Posted Jumanne,Agosti26 2014 saa 9:56 AM
KWA UFUPI
“Tunaomba wanachama wetu wajiandae kupinga kwa nguvu zote dhamira hii ya Serikali ya kutaka kutunyonya, kwani sababu zilizotolewa kupunguza mafao haya siyo za msingi,”
Dar es Salaam. Vyama zaidi vya wafanyakazi, vimeendelea kujitokeza na kuungana na kuibana Serikali na kuitaka ilipe deni la Sh7 trilioni inalodaiwa na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, kadhalika kuondoa mpango wake wa kupunguza mafao ya wastaafu.
Hatua hiyo imedhihirika jana baada ya Chama Cha Walimu Manispaa ya Kinondoni kutoa tamko rasmi kupitia kwa Mwenyekiti, Tabu Chilli kikiwataka wanachama kujiandaa kupinga mpango huo wa Serikali, ambao wameuita kuwa ni unyonyaji.
Vyama vingine ambavyo tayari vimeshatoa tamko kupinga mpango huo ni Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU) na Chama cha Walimu Tanzania(CWT), Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU).
Katika tamko hilo, CWT Kinondoni ilieleza kuwa kufilisika kwa mifuko ya jamii kumechangiwa na madeni makubwa kutoka serikalini.
“Tunaomba wanachama wetu wajiandae kupinga kwa nguvu zote dhamira hii ya Serikali ya kutaka kutunyonya, kwani sababu zilizotolewa kupunguza mafao haya siyo za msingi,” alisema Chilli.
Tamko hilo linaunga mkono lile la Julai mwaka huu la Rais wa CWT Taifa, Gratian Mukoba kupinga mpango huo, ambao unadaiwa kubuniwa na Serikali kutokana na deni kubwa linaloikabili kutoka kwenye mifuko ya hifadhi.
Alitoa wito kwa wafanyakazi nchini kutafakari upya kama mfumo wa sasa wa uwakilishi katika masuala yao muhimu unakidhi kwa kiasi kikubwa matarajio yao.
“Ni dhahiri kwamba wafanyakazi wa Tanzania wamejikuta katika mkwamo katika kudai haki zao mbalimbali, ni wakati mwafaka sasa kujipanga upya ili hatimaye waweze kuondoka katika mkwamo huo,” alisema Mukoba katika tamko lake.
Field Marshal
Comrade GS,
Nafikiri hii ni fursa kwetu pia kupitia humo humo kupenyeza yale madai yetu wafanyakazi wa migodi kupinga mswaada wa sheria ya kufuta fao la kujitoa.
Nashauri jambo hili tulizungumze kwenye kikao chetu kijacho cha kamati ya utendaji ya taifa Iliad litolewe tamko kwa vyombo vya habari kuhusiana na jambo hili.
Shigela.
--
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "NUMET Media Release" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to numet-media-rel...@googlegroups.com.
To post to this group, send email to numet-med...@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/numet-media-release.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
Nico,
Nafikiri kulielekeza huko tuliko hivi sasa itakuwa ni kuzingatia ushauri wako wa kutofuata mkumbo, nafikiri cha kutafiti ni namna mambo haya yanavyoweza kuhusishwa ili kuleta mantiki na kutupa publicity.
SA.