Ili kuhakikisha sekta ya nishati na madini inawanufaisha Watanzania, wafanyakazi wa sekta hii wameunda umoja wao; Chama cha Wafanyakazi cha National Union of Mine and Energy Workers of Tanzania (NUMET) kilichosajiliwa tarehe 20/2/2013 kwa Na. 029 kikiwa na wanachama 41, na sasa kina wanachama zaidi ya 1,200 katika migodi ya Kanda ya Ziwa. Makao Makuu ya NUMET ni Jijini Mwanza.
Katika kuadhimisha mafanikio yaliyopatikana ndani ya mwaka mmoja, NUMET imepanga kufanya uzinduzi rasmi ambapo mgeni rasmi atakuwa Waziri Nishati na Madini Mh. Professor Sospeter Muhongo.
Ili kumuunga mkono, wamealikwa wadau wapatao 300 ambao ni pamoja na, wakuu wote wa mikoa ya Kanda ya Ziwa, Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Mwanza, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Wabunge wote wa majimbo ya Mkoa wa Mwanza, Wakuu wa Kampuni za uchimbaji wa Madini na kampuni mbali mbali za utafiti wa gesi na mafuta, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, mahakama, asasi za kiraia,Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) na wadau wengine mbali mbali.
Uzinduzi rasmi wa chama utafanyika tarehe 20.02.2014, Jijini Mwanza katika viwanja vya Nyamagana.
Madhumuni ya uzinduzi huu ni;-
1. Kukitambulisha chama kwa Umma wa Watanzania;
2. Kufanya harambee ili kutunisha mfuko wa Chama kwa lengo la kukidhi mahitaji ya sasa ya chama ambayo ni;
a. Kununua gari ya chama itakayosaidia katika utoaji wa huduma kwa wanachama kwa wakati na kwa ukamilifu.
b. Kununua kiwanja na kuanza ujenzi wa jengo la ofisi za makao makuu ya chama.
3. Kuwakutanisha wadau mbalimbali wa Tasnia ya Nishati na Madini kwa lengo la kujenga mtandao wa mashirikiano ili kufanikisha harakati za kufikia malengo husika.
4. Kubainisha haki na wajibu wa NUMET kwa wadau ikiwemo harakati za kudai, kutetea, kulinda, na kuboresha hali na maslahi ya wafanyakazi wa sekta hii.
Nachukua fursa hii kwa namna ya pekee kuwaalika wanamabadiliko wote kwenye shughuli hii muhimu.
Kama huwezi kufika lakini unania ya kujumuika nasi katika harambee, unaweza kutoa mchango wako kupitia Account ya Chama.
BANK YA CRDB
JINA LA ACCOUNT : NUMET
NAMBA YA ACCOUNT : 0150352489700
UNITED WE BARGAIN, DIVIDED WE BEG.
Nyote Mnakaribishwa.
--
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "NUMET Media Release" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to numet-media-rel...@googlegroups.com.
To post to this group, send email to numet-med...@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/numet-media-release.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
marjorie mbilinyi <marjorie...@gmail.com> wrote:
>Hongereni kwa hatua kubwa. Sema msiogopi sema!!!!
>
>
>2014-02-05 Nicomedes Kajungu <nicom...@gmail.com>:
>
>> Ili kuhakikisha sekta ya nishati na madini inawanufaisha Watanzania,
>> wafanyakazi wa sekta hii wameunda umoja wao; Chama cha Wafanyakazi cha
>> National Union of Mine and Energy Workers of Tanzania (NUMET)
>> kilichosajiliwa tarehe 20/2/2013 kwa Na. 029 kikiwa na wanachama 41, na
>> sasa kina wanachama zaidi ya 1,200 katika migodi ya Kanda ya Ziwa. Makao
>> Makuu ya NUMET ni Jijini Mwanza.
>>
>>
>>
>> Katika kuadhimisha mafanikio yaliyopatikana ndani ya mwaka mmoja, NUMET
>> imepanga kufanya uzinduzi rasmi ambapo mgeni rasmi atakuwa *Waziri
>> Nishati na Madini Mh. Professor Sospeter Muhongo. *
>> *BANK YA CRDB*
>>
>> *JINA LA ACCOUNT : NUMET*
>>
>> *NAMBA YA ACCOUNT : 0150352489700 *
>>
>>
>> *UNITED WE BARGAIN, DIVIDED WE BEG.*
>>
>>
>> *Nyote Mnakaribishwa. *
>>
>>
>> *_________________________________________________*