Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam anawatangazia wahitimu wote wa Vyuo vya Elimu ya Juu Tanzania kuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimeandaa mafunzo ya ujasiriamali yatakayotolewa katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Arusha, Unguja, Pemba, Kigoma, Kagera, Iringa na Lindi. Mafunzo haya yataanza mwezi Septemba hadi mwezi Oktoba mwaka 2023.
Kuwapatia vijana uelewa, taarifa, maarifa, ujuzi na uwezo wa kuainisha fursa zinazowazunguka na kuweza kuzitumia fursa hizo kuanzisha ajira/biashara kwa ajili yao na wenzao na hivyo kuboresha maisha ya jamii kwa ujumla.
Mafunzo haya yanawalenga vijana wahitimu wa Vyuo vya Elimu ya Juu kuanzia ngazi ya Diploma na kuendelea wenye nia ya kujiajiri. Pia vikundi vya vijana wajasiriamali waliosajiliwa katika ngazi ya manispaa kwa mikoa ya Lindi, Dar es Salaam na Iringa wanahamasishwa kutuma maombi. Sharti ni kwamba katika vikundi hivyo mwanachama mmoja au zaidi awe ni mhitimu wa chuo cha elimu ya juu.
Shule ya Ujasiriamali ni jukwaa linalotoa mafunzo ya ujasiriamali yenye lengo la kukuwezesha kujiajiri na kuongeza kipato chako. Tunahakikisha unapata uelewa kamili na kupokea cheti cha mafunzo yako yaliyothibitishwa.
Mafunzo ya ujasiriamali wa kutengeneza sabuni ya maji kwa vitendo yamefanyika tarehe 10 mwezi Machi 2023 katika Shule ya Sekondari ya Prince Claus (SSPC), yakiendeshwa na Bi. Ewaldina Paul kutoka Taasisi ya YPM, kwa lengo la kuhamasisha vijana wadogo kujihusisha na ujasiriamali.
Mwalimu Mkuu wa SSPC Richard Onai Shembwana amewashukuru YPM kwa kuwapatia fursa hii na ameahidi kutumia ujuzi huo kuwahafundisha wanafunzi utengenezaji wa sabuni hizo kwa ajili ya matumizi ya shule na nyumbani pia.
Entrepreneurship training on how to make liquid soap was held on March 10, 2023 at Prince Claus Secondary School (SSPC), conducted by Ms. Ewaldina Paul from the YPM Institute, with the aim of encouraging young people to get involved in entrepreneurship.
The Principal of SSPC Richard Onai Shembwana thanked YPM for giving them this opportunity and has promised to use that knowledge to teach the students how to make soaps for school and home use as well.
ZAIDI ya vijana 600 kutoka Wilaya ya Sengerema na Ilemela mkoani Mwanza wanatarajia kunufaika na mradi wa kuimarisha ujasiriamali na ajira kwa vijana (EYEE) unaosimamiwa na Shirika la kimataifa la kujitolea(VSO).
Hayo yamesemwa leo na mshauri wa shughuli za uwezeshaji wa vijana wa shirika la VSO, Eziboni Mnahi wakati wa mahojiano malumu na HabariLEO katika manonyesho ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Nyamhongolo.
Akielezea zaidi kuhusu mradi wa EYEE, Mnahi amesema mradi huo una lengo kuu la kuwezesha vijana kuanzia umri wa miaka 18 mpaka 34 kushiriki katika shughuli za ujasiriamali kuanzia hatua za awali za uanzishaji wa biashara ili waweze kukua katika biashara kwa kuongeza kipato na wigo wa masoko.
Arusha. Jumla ya vijana 200 kutoka mikoa minne Tanzania wamenufaika na mafunzo ya ufundi na ujasiriamali baada ya kufadhiliwa na Shirika la maendeleo la Ujerumani (GIZ) kupitia programu ya kukuza ujuzi na ajira kwa maendeleo ya vijana (E4D).
Hayo yamesemwa jijini Arusha na Meneja miradi wa kuwezesha ajira za vijana kwenye sekta ya sola kutoka shirika la GIZ programu ya EFD, Faustine Msangira wakati akizungumza katika kikao cha majadiliano na wawakilishi wa makampuni ya sola kutoka Tanzania, taasisi mbalimbali za umma na binafsi.
Aidha kikao hicho kililenga kujadili namna sekta ya nishati jadidifu ya sola itakavyoweza kutoa ajira kwa vijana na kuondokana na changamoto hiyo ili vijana waweze kujiajiri na hata kuajiri wengine kupitia sekta hiyo.
Msangira amesema shirika hilo limefikia hatua ya kutoa ufadhili kwa vijana hao kulingana na uhitaji wa kampuni za sola kuhusu vijana wenye utalaamu wa kutosha kuhusu masuala ya nishati mbadala ambapo vijana hao ni kutoka mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Manyara na Geita .
Amesema mafunzo hayo yanatolewa kwa vijana hao kupitia mradi unaotekelezwa na shirika hilo wa kukuza ujuzi na ajira kwa maendeleo ya vijana Tanzania mradi unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) kwa kushirikiana na serikali ya Ujerumani (GIZ) chini ya mradi wa Sola unaotekelezwa kwa kushirikiana na TAREA.
"Mafunzo haya yanasaidia sana vijana wetu kuweza kujiajiri pindi wanapohitimu kwani huwa tunawapatia na vitendea kazi kwa ajili ya kujiajiri na tumechukua vijana 200 wa mfano tu ila awamu ya pili tutaongeza vijana wengine kwani maombi yaliyotumwa yalikuwa mengi sana na mradi huu ulianza mwaka 2022 na unaishia mwishoni mwa mwaka 2023," amesema
Aidha amefafanua kuwa mwitikio wa wanawake katika mafunzo hayo ya ufundi ni mkubwa kwani wanawake ni asilimia 40 huku wanaume ni asilimia 60 jambo ambalo linaleta hamasa kubwa ya wanawake kujitokeza katika masuala ya ufundi kwa ujumla.
Amesema wadau hao wameweza kukutana na kuangalia namna ya kuwasaidia vijana kupitia sekta hiyo ya nishati ya sola na kuweza kuweka mikakati mbalimbali katika kipindi hiki ambacho mradi unafikia mwisho ili waweze kuwasaidia vijana hao hata kama hakuna hela za wafadhili.
Naye Mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja kutoka kampuni ya sola ya Mysol, Emmanuel Meisilal amesema kampuni hiyo inahusika na ukuzaji na usambazaji wa sola Tanzania ambapo ilianzishwa mwaka 2011 na hadi sasa hivi imeweza kupata soko mikoa yote ya Tanzania.
Meisilal amesema katika kukabiliana na changamoto ya ajira kwa vijana wameweza kutoa ajira kwa vijana 400 kwenye ufundi huku zaidi ya vijana 500 wakiajiriwa na imewasaidia kwa kiasi kikubwa sana kuondokana na changamoto ya ajira .
Ofisa biashara Mkuu wizara ya Viwanda na Biashara, Wilfred Kahwa amesema mjadala huo ni muhimu sana kwani wameweza kujadili namna ya kuweza kuondokana na changamoto ya ajira kwa vijana kupitia sekta hiyo ya nishati jadidifu ya sola.
Kahwa amesema sekta ya umeme jadidifu ni moja ya eneo ambalo ni kivutio kwa sasa na ina fursa nyingi kwa vijana kuweza kujiajiri hivyo ni vizuri makampuni hayo yakatumia fursa hiyo kuweza kuajiri vijana wengi iwezekanavyo ili waweze kuondokana na changamoto ya ajira ambayo imekuwa ni janga la kitaifa.
Kwa upande wake Mwalimu wa umeme kutoka chuo cha Veta Shinyanga, Aziza Abdallah amesema kutolewa kwa mafunzo hayo kwa vijana hao kumewasaidia sana kuweza kujiajiri na hata wengine kupata ajira katika makampuni mbalimbali ya sola.
Kama sehemu ya mafunzo haya, washiriki walipata fursa ya kupata maarifa muhimu kwa ajili ya kutekeleza mipango thabiti ya biashara na kutengeneza kifurushi cha fedha cha kutosha. Mkuu wa Idara ya Kemia na Viwanda UNIKIN Profesa Jean Mbala Mavinga alisisitiza umuhimu kwa mjasiriamali yeyote chipukizi kuwa na mradi unaoeleweka na kuwa na maono yaliyoeleweka ili kutimiza azma yake.
Wajasiriamali wachanga pia walifahamishwa umuhimu wa kubadilisha uwekezaji wao na kuzidisha vyanzo vyao vya mapato ili kuhakikisha uendelevu na uendelevu wa biashara zao. Wafanyabiashara hawa wapya walihimizwa kushiriki kikamilifu katika maonyesho ya biashara ya ndani, kutoa fursa ya kukuza na kuuza bidhaa zao kwa watazamaji wengi.
Crispin Mulaji, profesa katika Kitivo cha Sayansi, alisisitiza juu ya haja ya wajasiriamali wadogo kuzalisha bidhaa bora, zenye uwezo wa kushindana katika soko linalozidi kuwa la ushindani. Pia alisisitiza umuhimu wa usimamizi madhubuti wa fedha ili kuhakikisha utulivu na maendeleo ya shughuli za ujasiriamali.
Kwa upande wake, msaidizi Jol Kabuya, mwanafunzi wa shahada ya udaktari katika Sayansi, alionyesha umuhimu muhimu wa kuandaa mpango wa kina wa biashara, ikiwa ni pamoja na uchambuzi wa kina wa soko, bidhaa na huduma zinazotolewa. Hatua hii ya msingi inawaruhusu wafanyabiashara kupanga mradi wao na kufafanua mkakati wazi wa kufikia malengo yao ya biashara.
Hatimaye, mafunzo haya hayakuwapa tu wajasiriamali wachanga zana za vitendo na maarifa muhimu ya kuendeleza shughuli zao, lakini pia yalihimiza ubadilishanaji wa manufaa kati ya wasomi, washiriki na watendaji wa kiuchumi. Kwa dhamira hiyo na hamu kama hiyo ya kujifunza, vijana hawa wameandaliwa kukabiliana na changamoto za ulimwengu wa biashara na kuchangia kikamilifu maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya jamii yao.
Awali akitoa mafunzo hayo Mkufunzi wa mafunzo hayo Benjamini Chahe amesema mafunzo hayo aliyoyatoa wakiyazingatia yatasaidia kuongeza kipato cha wajasiriamali hao kwani ni watu wengi wamefanikiwa kupitia mafunzo kama hayo aliyoyatoa.
Akifunga mafunzo hayo Afisa Maendeleo ya Jamii Respista Kalugendo akimuwakilisha Mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii manispaa ya Mpanda ,amewataka Wajasiriamali hao kuunda vikundi vya pamoja na kujisajili ili waweze kutambulika kisheria na kuwa na sifa za kukopesheka.
CHUO Kikuu cha Dar es Salaam, (UDSM) inatazamiwa kuwafikia vijana wahitimu takribani 1,200 katika Mafunzo ya Ujasiriamali kwa wahitimu wa Vyuo Vikuu Vya Elimu ya Juu Tanzania ambayo yanatarajia kuanza Septemba 25 hadi Oktoba 12,2023 kwa Mkoa wa Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo Septemba 19,2023 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Ubunifu na Ujasiriamali, Prof. Hannibal Bwire amesema mafunzo hayo yanalenga kuwapatia vijana uelewa, taarifa, maarifa, Ujuzi na uwezo wa kuainisha fursa zinazowazunguka na kuweza kuzitumia fursa hizo kwa kuanzisha ajira kwa ajili yao na wenzao na hivyo kuboresha maisha ya jamii kwa ujumla.
Aidha amesema kuwa washiriki watapata fursa ya kujifunza kutoka kwa wataalamu wa biashara na kuungana na taasisi za Serikali na binafsi zinazotoa huduma kwa wajasiriamali kama vile SIDO, TBS, TRA, BRELA, TANTRADE, Manispaa za mikoa husika na baadhi ya washiriki waliokwishapata mafunzo hayo mwaka 2019, 2021 na 2022.
Amesema Mafunzo yatatotolewa katika makundi ya watu wasiozidi 50 kwa darasa,na washiriki wa mafunzo hayo watajigharamia usafiri na malazi na gharama nyingine zitagharamiwa na Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
Kwa upande wake Mratibu-Ujasiriamali Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt.Winnie Nguni amesema mafunzo hayo yanalenga kumuimarisha kijana kuweza kutengeneza bidhaa ambayo itauzika na kuweza kumfikisha katika mahala ambapo anaweza kusaidia na wengine kupitia biashara yake.
c80f0f1006