Tuzo za uanaharakati za Africans Rising zinanuia kutambulisha na kuendeleza wanaharakati, pamoja na harakati za Kiafrika, na vile vile kuangazia ushirikishi wao wa uanaharakati kama njia ya kufanikisha mabadiliko chanya katika jamii za Kiafrika. Kupitia mfano wa wateule na washindi wa tuzo, mpango huu wa tuzo unaonyesha uanaharakati kama swala la kudhaminiwa katika jamii ya Kiafrika, na unalenga kuhamasisha vitendo sawa miongoni mwa wahusika wengine katika asasi za kiraia katika bara la Afrika pamoja na ughaibuni.
Uteuzi wa tuzo hizo hufanywa na raia kupitia tovuti ya Africans Rising (africansrising.org). Baada ya uteuzi, wateule watahakikiwa na jopo teule la majaji, kisha wagombeaji wachache wataorodheshwa kama wateuliwa bora zaidi. Kwa kila kategoria (Mwanaharakati Bora wa Mwaka, Harakati Bora ya Mwaka na Mwanaharakati Bora wa Kisanaa wa Mwaka), wateule wawili bora zaidi watachaguliwa kuwakilisha Afrika Kaskazini, Afrika Mashariki, Afrika ya Kati, Afrika Magharibi, Kusini mwa Afrika, na wanadiaspora, kwa jumla ya wateule 36.
Watakaorodheshwa kama wateule bora zaidi wataarifiwa kwa barua pepe au WhatsApp. Wateule hao wataombwa kuwasilisha picha, wasifu, na video (kwa hiari) ili kuonyesha kazi zao. Habari hizo zitawekwa kwenye tovuti ya Africans Rising ili wanachama wetu wapate kujifunza zaidi kuhusu wateule, pamoja na uharakati zao wanapoamua ni nani wa kumpigia kura kama chaguo lao kuu wakati wa duru ya mwisho ya upigaji kura.
Matokeo ya kura yatafichuliwa na wapokeaji tuzo watatangazwa wakati wa hafla ya tuzo, itakayoandaliwa mtandaoni. Wateule watatu wataopokea jumla ya kura za juu zaidi katika kila kitengo wataalikwa kwenye hafla ya tuzo za uanaharakati, itakayoandaliwa mtandaoni. Hii itakuwa fursa kwao kupokea tuzo zao na kuonyesha uharakati zao kupitia jukwaa la kimataifa la Africans Rising. Washindi wa Nafasi ya Kwanza, Washindi wa Nafasi ya Pili, na Washindi wa Nafasi ya Tatu vile vile watatangazwa wakati wa hafla hiyo.
Ole wetu tungeuona na kuhisi jinsi ilivyo hali ya kukataliwa, kuudhi, mwiko kuwasilisha chochote kwa muumba, kumpuuza, kutomwamini, kumdunisha na hata kutompa nafasi ndani ya mioyo yetu kuliko vile tunavyofanya kwa zulia lililo sebuleni. Sharti tuyaone haya la sivyo, hatutarudi kwa Kristo kwa wokovu wa dhambi zetu na hatutahitaji mbingu kwa sababu yoyote ila afueni. Na kwa kuhitaji mbinguni kuwa mpumziko ni kuachwa nje.
760c119bf3