Minutes za Kikao cha Wana-Mugabe89 (Shukrani to Dennis Rwegoshora)

25 views
Skip to first unread message

William Kaijage

unread,
Jul 25, 2007, 5:10:10 AM7/25/07
to muga...@googlegroups.com

Kikao cha III cha wana Mubage 89 kilichofanyika Vatican Hotel Sinza tarehe 23/06/2007. 

Waliohudhuria: 

  1. Dennis Francis Rwegoshora
  2. Ernest Haule
  3. Langeni Mpokera
  4. Edgar Chibura
  5. Geofrey Mwakajonga
  6. Magnus R Kibonde
  7. Godwin Liamba
  8. Moses Hella
  9. William Kaijage
  10. Henry Msofe
  11. Namundi Simwanza
  12. Leticia Erasmus
  13. Nyarukanda (Lachel) Nyega
  14. Bahati (Japhet) Kalewe
  15. Nicodemus Jackson Warioba
  16. Moses Hella
 

Agenda: 

  • Uchaguzi. 
    Viongozi walikuwa ni walewale ila Katibu Dickson Paschal alitoa hudhuru kwa kutoweza kufika na ndipo kikao kilimchagua Dennis Francis Rwegoshora kama katibu.  
  • Uchakavu. 
    Wajumbe walijadili kwa kina suala la kutoa "uchakavu" katika vikao vya wanamugabe 89. Iliamriwa kwamba suala la kutoa uchakavu linaweza kuathili mahudhurio kwa kuwa mjumbe kama hana fedha inawezekana angependa kuhudhuria ila kwa sababu hana cha kuchangia inakuwa vigumu kuhudhuria.  
  • Taarifa ya msiba. 
    Mwenyekiti alitoa taarifa ya msiba uliompata Leticia Erasmus kwa kufiwa na mama yake mzazi. Na ndipo wajumbe walipoamua kujiunga naye katika majonzi kwa kutoa rambirambi kama ifuatavyo:  
        • Mugabe Group                            20,000/=
        • Dennis Rwegoshora                      2,000/=
        • Ernest Haule                                 2,000/=
        • Langeni Mpokera                         2,000/=
        • Edgar Chibura                              2,000/=
        • Geofrey John                                2,000/=
        • Magnus Kibonde                          3,000/=
        • Godwin Liamba                            3,000/=
        • Moses Hyela                                 5,000/=
        • Nyarukanda Rachel                      5,000/=

          Jumla                                           46,000/= 

NB:  Idadi inayoonekana kwenye michango ni tofauti na inayoonekana kwenye mahudhurio hii ni kwa sababu ya hudhuru mbalimbali zilizotolewa na wajumbe nakuondoka kabla ya agenda hii.  

Kama shukrani, Leticia alishukuru sana wanamugabe kwa kuwa naye pamoja katika kipindi kizito cha huzuni kwa njia mbalimbali, pia aliwashukuru kwa mchango na aliomba ushirikiano zaidi uendelee kudumu zaidi na zaidi.  

  • Mwenyekiti aligusia suala la trip ya Bagamoyo kama lilivyotolewa na Rockus Kahanda alisema idadi bado ni ndogo kuweza ketekeleza safari hiyo ni mpaka hapo idadi itakapokuwa ya kuridhisha ndipo suala linaweza kutekelezeka.   
  • Langeni alikijulisha kikao kwamba kazi aliyopewa kwenye kikao cha pili ya kufuatilia pale shuleni Mugabe haikuwezekana kwa sababu zilizokuwa nje ya uwezo wake lakini akaahidi kutoa taarifa rasmi kwenye kikao kinachofuata.   
  • Mwenyekiti alitoa taarifa kuhusu katiba kwamba anawasiliana kwa karibu na Bahati Kalewe kuhusiana na hilo hivyo ameomba tumpe muda kidogo aweze kulikamilisha kwa kuwa ni taratibu zinazohusiana na mambo ya kisheria.   
  • Mwenyekiti pia alikitaarifu kikao kuhusu tovuti kwamba mhusika alisafiri kwa hiyo ilikuwa vigumu kidogo kuweza kukamilisha zoezi hilo ila akaongeza kuwa zoezi linaendelea vizuri.   
  • Wajumbe katika kujadili suala la kwanini mahudhurio ya wajumbe yalishuka ilionekana tarehe za vikao zisiwe zinapangwa katika siku za weekend kwa kuwa siku hiyo watu wengi huwa wanajihusisha zaidi na mambo ya kijamii kama harusi n.k. 
  • Hivyo Mwenyekiti aliomba kikao kijacho kifanyike siku ya nanenane yani tarehe 08/08/2007, Vatican City Hotel kuanzia saa 9 kamili mchana.
Mugabe89 Meeting Vatican 23 Jun.doc

Benson Kidenya

unread,
Jul 25, 2007, 11:21:12 AM7/25/07
to muga...@googlegroups.com
Sema wana Mugabe89 watoto wa kula AishKrim za Ukwaju!
 
Dennis huyo jamaa namkumbuka sana jina kamili ni Patrick Mazuki huyu alikuwa mtoto wa Mwl Mazuki ambaye alitufundisha darasa la pili mambo ya Manenge na Mandawa katika kusoma bila sauti! (aka kusoma kimya!) Mwl Mazuki pia alikuwa ni balaa kwa kushusha nyiti next to Mwl Muhana yule Mwl wa Mabetirii (Battery) kwa ajili ya kuchorea ramani!. Huyu Patrick Mazuki alikuwa Mission Town na alishawahi kumuibia mama yake godoro na kwenda kuliuza pale sinza kijiweni! kwa hiyo zile "per diem" alizokuwa akija nazo shule kununua mazagazaga wakati wa break ya sa 4 zinatokana na juhudi zake katika kujiongezea kipato! (Mkukukuta).   Patrick mazuki baadae alihama hakumalizia pale Mugabe na sisi!
 
Lile jopo la wauza vitu kama banquet la ma-server wa harusi za sikuhizi liliundwa na wauza Icecream za aina mbalimbali, za ukwaju, za ndimu, za fanta n.k. kulikuwa na hizo sambusa za viazi vitatu, ufuta, mabisi(aka Mabumunda), viazi ulaya  vya mchuzi kwenye kibakuli, ubuyu, uji wa Mwl Naubena (huu ulikuwa mradi wa shule), mihogo ya kukaanga na chumvi ya pilipili nyekundu, mihogo ya kuchemsha na kachumbari, maembe mabichi na chumvi yenye pilipili nyekundu! (Haya maembe mimi bado huya nayala mpaka sasa na nimeya-miss sana!), n.k. Wenye fedha zao, Mazuki et al walikuwa wakizifuata chipsi mayai kule ubungo NHC Social Club kwa Seba!
 
Amina Massenga wife yuko safi na salama tu! si unajua tena kwa sasa niko kifungoni mpaka wiki sita zipite hakuna kumsogelea mtu ni bila bila mwanawane!
 
Bahati Kalewe Mtoto wa Town, Mtoto wa jiji la Kandoro, Jiji la njia tatu ukizubaa unagongwa! Mkarbishe John Isack Mtoto wa Killage(Kijijini) asije gongwa na atoe nauli kamili kwenye daladala manake nauli imepanda sio ile ya zamani! Labda ajifanye mwanafunzi wa secondari! Na mwambie siku hizi wapiga debe hakuna vituoni atataabika tu! manake hawa jamaa japokuwa walikuwa wanatuibia pia walikuwa wanatusaidia kujua nauli za daladala na route zake sisi watu wa mikoani! Ilikuwa kama mwanawane ndio una mia tu mfukoni, basi ni kumsikiliza tu mpiga debe kwa makini! akisema "Kariakoo Mia!" -unapanda!, Ukisikia "Kariakoo mia Hamsini" -Unachuna kimtindo, Hupandi! 
 
Dennis hongera kwa kazi nzuri ya kuandaa Ripoti ya kikao cha 3! Nimefurahisha na mlivyolihitimisha suala zima la mambo ya uchakavu!. Ila kuna watu wengine walihudhuria kikao na majina yao siyaoni kama Angela Killewo na Hussein Nkalami! Pia kwenye mchango wa Leti naona kuna Mugabe group 20,000. Hii ni group gani tena!?  
 
Kikao kingine kama kuna ajenda muhimu zitolewe mapema ili hata kama mtu ana udhuru basi anaacha kitu kidogo na kutambaa zake! kuliko watu kuondoka na mafao ambayo pengine wangeyatoa!
 
King Kaijage unatuyeyusha na picha za kikao cha 3 au picha za Digital Camera nazo huwa zinaungua!? Au mpigapicha bado atawadai!
 
Hafidh Mohamed Karibu sana kwenye blog letu! Mwenzio nina mke mmoja na mtoto mmoja!
 
All the Best wana MGB89!
 
Baba Prosper!


 


Sick sense of humor? Visit Yahoo! TV's Comedy with an Edge to see what's on, when.

japhet stephen

unread,
Jul 26, 2007, 12:15:19 AM7/26/07
to muga...@googlegroups.com
Nimekupata vilivyo Baba Prosper, bwana John karibu
Kandoro Town na Bwana Hafidh Mohamed karibu sana
habari za KANDAHAL au TORABOLA hapa bwana kama
hautachakaa mwenyewe basi utachakazwa kwa vumbi la
Kandoro Town, na suala la kugongwa kwa kutojua njia
tatu hili ni la msingi kuzingatiwa kwa sasa hatuko
tayari kumpoteza mwana mugabe aliyetughalimu kuwa naye
kwa miaka miiiingi alafu aji-muvuzishe kwa Mungu
mwanawane wakati tunamuhitaji kwa ujenzi wa JK
Country.

Ooookey,Kwanza wanawane ni kweli kama alivyosema baba
Prosper naunga mkono kama si mguu kuwa wajumbe
tuliohudhulia tulikuwa wengi ila michango ni kidogo ni
sahihi kabisa kama ikiwezekana next time kuna
immergency yeyote imetokea tupate taarifa mapema kama
kuna mtu anaudhulu wake na amefika atoe mchango wake
alafu kama ni kuji-muvuzisha aruhusiwe wakati
ameshatoa mchango kinachohitajika.

Pili kuhusu njia tatu hii bwana ni BIG ISSUE very BIG
ISSUE. Kuna utata unaweza ukajitokeza siku yeyote
kutokana na taratibu hii ya uendeshaji wa magari
kutumia njia tatu, makampuni ya BIMA yanaweza kukataa
au kukwepa kwa makusudi kulipa fidia(Compensation)kwa
yeyote atakayepata ajali akiwa kwenye upande wa tatu
yaani aliyeingia upande mwingine wa barabara ambayo si
sahihi kiutaratibu kutumika wakati wa kuendesha vyombo
vya moto.

Utaratibu huu umekurupukiwa ili kuondoa msongamano
barabarani lakini haukuangalia sheria na taratibu za
usalama na uendeshaji wa vyombo vya moto barabarani
hivyo basi mwanawane wale wenzangu wenye magari ya
mikopo au urithi wawe makini kabla ya kujimuvuzisha
kwa madai ya kuwahi wanakoenda tulieni kidoooooogo
usije ukawahishwa kwa Sir God baada ya nyumbani.

Dondoo by JAPHET.
Asalaaam alkhum.

> ---------------------------------


> Sick sense of humor? Visit Yahoo! TV's Comedy with
> an Edge to see what's on, when.
>
>
>

___________________________________________________________
Yahoo! Mail is the world's favourite email. Don't settle for less, sign up for
your free account today http://uk.rd.yahoo.com/evt=44106/*http://uk.docs.yahoo.com/mail/winter07.html

Jefta Malaba

unread,
Jul 8, 2008, 6:14:56 AM7/8/08
to muga...@googlegroups.com
TRIP NI NINI LBDA NIULIZE KIDOGO ,SITOI MAANA YAKE LEO NI VYEMA NIKAACHA UWANJA KWENU.ILA MIE NAOMBA TUPANGE TRIP LENGO NA MADHUMUNI NI YALE YALE .JE MWENYEKITI UPO????????????WATU HAWA VIPI??????SIWAELEWI NI LIPI WATAKA ATI .KILA KITU TUKO NYUMA JE TUBEBWE MIGONGONI?????.NAOMN=BA NEXT KIKAO KIWE HUKO BAGAMOYO MSISITIZO FAMILIA ZETU TUWE NAZO

--- On Wed, 7/25/07, William Kaijage <kai...@gmail.com> wrotemail.com>
Subject: Minutes za Kikao cha Wana-Mugabe89 (Shukrani to Dennis Rwegoshora)
To: muga...@googlegroups.com
Date: Wednesday, July 25, 2007, 2:10 AM

Dennis Francis

unread,
Jul 8, 2008, 7:13:51 AM7/8/08
to muga...@googlegroups.com

Kama sijakosea tulikubaliana itegemee na idadi ya watakaokuwa tayari. Sio busara ikiandaliwa halafu wakajitokeza watu 6 tu.

 

Halafu mwenyeji mwenyewe ROCKUS hashikiki yupo bize kumzidi hata KIKWETE.

 

Dennis.

--- On Tue, 7/8/08, Jefta Malaba <jdma...@yahoo.com> wrote:

john isaac

unread,
Jul 21, 2008, 9:13:57 AM7/21/08
to muga...@googlegroups.com

Wanawane kunani paleeeeeeeeeeeeee???

Haloo mabibi na mabwana kimya kingi kina mshido mkuu!!!!!!!!!!!!!!!

Mara Bwagamoyo Mara vatican City niweke wapi maguu kwenye nanenane hii natarajia kuhudhuria kwenye mjumuiko huo kama itawezekana kwa kudura za Mnyezi Mungu.


Mr John


--- On Tue, 7/8/08, Jefta Malaba <jdma...@yahoo.com> wrote:

From: Jefta Malaba <jdma...@yahoo.com>
Subject: TRIP YA BAGAMOYO VIPI WANA MUGABE?
To: muga...@googlegroups.com
Date: Tuesday, July 8, 2008, 3:14 AM

Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages