika na kukuwa kiroho.

3.Kuna utafauti sana kati ya maandiko: Yoh.20:22 na Mtndo 1:8(hii inaambatana na Mtdo 2.
 ni utafauti gani? Yoh20:22 ni njia ya kuzaliwa mara ya pili. Biblia inasema ni uwezo kwa njia nyingine ni KIBALI au HAKI...Sawa sawa na Yoh.1:12 pia Yoh.3
Na Mtdo 1:8 ni Nguvu za kuwezesha kufanya kazi. ktika lugha ya Kifaransa Yoh.1:12 biblia inasema LE POUVOIR na Acts 1:8 biblia inasema PUISSENCE ni mambo mawili tofauti. HATA KWA KISWAHILI NINAAMINI UKITAFUTA SANA UTAONA UTAFAUTI WA NENO "UWEZO" na "NGUVU"
Unasema huyu aliye pewaUWEZO wa kufanyika mwana wa Mungu YUKO JE? nisayidiye  tuusome katika 1wakor.3 au Hebr. 5:11-12 hapo itatusaidia kutafakari mengi na Roho wa Mungu atatufundisha mengi bila shaka.

Ndugu unauliza tena ni hasara gani kama mtu hajanena kwa lugha?

1. Kristo mwenyewe aliyasema kama ni ahadi kwa wote wamuaminio. Inamaana anajuwa umuhimu wa kunena kwa luhga.
2. Biblia inasema mtu akinena kwa lugha huongea na a) Mungu direct!!! b)hunena siri za Mungu c) Hujijenga d) anaomba katika Roho tu! 1 Wakor.14:2... Yuda 20.

Unasema tena ni kosa la nani kama mtu ameokoka na kumpenda Mungu na huku hajawahi kunena kwa lugha mpya?
Kwa kweli hayo nimeyaishi mda wa myaka mingi namwisho nilijifikiri kwamba labda ni jambo lisilonihusu mimi.
mwisho niliona kosa ni kukosa kujuwa haki yangu katika Kristo na upungufu wa kujuwa maandiko.
Imefika kipindi muda wakupokea unafika mara nyingi, lakini kicwa cangu  kikaniambia tafauti na imani:.. siyo Roho wa Mungu bali ni tamaa..labda ninataka kujifanyisha.... oh ni vile nilisikia kwa wengine .....mpaka nilipo hudhulia semina Kigoma Tanzania Mwalimu alikuwa KRISTOFA MWAKASEGE bila shaka unamufahamu ilikuwa 2004 alifundisha kuhusu ubora wa agano jipya. Alifundisha kuhusu JINA LA YESU, DAMU YA YESU, ROHO MTAKATIFU na NENO LA MUNGU. basi hapo nimeelewa mengi na ninamshukuru Mungu nimepokeya sasa. Alelua!!!

Ubarikiwe sana Mpendwa nami ninakupenda sana na ninapenda uchunguzi wako wa neno la Mungu, nanaamini tutaonana tu.
Jina langu NSHIMIRIMANA linamaanisha "Shukrani za Mungu" na HAKIZIMANA ni kama "JEHOVA RAFA" "MUNGU APONYAYE" asante sana mpendwa na usikose kuniambia chochote Poho wa Mungu akinena na wewe.

Ningekuomba kama vema utiye coments kwa yale niliyo sema kwa mada yako ku facebook. nanapenda kupokea mchango wa nadugu zangu wamendwa. Shalom, shalom!!!!!!!!!!

Seleli Edwin

unread,
Jun 3, 2014, 9:26:54 PM6/3/14
to strictlygospel
Ziragola,

Nimekusikia Kamanda wa Bwana, ubarikiwe kwa mchango

Emmanuel Nshimirimana,

Yaani  rafiki yangu, ubairikiwe sana, nimesoma taratibu na kurudia tena, ni tamu sana kazi yako. Sifa kwa Bwana kwa yoote umesema juu yangu na mada hapa na kule facebook, asante sana. Tutawasiliana later nielewe wapi umenitaka nitoe comment kule facebook

Press on,

Edwin Seleli


Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages