Kwa kuzingatia uhusiano unaopatikana kupitia Ubia wa Kikakati wa Uzalishaji wa Maziwa wa SAGCOT na mpango mkakati wake wa muda mrefu ili kuibua uwezekano mkubwa wa ukuaji wa soko la maziwa, Kiwanda cha Maziwa cha Njombe kinafanya mabadiliko ya ufugaji wa ng'ombe wa maziwa kupitia uboreshaji wa mifugo, uboreshaji wa malisho, usaidizi wa usimamizi wa biashara na mafunzo kwa wafugaji kanuni bora za afya ya wanyama. Hii inaendelea kutoa mchango mkubwa katika ukuaji wa mnyororo wa thamani wa maziwa na maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika eneo la SAGCOT na kwingineko.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos Makalla ametoa rai kwa Maafisa Ugani wa Kanda ya Ziwa Magharibi kuwatembelea wakulima na wafugaji ili kuwakumbusha juu ya kuzingatia kanuni bora za kilimo na ufugaji ili kuweza kupata tija kubwa kwenye uzalishaji.
CPA Makalla ametoa rai hiyo leo tarehe 8 Agosti 2023 wakati akizungumza na wananchi wa Kanda ya Ziwa Magharibi katika kilele cha maonesho ya Wakulima (Nane Nane) yaliyowakutanisha kwa Siku 8 Mikoa ya Geita, Kagera na Mwanza ambapo ameyafunga rasmi.
"Kwakua ninyi ni wataalamu na ndio kazi yenu msichoke kuwatembelea wakulima na wafugaji na kuwapa ushauri stahiki na katika maeneo yenu ya kazi anzisheni mashamba darasa ili wakulima waendelee kujifunza na kuyaona mafanikio." Amesisitiza.
Aidha, ametoa wito kwa vijana kuacha kufanya kilimo mtandaoni na uvuvi haramu badala yake amewataka kujikita kwenye kilimo na ufugaji wa kisasa wa samaki kwani Rais Samia amekua akitoa fedha nyingi kwenye kuwainua vijana kiuchumi kwa kuwapatia mikopo ya aina mbalimbali.
"Tafiti mbalimbali juu ya zao la pamba zinaonesha kwenye hekari moja mkulima anaweza kupata kilo 800 hadi 1200 wakati hali halisi ya mavuno kwa mkulima ni kati ya kilo 150 hadi 300 na kwa ng'ombe wa maziwa anaweza kufikia lita 25-30 kwa siku wakati hali halisi kwa sasa lita 10 kwa ng'ombe". Mhe. Makalla.
kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Emil Kasagara amefafanua kuwa maonesho hayo yamewapa fursa wadau kutoka sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi ambazo huhusisha Utafiti, Umwagiliaji pamoja na hifadhi za Mazao kujifunza kwa vitendo.
"Katika maonesho ya kilimo na sherehe za Wakulima (Nane nane) 2023 jumla ya wadau 863 wameshiriki. Idadi hii inajumuisha Mamlaka za Serikali za Mitaa13, Taasisi za Serikali 11, Taasisi za Fedha 07, Taasisi za Elimu 10, Makampuni ya zana za kilimo 09 pamoja na wajasiriamali wakubwa na wadogo 746." Kasagara.