MATIBABU YA BABU WA LOLIONDO HAYAJATOKANA NA BWANA YESU!!

34 views
Skip to first unread message

Ezekiel Nungwi

unread,
Mar 22, 2011, 7:50:23 AM3/22/11
to pcasf...@googlegroups.com, timothy...@yahoo.com

 

Wapendwa salaam sana katika jina la Yesu.

Nimekuwa nikifuatilia juu ya habari za uponyaji na matibanu ambayo yamekuwa yakifanyika huko Loliondoa kwa Babu. Biblia imetupa ruhusa ya kuzijaribu kila roho na kulishika lililo la Bwana tu. 2Watethalonike 5:21.

Kwa mtazamo wangu mimi kama mtumishi wa Bwana na kwa jinsi ambayo nimesoma biblia nimegundua kwamba matibabu hayo hayatokani na Mungu kama jinsi watu wengi wanavyo amini kuwa Mungu ndiye aliye mwotesha babu ndoto na kumpa hiyo dawa ili kuwaponya watu.

Baadhi ya watu wameniandikia na kuniuliza, kama ni kweli Mungu anahusika katika matibabu hayo?

Jibu langu limekuwa HAPANA Mungu hahusiki kabisa katika matibabu hayo. Kila kitu tunacho kifanya lazima kiwekwe katika mizani ya biblia na kikishindwa kusimama katika mizani hiyo basi hicho hakitokani na Mungu.

Zifuatazo ni baadhi ya “Facts” kwanini ninasema matibabu hayo hayatokani na Mungu.

1.    Interest ya Mungu.

Interest ya Mungu kwa mwanadamu sio uponyaji wa mwili, bali ni uponyaji wa roho yake.

2.    Afadhali Ufe na Kansa au UKIMWI uende Mbinguni.

Kwa Mungu, ni afadhali mtu afe kwa Kansa au UKIMWI, halafu aende mbinguni kuliko kupona Kansa au UKIMWI huku akielekea jehanamu.

Marko 2:5

“Naye Yesu alipoiona imani yao, akamwambia mwenye kupooza. Mwanangu umesamehewa dhambi zako.”

Watu hawa walimleta mgonjwa wao kwa Yesu ili Yesu apate kumponya. Waliuona ugonjwa wa kupooza wa ndugu yao kuwa ni ugonjwa mkubwa sana . Lakini Yesu aliuona ungonjwa wa dhambi kama ugonjwa mkubwa kuliko kupooza, kuliko ukimwi, kuliko kisukari na kanasa n.k

Yesu alishughulika na uponyaji wa roho ya mtu kwanza kabla ya kushughulikia na ugonjwa wa mtu kwanza.

3.    Uponyaji wa Babu Hauna Neno la Mungu.

Babu katika uponyaji wake, anatoa tu kikombe cha dawa kwa mtu yeyote haijalishi, hatoai neno lolote linaloashiria kwamba linamuelekeza mtu katika njia ya kuuacha uovo na kumwelekea Mungu. He is more concern of getting the DAWA to the people and nothing more.

4.    Ugonnjwa Mkubwa Kuliko yote ni Dhambi.                                                      

Sehemu mbalimbali katika maandiko Yesu alipowaponya watu, aliwaonya kwamba usitende dhambi tena

Yohana 5:14

“Baada ya hayo Yesu akamkuta ndani ya hekalu, akamwambia, angalia, umekuwa mzima, usitende dhambi tena…”

Sijasikia mahali popote babu akiwasomea maandiko watu na kuwafundisha juu ya athari za dhambi na kuwashauri wampokee Yesu kama Bwana na Mwokozi wako. Watu wanapokea dawa na kuondoka na uponyaji wa mwili, kasha wanarudi katika maisha yao ya dhambi kama kawaida. HUYO HAWEZI KUWA MUNGU NINAYE MFAHAMU MIMI JEHOVAH.

Wokovu kwanza Mengine Baadaye.

5.      Yesu alishughulika na kwanza na waokovu wa Yule mama aliyekamatwa kwa tuhuma za uzinzi. Hakujali mambo ya kesi au hukumu, alijali uponyaji wa roho ya mama Yule kwanza.

Yohana 8:10

…Bwana Yesus akamwambia, wala mimi sikuhukumu. Enenda zako. Wala usitende dhambi tena.

6.    Kupona Ugonjwa ni kurudi Nyuma ya Foleni.

Mungu hashitushwi na swala la mtu kufa kwa ugonjwa Fulani, kwani kila mtu mwisho wa siku lazima atakufa. Tunapokimbizana kutafuta uponyaji wa miili yetu, ni sawa na kurudi nyuma ya foleni ili watangulie kuondoka kwanza walioko mbele lakini ukweli ni kwamba foleni yako lazima itafika baadaye. Wote lazima tutakufa. Kwa hiyo kwa mungu shwala sio kufa, swala ni utakwenda wapi baada ya kufa.

7.    Kifo sio Issue.

Kwangu ninachukulia kifo kama mlango mmoja wapo wa kuendea mbimguni au jehanamu.

8.    Dunia ni sawasawa na Ukumbi.

Sisi wote ni kama tupo ndani ya ukumbi mmoja(duniani) na humu ndani ya ukumbi huu kuna makundi mawili tu. Watakatifu na wenye dhambi. Nje ya ukumbi huu (dunia) kuna mabasi mawili. Moja basi jeupe kwaajili ya abiria ambao ni watakatifu na jingine ni basi jeusi kwaajili ya abiria ambao ni watenda dhambi. Mabasi hayo yote mawili yapo nje ya ukumbi huu (dunia yakisubiri abiria wake watoke ukumbini waingie kwenda kunako husika.

9.    Filosofia ya milango.

Ukumbi huu (dunia) una milango mbalimbali ya kutokea kwenda nje exit. Watu wote wa makundi yote hupita katika mojawapo ya hiyo milango.

10. Milango Mitatu ya Kutokea.

Baadhi ya hiyo milango nipamoja na:

a.     Mlango wa Magonjwa.

b.     Mlango wa Ajali.

c.     Mlango wa jumla “a general gate”

11. Tunajaza Fomu kabla ya kutoka Ukumbini.

Watu wote hutokea kupitia mlango mmojawapo. Ndo maana nimesema kwamba Mungu ashitushwi kwa mtu yeyete kufa kwa ugonjwa kwasabau huo ni mlango wa kukutoa nje. Kinachomshitua Mungu ni uchaguzi wa kuingia basi gani baada ya kutoka katika ukubi huu (dunia) kwasababu kila mtu ni lazima ajaze fomu ya uchaguzi wake kabla ya kutoka ukumbini.

12. Uponyaji lazima Uelekeze Watu Kwa Yesu.

Uponyaji wowote wa Kimungu lazima uwaelekeze watu kwa Bwana Yesu.

Kama mtu ataombewa na mwisho wa maombi hayo akapona lakini asielekezwe kwa Bwana yesu, basi uponyaji huo hautakuwa umetoka kwa Mungu wambinguni.

            Luka 18:43

“Mara hiyo, akapata kuona, akamfuata huku akimtukuza Mungu. Na watu wote walipoona hayo, walimsifu Mungu”

Babu huyo, anawapa watu dawa lakini hawaelekezi kwa Mungu aliye hai. Hiyo inanifanya niamini kabisa kuwa uponyaji wake sio wa Kimungu.

13. MunguHafanyi Miujiza kwaajili ya Maonyesho.

Mungu huwa hafanyi miujiza kwaajili ya “show” watu wanaofanya miujiza kwaajili ya show au kujipatia kipato ni waganga wa kienyeji pamoja na watu wa mazingaombwe ambao hao wote tunajua kwamba hutumiwa na shetani kufanya hayo. Kwa kigezo hiki, kwakuwa babu haelekezi watu kwa yeu bali ni kuwapa dawa na kuonyesha jinsi ambavyo dawa hiyo inafanya maajabu, hiyo ni ishara tosha kwamba dawa hiyo sio ya kimungu.

14. Vigogo Waliopona na Kuokoka.

Muujiza huu ulipelekea ofisa huyu na familia yake kumwamini Yesu yeye na familiya yake yote.

Yohana 4:53

“Basi babaye akafahamu ya kuwa, ni saa ili ile aliyoambiwa na Yesu, mwanao yu hai. Akaamini yeye na wote wa nyumbani mwake.”

Kunaviongozi, vigogo wengi na wafanya biashara wengi waliokwenda kwa babu kupata uponyaji, lakini hakuna yeyote miongoni mwao aliyeamua kumpa Yesu maisha yake yeye na familiya yake baada ya kupata uponyaji huo. Wote walioaaminika kupokea uponyaji huo, walirudi na kuendelea na maisha yao ya kawaida.

15. Uponyaji wa Mungu, Utaridisha Sifa na Utukufu kwa Mungu.

Uponyaji wowote wa Kimungu ni lazima uelekeze sifa na utukufu kwa Mungu na sio kwingine popote.

Luka 7: 14 -16

“Akalikaribia, akaligusa jeneza; wale waliokuwa wakilichukua wakasimama. Akasema kijana nakuambia inuka. 15 Yule maiti akainuka, akaketi, akaanza kusema. Akampa mama yake. Hofu ikawashika wote, wakamtukuza Mungu.”

16. Babu Hana Sifa Hizo.

Uponyaji wa babu, hauelekezi sifa wala utukufu kwa Mungu, unaelekeza sifa nyingi na utukufu kwa babu mwenyewe na kwa hiyo dawa. Kama kweli angekuwa ni Mungu anafanya kazi hapo, sifa na utukufu usingekwenda kwenye dawa au kwa babu vingemrudia Mungu. Ilitakiwa watu wakimaliza kunywa hicho kikombe waseme hakika kweli Yesu anaponya, sio hakika kweli babu ni “nuksi” na dawa yake inaponya kweli kweli.

MAONYO MATANO KWA WATEULE. (WATCH OUT!!!!!!!!!!!!!!)

1.   Msifanyike Mateka.
Wakolosai 2:8
Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu…”
 

2.   Mtu Asiwadanganye kwa kutumia cheo cha Uchungaji.
Mathayo 24:4-5
Yesu akajibu akamwambia, Angalieni, mtu asiwadanganye. Kwasababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ni Kristo; nao watawadanganya wengi.”
 

3.   Watu wanao wadanganya Wengi.
Marko 13:5-6
“Yesu akaanza kuwaambia, Jihadhalini, mtu mtu asiwadanganye. Wengi watakuja kwa jina langu wakisema mimi ndiye, nao watawadanganya wengi.”
 

4.   Shetani hujigeuza kama Maraika wa Nuru.

2 Wakoritho 11:13 – 15

“13 Maana watu kama hao ni mitume wa uwongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo. 14 Wala si ajabu maana shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa maraika wa nuru. Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki.”

5.   Manabii wa Uongo Watatoa Ishara Kubwa na Maajabu.

Mathayo 24:24 – 26

“Kwamaana watatokea makristo wa uwongo, na manabii wa uwongo nao watatoa ishara kubwa na maajabu wapate kuwapoteza, kama yamkini hata walio wateule. 25 Tazama nimekwisha kuwaonya mbele. 26 wakiwaambia yupo jangwani, msitoke, yumo nyumbani , msisadiki.”

Yapo mambo mengi ningeweza kuyasema lakini ngoja nianzie na haya kwanza.

 

 

Ezekiel Nungwi

Location: Vodashop, Mbeya

Group: Sales, Vodacom Tanzania Limited

Office: ; Extension: +255754702868

Mobile: +255754711213

 

C2: VODACOM RESTRICTED

[This Information is restricted for internal employees use only, or authorised partners / third-parties who have signed a non-disclosure agreement]

 

Amani Golugwa

unread,
Mar 22, 2011, 8:12:59 AM3/22/11
to pcasf...@googlegroups.com, Ezekiel Nungwi, timothy...@yahoo.com
Mtu wa Mungu Ezekiel,
You have made your point very clear!!!!

Amani.


2011/3/22 Ezekiel Nungwi <enu...@vodacom.co.tz>



--
Amani S. Golugwa
Finance & Administration Officer
EANNASO
P O Box 6187
Arusha, Tanzania
Tel: +255 27 254 9525
Fax: +255 27 254 9524
Mobile: +255 754 912914
Email: gol...@eannaso.org
www.eannaso.org

rehema kweka

unread,
Mar 22, 2011, 8:39:04 AM3/22/11
to pcasf...@googlegroups.com
Mpendwa naunga mkono kabisa maneno yako


--- On Tue, 22/3/11, Ezekiel Nungwi <enu...@vodacom.co.tz> wrote:

REGULAR RETER

unread,
Mar 22, 2011, 9:23:05 AM3/22/11
to pcasf...@googlegroups.com
Mungu anajua kuchunguza mioyo ya wa2 mimi iwapo wa2 wanapona wanasaidika kutokana na shida mbalimbali mf. kansa inamla m2 mpaka anaisha kama tiba imepatikana acha watu wapone 4 sure.

No other comments

"I believe in being strong when everything seems to be going wrong.I believe that tomorrow is another day and I believe in miracles"-- Audrey Hepburn


--- On Tue, 3/22/11, Ezekiel Nungwi <enu...@vodacom.co.tz> wrote:

From: Ezekiel Nungwi <enu...@vodacom.co.tz>
Subject: MATIBABU YA BABU WA LOLIONDO HAYAJATOKANA NA BWANA YESU!!
To: "pcasf...@googlegroups.com" <pcasf...@googlegroups.com>
Cc: "timothy...@yahoo.com" <timothy...@yahoo.com>

Ezekiel Nungwi

unread,
Mar 22, 2011, 10:17:16 AM3/22/11
to pcasf...@googlegroups.com

Ni kweli Regular Mungu huchunguza mioyo lakini ndugu yangu, Biblia inasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa tena biblia inasema nanyi mtaifahamu kweli na hiyo kweli itawaweka huru. It doesn’t matter if you die but it is better if you die in Christ than believing in gods.  My sister you better review your statement.

 

Ezekiel Nungwi

Location: Vodashop, Mbeya

Group: Sales, Vodacom Tanzania Limited

Office: ; Extension: +255754702868

Mobile: +255754711213

 

C2: VODACOM RESTRICTED

[This Information is restricted for internal employees use only, or authorised partners / third-parties who have signed a non-disclosure agreement]

 

Erick Gabriel

unread,
Mar 22, 2011, 11:10:01 AM3/22/11
to pcasf...@googlegroups.com

Yeeeeeeeees
wajoli wa BWANA.

Huu ni wakati wa kushika na kutembea na NENO LA BWANA.

Thanks,
Stay blessed.


--- On Tue, 3/22/11, Ezekiel Nungwi <enu...@vodacom.co.tz> wrote:

From: Ezekiel Nungwi <enu...@vodacom.co.tz>
Subject: MATIBABU YA BABU WA LOLIONDO HAYAJATOKANA NA BWANA YESU!!
To: "pcasf...@googlegroups.com" <pcasf...@googlegroups.com>
Cc: "timothy...@yahoo.com" <timothy...@yahoo.com>
Date: Tuesday, March 22, 2011, 4:50 AM

 

Wapendwa salaam sana katika jina la Yesu.

Flora Kibusi

unread,
Mar 22, 2011, 11:33:19 AM3/22/11
to pcasf...@googlegroups.com
Nungwi Mungu akubariki sana mwinjilist wangu,umefafanua kwa kina.Pia mwl Kiwango ubarikiwe sana umetusaidia .
Tuwe macho watu wa Mungu kwani ibilisi anao muda
mchache wa kutenda kazi na anautumia ipasavyo.Tujitahidi wapendwa kusoma neno na tudumu ktk maombi ili tusiyumbishwe.
Kama alivyosema Mr Kiwango haya ni madogo kuna mengine makubwa yatatokea je tutahimili?
God bless you all.


From: Amani Golugwa <gol...@eannaso.org>
To: pcasf...@googlegroups.com
Cc: Ezekiel Nungwi <enu...@vodacom.co.tz>; "timothy...@yahoo.com" <timothy...@yahoo.com>
Sent: Tue, March 22, 2011 3:12:59 PM
Subject: Re: MATIBABU YA BABU WA LOLIONDO HAYAJATOKANA NA BWANA YESU!!

JOHN MMASI

unread,
Mar 22, 2011, 3:03:31 PM3/22/11
to pcasf...@googlegroups.com
YOUR ABSOLUTELY RIGHT NUNGWI MAANA MPAKA SASA YAMKINI ATA WATEULI KAMA MAANDIKO YASEMAVYO WAMESHAKUNJWA KIKOMBE! LAITI WATU WANGE KIMBILIA KWA YESU KAMA WANAVYOELEKEA LOLIONDO HAKIKA MAMBO MAKUU YANGEFUNIKA ULIMWENGU

_______________________________________________________
John L. Mmasi
Private contact
0255787458912

_______________________________________________________

--- On Tue, 3/22/11, Amani Golugwa <gol...@eannaso.org> wrote:

From: Amani Golugwa <gol...@eannaso.org>
Subject: Re: MATIBABU YA BABU WA LOLIONDO HAYAJATOKANA NA BWANA YESU!!
To: pcasf...@googlegroups.com

faida tole

unread,
Mar 23, 2011, 7:25:41 AM3/23/11
to pcasf...@googlegroups.com
Mpendwa Nungwi you are so right, Dawa zenyewe za kuchota kama tunavyochota maji bwawani au malambo (kwa wasukuma watanielewa vzr) halafu ukiziangalia rangi yake inafanana sana na mkojo wa punda!. Kwa ufupi tu wapendwa shikeni neno la Mungu hiyo ndo dawa ya magonjwa yote sugu na yasiyo sugu!

Yohane.T.Faida
contact:0754943243 mob
:faid...@yahoo.com
:Box 918 iringa


--- On Tue, 3/22/11, Amani Golugwa <gol...@eannaso.org> wrote:

From: Amani Golugwa <gol...@eannaso.org>
Subject: Re: MATIBABU YA BABU WA LOLIONDO HAYAJATOKANA NA BWANA YESU!!
To: pcasf...@googlegroups.com
Cc: "Ezekiel Nungwi" <enu...@vodacom.co.tz>, "timothy...@yahoo.com" <timothy...@yahoo.com>
Date: Tuesday, March 22, 2011, 5:12 AM

Richard Mnyawi

unread,
Mar 23, 2011, 8:29:29 AM3/23/11
to pcasf...@googlegroups.com
Mimi msukuma mwenzako nimekupata-malambo.
Nafurahi kukuona kwenye mtandao

Ephesians 3:20-21 (NIV)

Now to Him who is able to do immeasurably more than all we ask or imagine,
according to his power that is at work within us, to Him be glory in the church
and in Christ Jesus throughout all generations, for ever and ever! Amen.

RICHARD WILLIAM MNYAWI
P O BOX 7463 ARUSHA
TANZANIA

+255 0573 037987
mny...@yahoo.co.uk

--- On Wed, 23/3/11, faida tole <faid...@yahoo.com> wrote:

Gervas Mweta

unread,
Mar 24, 2011, 7:09:44 AM3/24/11
to pcasf...@googlegroups.com
Nimefurahi saaaana jinsi Ezekiel Nungwi alivyo elezea suala zima la "LOLIONDO KWA BABU" NA ninaungamkono asilimia 150% kwamba wateule tujihadhari saana na watatokea wengi na kipimo chetu kiwe Neno la Mungu. Niliwahi kusikia Babu akiwaambia watu waliokunywa kikombe kwamba wasitende dhambi tena lakini nahisi haikuendelea ni kama danganya toto ili mradi aliwahi kuwa pastor basi mambo fulani ya kipastery atajiingiza aonekane ni wa Mungu na kisha kudanganya wengi LETS BE CAREFUL
 
God bless you ndio maana Yesu alisema enyi binti za Yerusalemu msinililie mimi, jililieni nafsi zenu na za watoto wenu LUKE 23:27 -28.  Nazidi kuelewa maana ya neno : YAMKINI HATA WATEULE lina maana kubwa sana tusikubali kutekwa kwa Jina L Yesu Amen.

Mwalimu Mweta Arusha: JOMO KENYATTA UNIVERSITY OF AGRICULTURE AND TECHNOLOGY (JKUAT) 



2011/3/22 Ezekiel Nungwi <enu...@vodacom.co.tz>

joseph mkose

unread,
Mar 24, 2011, 1:52:10 PM3/24/11
to pcasf...@googlegroups.com
Shaloom watu wa Mungu,
Namshukuru Roho wa Mungu kumtumia Kaka Ezekiel kunimalizia yale niliokuwa nataka kumalizia kuwasilish, maan nipo safari, kwa HERUFI KUBWA BABU LOLIONDO HATOKANI NA MUNGU. Kama Ezekiel alivyofafanua.
Na shukuru sana but please wapendwa unapopata nafasi ya kuomba wakumbuke hata wale waliookoka ambao bado wanamtazamo wa babu loliondo.

2011/3/22 Ezekiel Nungwi <enu...@vodacom.co.tz>

Ni kweli Regular Mungu huchunguza mioyo lakini ndugu yangu, Biblia inasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa tena biblia inasema nanyi mtaifahamu kweli na hiyo kweli itawaweka huru. It doesn’t matter if you die but it is better if you die Min Christ than believing in gods.  My sister you better review your statement.

Edwin Alexander

unread,
Mar 26, 2011, 7:29:22 PM3/26/11
to pcasf...@googlegroups.com
I have read & understood your comments about babu wa loliondo, but when people consulted you for advice, concerning whether the service offered by babu came from God, did you pray and receive clear visions from God that he didn't send him? If NO ! How and where you getting confidence that God didn't send babu? We better fast & pray listening to God's voice concerning the matter and receive answers for which we can relly for clear and justified remarks, rather than drafting our ideas to our own vision! Let me ask you, we unajua story ya punda kwenye bible, what if leo hii akaongea na watu? Would you rash onto saying God hasn't sent people to make conversion with animals! if that was possible, why can't he show a tree for medicine ? Tusifikiri au kumpeleka mungu kwenye aina fulani ya uponyaji ndo tuseme huu unatoka kwa mungu, yeye anasema mawazo yetu si kama ya kwake, na wala njia zetu, soma isaya 55:8, pia tusiseme mungu hajamtuma kwani biblia inasema
na wajua walio wangu, kwani yeye huangalia mioyo, si unakumbuka mungu alivyo mwambia samweli, umeona vyema lakini mim si angalii kama uonavyo, kwani mimi naangalia moyo, hvyo anaweza kuonekana si mtu wa mungu lakini kumbe hujui mungu anamwonaje ! Hvyo tumuachie mungu mwenyewe anajua. We should not rush into final comments rather we first seek the truth from God for confirmed remarks. If God is yet to speak let us maintain calmness, and remain indifference ! !

On Tue Mar 22nd, 2011 5:39 AM PDT rehema kweka wrote:

>Mpendwa naunga mkono kabisa maneno yako
>
>

>--- On Tue, 22/3/11, Ezekiel Nungwi <enu...@vodacom.co.tz> wrote:
>
>
>From: Ezekiel Nungwi <enu...@vodacom.co.tz>
>Subject: MATIBABU YA BABU WA LOLIONDO HAYAJATOKANA NA BWANA YESU!!
>To: "pcasf...@googlegroups.com" <pcasf...@googlegroups.com>
>Cc: "timothy...@yahoo.com" <timothy...@yahoo.com>

>Date: Tuesday, 22 March, 2011, 11:50
>
>
>
>
>
>
>
>

Edwin Alexander

unread,
Mar 26, 2011, 7:48:20 PM3/26/11
to pcasf...@googlegroups.com
I have read & understood your comments about babu wa loliondo, but when people consulted you for advice, concerning whether the service offered by babu came from God, did you pray and receive clear visions from God that he didn't send him? If NO ! How and where are you getting confidence that God didn't send babu? We better fast & pray listening to God's voice concerning the matter and receive answers for which we can relly for clear and justified remarks, rather than drafting our ideas to our own vision! Let me ask you, we unajua story ya punda kwenye bible, what if leo hii akaongea na watu? Would you rash onto saying God hasn't sent people to make conversion with animals! if that was possible, why can't he show a tree for medicine ? Tusifikiri au kumpeleka mungu kwenye aina fulani ya uponyaji tunaotaka uwe ndo tuseme huu unatoka kwa mungu la, na pia tusiwe tunampa shetani utukufu kuwa anaweza kuponya, hakuna popote kwenye biblia kunaonyesha kuwa
shetani anaweza kuponya, bali alitupwa na malaika zake, kama ilivyo andikwa kwenye ufunuo 12:11, na pia mungu anasema mawazo yetu si kama ya kwake, na wala njia zetu, soma isaya 55:8, je NAIMAN si aliponywa ugonjwa wake wa ngozi kwa kuoga mara 7 kwenye mto jordani, unaweza kuelezaje huu uponyaji? Au mtu anavyotoa nguo, au picha, au anapoandika tu maombi kupitia internet au barua kwa watumishi nakupata uponyaji tuseme juu ya huo uponyaji? Au petro alivyotumia kivuli chake kuponya? Ebu tutafakari! pia tusiseme mungu hajamtuma kwani biblia inasema na wajua walio wangu, kwani yeye huangalia mioyo, si unakumbuka mungu alivyo mwambia samweli, umeona vyema lakini mim si angalii kama uonavyo, kwani mimi naangalia moyo, hvyo babu ( mchungaji) anaweza kuonekana si mtu wa mungu lakini kumbe hujui mungu anamwonaje ! Hvyo tumuachie mungu mwenyewe anajua. We should not rush into final comments rather we first seek the truth from God for confirmed remarks.
If God is yet to speak let us maintain calmness, and remain indifference waiting for him ! !

Thadei A. Kiwango

unread,
Mar 28, 2011, 8:43:41 AM3/28/11
to pcasf...@googlegroups.com
Shalomu,

Ni kweli tunakubali kwamba kitendo cha kumtegemea Mungu kwa njia ya kuomba na kumwabudu ili kupata mafunuo juu ya mambo fualni ni cha muhimu na tusingekiepuka kama watumishi wa Mungu. Lakini pia shetani kwa kujua uhitaji wetu huo, huwa anapitia huko huko kuwapotosha watu wengine. Katika eneo hili pia tunahitaji kuwa makini saana wapendwa. Tumkumbuke Balaki ambaye alisukumiziwa nguvu ya upotofu na Mungu akakusudia kumwangamiza kwa sababu alienda kuomba mafunuo huku akijua kwa usahihi kabisa kwamba anachokiomba ni kinyume cha Mungu - hii ilikuwa kama hadaa kwa Mungu. Nimewahi kukutana na cases nyingi kama hizi ambazo watu walimpa shetani nafasi ya kuwatoa katika njia ya Mungu kwa sababu walikuwa wakitafuta mafunuo katika naman siyo sahihi.

Mtu mmoja mtumishi wa Mungu, namfahamu alikuwa katika viwango vya juu sana, alimwacha mke wake wa ndoa na kuoa mke mwingine eti kwa vile alitabiriwa na watu. Mtu mmoja alikuwa mpinzani sana wa ubatizo wa maji mengi akidai kwamba alionyeshwa na Mungu kwamba ubatizo wa maji kidogo unatosha.

Miaka ya tisini hivi nilifika katika kanisa moja, nikakuta ugomvi mkubwa unaendelea, kanisa limegawanyika lakini wanagombea jengo. Kila upande niliokaa nao walinishuhudia jinsi ambavyo wao wana haki na wamefanya maombi hadi ya siku tatu kavu na wamefunilwa kuwa wao ndio wenye haki. Na sheatani alitumia triki hiyo ili badala ya kutafuta suluhu na amani kila upande ujihesabia haki- na vurugu na mpasuko ule uliendelea kuwa mkubwa. Kila upande ulikuwa unakuja na mafunuo yake. Lakini mimi niliona ni adui anawachezea. Kilichotakiwa ni kuomba amani, kumkemea shetani na kutafuta suluhu-hilo ndilo NENO.

Nimesikia watu kadhaa waliopo makanisani ambao kwa tama zao waliwapenda wanawake wasiookoka na wanaingia kwenye maombi kumwomba Mungu awadhibitishie, na wengine huishia kuoa mabinti wa mataifa. Mafuno ni mazuri lakini tuwe makini nayo maana sheatani anajichomekaga humo humo.

Kwenye eneo la mafunuo, kanuni zifuatazo ni muhimu.

1. KILA ANAYEKWENDA KUOMBA MAFUNUO MBELE ZA MUNGU AHAKIKISHE KUWA NJIA ZAKE ZIKO SAWA MBELE ZA MUNGU

2. KABLA YA KUOMBA MAFUNUO, TUANGALIE KWANZA KAMA HILO JAMBO HALINA JIBU KATIKA BIBLIA NA TUJIPIME KAMA NI ROHO YA KUTOTII INAYOTUPELEKEA KUOMBA UFUNUO AU LA. Kama hilo jambo lipo wazi katika biblia tunapaswa kutii, au kama ni jambo linalohitaji maelekezo maalumu, basi tuombe Mungu atupe maelekezo hayo.

3. UFUNUO WOWOTE TUTAKAOUPATA LAZIMA TUURUDISHE NA KUUPIMA KATIKA NENO LA MUNGU KABLA YA KUUFANYIA KAZI.

Kwa upande wa Babu wa Loliondo, ni kitu wazi kwamba hapo Mungu hayupo - Mungu hajatuacha gizani amaetupa neno lake ambalo ni taa ya miguu yetu na mwanga wa njia zetu. Kwa hilo sishauri kwenda kutafuta ufunuo wa kitu ambacho kimeshawekwa wazi, kuna hatari ibilisi akapata nafasi ya kulivuruga kanisa, maana mwingine atakuja na hili mwingine atakuja na lile. Tubaki kwenye NENO.

Stay blessed

TK

>"Baada ya hayo Yesu akamkuta ndani ya hekalu, akamwambia, angalia, umekuwa mzima, usitende dhambi tena..."

>Sijasikia mahali popote babu akiwasomea maandiko watu na kuwafundisha juu ya athari za dhambi na kuwashauri wampokee Yesu kama Bwana na Mwokozi wako. Watu wanapokea dawa na kuondoka na uponyaji wa mwili, kasha wanarudi katika maisha yao ya dhambi kama kawaida. HUYO HAWEZI KUWA MUNGU NINAYE MFAHAMU MIMI JEHOVAH.
>Wokovu kwanza Mengine Baadaye.
>5.      Yesu alishughulika na kwanza na waokovu wa Yule mama aliyekamatwa kwa tuhuma za uzinzi. Hakujali mambo ya kesi au hukumu, alijali uponyaji wa roho ya mama Yule kwanza.
>Yohana 8:10

>...Bwana Yesus akamwambia, wala mimi sikuhukumu. Enenda zako. Wala usitende dhambi tena.

>"Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu..."


>2.   Mtu Asiwadanganye kwa kutumia cheo cha Uchungaji.
>Mathayo 24:4-5
>Yesu akajibu akamwambia, Angalieni, mtu asiwadanganye. Kwasababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ni Kristo; nao watawadanganya wengi."

>3.   Watu wanao wadanganya Wengi.
>Marko 13:5-6
>"Yesu akaanza kuwaambia, Jihadhalini, mtu mtu asiwadanganye. Wengi watakuja kwa jina langu wakisema mimi ndiye, nao watawadanganya wengi."

>4.   Shetani hujigeuza kama Maraika wa Nuru.

>2 Wakoritho 11:13 - 15

>"13 Maana watu kama hao ni mitume wa uwongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo. 14 Wala si ajabu maana shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa maraika wa nuru. Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki."
>5.   Manabii wa Uongo Watatoa Ishara Kubwa na Maajabu.

>Mathayo 24:24 - 26

rehema kweka

unread,
Mar 29, 2011, 7:00:11 AM3/29/11
to pcasf...@googlegroups.com
Jamani wapendwa hebu tuombe tu Mungu atusaidie Dunia ya sasa hasa watakatifu wake.Nimesoma maoni meng kuhusu Loliondo lakini mengine ni makali sana nani anajua Babu katumwa na Mungu au Laa  ndo Jambo la kuomba Ufunuo maana hiz ni siku za Mwisho tusiongee sana bali Tuombe sana.
Mungu awabariki

--- On Sat, 26/3/11, Edwin Alexander <ednal...@yahoo.com> wrote:

lazaro seni

unread,
Mar 29, 2011, 7:53:58 AM3/29/11
to pcasf...@googlegroups.com
Babu babu babuuuuu!!!!!
Nimengi sana yamesemwa na watu wengi wanaendelea kusema katika tiba hii ya babu, lakini mimi ninapata shida kidogo katika suala  hili. Je dawa za hospitalini ziko kwenye NENO?Je tulishawahi kujiuliza kuwa Asprini inatokana na nini? Au ARV inatokana na nini? Kwa nini tunaenda hosptalini tukiugua? Je nani atakubali kuwa mwarobaini ni dawa ya malaria? Au mpaka mzungu atakapogundua dawa ndo tuiamini kuwa ni ya kweli? . Kunawaumini wa madhehebu ya mashahidi wa Jehova wao haruhusu muumini wao kuongezewa damu, Je wako sawa? Haya ndo maswali machache kati ya mengi yanayonisumbua kichwa changu, tujalibu kuliangalia suala hili kwa undani na tumuobe sana Mungu atupe neema ya ufaham tuweze kujua kama ni ya kutoka kwake au la. Nakumbuka mm nilikuwa napinga suala DECI  kipindi hicho na nilikuwa na sehemu ndogo ya kiuchumi nilikuwa nasimamia, lakini viongozi wa dini ndo wakanishawishi nikaingia lkn yaiyotokea kila mmoja tunajua. NEEMA YA MUNGU INAHITAJIKA SANA NA WATELE KAMA SISI TUOMBE SANA MAANA KAMA ATAKUWA shetani NIWENGI SANA WAANGAMIA.
 
 
MIMI SISHAURI MTU AENDE AU ASIENDE ILA KILA MTU AONAVYO NAFSINI MWAKE NA AMANI YA BWANA IPITAYO AMANI ZOTE ACHA  IAMUE MIOYONI MWETU.
 
 
 

--- On Tue, 3/29/11, rehema kweka <rhmk...@yahoo.co.uk> wrote:

Thadei A. Kiwango

unread,
Mar 29, 2011, 8:51:04 AM3/29/11
to pcasf...@googlegroups.com

Ndugu Seni, issue ya kutumia dawa za hospitali au mwarabuni au kwenda hospitalini haina utata maana mtu anapata matibabu ya kisayansi. Kama Babu angekuwa anatoa matibabu ya huo mzizi kisayansi isingekuwa na shida yoyote ile. Shida hasa ni pale ambapo matibabu hayo yanalink na maswala ya imani/roho. Ambapo tukipima utndaji wa hiyo roho katika NENO, hatumwoni Roho Mtakatifu hapo. Kama kwa mfano wanasayansi wanavyofanyia utafiti huo mti na ikaja kugundulika kwamba kwa kutumia fomula Fulani huo mti unaponya, hapo hakuna shida kabisa maana itakuwa ni ulimwengu wa kisayansi. Wapo watu wa Mungu ambao walifunuliwa formula za kisayansi amabzo hadi leo zinatumika kufanya mambo makubwa, lakini ufunuo wao haukuwa na sura hiyo tunayoiona loliondo. Mathalani Babu angesema amefunuliwa na Mungu kwamba huo mti ni dawa na watu wakautumia kama kawaida, isingekuwa tatizo, lakini jinsi huduma ya kikombe inavyotolewa, ina maana kuna roho inayotenda kazi nyuma yake. Kama sivyo atoe hiyo formula na watu wasiwe na haja ya kuunga foleni, au watu waende wakawachukulie wagonjwa wao. Ni kwa nini hadi mtu ukaunge foleni na unwe unywee pale ndipo upone? Hivi kuna tofauti sasa na mganga wa kienyeji? Kwa hiyo kama mtu akienda kwa mganga wa kienyeji akapona ni sawa? Na hapo tungekuwa na utata kwamba kwa vile watu wanapona na kusaidika labda ni Mungu? Au kupona peke yake au kwa vile mtu anajiita mchungaji ndio kigezo?

 

 

Mtume Paulo ameadika kwamba Mungu zamani alisema na watu zaidi kwa maona na ndoto na unabii, lakini mwisho wa siku hizi anasema nasi kwa njia yam wane yaani NENO.Tusingeogopa kunena waziwazi kile ambacho neno linadhibitisha. Kama tunaweza kujibu kwa ujasiri kwamba tunaenda Mbinguni kwa sababu tumethibitisha katika NENO, je tutaogopaje kujibu kuhusu mambo ya Loliondo kwamba sio Mungu? Ndugu zangu sisi ndio tunaohitajika kuwasaidia wengine, je kama sisi wenyewe hatuamini kile NENO limeweka wazi tutawasiadiaje watu?

 

 Kama wanasayansi wanaofanyia utafiti matibabu hayo wakigundua kwamba dawa hiyo inaponya kwa kutumia fomula Fulani na kweli watu wakaitumia kama wanavyotumia dawa nyingine za kisayansi na wakapona kama wanavyoadi kupona huko Loliondo, walao inaweza kushawishi kwamba hakuna mahusiano ya kiroho na matibabu ya loliondo ila ni ujanja wa Babu kuficha hiyo fomula na kuweka masharti faulani au kwa sababu anazozijua yeye. Kama sivyo kwa mujibu wa neno la Mungu na tahadhari tulizopewa, issue ya Loliondo inafungamana na roho isiyotoka kwa MUngu amabyo itakuwa na matokeo mabaya katika Ulimwengu wa roho na kwa kazi ya Mungu na kwa kanisa- Tuwaambie watu ukweli na tuwasaidie na kuwatahadharisha.

 

TK

 


lazaro seni

unread,
Mar 29, 2011, 9:39:27 AM3/29/11
to pcasf...@googlegroups.com
Nashukru Mwalimu umenifumbua na nimekuelewa vizuri sana na si mimi tu ila na wengine ambao kwa namna mmoja ama nyingine walikuwa wakijiuliza kama mimi na kupitia haya majibu watakuwa wamelewa.
 
Seni.

--- On Tue, 3/29/11, Thadei A. Kiwango <tkiw...@iaa.ac.tz> wrote:

 

TK

>“Naye Yesu alipoiona imani yao , akamwambia mwenye kupooza. Mwanangu umesamehewa dhambi zako.”

imani adam

unread,
Mar 29, 2011, 10:13:33 AM3/29/11
to pcasf...@googlegroups.com
Mungu akubariki kwa maelezo mazuri.
 
Ila mimi nina suala linanitatiza kidogo. Ukisoma Biblia tunaona jinsi Musa alivyotengeneza nyoka wa shaba ili lika atakaye mwangalia aweze kupona. Hii inatokana na pale Wanaisrael walipomkosea Mungu kwa kuabudu Miungu mingine.
 
Suala hili linahusisha Imani kwani ilimpasa mtu kuchukua hatua ya kumwangalia yule nyoka wa shaba. Na wale waliopuuzia walikufa kwa kuwa walikaidi maagizo ya MUSA.
 
Hivi wapendwa, kama suala hili lingetokea katika kizazi hiki cha leo ni nani atakayeamini kuwa hilo ni la MUNGU? Mungu angeweza kuwaponya kwa njia ya maombezi lakini aliamuamuru Musa atengeneze nyoka wa shaba na kila takakaye mtazama atapata uponyaji. Hivi leo Mungu akumfunulia mtu suala hili ni nani angekubali hivi leo?
 
Wapentekosti wengi tunaamini imani ya kuombewa kwa kuwekewa mikono. Na haya yote ni mapokezi tuliyoyapokea kutoka kwenye dhehebu letu.
 
Au kwa kuwa Babu si mpentekosti ndio maana hatutaki kumwamini? sina maana mimi nimekubali ila mi nadhani tusitumie utashi wetu na mafunuo yetu kupinga suala hili, ila tumwombe MUNGU atupe macho ya kiroho.
 
Mi kwa mtazamo wangu biblia inahitaji uvuvio wa roho mtakatifu ili tuweze kuielewa vyema na si kusoma kama kitabu cha hadithi.
 
Siku zote MUNGU hutumia kitu kinyonge na kidhaifu ili kujidhihirisha kuwa yeye ni MUNGU awezae.
 
Ni hilo tu wapendwa. 

With kind regards,

Imani Adam Mwakalinga,
System Administrator,
Ministry of Energy and Minerals,
P.O Box 2000, Samora Street, Dar Es Salaam.
       im...@mem.go.tz
 


--- On Tue, 3/29/11, Thadei A. Kiwango <tkiw...@iaa.ac.tz> wrote:

From: Thadei A. Kiwango <tkiw...@iaa.ac.tz>

 

TK

>“Naye Yesu alipoiona imani yao , akamwambia mwenye kupooza. Mwanangu umesamehewa dhambi zako.”

Thadei A. Kiwango

unread,
Mar 29, 2011, 10:43:42 AM3/29/11
to pcasf...@googlegroups.com

Ndugu yangu Imani, umenena vyema kwamba hujakubaliana na kikombe cha Babu. Mungu  ni mwaminifu sana, ndio maana umejisikia kwa ndani roho yako inasita japo kwa kigezo cha Musa unaona kuwa Babu katokewa na Mungu. Hicho kinachokupa kinachogonga kengele ndani yako na kukukosesha amani kuhusu  kikombe cha Babu ni Roho Mtakatifu. La sivyo Roho Mtakatifu angetia tiki ndani yako na ungekuwa na amani na kikombe chenyewe. Hiyo pia kwa mujibu wa Biblia ni njia ya kuzipima roho zidanganyazo – yaani hata kama akili zako zinakubalinan na jambo faulani, lakini ndani yako hakuna amani, ni bora ufuate uongozi wa ndani.

 

Mungu katika Agano la kale alifanya ishara mbali mbali kwa kusudi Fulani. Alimfanya yule nyoka wa uponyaji kama njia ya kuhubiri na kuatabiri ujio wa Yesu Kristo ambaye angeakiwa msalababni kila amtazamaye aishi. Mwamba ule uliotoa maji ulikwa ni Yesu Kristo mwenye kama ilivyoanishwa katika kitabu cha Wakorintho. Nk.N autaona kwamba Mungu alitumia njia hizo mara moja tu in special circumstance na haikurudia tena watu kuponywa kwa kutundika nyoka mtini. Hata leo ninakubalinana na ishara au vitendo vinavyoweza kufanyika na mtu akaponywa pasipo kuwekewa mikono, lakini kitendo hicho hakitakuwa formula. Formula ni kuwekewa mikono/kuombewa kwa Jina la Yesu ambayo si mapokeo ya wapentecoste bali NENO la Mungu.

 

Pamoja na kuweka msisitizo kwenye kuomba Mungu ili atufuniliwe yanayojiri Loliondo njia iliyo bora na salama tungesisitiza kusoma NENO la MUngu. Kanisa la Beroya walisifika kwa uungwanaa wao kwa sababu tabia yao ilikuwa kila wanaposikia mafundisho wanarudi kupekua maandiko ili kudthibitisha ukweli. Yesu alipojaribiwa alimshinda sheatani kwa NENO, na sisi hatuna shortcut.

 

TK

 


imani adam

unread,
Mar 30, 2011, 4:19:24 AM3/30/11
to pcasf...@googlegroups.com
Ahsante sana Mwl, nimekuelewa vyema. Mungu akubariki kwa huduma yako ya kutoa mda wako ili kuelemisha wapendwa.


 
With kind regards,

Imani Adam Mwakalinga,
System Administrator,
Ministry of Energy and Minerals,
P.O Box 2000, Samora Street, Dar Es Salaam.
       im...@mem.go.tz
 


--- On Tue, 3/29/11, Thadei A. Kiwango <tkiw...@iaa.ac.tz> wrote:

From: Thadei A. Kiwango <tkiw...@iaa.ac.tz>
Subject: RE: MATIBABU YA BABU WA LOLIONDO HAYAJATOKANA NA BWANA YESU!!
To: pcasf...@googlegroups.com
Date: Tuesday, March 29, 2011, 7:43 AM

Ndugu yangu Imani, umenena vyema kwamba hujakubaliana na kikombe cha Babu. Mungu  ni mwaminifu sana , ndio maana umejisikia kwa ndani roho yako inasita japo kwa kigezo cha Musa unaona kuwa Babu katokewa na Mungu. Hicho kinachokupa kinachogonga kengele ndani yako na kukukosesha amani kuhusu  kikombe cha Babu ni Roho Mtakatifu. La sivyo Roho Mtakatifu angetia tiki ndani yako na ungekuwa na amani na kikombe chenyewe. Hiyo pia kwa mujibu wa Biblia ni njia ya kuzipima roho zidanganyazo – yaani hata kama akili zako zinakubalinan na jambo faulani, lakini ndani yako hakuna amani, ni bora ufuate uongozi wa ndani.

 

Mungu katika Agano la kale alifanya ishara mbali mbali kwa kusudi Fulani. Alimfanya yule nyoka wa uponyaji kama njia ya kuhubiri na kuatabiri ujio wa Yesu Kristo ambaye angeakiwa msalababni kila amtazamaye aishi. Mwamba ule uliotoa maji ulikwa ni Yesu Kristo mwenye kama ilivyoanishwa katika kitabu cha Wakorintho. Nk.N autaona kwamba Mungu alitumia njia hizo mara moja tu in special circumstance na haikurudia tena watu kuponywa kwa kutundika nyoka mtini. Hata leo ninakubalinana na ishara au vitendo vinavyoweza kufanyika na mtu akaponywa pasipo kuwekewa mikono, lakini kitendo hicho hakitakuwa formula. Formula ni kuwekewa mikono/kuombewa kwa Jina la Yesu ambayo si mapokeo ya wapentecoste bali NENO la Mungu.

Pamoja na kuweka msisitizo kwenye kuomba Mungu ili atufuniliwe yanayojiri Loliondo njia iliyo bora na salama tungesisitiza kusoma NENO la MUngu. Kanisa la Beroya walisifika kwa uungwanaa wao kwa sababu tabia yao ilikuwa kila wanaposikia mafundisho wanarudi kupekua maandiko ili kudthibitisha ukweli. Yesu alipojaribiwa alimshinda sheatani kwa NENO, na sisi hatuna shortcut.

 

TK

 


From: pcasf...@googlegroups.com [mailto: pcasf...@googlegroups.com ] On Behalf Of imani adam
Sent: Tuesday, March 29, 2011 5:14 PM
To: pcasf...@googlegroups.com
Subject: RE: MATIBABU YA BABU WA LOLIONDO HAYAJATOKANA NA BWANA YESU!!

Mungu akubariki kwa maelezo mazuri.

 

Ila mimi nina suala linanitatiza kidogo. Ukisoma Biblia tunaona jinsi Musa alivyotengeneza nyoka wa shaba ili lika atakaye mwangalia aweze kupona. Hii inatokana na pale Wanaisrael walipomkosea Mungu kwa kuabudu Miungu mingine.

 

Suala hili linahusisha Imani kwani ilimpasa mtu kuchukua hatua ya kumwangalia yule nyoka wa shaba . Na wale waliopuuzia walikufa kwa kuwa walikaidi maagizo ya MUSA.

Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages