WAJAMENI…
This is sad news ---------- Forwarded message ---------- MFAMASIA wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu mkoani hapa, Kanuti Kimaro ametiwa mbaroni akituhumiwa kutokuwa mwaminifu kwa mwajiri wake na kisha kuuza mgawo wa dawa za binadamu pamoja na vitendanishi vya kisasa (M.R.D.T) ambavyo vinatumika katika upimaji wa ugonjwa wa malaria; vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 30. Chanzo cha habari kimeifahamisha FikraPevu kwamba Mfamasia huyo alikamatwa Disemba 13 mwaka huu na kwamba hadi sasa anashikiliwa katika kituo kikuu cha Polisi Wilayani Magu. Inadaiwa kuwa wizi huo utasababisha wakazi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kukoswa dawa kupitia katika zahanati, vituo vya afya pamoja na Hospitali ya wilaya hiyo kwa muda wa miezi minne mfululizo. Kwa sharti la kutotajwa jina, chanzo chetu kinadai kwamba Kimaro alikamatwa na maafisa kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilayani humo. Inadaiwa kwamba Mfamasia huyo anatuhumiwa kuuza dawa mbalimbali za binadamu pamoja na ‘kit’ 8 zenye jumla ya vipande 800 vya vitendanishi vinavyotolewa na wafadhili kwa ajili ya kurahisisha zoezi la upimaji wa viini vya ugonjwa wa malaria. “Akiwa peke yake Mfamasia huyo alikiuka taratibu za Wizara kisha akaenda Bohari Kuu ya Dawa (MSD) Jijini Mwanza ambapo alikabidhiwa mgawo wa dawa pamoja na vitendanishi kutoka serikalini. Lakini cha ajabu, Kimaro akaziuza kwa wafanyabiashara binafsi, badala ya kuzifikisha ofisini ili ziweze kuwasaidia wananchi“ kilidai chanzo cha habari. Inadaiwa kuwa kwa kutumia wadhifa wake, baada ya kuuza dawa Kimaro alirejea Magu na kumtaka mtumishi katika kitengo cha stoo aandike kuwa amepokea dawa pamoja na vitendanishi hivyo. “Alipofika Magu akamtaka mfanyakazi kitengo cha ‘Stores’ eti aingize dawa hizo kwenye ‘Ledger Book’. Kilichotokea ni kwamba mtumishi huyo aligoma kuingiza taarifa hewa; na huenda taarifa zikawafikia Takukuru” kilisema chanzo cha habari. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Col. Ngudungi alikiri kuwepo kwa suala hilo. “Ni kweli suala hilo lipo na tayari limeshaanza kujadiliwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya” Ngudungi alithibitisha ofisini kwake, Desemba 27 mwaka huu. Alisema tayari ofisi yake imeanza kuchuku hatua ikiwemo kumsimamisha kazi kwa sababu amekiuka kanuni namba 37 ya sheria ya mwaka 2007 ya utumishi wa umma. Alisema mtuhumiwa huyo amesimamishwa kazi tangu Disemba 19 mwaka huu. “Kusema kweli mfamasia amefanya kitendo cha ajabu; kwamba badala ya kulinda dawa za serikali na mwajiri wake, yeye ndiye anashiriki katika kuhujumu. Mimi ninasema lazima sheria ichukue mkondo wake dhidi ya afisa huyo ambaye kwa kweli ameidhalilisha Wilaya ya Magu” alisema Mkuu wa Wilaya ya Magu, Zainab Kondo. Alisema ana wasiwasi na utendaji kazi wa Bodi ya Hospitali na kwamba ofisi yake kwa kushirikiana na Takukuru, Jeshi la Polisi na Usalama wa Taifa wanaendelea na uchunguzi zaidi. Kamanda wa Takukuru Mkoani hapa, Christopher Mariba hakupatikana ofisini kwake wala kwa njia ya simu ili aweze kuzungumzia suala hilo. Ilidaiwa kuwa alikuwa nje ya ofisi kwa ajili ya kazi nyingine. Hata hivyo, simu yake mara kadhaa iliita bila kupokelewa. Habari hii imeandikwa na Juma Ng’oko, Mwanzahttp://www.fikrapevu.com/jamii/mfamasia-wa-wilaya-ya-magu-mbaroni-kwa-wizi-wa-dawa -- To post to this group, send email to muXa...@googlegroups.comTo unsubscribe from this group, send email to muXalumni-...@googlegroups.comOn the WEB: http://groups.google.com/group/muXalumni?hl=enBLOG: http://muhimbili.blogspot.com/ |
_________________________________________________________________
Mavere Tukai
Principal Technical Advisor - Supply Chain Management
Systems for Improved Access to Pharmaceuticals and Services
Management Sciences for Health | 4301 N. Fairfax Dr. Suite 400, Arlington, VA 22203
Tel (Direct): 703.310.3461 | Tel (Main): 703.524.6575 |
Email: mtu...@msh.org | Website: www.msh.org | Skype: Maveretukai1![]()
Du!!!
Kazi kwelikweli………Commodity management activity… NGUMU sana kui manage!!!!
Ama kweli, hii taarifa kama ni ya kweli inasikitisha sana especially inapofanywa na professionals. Real we have a long way to go on commodity management.
![]()
![]()
Yefta Emmanuel |Supply Chain Manager, AIDSRelief Tanzania Program.
Plot No. 144, Migombani Street - Mikocheni, P.O. Box 34701, Dar Es Salaam|Landline: +255 22 2773141/ 2774273
Fax: +255 22 2774059| Mobile: +255 784499278 , +255 767412596
Email: yefta.e...@crs.org |Web: www.crs.org
From: psmwgt...@googlegroups.com [mailto:psmwgt...@googlegroups.com] On Behalf Of Ondo Baraka
Sent: Thursday, December 29, 2011 3:56 PM
To: psmwgt...@googlegroups.com
Subject: RE: MFAMASIA... MFAMASIA
Sikio la kufa halisikii dawa!
| Hii kwakweliu ni aibu na anaharibu reputation ya pharmacists wote even those who are clean wataanza kuonekana wezi. He should be punished ili iwe lesson learnt --- On Fri, 12/30/11, Emmanuel, Yefta <Yefta.E...@crs.org> wrote: |