Bandugu, Kwa mara nyingine tena, Mtandao wa Jinsia unawaletea Tamasha la Jinsia 2015. Tamasha litafanyika Dar es Salaam, Mabibo, kwenye viwanja vya TGNP tarehe 1-4 September, mwaka huu. Mabanda ya maonyesho tunakodisha kwa bei poa, hususan, kwa wanawake wajasiriamali wa ngazi ya Jamii ili waonyeshe, waelezee na wafanye promosheni ya kazi zao, mafanikio na changamoto zao. Sekta ya madini ni moja katika harakati zetu za kutukomboa kwenye umasikini uliotuvaa kama koti la chuma. Shime! Shime! Kwa maelezo zaidi, wasiliana na mimi kuhusu mabanda ya maonyesho kwa wanawake waliopo kwenye sekta ya madini. Karibuni Leila |
Ahsnte Leilah,
Nitakutafuta.
--
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "NUMET Media Release" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to numet-media-rel...@googlegroups.com.
To post to this group, send email to numet-med...@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/numet-media-release.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
Kila laheri comrades, kwa sisi wanasiasa pia naona kipindi hiki ni kigumu kidogo kwa ajili ya maandalizi ya kampeni za mwaka huu za uchaguzi mkuu maana tutatakiwa kushiriki kwa njia moja ama nyingine ili kufanikisha vyama vyetu kupata fursa za kutosha kwenye serikali ijayo na/ama kwenye vyombo vya kutunga sheria na kuisimamia serikali.
Ila niseme tu kuwa shughuli hii ni muhimu sana katika harakati zetu za kupigania haki na usawa kwenye makundi yetu ya kijamii.
Lakini pia, ni wakati muhimu wa kukutana, kufahamiana, kubadilishana uzoefu na kuangalia maeneo ya ushirikiano katika kukuza harakati za haya makundi yetu ya kupigania haki na usawa. Pia kujitangaza maana NUMET bado ni chama kichanga sana!
Nashauri tu kuwa itafutwe fursa yoyote hata kama itakuwa ni ndogo sana kwa NUMET pia kushiriki katika shughuli hizi za TGNP maana ni mwanzo mzuri wa kujenga mahusiano na ushirikiano. Hii ndio njia rahisi ya kufungua milango ya ushirikiano na makundi mengi zaidi ya kijamii hapa nchini na hata kimataifa maana hawa wenzetu ni wakubwa tayari!
Shigela.
Asante Ba Shige, Ni muhimu sisi wanaharakati wa ukombozi wa wanawake kutoka kwenye umasikini uliyokithiri, kupata washirika kwenye sekta ya madini. Leila |
Ni kweli mwanangu Leila, mimi pia nakuja Dar wiki ijayo, kama utakuwa Dar nitakutafuta ili tujadili ushiriki wetu.
Najua tuna fursa ya kusaidiana katika haya. Nitatamani kukutana na hawa akina mama wachimbaji wadogo wadogo maana najua yapo ya kushauriana na kupeana misaada ya kitaalam.
Shigela.