JE VALENTINE HAICHANGII UFUKSA?

3 views
Skip to first unread message

Fusha

unread,
Feb 5, 2007, 7:02:59 AM2/5/07
to Mtaa Kwa Mtaa
Asalaam aleykum ndugu zangu,wasomaji wangu wa blog hii leo nimeamua
kuweka hilijambo wazi iliniwezekupata ufafanuzi wakina kutoka kwenu.
kwauelewa wangu ulio finyu ninaonakuwa sikuhii huwa ni ya sherehe kwa
wapendanao wote duniani haijachagua awenimtoto au mkubwa ilimradi tu
awe na anayempenda au sio wasomaji wangu. hivyo basi wengi wao hununua
vitu ambavyo vinaweza kumpendeza mpeziwe ilimraditu kumfurahisha
sikuhiyo na kumuonyesha ni jinsigani anavyompenda.lakini wapo wanao
itumia siku hiyo vizuri sana kama ilivyo kusudiwa na kuna wengine
sijui niseme hawaeliwi maana ya siku hiyo kama mimi inavyo nichanganya
kutokana na matendo mengine yanayofanyika siku hiyo kwani ni aibu.huwa
kunautaratibu wa klabu nyingi sana za usiku huwa wana tayarisha show
flani maalumu kwa siku hiyo ni pamoja na vinywaji kuongezwa ilimradi
kukidhi mahitaji ya wateja wao. sasa hapo ndio pana mtafaruku kwani
unakuta mtu siku hiyo anakunywa kupita kiasi sasa nashindwa kumuelewa
mtu kama huyu je yeye mwenza wake ni hicho kinywaji anacho kikomelea
mpaka pomoni nini?.Clubu za music na zo sikuhiyo ndio wanayo make
money kwani hao wanaojiita eti wapendanao huenda kwenye club hizo na
siku hiyo cha kushangaza bei huwa inabadilika .Upande mwengine
unaonistajabisha zaidi kuliko zote na upande wa Nyumba za wageni kwa
siku hiyo huwa zinajaa hata zile zisizojaa hadi unakuta kiboa HAKUNA
NAFASI AU NAFASI ZIMEJAA sasa nisaidieni hizi nyumba hujazwa na
wapendanao hawa na kama ni wenyewe kwanini sikunyingine hua hazijai?
au huwa hawapendani!

Reply all
Reply to author
Forward
0 new messages