Mwalimu wangu Marjorie, uanachama wako NUMET uko wazi kwa mujibu wa sheria na katiba ya chama. Tumsubiri Katibu Mkuu akupe maelekezo ya namna ya kurasimisha uanachama huo ili uingie kundini rasmi.
Mimi kama mmojawapo wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Taifa ya NUMET najisikia furaha na fahari kubwa kuona wafanyakazi makini kama wewe mnapata hamu ya kujiunga na chama chetu.
Karibu sana. Kauli mbiu ya NUMET ni "United we bargain, divided we beg" ambayo inaenda sambamba na kauli mbiu "United we stand, divided we fall".
Shigela.
--
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "NUMET Media Release" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to numet-media-rel...@googlegroups.com.
To post to this group, send email to numet-med...@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/numet-media-release.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
Asante sana Prof. Marjorie kwa ufafanuzi huu, nimekuelewa vizuri kabisa. Labda nikutoa tu wasiwasi kuwa inavyoonekana tayari Comrade Nico alishakuunganisha kwenye group email hivyo michango yako tutakuwa tunaipata sote, hii ndio sababu niliweza kuiona hii e-mail yako, na ninatumaini kuwa wadau wengine wote wa NUMET wamekuona pia.
Karibu sana kwenye mtandao wetu, mchango wako kwetu tunauthamini sana. Jisikie huru kutuambia chochote unachopenda tukipate kutoka kwako, lakini pia kushiriki kwenye majadiliano yetu. Ujio wako kwetu ni fursa muhimu ya kupata mawazo mapya, ushauri, utaalam na hata maelekezo ya wapi huduma zetu zinatakuwa ili kuendeleza harakati ya kumkomboa mfanyakazi wa nchi hii.
Shigela.
Asante dada Marge, na pole sana kwa hiyo error. Mwanangu Leila kasahau pia kukueleza kuwa mimi ni baba yake, nafikiri siku moja atakueleza. Thank you all for this shake hand! Shigela. |
Naam Dada Marge, pole kwa kukosea kidogo jinsia yangu; mimi ni kaka sio dada, labda kwa uzuri tu jina langu litakuwa umelifananisha na la ninyi akina dada, sio vibaya maana sote ni binadamu wenye thamani ileile kwa Mungu na jamii yetu ya binadamu. Lakini pia nashukuru kwa kunijuza jina zuri ambalo ungelipenda nikuite; nafahamu kuwa maprofessor wengi hawapendi kuitwa kwa title zao, huo kwa hakika ni unyenyekevu mkubwa sana unaostahili pongezi za dhati. Nafurahi pia kwa kuwa umenipa jina ambalo nitajisikia huru kukuita nikijua kuwa utafurahia uonapo andiko langu. Asante kwa mawasiliano haya, na karibu sana. |
|
Shigela. |