Ndugu zangu wanachama wa NUME, wafanyakazi na wadau wenzetu.
Mtakumbuka kuwa NUMET Ilikuwa na majadilino ya muda mrefu na mwajiri katika kampuni ya dhahabu ya North Mara juu ya dhamira yake ya kupunguza wafanyakazi.
Kwa bahati mbaya katika majadiiano hayo hatukufikia muafaka, na hivyo tulikataa kwa mujibu wa sheria zoezi hilo kufanyika. Sababu kubwa ya kukataa ni kwasababu mwajiri hakuwa na sababu za msingi za kupunguza wafanyakazi, na pia taratibu zingine muhimu za kisheria alizikiuka.
Mwajiri alitufungulia kesi tarehe 25.09.2013 akiomba Tume ya Usuluhishi na Uamuzi, impe kibali cha kuendelea na zoezi la kupunguza wafanyakazi kwa vigezo vyake alivyoviweka
Tulipata wito wa kwenda mahakamani tarehe 30.09.2013, na tulipofika tulianisha mapungufu mbali mbali ya kisheria na kuitaka tume iifutilie mbali kesi hiyo.
Mwajiri aliomba aiondoe kwenye tume ili aweze kuileta tena upya, ombi lake lilikubaliwa. Na tarehe hiyo hiyo mwajiri alifungua kesi upya.
Tuliitwa jana tarehe 04.10.2013 (yaani siku 4 baada ya kesi kufunguliwa badala ya siku 14) kwenye tume (CMA) kwa ajili ya usuluhishi, na kwa bahati mbaya usuluhishi ulishindikana.
Kesi imeishapangiwa tarehe 23.10.2013 kwa ajili ya kuanza hatua ya kusikiizwa kati ngazi ya uamuzi (Arbitration).
naendelea kuwaomba wadau kutusaidia kwa hali na mali, hasa kwa wanasheria wanaoweza kujitolea katika hatua hii ya Arbitration tutawashukuru sana.
"AN INJURY TO ONE, IS AN INJURY TO ALL!"
SOLIDARITY FOREVER.
___________________________________________________________________________
Nicomedes M. Kajungu
General Secretary
National Union of Mine & Energy Workers of Tanzania (NUMET)
P.O.Box 7733
MWANZA.
+255782315688, +255767483271_________________________________________________________________