NUMET ITAITISHA MAANDAMANO MAKUBWA KUPINGA UDHALIMU WA MWAJIRI WA MGODI WA BULYANHULU GOLD MINE.

7 views
Skip to first unread message

National Union Of Mine and Energy Workers of Tanzania

unread,
Jul 24, 2015, 6:01:28 AM7/24/15
to numet-media-release

Katika kikao baina ya NUMET na kampuni ya ACACIA Bulyanhulu Gold Mine Ltd, kilichojadili suala zima la kupunguza wafanyakazi 250 tulikubaliana mambo muhimu yafuatayo.

1. mwajiri atawapangia kazi nyingine wafanyakazi 145 ndani ya mgodi au katika migodi mingine ya ACACIA.

2. Wagonjwa 65 watashughlikiwa kwa mujibu wa sheria kwa kuzingatia maelekezo ya madaktari bingwa wanaowatibu, na hivyo hawawezi kuwa sehemu ya mjadala wa "retrenchment".

3. Wafanyakazi wapatao 40 watapunguzwa kazi kama tutakubaliana mafao ya upunguzwaji wao, yaani "separation package".

Katika mjadala huo, mwajiri alipendekeza kulipa mshahara wa mwezi mmoja (Basic salary) kwa kila mwaka aliofanya kazi pale mgodini.

NUMET tukapendekeza malipo ya mshahara ghafi (gross salary) wa miezi miwili kwa kila mwaka mfanyakazi aliofanya kazi.

Hapo ndipo tuliposhindwa kukubaliana, na hivyo tukakubaliana kutokukubaliana. Katika kukubaliana kutokukubaliana mambo yafuatayo ilikubalika yafanyike,

1. zoezi linasimama kwa mujibu wa kifungu cha 38 cha sheria ya ajira na mahusiano kazini, No.6/2004, na Kanuni ya 23-25 ya Tangazo la Serikali No. 42 ya mwaka 2007.

2. Ili mwajiri aweze kuendelea na zoezi alikubali kwenda mahakamani ili kupata kibali cha kupunguza wafanyakazi.

3. alisema ataendelea na zoezi la kupunguza wafanyakazi ambao si wanachama wa NUMET maana NUMET haina mamlaka ya kisheria kuwa msemaji wa wafanyakazi wote pale mgodini.

Aidha tulionya juu ya hatua hiyo maana itaonekana ni ubaguzi.
Akasema anayo makubaliano na wafanyakazi wasio wanachama wetu kupitia Workers Representative Council.

Baada ya makubaliano hayo hakwenda mahakamani, na sasa amekiuka makubaliano yote ameamua kupunguza wafanyakazi kwa nguvu.

NUMET INAANDAA MAANDAMANO MAKUBWA KIJIJINI KAKOLA , MKOANI SHINYANGA kupinga matumizi ya nguvu na uvunjaji wa sheria za nchi.

Tunaomba wanachama wote wa NUMET, wafanyakazi na wadau mbali mbali mtuunge mkono kukomesha udhalimu huu.

Tunashughulikia vibali vya maandamano, na tutawajulisha utaratibu mzima baada ya vibali kukamilika.

UNITED WE STAND, DIVIDED WE FALL

Leila Sheikh

unread,
Jul 24, 2015, 8:22:35 AM7/24/15
to numet-med...@googlegroups.com
Asante kwa taarifa.
Msimamo wa NUMET ndiyo sahihi.
Maandamano yatakuwa lini?
Inawezekana tukaja kuungana kwenye maandamano.

Leila Sheikh
--
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "NUMET Media Release" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to numet-media-rel...@googlegroups.com.
To post to this group, send email to numet-med...@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/numet-media-release.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

National Union Of Mine and Energy Workers of Tanzania

unread,
Jul 22, 2016, 2:59:51 AM7/22/16
to numet-media-release
Yaani leo ndo nasoma email hii. Aibu kweli.



___________________________________________________________________________
Nicomedes M. Kajungu
General Secretary
National  Union of Mine &  Energy Workers of Tanzania (NUMET)
P.O.Box 7733
MWANZA.
+255782315688, +255767483271

_________________________________________________________________
Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages