Ni maono yangu kuwa ongezeko hili husababishwa hasa na migogoro ya
nyumbani hasa katika familia zetu hizi za kimaskini unakuta mtoto
inampelekea hadi kutoroka nyumbani na kwenda kuishi MTAANI irimradi tu
aepukane na adha anayoipata hapo home. Jambo lingine ni Vifo vya
wazazi, unakuta mtoto amepoteza wazazi wake angali mtoto (labda wa
miaka kumi hivi) sasa mtoto kamahuyu inabidi alelewe na ndugu au jamaa
wa wazazi wake nako huko mambo yanakuwa magumu labda kutokana na ugumu
wa maisha ya huyo mlezi inapelekea huyo mtoto kuhisi labda hatendewi
haki(labda akiomba daftari,kalamu,sare ya shule imechakaa hapatiwi)
katika hali ya utoto inapelekea kuhisi "eti kwa kuwa YATIMA ndio maana
wanamfanyia hivyo" kumbe hajui maisha magumu kwa mlezi anaemuhudumia
yanachangia.Income yake ni ndogo kiasi cha kuweza kujihudumia yeye Mke
wake na watoto wawili sasa ameongezeka watatu inakuwa vigumu
kubalance.Jambo lingine linaloweza kumpelekea Mtoto huyu kutoweka
maskani na kuelekea MTAANI ni Manyanyaso ya wazi wazi kutoka kwa mlezi
wake ukiangalia familia nyingi ndugu wanaangalia sana mali baada ya
mmoja kati ya wanafamilia kupoteza maisha yao (wakiwa na tamaa ya
kurithi mali, hivyo wanamtesa huyu mtoto irimradi tu aweze kuondoka na
kuacha mali hiyo ambayo ndio hasa muhimili wamaisha yake) badala ya
kuangalia ni kwajinsi gani wataweza kuihudumia familia hiyo.