Ndugu viongozi, wanacama na wadau wote wa NUMET .
Leo tarehe 1.10.2014, NUMET imetimiza miaka 3 tangu kuanzishwa kwake. NUMET ilianzishwa na wanachama 41 kutoka katika migodi ya Bulyanhulu, North Mara na Geita pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya Aveng Moolmans Mining (T) LTD. Mkutano uliopitisha azmio la kuanzisha chama hiki, ulifanyika katika Ukumbi wa Mkutano wa Hotel ya Alfendo mjini Geita.
NUMET Ilipata usajili wake tarehe 20.02.2013 na hatimaye kuzinduliwa rasmi tarehe 20.02.2014 Jijini Mwanza.
Leo tunajivunia ukuaji wake katika sekta zote. Wanachama wameongezeka hadi kufikia 1700 kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu. Wanachaa na viongozi wanayo ari kubwa sana ya mabadiliko katika kudai, kulinda, kutetea na kuboresha masilahi ya wafanyakazi wa tasnia ya NISHATI NA MADINI wakati wakiwa kazini na hata baada ya kuondoka kazini.
Natoa pongezi kwa wanachamwa waliotuamini wakajiunga na NUMET, nawapongza viongozi kwa kukubali kwa moyo wote kukitumikia chama bila kujali uchanga wake na au uhaba wa vitendea kazi uliopo na uliokuwepo.
Nawasihi viongozi na wanachama, tuendelee kushikamana na kushirikiana kujenga umoja ulioimara kwa faida ya wafanyakazi wa tasnia hii na Taifa lote kwa ujumla.
Natoa rai kwa wafanyakazi wote ambao hawajajiunga na NUMET kujiunga sasa ili tuyafikie malengo yetu tuliyoyapanga.
Happy Birthday NUMET.
Mungu ibariki NUMET, Mungu ibariki Tanzania.
Nicomedes M. Kajungu
General Secretary
Mobile: +255782315688 or +255767483271
Website: www. numet.co. tz
Twitter:@Numetz
Facebook: numet.tanzania
Sent from Blue Mail
--
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "NUMET Media Release" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to numet-media-rel...@googlegroups.com.
To post to this group, send email to numet-med...@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/numet-media-release.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.